Orijino komedi ya Masanja chali, haina mvuto tena

Aliyeona kipindi cha jana anipe hints jamani ilikuwaje! Nilichelewa kutoka kaizni, hivyo sikuwaona kina Masanja jamani.

Kwa ufupi hamna kitu zaidi ya tangazo la tb na shukran kwa waliomchangia sajuki, mi ni mpenzi wa comedy hasa ya kina masanja lkn walipofikia naona wanatutupa mkono
 
Hivi karibuni takribani mwaka huu wote hadi tulipo leo TBC1 na Komedi ya Masanja, Choti etc haina mvuto kabisa kwa watazamaji kiasi cha watu kukimbilia EATV kule kwa bambo ambao wanaonekana kuziba pengo la kifo cha mende cha komedi ya kinaMjuni.

Utafiti usio na gharama kubwa kwenye maeneo ya starehe wadau wamekuwa wakiomba sehemu za bar kuhamisha chanel kutoka TBC1 kwenda EATV ili kupata ujumbe wenye maudhui ya kuelemisha, burudani na vichekesho.

Ni dhahiri Masanja na wenzake ama wamekwisha au ndo uongozi wa TBC1 umeshindwa kuwasaidia inavyohitajika ili kuendelea kukalia usukani wa komedi TZ; Ni ama warudie kwenye fomu au tuwaage rasmi ktk fani hiyo na tuwakaribishe makundi yenye ujumbe na kuelimisha wakati ujumbe unafikishwa kwa kutoa burudani EATV/StarTV-Futuhi japo hawako serious sana na kazi pia.

Mlitulisha mua sasa ni wakati wa kutema makapi ya mua, hakuna utamu tena.

Taabu kubwa ya WASANII WETU ni UKOSEFU WA UBUNIFU NA KUSOMA MAHITAJI ya WATEJA WAO 9sisi watazamaji wa vipindi vyao; wasikilizaji wa miziki yao; wafuatiliaji ya watutengenezeacho. Wakiona wamefurahiwa wanasahau kuwa kuendelea kuwa unakubalika kunahitaji JITIHADA KUBWA NA KUSOMA MABADILIKO KATIKA WATAKACHO WATEJA WAKO....

Wasanii wetu wasipoweza kujifunza hili tutabakia KAMA MAZUZU TUUU....Unakuwa maarufu leo; kesho kama chewing gum iliyoishiwa ladha=kila mlaji anakutema utamu ukiisha
 
hivi kwani kibali cha kutumia tv ya taifa kumtangaza mtu mmoja kwa masaa kwa wiki kadhaa kama kwamba hana ndugu wa rafiki au jirani tu wametoa wapi? Au ugonjwa wake umegeuzwa kipindi na watu wanalipwa???? Wadhamini kama wapo nao wanaliwa tu kiujanja ujanja!!!

Kwani kweli walihitaji kumfanyia hivyo msaani mwenzao kwa kisingizio cha kumchangia?? Haki ya faragha iko wapi? Kwani hakuna njia nyingine kwa wao kufanya kitu cha msaada kama michango bila kutumia tv ya serikali na wabunge wauza sura??? Au ndo kuuishiwa kwa vipindi huko??? Kuishiwa kwa fikira sahihi.

Ina maana hao wabunge wasingetoa fedha kama sio mpaka waoneshwe kwenye tv? Ni ugonjwa wa saduki au umarufu wa wachangiaji na masanja mwenyewe ndo umezalilisha saduki?????

Ushauri wa bure pamoja na kumsaidia lakini umemzalilisha sana, kama kwamba hana hata senti moja, hana ndugu hata mmoja au ni chokolaa??? Au hajawai kufanya hata kazi moja bosi wake wa zamani akafurahi, ili amsaidie wakati wa shida??? Masanja na tbc kamuombeni radhi saduki ama kimya kimya au hadharani sio sahihi sana mlivyomfanyia.

ndo tatizo la wabongo kwa kupenda kujihisi kawa tuko right mda wote sasa kamdhalilisha kwa lipi...hivi ikitokea leo unaumwa na ugonjwa wa saduki unaweza kuniambia imekata bima ya kukutibu kwa million 20 sijui au nawe utatafuta michango tuache lawama na kuwapongeza kwani mi naona siku hzi atleast wana chekesha na kuelimisha madhara ya tb na kuwapa moyo watanzania wa harambee swala ambalo wenzetu wakenya wametuzidi...hapo ukute hata jero hujatoa af maneno kibao
 
hebu jaribu ku fikirikwanza kabla hujaongea,SAJUKI baada ya kupata maradhi na kuambiwa akatibiwe India kwa kuwa pesa ilikuwa ndefu(hawaimudu) 'mil 25' wife wake WASTARA alitangaza mwenyewe kuomba watz wamsaidie kupitia blogs,facebuk,twitter,radios ambapo alitoa na ac no,na no. Kwaajil ya kumchangia kupitia mpesa na tigopesa.Original comedy nao kupitia kipind chao wakaona wamsapot msaníi mwenzao,sasa tatizo liko wap hapo?Ama kweli TENDA WEMA UENDE ZAKO
 
Last edited by a moderator:
Hata Tembo akonde vp hawez kuwa kama swala n' viceversa.Original Comedy wamefulia ndio but bado ni wakali sana ukicompare na Futuhi na Ze comedy(me hawajaniconvice kwakweli).kikund ambacho naona kweli wanachekesha kuliko hata original comedy ni MIZENGWE na kile cha kina majuto ingawa watu wengi hawavifuatilii
 
iiiiiiivoooo?????aaalaaaaa!!!!!!
 
Mkare_wenu... u seem more interesting n fun to be with..ebu ni-PM tuone uwezekano wa kuanzisha comedy yetu...
 
Last edited by a moderator:
Hata Tembo akonde vp hawez kuwa kama swala n' viceversa.Original Comedy wamefulia ndio but bado ni wakali sana ukicompare na Futuhi na Ze comedy(me hawajaniconvice kwakweli).kikund ambacho naona kweli wanachekesha kuliko hata original comedy ni MIZENGWE na kile cha kina majuto ingawa watu wengi hawavifuatilii

Kweli umenena, vituko show ya ch10 ni nomaaa, na mizengwe wanaburudisha sana!!
 
sisemi asichangiwe pesa ya matibabu kama ni maskini, achangiwe tu. suala ninalosema mimi je ni haki kutumia saa nzima, wiki mbili etc kumtangaza mtu anaumwa harafu wachangiaji waje TV ya taifa kufanya changizo?? kwani kuchanga kimya kimya kulikosa nini?? au mpaka watz tujue na fulani kachangia???? Kuja kwnye TV sizani kama ulikuwa kwa manufaa ya Mgonjwa, ila imetumika watu kuonekana kwa mara nyingine.

Pili komedi ni kipindi chenye kusajiliwa na maudhui yake ni komedi, kwa hiyo suala la saduki ni komedi pia??? maana saa njia ni yeye. Nikweli anahitaji msaada lakini namna alivyofanyiwa ni dhihaka. Anyway mwenye njaa hana miiko, endeleeni lakini ujumbe umefika.
 
Ninakubaliana kabisa MIZENGWE wako juu sana. Elimu na Burudani kwa sana. Hawa Komedi Masanja hakuna kitu hata wakitetewa hali iko palepale wamekwisha. Cha msingi ni waje upya na kazi mpya yenye kiwango; sio kuuza sura kwa Masanja na maneno mengi ya kwake kwake wala siio kama timu ya Komedi.
 
tangazo la TB ni pesa tupu tu pale kamueni kina mujuni siliveri mupo ju kama taa za minara ya tigo
 
Hawa jamaa tangu njaa ilipowasumbua na kuanza kutumiwa na magamba kwa shughuli, wamepoteza imani na mvuto kwa jamii kama chama cha magamba chenyewe.
 
huyu aliyetuma hii post ni bambo au mtanga suala la kina mpoki kufulia ni uongo mfano mi binafsi kama nitaangalia comedi basi ni mpoki,joti,masanja mkandamizaji punjalishedo steringi mangisheduu the bigi sineki kutoka shinyanga vijijini. Wale ndo wakali hawa kina mathawe wanalazimisha vitu ambavyo sio talent yao

nakubaliana na wewe mkuu
 
Tuwaandalie kipindi Cha amefulia...... Wao siwalikuwa wakiwacheka wenzao sasa zamu Yao. Usitukane mamba wakati mto hujavuka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom