Orijino komedi ya Masanja chali, haina mvuto tena

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,449
2,000
Hivi karibuni takribani mwaka huu wote hadi tulipo leo TBC1 na Komedi ya Masanja, Choti etc haina mvuto kabisa kwa watazamaji kiasi cha watu kukimbilia EATV kule kwa bambo ambao wanaonekana kuziba pengo la kifo cha mende cha komedi ya kinaMjuni.

Utafiti usio na gharama kubwa kwenye maeneo ya starehe wadau wamekuwa wakiomba sehemu za bar kuhamisha chanel kutoka TBC1 kwenda EATV ili kupata ujumbe wenye maudhui ya kuelemisha, burudani na vichekesho.

Ni dhahiri Masanja na wenzake ama wamekwisha au ndo uongozi wa TBC1 umeshindwa kuwasaidia inavyohitajika ili kuendelea kukalia usukani wa komedi TZ; Ni ama warudie kwenye fomu au tuwaage rasmi ktk fani hiyo na tuwakaribishe makundi yenye ujumbe na kuelimisha wakati ujumbe unafikishwa kwa kutoa burudani EATV/StarTV-Futuhi japo hawako serious sana na kazi pia.

Mlitulisha mua sasa ni wakati wa kutema makapi ya mua, hakuna utamu tena.

Habari zenu

Tukiwa hapa kijiweni Bamaga, tukipiga story mbili tatu anakuja jamaa Mshikaji wetu anayefanyia TBC ambapo Ni mmoja kati ya waendesha kipindi fulani...Baada ya kupiga story mbili tatu tumejikuta tunamwuliza kuhusu hili kundi baada ya kupotea ghafla katika ramani ya vichekesho.

Naye alichotujibu ni anasikia kundi limevunjika Kimyakimya kila mtu anapiga issue zake..

Kuna mwenye habari zaidi kuhusu Kuvunjika Kwa Group Hili???
 

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
Nimependa hiyo MLITULISHA MUA SASA ni wakati wa kutema makapi ya mua HAKUNA UTAMU TENA.
NNA MUDA WA MREFU SIWAFUATILII HAWA WADAU,HUENDA WAMECHOKWA
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,912
2,000
wamefuliaaaaa,masanja nina wasiwasi kapiga mamilioni ya sajuki tunaomba ACG wa bongo movie awaulize wale wabunge 30 aliowataja kwamba watoe hela.
 

Gedeli

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
497
250
hivi bado wapo hawa?

kilichowamaliza hawa jama TBC yenyewe haina mvuto tena kwa wanachi wataifa hili. pili inaelekea TBC kama ilivyoselikalini wamekumbwa na ukata mkubwa wa kutisha hawana tena uwezo wa kutegeneza vipindi vipya wamebakia kutuwekea vipindi vya mwaka 47
 

KALYOVATIPI

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
1,415
0
huyu aliyetuma hii post ni bambo au mtanga suala la kina mpoki kufulia ni uongo mfano mi binafsi kama nitaangalia comedi basi ni mpoki,joti,masanja mkandamizaji punjalishedo steringi mangisheduu the bigi sineki kutoka shinyanga vijijini. Wale ndo wakali hawa kina mathawe wanalazimisha vitu ambavyo sio talent yao
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,449
2,000
Hivi kwani kibali cha kutumia TV ya taifa kumtangaza mtu mmoja kwa masaa kwa wiki kadhaa kama kwamba hana ndugu wa rafiki au jirani tu wametoa wapi? au ugonjwa wake umegeuzwa kipindi na watu wanalipwa???? wadhamini kama wapo nao wanaliwa tu kiujanja ujanja!!!

Kwani kweli walihitaji kumfanyia hivyo msaani mwenzao kwa kisingizio cha kumchangia?? haki ya faragha iko wapi? kwani hakuna njia nyingine kwa wao kufanya kitu cha msaada kama michango bila kutumia TV ya Serikali na Wabunge wauza sura??? au ndo kuuishiwa kwa vipindi huko??? kuishiwa kwa fikira sahihi.

Ina maana hao wabunge wasingetoa fedha kama sio mpaka waoneshwe kwenye TV? ni ugonjwa wa Saduki au Umarufu wa wachangiaji na Masanja mwenyewe ndo umezalilisha Saduki?????

Ushauri wa bure pamoja na kumsaidia lakini umemzalilisha sana, kama kwamba hana hata senti moja, hana ndugu hata mmoja au ni chokolaa??? au hajawai kufanya hata kazi moja bosi wake wa zamani akafurahi, ili amsaidie wakati wa shida??? MASANJA NA TBC KAMUOMBENI RADHI SADUKI ama kimya kimya au hadharani sio sahihi sana mlivyomfanyia.
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,296
2,000
Hawana jipya kwakweli masanja anafanya vitu vywa kiwazimu wazimu tuu
kama hawajawekeza sehemu ingine imekula kwao teheteheteheteheteheteheteheteete
 

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
2,000
Aliyeona kipindi cha jana anipe hints jamani ilikuwaje! Nilichelewa kutoka kaizni, hivyo sikuwaona kina Masanja jamani.
 

AZIMIO

Senior Member
Jun 15, 2011
188
195
huyu aliyetuma hii post ni bambo au mtanga suala la kina mpoki kufulia ni uongo mfano mi binafsi kama nitaangalia comedi basi ni mpoki,joti,masanja mkandamizaji punjalishedo steringi mangisheduu the bigi sineki kutoka shinyanga vijijini. Wale ndo wakali hawa kina mathawe wanalazimisha vitu ambavyo sio talent yao

Nakuunga mkono moja kwa moja Mimi nimeacha kabisa kuangalia Komedi sjaona watu wanalazimisha fani ni kinyaa kitupu,kama wao ni wazuri kwa nini hawana mpya kazi ni kuiga wa akina masanja?
suala hapa ni TBC wamefulia ndio maana hawajarenew mkataba ila ipo siku mambo yatajipa na sisis wapenzi wa the original komed tutafurahi.
salamu kwa members wote wa the original komdi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom