Orijino Komedi: Kwa faida ya nani?

The comedy wanahitaji kubadilika. Hivi unajua wameweka show yao moja hapa dar ukiwahitaji uwape millioni SABA za Kitanzania?

Halafu wanakuja kucheza tu nyimbo, Vichekesho vya kuongea labda anaweza Masanja na JOTI. The rest hamna kitu.

Ushauri mzuri ni kuwa waruhusu watu kupeleka vichekesho wakikitoa wanamlipa lets say laki mbili au moja kutokana na maelewano. Hii itawafanya wawe juu tu, general sio wabaya ila shule inawakosesha uwezo wa ku analyze issue zao. Wanahitaji kiongozi ambaye shule anayo.

Huwezi KULA bila KULIWA - JK
 
......... sio wabaya ila shule inawakosesha uwezo wa ku analyze issue zao.

Nyani haoni kundule, walivyokua wanam-dc Kanumba kuhusu english yake utafikiri wao ni wasomi.

Kwanza wananuka rushwa, siku hizi ukitaka kumshambulia mtu maarufu basi wape kitu kidugo wanamtoa kuwa kafulia. Dhambi ya kununuliwa na Manji inaendelea kuwafuata. Nanukuu usemi wa Mwl. Nyerere, ''ukishakula nyama ya mtu huwezi acha''
 
when sugar saturates in solutions don expect utamu kuongezeka. Jamaa hawaja fulia wamefikia kikomo cha kuwaza na kubuni. Niwakatik muafaka sasa kushirikisha wadau wengine wa vichekesho kwenye vipindi vyao ili kuleta ladha mbadala.
 
Vijana wamelewa sifa, siwalaumu sana jamani mnajua kati yao aliejitahidi kusoma alama za nyakati ni Seki (Director wao sijui kapata lini ujuzi huo), jamaa sasa yuko chuo hana muda wa kuwabunia vituko....we unafikiri joti au mpoki atakuja na wazo gani jipya? Nawaonea huruma itakapofika wakati Tido atafumbua macho na kuwatolea uvivu na kusema sasa mwaweza kwenda. Nimetonywa kuwa jamaa siku hizi vipindi vyao ni zima moto yaani kinatengenezwa siku hiyo hiyo.
 
"Vijana wamelewa sifa, siwalaumu sana jamani mnajua kati yao aliejitahidi kusoma alama za nyakati ni Seki (Director wao sijui kapata lini ujuzi huo), jamaa sasa yuko chuo hana muda wa kuwabunia vituko....we unafikiri joti au mpoki atakuja na wazo gani jipya? Nawaonea huruma itakapofika wakati Tido atafumbua macho na kuwatolea uvivu na kusema sasa mwaweza kwenda. Nimetonywa kuwa jamaa siku hizi vipindi vyao ni zima moto yaani kinatengenezwa siku hiyo hiyo."


hapo hapo inatosha.BRAVO
 
Wakuu kwa wanaopenda ze commedy mtakubaliana nami jana Manji alionekana na Mpoki ndani ya Commedy. Mpoki alikuwa anamwezesha Manji pesa ili aisaidie club ya Yanga.
 
Wakuu kwa wanaopenda ze commedy mtakubaliana nami jana Manji alionekana na Mpoki ndani ya Commedy. Mpoki alikuwa anamwezesha Manji pesa ili aisaidie club ya Yanga.

Nilimwona akiomba nauli. Jana walikuwa bize wanawaandama wacheza sinema. Nadhani ile ishu ya Kanumba na kimombo chake. Baadaye niliangalia Futuhi nikafurahi zaidi. Mkuu Futuhi wako juu. Ze Komedy bila Masanja Mkandamizaji imekwisha. Yule ndo staa wao.
 
Nilimwona akiomba nauli. Jana walikuwa bize wanawaandama wacheza sinema. Nadhani ile ishu ya Kanumba na kimombo chake. Baadaye niliangalia Futuhi nikafurahi zaidi. Mkuu Futuhi wako juu. .

Duh Futuhi niliikosa.
Lakini na hao Futuhi mchekeshaji yupo mmoja tu.
 
Duh Futuhi niliikosa.
Lakini na hao Futuhi mchekeshaji yupo mmoja tu.

Inawezekana ikawa kweli, lakini hata asipokuwepo at least bado wenzie watajikongoja. Ila kwa ze komedy: No Masanja No zekomedy.
 
we futuhi wakali sana, niliwaangalia jana wana mada zinazofundisha, Manji nae asipoangalia anafulia muda sio mrefu haiwezekani mtu kama yule awe anaigiza igiza na watoto
 
Nimegundua hapa watu wengi saaaaaaaaana wanawachukia Ze Komedi...sasa sitapata tabu tena..watu wengi ni wanafiki humu, jana nilifanikiwa kuangalia both Ze Komedi na hao Futuhi, ila to be honest Futuhi baaaaaaaado saaaaaaana tena saaaana tu kufikia level za Ze Komedi, labda muendelee kuwapigia debe hivo hivo ndio wataweza kujaribu kuwafikia akina Masanja japo kidoogo....ni hayo tu.
 
Mie futuhi haijawahi kunivutia hata kidogo so hata sidhani kama nilivyoangalia mala ya kwanza nilipata mvuto huwa nacheki kama kuna wenzangu wanacheki laa sivyo bora nijipatie kiusingizi murua

hola fo now
 
we futuhi wakali sana, niliwaangalia jana wana mada zinazofundisha, Manji nae asipoangalia anafulia muda sio mrefu haiwezekani mtu kama yule awe anaigiza igiza na watoto

hivi ukuiwa muigizaji inamaanisha umefulia duuh basi kazi ipo ..
 
Nimegundua hapa watu wengi saaaaaaaaana wanawachukia Ze Komedi...sasa sitapata tabu tena..watu wengi ni wanafiki humu, jana nilifanikiwa kuangalia both Ze Komedi na hao Futuhi, ila to be honest Futuhi baaaaaaaado saaaaaaana tena saaaana tu kufikia level za Ze Komedi, labda muendelee kuwapigia debe hivo hivo ndio wataweza kujaribu kuwafikia akina Masanja japo kidoogo....ni hayo tu.

kabisa mkuu! Futuhihamna kitu kule, tatizo la wale jamaa sio wabunifu hata kidogo, na ndio hapo Watanzania tutakufa na umasikini wetu, ukimuona mtu anauza mihogo anapata chochote na wewe kesho unaanza kuuza mihogo, badala ya kuwa mbunifu labda uuze maji kwa kuwa watu baada ya kula mihogo watakuwa na kiu, unaishia kucopy na kupaste kazi za watu. Hebu mtu aseme ni lipi jipya hawa jamaa wa Futuhi waliloanzisha ambalo halipo kwenye comedy ya kina masanja?
Futuhi baaaaaado kabisaaaaaaaaaaaa.
 
jamaani kwani Manji kuwe po pale kuna ubaya gani ? amekwenda kwenye Tv show tu kwani huko Ulaya na marekani tunako iga sisi hamna watu mashuhuri kama kina manji ? jamaani tuache mambo yetu hayo ya kuona kila kitu chetu kibaya tubadilike na tuungane mokono.:eek:
 
Back
Top Bottom