wawe wazuri ama wabaya, wanakipaji ama hawana......hapa hoja ni moja tu kua umaarufu wao umepungua na hiyo ndio maana yakupoteza mvuto, unapopoteza mvuto hata thamani ya maonesho yako hushuka, na thamani nazungumzia ktk maana ya pesa, sasa kama mapato yameshuka ndo maana twasema wamefulia. na kama wamefulia sasa sababu yaweza kua kuporomoka kiusanii au macho yamezoea,Ninaachoona mimi wale vijana tumewazoea machoni hawana jipya la kutuchekesha, kwa swala kwamba usanii umewapungua si kweli. Huyu ndugu yetu na maosia yake hayasaidii kwa wakati huu, halafu amejuaje hayo yote kama si kumdhihaki mwenzio mashaka matongo ambaye inawezekana hata hicho kipingi hakukiona wala kukisikia popote.
Huyu bwana ana mambo ya kujifanya baba wa taifa kutoa wosia kwa wenzie!
he kweli ni balaa kama si blaaa.
Mara nyingi wengi wetu huvimba kichwa na kujiona tumefika , hali hiyo hutusababishia kiburi, na kiburi huleta dharaau na dharau hupunguza juhudi, na juhudi ikipungua ubunifu hushuka , na kama hakuna ubunifu hiyo sanaa ni mfu, tupa shimoni.
Inawezekana macho na akili zetu zimewazoea, .....lakini mr Been mchekeshaji mwenye vutuko vingi mbona amedumu kwa miaka mingi sana bila kuchuja.....mimi hapo ndo narudi kwenye wazoi moja sanaa yao haina ubunifu mwingi.
Lakini kwanini nahisi umaarufu umewapungua, kwenye maeneo ambayo zamani watu walikua wanajaa kuwatizama hawa vijana siku hizi utakuta watoto wadogo tu, na watu wazima wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, lakini kumbuka miaka miwili iliopita, nani angekua salama kwa kubadili channel wakazi ze Comedy wakiwa kazini , enzi masanja mkandamizaji anakandamiza kisawasawa. kifupi w2amefulia.
Shigongo au yoyote anahaki yakuwashauri hawa vijana, wala hakukosea kuwapa kile ulichoita WOSIA......KWANI KUNA UBAYA GANI. NAONA MAWAZO YAKO YANAJIELEKEZA KWENYE MIPASHO.