Elections 2010 Opposition threatens to boycott 2010 elections

Makame na wenzie wako Dar, Kura zinahesabiwa Katoro wakiwemo mawakala wa vyama, hapo makame etal wanahusika vipi? hata akija Bisimba naye hatakuwepo kwenye kuhesabu wala kujumlisha hizo kura. yatakuwa yale yale. Nadhani sheria za uchaguzi ndizo hasa za kuangaliwa upya.
 
Sio kugomea ruzuku. Wapeleke hoja Bungeni kuifuta sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa. Haitafika hata kesho, CCM itakuwa haipo.
 
Pakacha,
Wapinzani kule DRC walikuwa na malalamiko kama haya katika uchagizi mkuu wa 2006, serikali ikaona hebu imchague mtu ambaye ataaminiwa na wadau wote, akamteua Askofu Apolinary Malumalu kuwa kiongozi wa tume, na wacongo wakafanya angalau kitu kinaitwa uchaguzi,sisemi na tz wafanye kama congo lakini uwepo mchakato wa kuteua tume itakayoridhiwa na vyama vyote na wadau wengine wa uchaguzi, wajumbe wachekechwe na watoke katika makundi ¨"fair" katika jamii,kama taasisi za haki za binaadamu mfano akina mama Kidjo Bisimba, Prof. Haroub Othman etc namna kama hiyo(si lazima wawe hao,lkn wanaweza kuwa kama hao).
Bora ulivyosema kuwa si lazima hao uliowataja katika mfano wako. Kwani nafikiri pia watajitokeza watu kusema kuwa hao hawakipendi Chama fulani na wana msimamo wa kuchukia wadau fulani wa uchaguzi. Hili tatizo nafikiri jibu lake ni kubakia katika misingi mikuu- nayo ni Tume Huru na kufuata sheria za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba. Usihukumu watu kabla ya kufanya kazi yao kwa hisia tu. Hivyo ni sahihi Rais (Siyo Mwenyekiti wa CCM kama unavyotaka tuamini) kwa mujibu wa Katiba kama akiwa ni (institution) kuendelea kuchagua tume, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume hiyo kwa mujibu wa katiba. CUF na Lipumba wao hawana mpya. Wanataka Tume ibadilishwe ili waingizwe Wajumbe ambao tayari wana msimamo wa kulinda na kuyatetea maslahi ya Chama fulani (CUF), Hapo huo Uhuru wa Tume uko wapi. CUF wanatuyumbisha Bwana. Nasikitika kuwa mfano wako wa DRC haukidhi haja hapa. DRC ilikuwa katika crisis. Tz haiko katika mazingira hayo.
 
Hivi walijua lini kuwa hawawezi kushinda uchaguzi? Bora wasiwapotezee wananchi muda bure kama wanajua kuwa NEC inawasaidia CCM. Hizi siasa za pree sonference hazitufikishi popote!

mark my words, watashiriki tena 2010. na wagombea watakuwa wale wale.....
 
Pakacha,
lakini uwepo mchakato wa kuteua tume itakayoridhiwa na vyama vyote na wadau wengine wa uchaguzi, wajumbe wachekechwe na watoke katika makundi ¨"fair"
Naona unajizonga Ndugu yangu. Kama ni ridhaa ni ya wananchi wa Tanzania na siyo ya Vyama vya siasa. Na wananchi wa Tanzania hawawezi wote kukaa kufanya mchakato na kusema wanateua Tume. Hivyo Mwakilishi wao (U-rais) unafanya hivyo. Huo mchakato unaoutaka wewe ni upi? Seif amewakoroga kule Zanzibar. na matokeo yake ZEC siyo ZEC na kamwe haiwezi kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba.
 
Kina freeman wanavyosubiri kuponea misaada ya vyama vya nchi za nje. Wote njaa tuu at the end of the day... Situtaona, na hivyo wanajua wanashindwa.. hizo bilioni 2-3 za misaada itatumika million 600 tuu nchi nzima...lol.. half on it kwenye ka chopper.. Sasahivi nikuongeaza majimbo tuu ya ubunge.. wasigombee urais wala nini.. That will make Kikwete look like a tyrrant kwa wazungu watafanya tuu mabadiliko ya tume.. Lakini NJAA.. ndio maana I cant take any of these fools seriously.
 
Pakacha,
Tume itakayoridhiwa na vyama vya siasa(wafuasi wao ni wananchi) na wadau wengine wa uchaguzi(wataowakilisha makundi mengine ya kijamii), hapa wananchi watakuwa wameshirikishwa. Ninachokusudia hapa ni kuwa kabla ya kuingia katika gemu, washiriki wote wakubaliane mwamuzi yupi ni muafaka ili mwisho wa mchezo pasiwepo malalamiko ya upendeleo.
tusikatae kuwa tokea mfumo wa vyama vngi urejee tume imekuwa ikichangia matatizo mengi yanayoepukika katika kuendesha zoezi la uchaguzi.
 
Pakacha,
Tume itakayoridhiwa na vyama vya siasa(wafuasi wao ni wananchi) na wadau wengine wa uchaguzi(wataowakilisha makundi mengine ya kijamii), hapa wananchi watakuwa wameshirikishwa. Ninachokusudia hapa ni kuwa kabla ya kuingia katika gemu, washiriki wote wakubaliane mwamuzi yupi ni muafaka ili mwisho wa mchezo pasiwepo malalamiko ya upendeleo.
tusikatae kuwa tokea mfumo wa vyama vngi urejee tume imekuwa ikichangia matatizo mengi yanayoepukika katika kuendesha zoezi la uchaguzi.

Ni kweli kabisa hayoyote uliyoyasema. Tume iliona tatizo kwa mfano hili la kununuliwa matandiko wapiga kura wa CCM lililofanywa na CCM. Tume hiyo kwa kuwa ina upendeleo dhahiri kwa CCM ikaangalia upande mwingine huku wakiacha CCM inatembeza rushwa mchana kweupe bila kutoa hata mguno.
 
Waungane basi kwa dhati waache unafiki.undumila kuwili wao ni manufaa kwa mafisadi walio nyuma ya CCM.
 
Back
Top Bottom