Opportunists. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,808
59,358
Ni rahisi sana kwa baadhi ya watu kuwatumia wenzao kupata yale wanayotaka bila kujali hisia za wanaowatumia. Unakuta mtu anamwaminisha mwenzake anampenda kweli ,wengine hufikia hata hatua ya kutangaza ndoa ili kujiweka sawa kiuchumi, kielimu, kijamii, kupata makaratasi na visa kwa wale wanaotaka nafasi za kuishi nje ya nchi, kujiridhisha kimwili n.k. Wakishapata walichokua wanataka haoo wanaondoka zao.

Swali. . . .
Je ukikutuna na mtu ambae. . .
..Amewahi kuolewa kwaajili ya pesa na zilipoisha alimkimbia mwenzake.
..Amewahi kutembea na msichana akakimbia baada ya kumpa mimba.
..Amewahi kuoa/olewa/ishi mtu kwaajili ya makaratasi akamwacha solemba baada kuyapata.
..Amewahi kuvunja ndoa ya mtu mwingine ili amfaidi huyo aliyeoa/olewa mwenyewe.
na mengine kama hayo. . . UTAWEZA KUANZISHA MAHUSIANO NA HUYO MTU BILA KUA NA WASIWASI KWAMBA HATA WEWE UNAWEZA UKAWA SEHEMU YA KUPATA MAHITAJI YAKE NA SIO ANAKUPENDA KWELI?Unaweza ukaamini kwamba hisia zake ni za kweli japo kuna mwenzako aliwahi kuamini hivyo akajikuta ametumiwa na kuachwa solemba?
 
siogopi watu kunitumia ili nipate nachotaka

hata kama aliwatumia wengine, napima kina kama naona nakitosha naingia mzima mzima.
 
Lizzy tatizo ni vigumu kuverrify kuwa alifanya hayo I.e alioa/lewa kwa ajili ya pesa,e.t.c ndio maana people tends to buy stories za oh nilimpenda but hakunipenda, alinitenda blabla nyingine.
 
Absolutely. Ni vigumu kuthibitisha hususan kama unayoyasikia yanatoka kwa watu wengine au hata mtendwa mwenyewe.
 
Ni rahisi sana kwa baadhi ya watu kuwatumia wenzao kupata yale wanayotaka bila kujali hisia za wanaowatumia. Unakuta mtu anamwaminisha mwenzake anampenda kweli ,wengine hufikia hata hatua ya kutangaza ndoa ili kujiweka sawa kiuchumi, kielimu, kijamii, kupata makaratasi na visa kwa wale wanaotaka nafasi za kuishi nje ya nchi, kujiridhisha kimwili n.k. Wakishapata walichokua wanataka haoo wanaondoka zao.

Swali. . . .
Je ukikutuna na mtu ambae. . .
..Amewahi kuolewa kwaajili ya pesa na zilipoisha alimkimbia mwenzake.
..Amewahi kutembea na msichana akakimbia baada ya kumpa mimba.
..Amewahi kuoa/olewa/ishi mtu kwaajili ya makaratasi akamwacha solemba baada kuyapata.
..Amewahi kuvunja ndoa ya mtu mwingine ili amfaidi huyo aliyeoa/olewa mwenyewe.
na mengine kama hayo. . . UTAWEZA KUANZISHA MAHUSIANO NA HUYO MTU BILA KUA NA WASIWASI KWAMBA HATA WEWE UNAWEZA UKAWA SEHEMU YA KUPATA MAHITAJI YAKE NA SIO ANAKUPENDA KWELI?Unaweza ukaamini kwamba hisia zake ni za kweli japo kuna mwenzako aliwahi kuamini hivyo akajikuta ametumiwa na kuachwa solemba?

Lizzzy inategemea hayo mahusiano yako based on what. Kama ni love, umeshasikia sana i believe kuwa love is blind, it does not see, sasa hayo ya past ya hayo mtu utayaona kweli?
 
Lizzy tatizo ni vigumu kuverrify kuwa alifanya hayo I.e alioa/lewa kwa ajili ya pesa,e.t.c ndio maana people tends to buy stories za oh nilimpenda but hakunipenda, alinitenda blabla nyingine.
Kama mwenyewe amejitoa mhanga na kukiri je?
 
Lizzzy inategemea hayo mahusiano yako based on what. Kama ni love, umeshasikia sana i believe kuwa love is blind, it does not see, sasa hayo ya past ya hayo mtu utayaona kweli?
Kupenda hakutakiwi kumfanya mtu mjinga, siku hizi kwa jinsi watu walivyo wasanii ni muhimu kichwa kikahusishwa kwenye maamuzi badala ya kutegemea moyo pekee.
 
Unapompenda mtu, mara nyingi unajitahidi kuvumilia mapungufu yake huku ukijitahidi kumsaidia abadilike. Tena anapokiri mwenyewe ubaya wake na pengine kuahidi kutorudia, inakupa moyo. Nadhani unaweza kumpa nafasi mtu wa namna hiyo. Ila unaingia, mguu nje mguu ndani
 
Yessss. Kisayansi maamuzi yanayohusisha hisia zaidi hayana tija kwa kuwa fikra zinahusika kwa kiwango kidogo sana. Dunia ya leo, akili itumike nyingi kwn maamuzi yote na si kuacha hisia zitawale!
 
..Ktk dunia ya kibepari, kama wewe sio opportunist, lazima utakuwa sucker aka looser ktk kila kitu!
 
siogopi watu kunitumia ili nipate nachotaka

hata kama aliwatumia wengine, napima kina kama naona nakitosha naingia mzima mzima.

Loh umenikumbusha mbali mh. kupima kina muhimu usija ukajikuta umezama nungwi buure.
 
Kumbuka pia Lizzy mara nyingi hadithi tunazopewa ni zilezinazoonyesha Ex alikuwa mbaya,mkorofi na muhusika alionewa na since huwezionana na Ex wake si rahc kupata the other side of the story.
The trust comes naturally I guess!
 
Unapompenda mtu, mara nyingi unajitahidi kuvumilia mapungufu yake huku ukijitahidi kumsaidia abadilike. Tena anapokiri mwenyewe ubaya wake na pengine kuahidi kutorudia, inakupa moyo. Nadhani unaweza kumpa nafasi mtu wa namna hiyo. Ila unaingia, mguu nje mguu ndani
Hivi unaweza ukawa na malengo ya muda mrefu na mtu ambae hujajikabidhi kwake jumla (mguu mmoja ndani mwingine nje)?
 
siogopi watu kunitumia ili nipate nachotaka

hata kama aliwatumia wengine, napima kina kama naona nakitosha naingia mzima mzima.

Sasa kama wewe ndie unaepimiwa hicho unachotaka unakipata vipi?
 
Lizzy, nadhani kila mtu ana degree ya opportunism. Kinacho tutofautisha ni kua wazi about nia zetu tunapoanza uhusiano. Ukimpenda mtu because of his hability of making you happy, there is a dose of selfishness and opportunism right there... if he fails to make you happy you will fly to a better sky.
Kwangu mimi opportunism mbaya ni pale mtu anapo tumia uongo na fake faces kwa kufikia lengo lake. Ila kama tuko wazi toka mwanzo nampa heshima yake tu kama kawaida, na kama opportunity anayo itafuta kwangu itanisaidia na mimi kuendelea mbele, why not?
 
maisha ya mapenzi ni try and erroe hadi upate mnayetoshana.
Na kila shetani na mbuyu wake, waweza tumia watu wengine na ukanaswa na mmoja kiukweli.
Hata opportunist kuna mahali anapenda lkiukweli, labda ndo kanipenda mie. Nampokea tu kwa kweli.

Sasa kama wewe ndie unaepimiwa hicho unachotaka unakipata vipi?
 
....lol....ama sasa mapenzi yamegeuka adhabu....!
mnaogopana kiasi hiki? pendaneni tu bana, yakiisha unabadilisha muziki!
 
Back
Top Bottom