Elections 2015 Operesheni Zinduka: Uamuzi Sahihi 2015

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,483
40,002
NB: Video Inafuata

Operesheni Zinduka imeanza kama nilivyoahidi (jana haikuwezekana kwa sababu moja tu ya heshima ya Mch. Mtikila na haihusiani na mipango ya watu wengine). Nitajitahidi kuwa na onesho hili kila siku (ukiondoa mwisho wa Juma) na nitazungumzia mada mbalimbali. Wiki hii ya kwanza zaidi nitagusia hoja nyingi zilizoibuliwa kutushangaa tunaomkataa Lowassa kama mgombea Urais kwa tiketi ya upinzani.

La pili nitajitahidi hasa wiki ile inayokuja kutoa nafasi kwa wagombea wa CHADEMA kwenye Ubunge (ambao tutaweza kuwafikia) ili wajiuze kwani ninaamini Bunge lenye nguvu lililoundwa na watu waliolelewa na kukomaa katika upinzani na wenye kuelewa hasa ajenda ya upinzani ndio chachu ya kweli ya mabadiliko tuyatakayo. Hivyo, wiki ile inayokuja tutatoa nafasi hii kwa wote tutakaoweza kuwapata.

Tatu, kwa vile nina uhakika wapo wengi ambao hawajakubaliana na uamuzi wangu huu (ambao naamini ni sahihi) basi nitatoa nafasi pia kwa watu wengine kutoa hoja zao dhidi ya ninachosema (sikiliza onesha hili juu ya 'mashart kuzingatiwa'). Kwa barua pepe anuani yangu ipo chini na namna nyingine ya mawasiliano nitawajulisha siku chache zijazo.

Nitajitahidi kuweka shows zote kwenye uzi huu huu kila siku, na video zitafuata chini toka ya zamani zaidi hadi mpya zaidi.

Mwisho, ninaamini na nina uhakika kuwa kwa atakayeamua kunisikiliza kuanzia sasa hadi kuamkia Uchaguzi Mkuu hatoweza kumpigia Lowassa kura ya Urais. Ni kwa sababu hiyo wale ambao tayari wameshaamua kuwa haijalishi nini kitasemwa juu ya Lowassa nawaomba au kuwashauri wasisikilize mada hizi wasije kujikuta wanabadili mawazo. Mada hizi ni kwa wale tu ambao bado hawajaamua au wale ambao wameamua lakini bado wanajikuwa wanavuta na upepo wa 'nyomi' kiasi kwamba bado hawajathibitika katika msimamo wao.

"Uamuzi Makini, Uamuzi wa Lazima, Uamuzi Sahihi"

MMM

ONESHO 1. "Baada ya Kelele Sauti za Hoja Zitashinda"


ONESHO 2. "Makosa 2 ya Dr. Slaa na 1 la Mbowe - Jumatano Oktoba 7, 2015)

<strong>
 
Last edited by a moderator:
Hiki kizazi chenu ni cha ajabu sana. Mimi naita kizazi cha kula kulala na porojo. Mmeacha nchi nzuri ikichezewa na familia chache za watu wa ccm huku mnawapigia makofi miaka nenda rudi. Watu wanataka angalau wavuunje mfumo wa kutafuna nchi. Nyie mnaleta POROJO na UNAFKI ni ajabu, uoga na ujinga. Hiki kizazi chenu mtalaaniwa milele kwa kuonesha udhaifu na unafki.
 
Hivi Mwanakijiji unajifanya unaakili sana kushinda sisi?

Unajiaminisha kabisa kwamba unaweza kubadili fikra za Maelfu na maelfu zinazomuunga mkono Lowassa? Umechelewa sana kaka, kazi hii uliyojitwisha sasa ni ngumu kama kujaza maji kwenye pakacha...... UTATOKA JASHO LA DAMU, MAJI HAYAJAI NG'OOOO!!

Nilijua umejifunza kitu kwa mada zako kinzani kwa wapenda Mabadiriko toka ulupoanza kuandika , kumbe sufuri kabisaaa.!!!

Jiandae kisaikolojia kaka, Lowassa hakwepeki pale Magogoni!!

BACK TANGANYIKA
 
No time to waste ..... nchi inakumbwa na ukame na kuna hitilafu ya chakula katika sehemu kubwa ya nchi ..... wewe unashabikia unafiki na chuki za kisiasa

Njoo kwenye majukwaa on the ground uwaeleze wananchi Wa mijini na vijijini utawafanyia mini ili waondokane na changamoto na ukali Wa maisha

Unless otherwise you are a puppet of all the time
 
Mkuu umesha amua kuua ua tuu, sio eti una ua kidogo ua kabisa usibakishe kitu umeanza kuua raisi ua wabunge mpaka madiwani ingewezekana mpaka wenyekiti wa vitongoji kwa kua unazidi nishawishi kupigia kura ccm kuanzia raisi mpaka diwani nishawishi vizuri mkuu nifanye hivo kazana kwa nguvu....ila cha kushangaza ccm wanasema watashinda kwa kishindo lakini wasiwasi mwingi mpaka inatia wasiwasi......

Mabadiliko lazima.
 
No time to waste ..... nchi inakumbwa na ukame na kuna hitilafu ya chakula katika sehemu kubwa ya nchi ..... wewe unashabikia unafiki na chuki za kisiasa

Njoo kwenye majukwaa on the ground uwaeleze wananchi Wa mijini na vijijini utawafanyia mini ili waondokane na changamoto na ukali Wa maisha

Unless otherwise you are a puppet of all the time

Hahaha mkuu hawezi panda jukwaani huyu anajificha kwenye keyboard
 
MMM nimekusikiliza katika operation zinduka day 1. Kwa leo nilichoambulia ni haya:-

1. Kwa leo naona umejihami zaidi.
2. Inaonekana una hofu kubwa juu ya Lowasa huenda nitajua huko mbeleni katika onyesho lijalo.

Nakuahidi kusikiliza mpaka mwisho lakini mimi kwenye MABADILIKO huniondoe hatanikikesha kukusikiliza.
 
Usiniambie wewe unamjua Lowasa kuliko JK? Wale tunaoamini wanamjua Lowasa wanakuja na hoja mfu ... Sasa, tusimpigie kura Lowasa, unataka tumchague nani? CCM au? Nategemea uniambie nimchague Spunda wa CHAUMA lkn sio Magufuli.
 
wewe ni zuzu huna jipya....
unapanga mambo ya baadye ..kwani wewe ni nani?toa hoja..husomeki!
 
  • Thanks
Reactions: LD
Hahaha mkuu hawezi panda jukwaani huyu anajificha kwenye keyboard

nilidhani atatumia chopa au basi hata Land cruiser kuzunguka angalau mikoa yote ya Tanzania kueneza fitina zake kumbe yupo studio anarekodi operesheni .... this is too low ....

half a hero half a coward is absolutely a coward
 
  • Thanks
Reactions: LD
Back
Top Bottom