Ngoja niongelee mambo machache hapa
1. Mwanakijiji jana alisema kuwa anatafanya tu introduction, na baada ya hapo angekuwa anaenda moja kwa moja kwenye hoja. Lakini cha kushangaza record ya leo kaanza tena na introduction hadi dakika ya 3.45
2. Mwanakijiji anasema kuwa mara tu baada ya uchaguzi uliopita Slaa aliamini yeye atakuwa raisi. Hata hivyo Mwanakijiji hatoi reference yeyote kuwa kwa nini anaamini Slaa aliamini hivyo. Badala yake anakuja kufanya reference kwenye kauli ya Lissu kuwa Slaa alipendekezwa mwezi January mwaka huu awe mgombea. Mwanakijiji anatakiwa atuambie yeye amejuaje kuwa Slaa aliamini yeye ndiye atakuwa mgombea
3. Mwanakijiji anasema kuwa Mbowe alifanya kosa kumpokea Lowassa na kumpa ridhaa ya kugombea. Katika hili Mwanakijiji hasemi kuwa kamati kuu na vikao vingine vya CHADEMA vilikuwa na nafasi katika kumpokea Lowassa na kumpa dhamana ya kugombea
4. Mwanakijiji anachukulia kuwa Lowassa kugombea na CHADEMA ni mabadiliko ya SURA, sio SERA. Lakini Mwanakijiji haongelei sera za CHADEMA zimebadilika vipi. Hatoi hata mfano mmoja wa SERA ya CHADEMA iliyobadilika baada ya kugombea Lowassa na imebadilika vipi.
5. Mwanakijiji anatoa mfano wa maneno ya hamasa ya ..."Lowassaaa... mabadiliko"... kama eti ndio kiashiria cha CHADEMA kumuachia Lowassa taasisi. Nashindwa kumuelewa Mwanakijiji anamaanisha kuwa CHADEMA haikutakiwa kutaja jina la Lowassa kwenye kampeni au vipi!
6. Mwanakijiji anazidi kusema kuwa CHADEMA wamemuachia Lowassa taasisi yote. Hapa nashindwa kumuelewa maana CHADEMA ni chama kinachojiendesha kitaasisi, kikiwa na viongozi, wanachama, katiba, sera na miongozo kama ilivyokuwa jana, juzi, na tangu kilipoanzishwa. Ukiacha dhamana ya kuwa mgombea, sijui Lowassa ana jukumu gazi zaidi jingine kama kiongozi wa CHADEMA
Wakati hayo yakionekena kama baadhi mambo yasieleweka katika hoja za Mwanakijiji, bado tunayo mambo ya kumuuliza mengi tu
1. Jana nilimuuliza MM katika hii operesheni yake anasema "wata....", yupo yeye na nani?
2. MM anaita suala la Lowassa kukaribishwa CDM na kupewa dhamana ya kugombea kuwa ni "kosa", lakini hasemi ni nini hasa kinachomfanya aamini kuwa ni "kosa"... nadhani kwa upeo wake atakuwa na majibu ya maana zaidi ya vihoja vyepesi kuwa "lowassa anatuhumiwa kuwa fisadi"...
Ninachoanza kuona
MM alikuwa na maslahi binafsi na uraisi wa Dr Slaa, na baada ya Dr Slaa kukosa nafasi ya kugombea, MM anajutia kukosa maslahi hayo. Je, MM atuambie aliahidiwa cheo gani Slaa kama angekuwa raisi? Ikumbukwe kuwa katika hii record ya leo MM anakiri kuwa hata yeye aliamini kuwa Slaa ndio atakuwa "mgombea bora". Hi ina maana kuwa hoja sio Lowassa, hoja ni kuwa hakuteuliwa Slaa. Yaani hata ingekuwa ni "Magufuli na UKAWA na Lowassa na CCM, bado MM angepinga, maana kwake yeye hoja ni Slaa...
Uko sahihi Mkuu, huyu MMM anasumbuliwa na bora tukose wote na hakuna lolote la maana.