Litakuwa tukio la kihistoria kwa Jimbo la Arusha na majirani zake , pale siku ya Jumamosi tar 5/5/2012 katika viwanja vya NMC Arusha. Mkutano wenyewe ni kuanzia saa nane mchana, pale ambapo wakazi wa Arusha na majimbo yanayolizunguka watakaposhuhudia watu mashuhuri wakirudisha kadi za CCM na kukabidhiwa Kadi za CHADEMA, yaani kuvua Gamba na kuvaa Gwanda..
Shughuli nzima inategemewa iwe na msisimko mkubwa kwani wanaojivua gamba watakuwa wanaongozwa na Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Ndg James Ole Milya.
Watu wote wapenda mabadiliko wanaalikwa waje kushuhudia tukio hili la Kihistoria katika mji wa Arusha.
Watu kwa mamia wameamua siku hiyo kurudisha kadi za CCM kwa pamoja.