Operation Jicho la Paka na dakika za Mwisho(with Wolf rules )

Mkuu Kudo ni bingwa wa arosto.Sasa hivi nitakuwa naacha hadithi zake ziishi ndio niingie kusoma!
Kuna namba zangu za simu hapo uliwahi kunitafuta walau ujue kwanini sijaposti?!
Nimetoa sababu ya kuwa nilikuwa naumwa na hadi sasa sipo vyema kiqfya bado unataka niingie kila muda kupost ili nikuridhishe wewe?!
Watu wamenipigia hadi simu na baadhi ya wadau walinifikia hospital tukajuana japo walikuja kunisabah bado unataka nipost huku nipo hovyo kimwili? Je ni kweli hujaona sehemu nilipotoa taarifa ya ukimya wangu?!
Aisee
 
Mkuu pole sana kwa kuugua. Pia hongera sana riwaya yako kali kinoma noma. Inatubamba mpaka basi.
 
Oparation Jicho la Paka

Sehemu ya saba
Na Bahati Mwamba

Taarifa hiyo iliibua tafrani ndani ya Kikao kile huku Waziri wa mambo ya ndani Zanzibar akichelea moyoni.
****

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania bwana Mwenda Mpya alichanganyikiwa kwa taarifa ile na alibaki akiwatizama wakuu wa idara za usalama bila kutia neno.
CDF alikuwa haamini macho yake na pia aliona ni kama kudharauliwa kwa kiasi kikubwa na meja jeneral Kambi kibeyo mnadhimu wa jeshi Zanzibar.

“Inawezekanaje hii CDF!” Rais alijikuta akiuliza bila kutaka

“Sielewi mheshimiwa Rais”alijibu CDF.

“Huelewi nini?! Inamaana hadi kikosi cha 309 kinaondoka wewe hujui na kwanini usijue ikiwa wewe ndie final say kwenye Idara yako?!” alihoji kwa ukali Rais Mwenda Mpya.

Mkuu wa majeshi Jeneral Tasi Kinoga hakuwa na la kusema zaidi alijiinamia na kushindwa atoe maamuzi au jibu gani wakati huo.

Ndani ya kikao kile watu wote walikuwa kimya wakijaribu kuwaza hili na lile,wapo waliowaza vyema na wapo waliokuwa wanafurahia mitego yao juu ya Rais wao.

Jeneral Tasi kinoga akanyanyua uso wake na kumtazama Rais kisha akayahamishia macho yake kwa waziri wa mambo ya ndani Zanzibar ndugu makoye kisha akaamua kumuuliza

“Kikao chenu ndo kilimshinikiza Meja jenaral Kambi Kibeyo kuhusu kufanya Operation Jicho la Paka nyingine tena?”

Waziri wa ulinzi na wakuu wengine wa Idara za usalama walitumbua macho baada ya kusikia swali lile lakini kati ya wote ni Rais aliechanganyikiwa zaidi hasa baada ya kusikia jina waliloipa operation hiyo ya kuwakomboa wachezaji wale wa mpira.

“Kwanini mnajiamulia nyinyi wenyewe siku hizi!?”aliuliza Rais ambae muda huo jasho lilikuwa linamtoka mwili mzima.

Waziri wa mambo ya ndani Zanzibar alibabaika kujibu.

SIKU MOJA KABLA

“Haiwezekani tuendelee kungojea tamko la Rais ambae naonekana wazi hahitaji kuwakomboa Wachezaji wetu”aliunguruma kwa jaziba makamu wa Rais Zanzibar Mwinjuma Tariq.

“Lazima tufanye jambo ndani ya siku hizi mbili bila kungojea amri kutoka serikali kuu”alikazia hoja waziri wa mambo ya ndani Zanzibar bwana Makoye.

“Hebu tupe taarifa ya uchunguzi wa mwanzo kuhusu kisiwa cha Kome”aliuliza makamu wa Rais huku akimgeukia mkurugenzi wa usalama kanda ya visiwa vya Zanzibar ambae alikuwa amepewa jukumu la kuhakikisha taarifa zinapatikana haraka kabla hakujapambazuka.

“taarifa za mwanzo zinasema vijana waliondoka wenyewe ndani ya uwanja na ndani ya ndege hakukuwa na abiria mwingine yeyote tofauti na marubani wawili waliokuwa wanaiongoza ndege hiyo”Mkurugenzi mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa alizungumza kisha akatulia na kumeza mate kisha akaendelea

“…kwa makadirio inaonekana ndege hii ilitekwa wakati ikiwa angani lakini swali la msingi ambalo hatujapata jibu lake ni kuwa kama waliondoka peke yao nani alieiteka ndege ile ?! Mwanzo tulidhani yaezekana waasi walitumia ndege nyingine lakini picha za setilite na kumbukumbu za kuongoza ndege zinaonesha hakukua na ndege nyingine kwenye njia iliokuwa inapita Airzanzibar,isipokuwa ilibadilisha uelekeo wa Entebe na kuelekea Kisiwa cha Kome ndani ya dakika kumi tangu itoke katika uwanja wa ndege wa Mwanza,kinachotushangaza ni kuwa ndege ile haikutakiwa kutua mwanza ilitakiwa kuendelea na safari hadi Entebe.uongozi wa uwanja wa Mwanza wanadai ilitua kwa dharura baada ya rubani kuhisi kuna kunguru aliejigonga kwenye bawa moja la ndege na walipoikagua hawakukuta hitilafu wakairuhusu iondoke.
Baada ya kutekwa ilibidi tuwasiliane na majasusi wetu walioko kule Uganda wametupa ramani nzima ya kisiwa kile na hadi ilipo hiyo ngome ya waasi wa LRA na hata uelekeo wa simu inayopigwa na kiongozi wao Mangazeni Nkunda imesaidia sisi kupata picha za eneo la ngome yao”alimaliza kueleza mkurugenzi wa usalama wa Taifa Zanzibar.

Meja jeneral Kambi Kibeyo alikuwa amekaa kimya muda wote akiwasikiliza mara akasikia akitajwa na makamu wa Rais Mwinjuma Tariq

“Meja inabidi uandae kikosi kizuri cha makomando na hadi kufikia kesho tujue hatima ya vijana wetu”

“Maagizo hayatolewi na kutekelezwa vile unavyodhani mheshimwa makamu jeshi linautaratibu wake na mambo Kama haya lazima yaamuliwe na serikali kuu na Kama unavyojua rais wa jamhuri hajataka sisi kutumia nguvu anataka tutumie demokrasia ya maelewano na isimwagike damu.”alimaliza kufafanua vyema meja jeneral Kambi.

“Tatizo nyinyi wabara mnayadharau maamuzi yetu, hivi tutawangojea hadi lini hao unaowaita wa serikali kuu? Lazima tufanye maamuzi na sisi tuna jeshi na linajitosheleza”alizungumza kwa jaziba waziri Makoye.

“Lazima tufanye kitu meja na mimi nasaini faili hili lenye kukutaka uteuee kikosi cha nguvu kiwakomboe vijana ifikapo usiku wa kesho kinyume na hapo utakuwa unagomea maamuzi ya jamhuri”alimaliza kusema makamu wa rais huku akisaini faili la kuruhusu operation hiyo kufanyika na aligonga muhuri kisha akawapa wahudhuriaji wote wa kikao hicho wasaini.

Walisaini wote ila meja jeneral akastuka baada ya kuona jina la faili lile na operation ilivyokuwa imewekwa katika maandishi makubwa “OPERATION JICHO LA PAKA”alamu ya tahadhari ikalia kichwani pake na hapo akakumbuka miaka zaidi ya Tisa nyuma paliwahi kutumika jina hilo katika mpango fulani uliozaa taharuki kwenye nchi na sasa anakutana na jina Kama hilo akajua kuna namna ila hakuwa na budi kusaini kisha kwenda kutekeleza jambo hilo na kuacha faili lile lihifadhiwe kama classified.

Meja jeneral alipotoka kwenye kikao kile akaamua kumpigia simu Jeneral Tasi kinoga na kusema nae mambo machache tu

“Ya mwaka 97 yanajirudia tena ila kwa tofauti Jeneral,nchi inaserikali mbili bila serikali kuu kuwa na taarifa”alipomaliza kusema hakutaka kusikia mkuu wake atajibu nini yeye akaamua kukata simu na kisha akaanza safari ya kwenda kukipanga kikosi kazi kikosi namba 309 unit au Gost Recon Alpha.
*****

Ikulu usiku

“zuieni operation hiyo na vijana warudi huku mara moja”alizungumza rais

Haraka Jeneral akapiga simu kwenda kwa Meja jeneral lakini simu ikawa inaita tu bila kupokelewa na baada ya dakika mbili simu ya Jeneral ikaita na alipoishusha chini hakuwa na cha kusema mbele ya kikao kile na hata ulimi wake ukawa mzito akabaki kujisemea mwenyewe tu
“Haiwezekani hii..”
Maneno yale yalisikiwa na kila mtu ndani ya chumba kile cha mikutano na hakuna aliemsemesha kila mtu akabaki akimshangaa vile alivyozubaa na kupigwa na mshangao.

Lakini hatimae akaipata kauli

“Meja jeneral Kambi Kibeyo amejiua kwa sumu usiku huu”

Kila mtu hakuamini si rais tu hata IGP alishangaa DG alishangaa pia waziri wa ulinzi yeye alianza na kulia kabisa maana meja alikuwa ni kama kaka yake waliezoeana sana.

Rais akakuna kichwa na kumtazama waziri wa mambo ya ndani Zanzibar kisha hakusema neno akaomba kikao kiishe na kesho alimtaka CDF akutane nae wajadiri upya suala hilo lakini hawakujua kuchanganyikiwa kwao na kuahirisha kikao ilikuwa ni pigo jingine ndani ya idara ya jeshi la kujenga taifa na taifa kiujumla.

Hawakujua!!!

Itaendelea
Nzuriii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuimalizia kufikia hapa ni sh ngapi kamanda? Nambie nichangie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom