wataongea sana lakini boss wao android..... hata idadi ya watu wanaotumia tu ni evidence tosha inavopendwa na wengi...
akifuatiwa na iOS... windows hana apps afu chache alizonazo za kikuda OS kimeo tu hiyo..
apps zipo chache sawa ila ukisema za kikuda hapana nakataa windows phone sasa hivi imeishaipita android kwenye enterprise market ipo nafasi ya tatu nyuma ya kinara blackberry akija ios wa tatu wp na mwisho android. by 2015 muda kama huu trend ikiendelea wp atakuwa wakwanza kwenye enterprises. ngoja nikuioneshe maeneo ambayo toka wp8.1 imetoka wp tayari amemuacha android nakupa personal experience tu.
1.os ya kwanza kuwa na file manager baada ya symbian
kabla ya hapo ilikua wp inachekwa kwa kutokua na file manager lakini watu wa android wakasahau kuwa wao pia hawana official file manager, android inatumia third party file manager tu ambazo hazina uhakika wala hatujui data zetu zinapelekwa wap. kwenye wp microsoft ametoa official file manager ili uweze kumanage mafile in simple way
2.video editors
nimekuwa nikitafuta video editors kwa muda mrefu sana kwenye android nikaambulia moja tu kinemaster pro ambayo nayo video ya dakika 3 inachukua hadi nusu saa kurender tu. cha kushangaza kutoka tu kwa wp8.1 kumekuja video editors za kumwaga kwenye wp zenye features sawa na movie maker ya pc ambazo zinatosha kabisa kwa mtu wa kawaida kama mimi kutengeneza movee na kuedit video zangu
3.camera experience
tukiachana na hardware ambazo si part ya os ukija kwenye app za camera hakuna kinachoifikia wp, siongelei mambo ya camera 360 na app za kitoto i mean real proffesional issues. kwenye wp unaweza kupata raw images kwa ajili ya photoshop kwa android huwezi na bila raw images huwezi kuwa proffesional wa camera so android ni useless kwenye camera. pia kwenye wp kuna app kama nokia camera ambayo imeshinda award ya app bora ya mwaka 2013 kwenye site nyingi ikiwemo phonearena na wpcentral, kuna cinemagraph na nyenginezo.
4.office apps
ukiwa na windows phone unapata app kibao za kiofisi kama ms word, excel na power point, kuna best note taking apps kama one note. utaweza kusync vitu vya kiofisi kutoka simu kwenda computer na hutopoteza compability sababu app ni zile zile
5.universal app
kwenye wp sasa hivi unaweza tumia app moja na mtu wa pc mfano wake ni hii microsoft office mpya inayokuja itakua version moja kwa simu na pc na tablet
6.best navigation ever
why apps za wp za navigation ni best?
1.unaweza download ukatumia offline wakati kwenye android hadi uwe na net na kama utapata za offline basi data zake wananunua kwa nokia
2.zinakuambia mahali ulipopaki gari yako
3. zinakuambia kuhusu foleni (baadhi ya nchi)
4. nk
7.nokia exclusive apps
nokia wana apps kibao za wp ambazo huwezi kuzipata sehemu nyengine mfano moja wapo mpya ni hii nokia beamer ambayo una mirror kioo chako kwa mtu mwengine. mfano hujui kupunguza mwanga kwenye simu basi unadownload nokia beamer then kila ninachokifanya kwenye simu yangu wewe utakiona kwenye kioo chako hivyo nitaweza kukufundisha kirahisi, nokia wana photo editor inaitwa studio, wana photo beamer, kuna video trimer ya ku upload video youtube kuna app zaidi ya 50 za nokia na zote ni amazing apps.
8.microsoft games
moja kati ya tofauti ya google na microsoft ni kutengeneza magame, japo android ina magame mengi ila wp ina magame bora ya microsoft kama vile solitaire, mahjong, halo na skull os shougan. ni game moja tu ninalolijua ambalo lipo android nalo ni wordament.
kama wewe ni mpenz wa turn based games sijaona game zuri kama hili kwenye simu skull of shougan
wale wa halo