Karibu sana waballa na ipo degree ya IT
Mlitangaza kuanza kutoa degree za data management alafu mkahairisha kihuni.....huu ni ukurupukaji.....nilimlipia dogo application fees then ikageuka hadithi za alinacha hadi kesho......acheni kutangaza course huku hamjajipanga.....huu ni wizi wa kishamba kwa chuo kikubwa kama OUT.....
Karibu sana waballa na ipo degree ya IT
Kwa degree ya education ada bei gani?
Samahani naomba niingilie hapa, hii degree ulihakikisha inatolewa au ulisikia kwa watu?? Uliiona kwenye documents za chuo especially msahafu wake (Prospectus)? Hii case inafanana na case ingine mtu kaambiwa kuna degree fulani inatolewa ila kwenye application form haipo so omba kwa kuapply Degree ya Sanaa (BA.General) then baadae utahamia hiyo kozi.
Mwisho wa siku amechaguliwa BA.Gen huku registration anadai anasoma kitu kingine, anaulizwa umepata maelekezo wapi anasema kwa mwenzie then OUT analalamika wababaishaji!! Hebu kuwa specific mkuu
Ada pale bei ni maelewano, chuo cha Gavoo hicho kaka.hawana shida saana.
Mkuu, hebu nifafanulie hapa ada bado ni 60,000 kwa somo? au washabadilisha.nime-google hata siion fee stracture ya out. pia kunaidadi ya unit ambazo ni lazima kuzichukua kwa semister? pia BACHELOR OF COMMUNITY ECONOMIC DEVELOPMENT ninaweza kuisoma kwa miaka mingapi?Hivi kuna chuo chenye gharama za maelewano kweli? Unaijua OUT au ndo wale wale?
mwalimumzalendo1 adani shs 60,000/ kwa unit. So ada ya mwaka inategemea na idadi ya unit ulizo opt kuchukua katika mwaka husika. Mfano umechukulia units jumla 12 ni 60,000/ x 12 = 720,000/ pia pana vigharama vingine vidogo vidogo.
Hicho cha mwanafunzi kuweza kuchagua idadi ya kozi nadhani ndicho kilichomfanya huyo jamaa hapo juu aseme ada ni maelewano