Open-space Jangwani: Kikwete adanganywa tena!?

Open-space Jangwani: Kikwete adanganywa tena!?

Nadhani Uwezo Tunao kapotea njia. Turudi kwenye mada.

Kikwete anatafuta sifa bila kutumia akili. Kuwapa mawaziri maelekezo ya kazi kupitia vyombo vya habari ni dalili kuu ya rais asiyejua kazi yake

Alipopita jangwani na kuona uzio wa mabati kwanini hakumpigia simu waziri na kumuuliza? Kwanini hakumtumia waziri huo ujumbe ili atekeleze mara moja?

Pia hiyo staili yake ya kuendesha nchi inatokana na kushindwa kwake kuweka na kusimamia mifumo ya utawala wa haki na sheria katika ngazi zote. Hivi ni hadi yeye akiona kosa ndipo alalamike kupitia vyombo vya habari ndipo litatuliwe? Anapita kila kona ya nchi hii? Wananchi wote wanaodhulumiwa haki zao wanaweza kumfikia ili aagize wasaidiwe?


Very well said. Kikwete is plainly beyond stupidity.
 
KATIKA HILI ZITTO KABWE YUKO SAHIHI KABISA NA KWAMBA BAADA YA OFISI YA SPIKA KUWAGAWIA WABUNGE NAKALA YA MUSWADA WA MOI SASA KILA MBUNGE ARUDI JIMBONI TUKASHAURIANE KWANZA TENA BILA KUKOSA!!!!

Katika hili mchangon wa Mheshimiwa Zitto IKO SAHIHI KABISA.

Kiukweli nawaasa Wapiganaji, tusiwe wanafiki kwamba kama hatukubaliani na Zitto juu ya mambo kaadha, sawa na mimi nisivyokubaliana naye juu ya mambo mengi, basi hata pale anapotetea msingi unaokubaliana na matakwa yetu kama Umma wa Tanzania (na wala si kutetea msingi wa mafisadi) basi sisi ni kukimbilia tu KUMWAGA MAJI NJE PAMOJA NA MTOTO NDANI YA BESENI.

Kimsingi kabisa, ni kwamba mara baada ya ofisi ya bunge kuwagawia kila mbunge nakala ya mswada wa CCM basi sasa ni muda muafaka kwa KILA MBUNGE KURUDI JIMBONI KWAKE KWENDA KUSHAURIANA NA MABOSI WA (Sisi Wapiga Kura) juu ya aina ya muswada uliowashilishwa bungeni, maana na mantiki yake, kwa kiasi gani inavyowakilisha maoni yetu.

Tena ni kwamba hadi hapo sasa SISI KAMA WAPIGA KURA TUNAMPA MHESHIMIWA MBUNGE WETU UJUMBE GANI WA KWENDA KUCHANGIA KULE bungeni pindi mjadala utakapoanza; yaani ni kwamba tutakuwa tunamwelekeza mbunge wetu juu ya kitu gani akiunge mkono, kipi kirekebishwe vipi na mambo yapi akayakatae moja kwa moja.

Hakika alichokisema Mhe Zitto endapo haitozingatiwa na Wabunge kudiriki kushiriki mjadala wa HUU MUSWADA BATILI WA CCM bila kwanza kuomba maelekezo ya wapiga kura basi mjue ya kwamba WABUNGE WENGI SANA WATAKAOPINGANA NA UMMA basi ni dhahiri kwamba kibarua chao kitaota mbawa.

Huu mswada, kwa watu makini na wadadisi wa mambo watagundua kwa AG Werema kaudesa kutoka kwa MUSWADA WA MOI WA KENYA enzi hizo alipojitia kicha ngumu kukubali wananchi wake kujiundia katiba mpya. Leo hii Moi hayupo madarakani huko lakini wananchi wapo wamejaa tele na KATIBA MPYA kabisa kutokana na wananchi moja kwa moja sasa hivi inafanya kazi.

Jamani huu mswada wa Moi ambayo hivi sasa Kikwete Kaudesa nukta kwa nukta isipokua kafanya tu kazi ya kuingiza 'Unite Republic of Tanzania' kila mahali kwenye ile nafasi iliyoandikwa Republi of Kenya, hata kule kwa Kibaki alikoidesea Kikwete nako pia iliwahi kukataliwa na kutupiliwa mbali na kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya sheria na katiba na AG kulazimishwa kushauriana kwanza na wadau wote na kuingiza mapendekezo yao moja kwa moja ndani ya muswada ndio mambo yaendelee kwenye sakafu la bunge.

Na hiyo ndio siri kwa nini huo mswada muhimu sana kwa kila raia haukuandikwa kwa lugha yetu ya Kiswahili. Maswali zaidi muulizeni Msekwa aliyeenda huko majuzi kuchukua zaidi ya MOI'S UNPOPULAR FILE ON CONSTITUTION ili waje kuvijaribishia kwetu kama tutakubali.

Tumsikilize Zitto katika hili na hatua ya kufuatia ya maandamano nchi nzima kupinga huu mswada dhalimu ni kwamba maelekezo tutapeana kwa wakati na mtindo stahiki endapo kweli serikali haitoingiza maoni ya Wadau wa katiba kwenye huo muswada.

Aluta Continua!! Vijana kote nchini tukae tayari mkao wa kulikomboa taifa letu, ONCE AND FOR ALL, kutoka mikononi mwa MAFISADI endapo maslahi yao ndio itakayoonekana wa muhimu zaidi hapa!!!!!!!!!!!!

Naona safari ya kamba kukatikia pabovu, baada ya kuibiwa sana kura zetu, kudhalilishwa sana kimaisha na MAFISADI, baada ya kulaghaiwa sana na na vingozi wa CCM, ndio huu!!!!!!

Oya mbona heading na uliyoyaandika hapa ni tofauti. unatuchanganya. au wewe mgeni humu jf?
 
attachment.php


This isit people

duuh!!!!!!!! hii nimeipenda
 
JK ana interst gani na mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi? Kwanza kamzuia Magufuli na ubomoaji wa pale Urafiki ambapo ni moja wapo wa njia hizo sasa hili la kituo cha mabasi hayohayo?
 
Kikwete ni kichwa cha mwendawazimu, kila mtu anadanganya, anatukana, anaimuibia etc yeye peace tu........... Raisi tunaye mbona........
 
MODS hawa wanaovuruga mada mu-delete post zao ili tuendelee kujadili mada husika.

Kwa kweli JK amechemka sana ni kama mfalme JUHA
 
Rais JK, inavyoonekana ni kama kadanganywa issue ya ujenzi jangwani, ambapo jana aliagiza ujenzi usimamishwe mara moja na kubomolewa... Leo ITV habari saa mbili usiku. Mafundi na wachina wanasema wanaendelea na ujenzi kituo cha mabus ya kwenda kasi, vituko tupu mwandishi ITV anashanga, nami nashanga ilikuwaje rais kasema pabomolewe aliakuwa ni kituo cha mabus kasi?

Raisi yuko sawa na wala hajdanganywa. Alipotembelea Wizara ya Ujenzi aliuliza hilo la kweka kituo kwenye viwanja vya michezo, Waziri na watendaji wake wakajiumauma.
 
Huyo Rais nadhani atavunja rekodi ya kudanganywa....ninahofia siku moja atashikwa mateka! ! !
 
Mimi nimeshachoka kum-discuss huyu jamaa, kwa sababu kila kukicha kuna kituko kipya, mimi naona ni afadhali angeendelea na safari zake za majuu kuliko kufuata ushauri wa waliomdanganya kwamba akianza ziara za ndani ataonekana ana deliver, nimeona hiyo habari nimeshangaa sana, hivikwa nini anakurupuka? halafu sijawahi kusikia rais amemuwajibisha yeyote kati ya washauri wake, yaani leo rais anasema mahali hapa pabaki wazi, kesho yake mchina anaendelea na kazi tena bila wasiwasi, kuna rais hapo,

Sitaki kusema awe mbabe lakini apunguze mambo ya kujichanganya yanazidi kuondoa heshima yake kidogo iliyobaki.
 
Nadhani hakudanganywa kwani hakuuliza kwa watendaji wake! Yeye amekurupuka tu kama kawaida yake labda alitaka kudondoka ndo akaropoka PAVUNJWE HAPA! Sasa hatujui itasimama amri ya kuvunja au ya kujenge njia ya mabasi yaendayo kasi Yetu macho!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tunapowaambia RAIS wenu mgonjwa mnauliza anaumwa nini?

Naomba kuuliza hivi hata akiwa mwanachama mwaminifu wa mirembe anaendelea kuwa kazini mpaka kifo kitutenge naye kama katika ndoa? Ama kweli nchi tunayo jamani yaani hakuna kitu cha raha kama kuwa mkulu wa TZ maana unalindwa na nchi bado inaendelea hata kwa auto pilot hii system aliyoisuka baba wa nyumba ni ukuta wa zege na ukiingia hata kama zimehamia mirembe hakuna atakayekugusa teh teh!
 
Raisi yuko sawa na wala hajdanganywa. Alipotembelea Wizara ya Ujenzi aliuliza hilo la kweka kituo kwenye viwanja vya michezo, Waziri na watendaji wake wakajiumauma.

Kujiumauma si ndio kudanganya kwenyewe?
 
Mimi nimeshachoka kum-discuss huyu jamaa, kwa sababu kila kukicha kuna kituko kipya, mimi naona ni afadhali angeendelea na safari zake za majuu kuliko kufuata ushauri wa waliomdanganya kwamba akianza ziara za ndani ataonekana ana deliver, nimeona hiyo habari nimeshangaa sana, hivikwa nini anakurupuka? halafu sijawahi kusikia rais amemuwajibisha yeyote kati ya washauri wake, yaani leo rais anasema mahali hapa pabaki wazi, kesho yake mchina anaendelea na kazi tena bila wasiwasi, kuna rais hapo,

Sitaki kusema awe mbabe lakini apunguze mambo ya kujichanganya yanazidi kuondoa heshima yake kidogo iliyobaki.

Naunga mkono hoja - aende zake nje kwenye vi-mikutano vya NGOs fake. Nchi ibaki kwenye 'auto president'!
 
nafkiri kikwete alikgundua baadaye kachemka .. huweazi ukasimamisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendya kwa kasi (kama ni kweli) ili eneo libaki wazi kuchezea watoto.. alikuwa anatupeleka mbele kuturudisha nyuma..?!
 
Back
Top Bottom