Ooooh yeah!

Ooooh yeah!

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,419
Reaction score
18,373
Dokta yuko na walevi anawapa
ushauri kuhusu afya zao: Jamani
hivi mnajua kwamba pombe inaua
polepole? Mlevi mmoja akaibuka
akamjibu: We dokta vipi? Kwani
nani kakwambia sisi tuna haraka?
 
Juma kaagizwa na mwalimu
atunge sentensi akitumia neno
'MIWANI'

Juma: mwalimu hii 'miwa ni' tamu
 
Zuzu kanunua gazeti alipofika
nyumbani tu
akaliweka ndani ya friji, Mama
yake alipomuona
akashangaa akamuuliza "mbona
umeweka gazeti
ndani ya friji?" Zuzu akajibu
"wameandika lina habari
motomoto acha zipoe
kiasi ndo nisome."
 
DOGO: Baba kwani mimi
nimetoka wapi?
BABA: Dah mwanangu
mbona unaniuliza swali
gumu hivyo? Nwei
hebu kaa hapo
nikuhadithie.
Mimi nilikutana na mama
yako siku moja wakati
anatoka kazini, tulikutana
kituo cha basi, mvua
kubwa ikaanza ikalazimika
tuchelewe sana
kupanda basi, hivyo
tukazoeana sana. Baada ya
kama miezi mitatu
tukaona ni vema tuoane,
tukawaeleza wazazi wetu
wakatukubali, harusi
ikafanyika, tena kubwa
sana, tukaanza kuishi
pamoja na kwa kifupi ndio
wewe ukapatikana.
Ukikua kidogo utanielewa
nina maana gani
DOGO: Haya, ila mwalimu
atanipiga
nisipomwambia kesho,
katuambia wote tuwaulize
wazazi wetu tumetoka
wapi. Mwalimu wetu
kasema
yeye ametoka Arusha
 
Back
Top Bottom