ONYO: Msizuzuke na wingi wa watu majukwaami

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
865

Wadau Hali zenu:

Napenda kuwazindua kwamba msizuzuke na uwingi wa watu majukwaani. Hii ni kwasababu Watanzania hawana kazi za kufanya, wengi wao hutumia mikusanyiko kama sehemu ya kujifariji na kujichanganya. Sio kama wanaokuja kwenye mikutano ya siasa kwamba ni wapigakura au washabiki wa mgombea fulani, la hasha, kuna kundi kubwa ambalo halina msimamo wowote ule. Akisikia Magufuli atakuja, akija Zitto atakuja, akija Slaa atakuja, na wengineo.

Kama ukitaka kujua, wewe toka nje ya nyumba yako na mke wako anzeni ugomvi fake tu, au wakemee watoto wako live watajaa Wabongo kibao.

Natamani Watanzania tungekuwa na aina ya tafiti ambazo zitatoa tathmini ya watu hawa ambao huenda ni wengi kuliko wanasiasa. Kuna watu Bongo wanapiga kura kimaslahi. Mfano anajua kama CCM itaendelea kuwepo basi baba yake ambaye ni mteuliwa sehemu fulani ataendelea kuleta riziki nyumbani. Hawa watu hawana sera. Pia wapo ambao dili zimeshindikana kwa kuwa CCM wanambania. Hawa hata Magufuli nani aseme nini lazima watapigia against.

So please tunapopiga kampeni, tusisahau or kutosheka kwakuwa watu wanafurika. Mrema alisukumwa mara kadhaa akaishia chaka...

Msijesema sijawatahadharisha!!
Mandokwa me.
 
Unachokisema ni sahihi, haohao ndio walikuwa hapa
 
Last edited by a moderator:
Yani mkuu umeongea kina point kinooma...yaani naunga mkono maneno yako kwa %100..ni kweli kabisa kabisa, Bongo watu hawajali sijui nani au nani, watu wapo kimaslahi zaidi,mimi mwenyewe nina kadi ya CCM coz kuna dili moja nataka kucheza kipindi hiki cha uchaguzi but siko interested in CCM... Wabongo wengi hawana kazi za kufanya ..we utakuta watu barabarani wanaangalia TV,,
 
Na hili la Watanzania wengi kukosa kazi ni kutokana na mipango mibovu ya serikali ya ccm ambayo toka uhuru haina mipango ya muda mrefu na mfupi wa ajira kwa wananchi. Badala yake wako busy kuwatafutia watoto mali na wawekezaji wa kuwalipa 10% kwa ajili ya maisha mazuri ya familia zao.

Wamebaki tu kupiga kelele tu Watanzania msiichezee amani, kumbe wanajua amani ikitoweka hata mali za watoto wao hazitakuwa salama, tutaanza upya wote.
 
Tunataka mabadiiko ila wapinzani hawana hotuba kama za Mtikila zinazoenda moyoni, wao hutuba zao kama za CCM, zinaenda kichwani halafu tunasahau waliongea nini kwenye kampeni
 
Alafu itabidi muwaombe watanzania msamaha kwa kuwatukana na kuwaita mamluki...nani apige kura sasa kama wasipokusanyika??? Au kwasababu una uhakika na goli la mkono????
 
CCM wakitaka kufanya mikutano wanatafuta mercenaries ili mkutano uonekane umejaza. Chadema watu wanajaa bila kuitwa. Watu wengi wanajiandikisha kupiga kura majina yao hayaonekani (uchaguzi 2010) na sasa BVR inawekewa mizengwe...

Uliyeleta mada hujatafiti kwa kina. Wingi wa watu kwenye mikutano ya siasa (na si majukwaani) wapo aina mbili: Wale genuine supporters for change na wengine bendera fuata upepo (washabikiao CCM bila kuwa na faida nayo, mleta mada akiwemo.

 
Duuuu, kweli huyu jamaa ana mahaba niue kwa CCM, yaani tangu Magufuli kaanza kuzunguka hakuona kama Watanzania hawana kazi, leo peoplez wameamsha popo kidogo tu ameibuka. Sasa kwa taarifa yako, hiyo ni peoplez peke yake bado UKAWA, tuliaaa dawa ikuingie na acha kutukana Watanzania kuwa hawana kazi za kufanya, kwani hawajawahi kuja kwako wakuomba hata mia.

Kama hawana kazi za kufanya mbona hawajafa njaa, au uliisha wahi kumnunulia hata nguo mmoja wapo? Acha dharau, Chadema wanamaanisha, sio kama CCM, usipoyapa rushwa yanakugeuka. Huku tuna Mungu na rushwa huwa tunaisikia huko CCM tu, tena uache dharau kuwaita watu hawana kazi, nakuheshimu sana usirudie tena na hizo kauli zako.
 
Watu wengine bwana!!! Cdm wakiwa na mkutano usipofurika watu "Cdm imekosa mvuto", watu wakifurika "Hawakua na kazi zakufanya" Jamani!!! mbona onyo hili ni baada ya Cdm kufanya mkutano wa kihistoria Mwanza? Watanzania wa leo sio wa jana.. Wanajitambua na haohao WAPINZANI ndio wamewafungua macho, kupitia MIKUTANO na BUNGE...

Nimefuatilia mkutano leo! Hata sura za wananchi zinaonesha ziko pamoja na wanachokisema viongozi wa CDM... Penye ukweli tukubali tuu... CHADEMA Mwanza mmeonesha umwamba wenu leo... Hongera sana.
 
Mbona haukuyaandika haya tangu Magufuli alivyoanza ziara zake za kampeni? Inakuwaje Leo, nini kimekusibu?

Hayo yameandikwa sana humu JF wala hayajaanza kwa Magufuli, nakukumbusha tu wakati Zitto na ACT wanafanya mikutano yao na kupata wingi wa watu BAVICHA mlikuwa mnachonga sana...usijifanye umesahau!
 
Wewe waache watu waendelee kubweteka. Wajanja tunalijua hilo na kwa bahati mbaya hawajifunzi. Majuzi tu hapa kuna watu walitumia helikopta 3 kule kalenga na watu wakajaa sana lakini hawakujua kuwa walikuwa wanakuja kushangaa chopa, kwenye uchaguzi wakapata 20% tu pamoja na nyomi nyote waliokuwa wanaiona.
 
Watu wengine bwana!!! Cdm wakiwa na mkutano usipofurika watu "Cdm imekosa mvuto", watu wakifurika "Hawakua na kazi zakufanya" Jamani!!! mbona onyo hili ni baada ya Cdm kufanya mkutano wa kihistoria Mwanza? Watanzania wa leo sio wa jana.. Wanajitambua na haohao WAPINZANI ndio wamewafungua macho, kupitia MIKUTANO na BUNGE...

Nimefuatilia mkutano leo! Hata sura za wananchi zinaonesha ziko pamoja na wanachokisema viongozi wa CDM... Penye ukweli tukubali tuu... CHADEMA Mwanza mmeonesha umwamba wenu leo... Hongera sana.

Mpe maneno kamanda naona huyu jamaa ni Gamba!
 
Back
Top Bottom