Ongeza ufanisi wa engine yako ya 1Hz ktk landcruiser 70 series kwa kuweka turbo na intercooler

Modification=TURBO na INTERCOOLER kwa 1HZ.

FAIDA MBILI KUU ZA TURBO

1. Kuongeza nguvu ya engine

-Turbo huongeza msukumo wa hewa safi kuingia katika engine na hivyo kupelekea uchomaji wa haraka wa mafuta kisha kuiongezea engine uwezo wa kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi,hapo ni katika kurahisisha kufikia RPM za juu kwa muda mfupi. Hivyo basi utaweza kupata acceleration kubwa.(Work÷Time=Power)

2. Kupunguza ulaji wa mafuta

-Turbo husaidia kupunguza ulaji wa mafuta kutokana na nguvu ya ziada inayoipa engine,hivyo basi uzito wa gari kwa engine kupungua kwa kiasi kikubwa(power to weight ratio)

Turbo pekeyake haitoshi kukupa matokeo yaliyolengwa na teknolojia,hivyo basi husaidiana na INTERCOOLER, kifaa ambacho kazi yake ni;
1. Kupoza hewa iliyopata joto kwenye njia za turbo.
2. Kusaidia kuongeza uzito(density) wa hewa itokayo kwenye turbo.
3. Kuchangia kiasi kikubwa cha ongezeko la nguvu na kupunguza ulaji wa mafuta Kutokana na kwamba hewa ya baridi huwa na kiasi kikubwa cha chembe za oxygen,hivyo basi itakamilisha uchomaji kirahisi(Ifahamike pia oxygen ni hewa kuu chochezi katika vyanzo vingi zaidi vya moto).
.
TAHADHARI: ENDESHA GARI KWA KUZINGATIA TARATIBU ZOTE ZA USALAMA BARABARANI,JAMII INAKUHITAJI KATIKA UBORA WAKO.

USIJARIBU KUFANYA ZOEZI HILI MWENYEWE BILA MAARIFA YA KITAALAMU,HASARA INAYOWEZA KUKUPATA ITAKUPA MAJUTO.

Wasiliana nasi tukuhudumie kwa simu namba: 0626409908

#teamcruiser
#teamcruisermechanics
#landcruiser70series
#1hzturbointercooler
Tyubo
 
Umeongelea faida zake tu , hujataja hasara zake
1hz imetengenezwa kwa ajili ya natural aspiration , kuongeza turbo utaongeza stress amabazo hazikufanyiwa mahesabu na mjapan , main ,con bearing , thrust washels zitachoka mapema , tegemea kufanya overhaul hii engine mara kwa mara kuliko kawaida yake

Pili fuel consumption itategemea aina ya kazi na terrain unazokwenda , if you are running light , flat urban cruiser , huna haja ya kuhangaika na modifications kama hiyo.
Tatu tegemea heat damage hata kama ukibadilisha radiator , especially when you are asking for more power from that modified engine , kwa sababu ya haikuwa designed ku run on heavy combustion ratios.

Sina maana ya kupinga ulichosema , ni kitu kizuri tu , ila at least watu wajue madhara yale pia
Take a Sip of your fav and i will pay forit
 
Modification=TURBO na INTERCOOLER kwa 1HZ.

FAIDA MBILI KUU ZA TURBO

1. Kuongeza nguvu ya engine
-Turbo huongeza msukumo wa hewa safi kuingia katika engine na hivyo kupelekea uchomaji wa haraka wa mafuta kisha kuiongezea engine uwezo wa kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi,hapo ni katika kurahisisha kufikia RPM za juu kwa muda mfupi. Hivyo basi utaweza kupata acceleration kubwa.(Work÷Time=Power)

2. Kupunguza ulaji wa mafuta
-Turbo husaidia kupunguza ulaji wa mafuta kutokana na nguvu ya ziada inayoipa engine,hivyo basi uzito wa gari kwa engine kupungua kwa kiasi kikubwa(power to weight ratio)

Turbo pekeyake haitoshi kukupa matokeo yaliyolengwa na teknolojia,hivyo basi husaidiana na INTERCOOLER, kifaa ambacho kazi yake ni;
1. Kupoza hewa iliyopata joto kwenye njia za turbo.
2. Kusaidia kuongeza uzito(density) wa hewa itokayo kwenye turbo.
3. Kuchangia kiasi kikubwa cha ongezeko la nguvu na kupunguza ulaji wa mafuta Kutokana na kwamba hewa ya baridi huwa na kiasi kikubwa cha chembe za oxygen,hivyo basi itakamilisha uchomaji kirahisi(Ifahamike pia oxygen ni hewa kuu chochezi katika vyanzo vingi zaidi vya moto).
.
TAHADHARI: ENDESHA GARI KWA KUZINGATIA TARATIBU ZOTE ZA USALAMA BARABARANI,JAMII INAKUHITAJI KATIKA UBORA WAKO.

USIJARIBU KUFANYA ZOEZI HILI MWENYEWE BILA MAARIFA YA KITAALAMU,HASARA INAYOWEZA KUKUPATA ITAKUPA MAJUTO.

Wasiliana nasi tukuhudumie kwa simu namba: 0626409908

#teamcruiser
#teamcruisermechanics
#landcruiser70series
#1hzturbointercooler
Hiyo intercooler kwa ajiri ya kupoza complessed air kutoka kwenye turbo,unaifunga wapi?
 
Back
Top Bottom