Ondoa gaga kwa kufanya haya

Issuna

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
3,168
7,513
Kuna watu hawawezi kwenda kuoga bila jiwe au brashi la kusugulia mguuu halafu bahati mbaya ni kwamba Brashi analotumia sugulia miguu ni Brashi gumu na wengine hawajaishia kwenye Brashi ila wameona hata brashi halitoshi wana mawe kabisa Bafuni kwake au kwenye kopo lake la kwenda kuogea.

Yote hiyo ni kupambana na magaga/masagamba/makenya,nk kila mtu anajua anavyoyaita sasa leo nawapa mbinu ambayo unaweza iona haifai au ukaona kama utani ila ndio dawa namba 1 kisha ikitoka hii ndio ifate hyo unayoijua wewe.

Ukitaka kuondoa magaga miguuni mwako usiende bafuni na brashi la mguu wala Jiwe. Ukitaka kuondoa magaga miguuni usisugue mguu wako na kwenye kitu kigumu.

Cha kufanya unapoenda bafuni: Kila mtu najua uso wake anausugua na kitambaa laini na soft hiyo ni sababu hataki kujiumiza uso wake kadhalika na katika miguu unapoenda bafuni tumia kitambaa kilaini kama unachosugulia USO wako, tena kama unataka matokeo mazuri tumia kitambaa laini kama kile cha kumwogeshea mtoto mchanga kile softiiiiii.

Unaposugua miguu yako osha vizuri kwa sabuni kisha usitumie nguvu we shika kitambaa chako sugua taratibu miguu yako hakikisha kama kitamba ni cheupe hadi unaposugua kitambaa kibaki na povu jeupe vile vile.

Kisha suuza miguu yako vizuri, baada ya kusuuuza utaona michirizi meusi ambayo ni kwasababu ya mguu wako kupasuka na ule uchafu wa vumbi na mchanga kuingia..watu wengi wanapoona ile michirizi meusi isiyotoka kwa brashi hutumia JIWE kusugua ili kufanya miguu iwe meupe wasichojua ni kwamba ndio wanavyozidi kuharibu miguu yao.

Basi kwa kua wewe hutaki magaga anza kuacha kusugua miguu yako kwa brashi ambalo huwezi sugulia uso..ile michirizi meusi isikupe shida Jambo lolote zuri halitaki haraka so ukimaliza kuoga nenda zako kalale (usipake chochote miguuni (nyayo) usiku, asubuhi amka oga paka mafuta mwili mzima vaa viatu/sendo nenda mishe zako.

Tabia yako iwe ni hiyo muda wote kwa miaka yote. Matokeo yake utayaona baada ya mwezi miguu itajifunga yenyewe na kule kwenye ile michirizi meupe kutapotea na utakua na miguu softiiiiiiii kama vile hujawahi kuwa na magaga.

Usitake haraka ya matokeo, inategemea na magaga yako yalikua yamechimbikaje ila hiki ninachokiandika kina fanya kazi kwa kila mtu na ni 100% achana na cream za miguu, sjui mafuta, sijui nini. Acha mwili ujitengeneze wenyewe, usaidie kazi yake kidogo sana ila any change unayoitaka kwenye mwli wako acha mwili ufanye wenyewe. Wewe ujue tu nini cha kufanya ili matokeo uyaone kwa haraka.

LEA nyayo za miguu yako kama USO wako, ukitaka kulea Nyayo tofauti na Uso shauri yako.
 
Back
Top Bottom