Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,140
- 1,983
Kwenu,
Nimekuwa nikifuatilia sana tabia za wanasiasa wa Tanzania hasa wanaCCM.
Toka enzi za akina Mrema wa NCCR-Mageuzi,kisha TLP lakini akionesha bayana kuwa moyo wake uko CCM,Nsanzugwako,Wasira na wengineo waliokuwa moto wakiwa NCCR-MAGEUZI,kisha wabunge waliokosa ubunge CCM wakakimbilia CHADEMA na kupata ubunge(Mwambe na wengine) mpaka Lowasa,Sumaye na wajumbe wao waliohamia CHADEMA na 'kurudi nyumbani' kwa kasi baada ya kukosa fursa,unajifunza kitu kimoja;Mtu aliyezaliwa na kukulia CCM,hawezi kufanya siasa za upinzani.
Lowasa aligombea urais akiwa CHADEMA baada ya chama chake kumkata na kwa kiasi fulani alifanikiwa ingawa hakupata urais.Sumaye aligombea uenyekiti wa kanda,akashindwa.Nyalandu aliwania kupitishwa kuwa mgombea urais kupitia CHADEMA,akashindwa baada ya kuzidiwa sana na Tundu Lissu.Hawa wote leo wamekimbia na kurudi CCM.
Viongozi na wanachama wa CCM hawawezi kuishi nje ya CCM.Ukiwatoa nje ya chama chao wana-suffocate,wanakosa pumzi.Ni sawa na kumtoa samaki majini na kumweka nchi kavu.Atadumu muda mfupi.Asiporudi majini atakufa.WanaCCM hawawezi tena kupambana,Wamezoea kusaidiwa na dola kwenye siasa zao.Hawawezi mapambano.
Siasa za upinzani Tanzania ni ngumu sana.Unakamatwa,unapigwa,unadhalilishwa,unaswekwa lupango,unafilisiwa na pia unauwawa.WanaCCM huja upinzani tu pale wanapokosa fursa za ulaji au uongozi.Wanapenda na wamezoea uongozi.Wakiukosa au wakipata msukosuko,wanarudi walikotoka na hupenda kuitisha press conference na kudai Upinzani hakuna demokrasia.
Once you are a CCM cader,you will always be CCM at heart.
TS.