Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,915
Historia ni kumbukumbu, historia ni mwalimu, historia haidanganyi, historia hutahadharisha na historia hutoa funzo na hujirudia baada ya muda fulani na katika nyakati tofauti.
Flashback: Mwaka 2011 dawa ya ajabu ilidaiwa kupatikana. Hii dawa ilidaiwa kutibu si tu ugonjwa moja, hapana, dawa ilitibu magonjwa yote mwilini na kuuacha mwili ukiwa na afya tele.
Wataalamu walionya sana kuhusu athari za dawa hii lakini walipuuzwa na wagonjwa walimiminika kijijini Samunge kwa nabii aliyedai kaoteshwa na mungu Babu wa Loliondo, Ambilikile Masapila.
Hospitali zilikimbiwa na wagonjwa wa aina zote na juhudi za madaktari kuwazuia hazikufanikiwa. Wapo waliosafiri kwa ndege, waliosafiri kwa magari, waliosafiri kwa baiskeli na waliotembea kwa miguu.
Watu wenye maradhi ya aina zote, wanawake kwa wanaume bila kujali dini, jinsia au rangi, bila kujali uwezo wa kifedha ama nyadhifa, bila kujali umri wao,walimiminika kuwahi kikombe, kikombe cha babu!
Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo
WAZIRI wa Ujenzi wa wakati huo, Dk John Magufuli, naye alitua Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila ili aweze kupata kikombe chake cha dawa kama anavyoonekana hapo juu. Baada ya kupata dozi yake Waziri Magufuli alitangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.
Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali ingetumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia usafiri wanaokwenda kunywa dawa kwa Babu Masapila.
Je ni Watanzania wangapi walikufa kwa kuacha kutumia dawa za hospitali na kukimbilia kikombe cha Babu?
Swali fikirishi: Je hali ingekuwaje wakati huo kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania angekuwa ni John Magufuli?
Presently: Je kwa dawa ya COVID-19, historia itajirudia?