Once bitten, twice shy...je historia itajirudia?

Once bitten, twice shy...je historia itajirudia?

Jifunze kuandika kwanza ueleweke
nadhani mtoa mada unahitaji kuchekiwa akili zako, akili zangu zinaniambia akili zako haziko sawa, mirembe hosp should be your new home!! dawa ile ya Madagascar ni bora acha uchawi na uzabizabina , nchi nyingi zimenunua nimeona mwenyewe leo Al Jazeera wakirusha hewani ndege za Guinea Bissau zinabeba maboksi lukuki!! nasikia hata Italy wanachukua kwa siri, na stori ni kuwa Madagascar wagonjwa wote wanaotumia hiyo dawa hupona!! Acha kulinganisha vitu visivyo lingana ile ni dawa inatoka kiwandani!! Tumejikinga kwa maombi kwa kujifukiza na sasa tumehamia tiba ya kisayansi, watu wa Ivory Coast wananua Chloroquine na kusubiri Coronavirus ije wanywe, kununua dawa Madagascar si lazima tuumwe, ni kujilinda na watakaoumwa kwa maombi ya Chadema Corona bus ijaze abiria basi wapewe! Kama dawa inaponya tukinunua ni faida manake tutafungua mashule na michezo haraka maisha ya mamilioni ya watu yaliyosimama yaendelee! Acha kuwaza ujinga!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!...hii nchi Ina vituko Sana.

Ila tukumbuke kipindi hicho mjadala wa malipo ya kampuni yenye utata ya kufua umeme ya 'Dowans' ulikuwa bado unagonga vichwa vya habari.

Hivyo babu Mwasapile alipewa promo kubwa na wakubwa ili kuzika ule mjadala muhimu wa kitaifa na kweli baada ya muda ule mjadala ulizikwa kabisa maana kikombe cha babu ndio iligeuka habari ya mjini.
 
Dah Tuna na first world war and second world war.


Sasa tuna first MajiMaji war (tanganyika tribes aganist ujerumani) second MajiMaji war ( Tanzania aganist COVID-19)

Chunguza the reason of MajiMaji failure,uchukulie Kama key points kwenye Vita mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawee!!........ Kwa akili za namna hii lazima tuburuzwe.
Na sisi wenyewe tunakubali kuburuzwa na kuswagwa kama mbuzi hata kama tunapelekwa machinjoni! But why? Will this stupidity ever end?
 
Historia ni kumbukumbu, historia ni mwalimu, historia haidanganyi, historia hutahadharisha na historia hutoa funzo na hujirudia baada ya muda fulani na katika nyakati tofauti.

Flashback: Mwaka 2011 dawa ya ajabu ilidaiwa kupatikana. Hii dawa ilidaiwa kutibu si tu ugonjwa moja, hapana, dawa ilitibu magonjwa yote mwilini na kuuacha mwili ukiwa na afya tele.

Wataalamu walionya sana kuhusu athari za dawa hii lakini walipuuzwa na wagonjwa walimiminika kijijini Samunge kwa nabii aliyedai kaoteshwa na mungu Babu wa Loliondo, Ambilikile Masapila.

Hospitali zilikimbiwa na wagonjwa wa aina zote na juhudi za madaktari kuwazuia hazikufanikiwa. Wapo waliosafiri kwa ndege, waliosafiri kwa magari, waliosafiri kwa baiskeli na waliotembea kwa miguu.

Watu wenye maradhi ya aina zote, wanawake kwa wanaume bila kujali dini, jinsia au rangi, bila kujali uwezo wa kifedha ama nyadhifa, bila kujali umri wao,walimiminika kuwahi kikombe, kikombe cha babu!


Magufuli apeleka Sh1bn Loliondo

WAZIRI wa Ujenzi wa wakati huo, Dk John Magufuli, naye alitua Kijijini Samunge kwa mchungaji Ambilikile Masapila ili aweze kupata kikombe chake cha dawa kama anavyoonekana hapo juu. Baada ya kupata dozi yake Waziri Magufuli alitangaza neema ya kujengwa kwa barabara kuu inayoingia kijijini hapo.

Magufuli aliuambia umati wa watu uliokuwa ukisubiri zamu yao kunywa dawa kuwa, Serikali ingetumia Sh1.05 bilioni kwa ajili kutengenenza barabara hiyo ili iweze kupitika wakati wote kwa lengo la kuwarahisishia usafiri wanaokwenda kunywa dawa kwa Babu Masapila.

Je ni Watanzania wangapi walikufa kwa kuacha kutumia dawa za hospitali na kukimbilia kikombe cha Babu?

Swali fikirishi: Je hali ingekuwaje wakati huo kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania angekuwa ni John Magufuli?

Presently: Je kwa dawa ya COVID-19, historia itajirudia?
Babu alikuwa tapeli tu
 
Nimesikia Leo BBC wakisema WHO wametoa onyo kuhusu hiyo dawa ya Madagascar na kwingineko zinazokuwa hazijafanyiwa utafiti na kuidhinishwa kwa matumizi ya binadamu.
Na wametaja kabisa Tanzania, DRC, Guinea Bissau na nyingine moja kwa kuzionya kuhusu kushobokea jambo hilo.
Madhara ya kuonekana primitive kama nchi sio ya sasa tuu bali yatatugharimu mpaka siku nyingi baadae mfano kama Haiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Babu alikuwa tapeli tu
Je umewaona hao wanaobugia vikombe? Kwa mbali naiona historia ikijirudia au siyo? Baadhi ya waliokubali kutapeliwa kwa sasa hatma ya taifa iko mikononi mwao, je tutapona?
 
Historia naona imejirudia tayari...

loliondo9.gif
2011.................>.......................................>.............2020
2393512_dawa_ya_corona (2).jpg


Badala ya kikombe sasa ni glasi.​
 
Back
Top Bottom