wewe hujui chochote kuhusu maisha ya ndoa. naona unaongelea theories tu hapa!!!!
wanawake ndo wanabadilika?
Wanawake alwayz wanapenda Players. Ndio maana huyo dada habanduki kwa huyo jamaa.
Habari zenu,
Katika kuchunguza maisha ya watu hasa wanaume nimegundua hawabadiliki. Kama mwanaume ana zaa zaa ovyo ataendelea hivyo, kama ni Malaya (player) ataendelea hivyo hivyo. Wanawake tunajipa moyo labda atatulia nk ila hapo ndo tunapokosea, they never change. Kama anakupiga hataacha kukupiga. Tusilazimishe ndoa na mwanaume yeyote mana majuto yatakuwepo. Kuna dada alimpata player akapata mimba na kufanya kila namna akaolewa na jamaa, sasa mwanaume anatembea na shosti zake, wadada wa kazi, wafanya kazi wenzie na watu wengine wasiojulikana na yeye anajua maana wengine walimpigia hata simu kwamba yeye yuko na huyo mwanaume kwasababu ya madawa yake tu! Ndoa imekuwa ngumu, mbaya zaidi alipoolewa alimtibua mama mkwe so na ndugu wa mwanaume wako mbali nae.
Shoga zake wote kagombana nao, kuanzia waliomwambia mumeo kanitongoza, waliotembea na mumewe na wale aliowahisi kwamba wanaweza kutembea nae.
Jamani wito wangu kwa wadada, ukigundua mwanaume wako ana tabia ya hovyo yoyote kimbia mapema usidhani atabadilika kwa ajili yako tena usijifunge nae katika ndoa maana atakutesa sana. Kama kawazalisha wenzio na kuwaacha atashindwaje kukufanyia wewe hivyo hivyo, kama anakutendea vibaya hata acha.
Sawa, lengo ni kusema fanya at your own risk. Halafu huyo dada wamefunga ndoa kanisani na wana watoto hawezi kubanduka tena atamwachia nani watoto.Wanawake alwayz wanapenda Players. Ndio maana huyo dada habanduki kwa huyo jamaa.
Kuna misemo mingi ya wanaume kujustify tabia zao, lkn kufeli kwa mwanaume mmoja haimaanisha wanaume wote wamefeli. Bado wapo wenye utu na wasiopumbazwa na siasa za kuburuzwa kwenye kundi.Na bahati mbaya asilimia kubwa sana ya wanaume ni maplayers sasa sijui watakimbilia wapi.
Wanawake wakiujua huu ukweli wala hawataumiza vichwa kutufuatilia
Kuna misemo mingi ya wanaume kujustify tabia zao, lkn kufeli kwa mwanaume mmoja haimaanisha wanaume wote wamefeli. Bado wapo wenye utu na wasiopumbazwa na siasa za kuburuzwa kwenye kundi.
okay sijui, at least Nimeona na wahusika wamenisimulia yanayowakuta.wewe hujui chochote kuhusu maisha ya ndoa. naona unaongelea theories tu hapa!!!!
Hilo ni Tatizo la wasio maplayer, hawajui mwanamke anataka kuambiwa au kufanyiwa nini na ubaya ni kwamba hii taarifa muhimu wameijua maplayer.Na Hao Maplayer Ndo Wanaoongoza Kwa Kushobokewa Na Wasichana Tena Leo Mnalalamika!Makubwaa..!!