Ona jinsi watanzania tunavyopigwa bei kubwa bora ununue mtandaoni tu!!

Ibrahim augustine

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
428
575
Leo katika pitapita zangu nikaona sio mbaya nitembelee website ya beforward inayo uza magari ya kijapani mapya mtandaoni.
Eeebwana we!! Si nikaona gari inauzwa $873 aina ya Toyota ist sawa na 1744000 yaani milioni moja na laki saba na ushee.
Duuh hii sibei ya pikipiki jamani.

Basi nikatuma ujumbe wa kutaka kuinunua nikapewa na invoice ya manunuzi cheki hapo
Screenshot_20180410-154357.png


Aisee lakini tukirudi hapa bongo hii gari unapigwa milioni 10-15 mtanisaidia mnaojua magari lakini hii screen shot ni invoice ambayo inaonesha bei ya kusafirisha mzigo yaani shipping ndio maana bei mnaona imeongezeka kidogo.

Duuh bado sikuridhika nikaingia eBay nikaona simu Kali balaa aina ya iPhone 7
View attachment 740367
Bei yake ni ndogo sana ukilinganisha na hapa bongo eti milion1
Halafu eBay inauzwa dolaa 300 sawa na kama laki 6 na usheee!!
Aisee juzi mzee wangu alinunua Samsung galaxy J7 pro imetoka 2017 kwa bei poa kabisa lakini ukiulizia hapa bongo utalazwa
Simu mzee aliyo nunua
IMG_20180407_182922.jpeg

Ndugu zangu nawashauri mnunue mtandaoni hapa bongo tunapigwa bei zaajabu ndio maana tunalalamika vyuma kumbe ni wafanyabiashara wanaotaka kujiongezea cha juu japo sikatai ukinunua mtandaoni kuna hasara zake kama kuibiwa ikiwa bandarini tena hapa bongo sijuii baadhi ya wabongo tupoje MTU unaweza kuagiza gari mpya ikigika unakuta TV.
Huo ndo ushauri wa leo asanteni
 
Kuna sehemu sijakuelewa, kuagiza IST, bei huwa kuanzia 9.5ml, na ni kweli wauzaji wanaotafuta faida huagiza kwa bei hizo na kuuza juu kidogo... Hilo ni soko huria, sio kila mtu hutaka kuagiza, wengine wanataka waione gari hapohapo...

Karibu pia nikuagizie mchakato wote... Nicheki kwa FB yangu fb/KIMIMAGARI
 
Huyu atakuwa hajawahi nunua vitu kwenye mtandao. Hiyo jumlisha $1200 ya ukaguzi na transport. Itakuwa $ 2200. Hujalipia TRA 4.3m tshs. Jumla inafka 11mtshs. Hivo hivo kwenye cm. Labda uwe unakwepa kulipa TRA
 
Acha ushamba wako wa ki Singida dogo! :eek:
Kuna sehemu moja ambayo hukuoneshwa bei. Ngoja niku scanie na kukutumia fasta...
================================================
Umeona hapo? That is what a tax man is waiting to axe you when you import your cheaply bought IST!
Hapo bado hujaweka some other landed costs such as clearing and forwarding, shipping line, storage costs etc...

tra.png
 
Nchi hii kinachokwamisha hata watu kununua magari mazuri ni kodi kuwa kubwa sana
 
Sasa kuna haja gani ya kuwa na viwanda wakati kodi inatosha kuwa kiwanda. Yaani kodi ni kubwa mara dufu ya bei ya gari???

Kudadeki. Bora kuboresha bandari kuliko kuwa na viwanda
 
Huwezi kuingiza gari aina yoyote Bongo chini ya milioni 7 hata kama umepewa bure Japan
 
Back
Top Bottom