Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 579
- Walianza kwa kumfukuza Zitto Kabwe Bungeni: Hili lilimpa umaarufu mkubwa sana, na alitumia wakati ule akiwa nje ya Bunge kuzunguka huku na kule kueneza sera za Chadema.
- Wakakataa Hoja Binafsi ya Dr. Slaa kuhusu EPA, wakamuita mzushi: Kwa hili Dr Slaa akalipeleka kwa wananchi, na wananchi wakaamua kwelikweli. Dr. slaa akataja wale aliowaita mafisadi; mpaka leo neno hili limekuwa na maana kubwa sana kwa Watanzania. Matokeo yake tuliyaona, Balali hayuko Benki kuu tena. Wamemnyamazisha mahali.
- Wakazuia hoja ya Dr. Slaa kuhusu Richmond. Kama kawaida yake, akalipeleka kwenye Mahakama ya Wananchi, mwisho likamng'oa Lowasa na kusababisha Baraza la Mawaziri Kuvunjwa.
- Wakazuia hoja za Kagoda, Meremeta na Deep Green. Hizi bado ziko zinaendelea, watu wanzidi kuichukia CCM.
- Wakamnyima Samwel Sitta Uspika wa Bunge: Bila shaka mmeona kiti cha Spika kinavyoyumba na kulipotezea Bunge heshima kila siku
- Wakataka kuzima hoja ya Katiba mpya. Chadema wakalipeleka kwa Mahakama ya Wananchi, na sasa tunatarajia kuwa na katiba mpya mwakani.
- Wakaua watu Arusha. Mpaka leo Arusha imeamka, na imekuwa ngome kubwa ya Chadema
- Wakamteka Dr. Ulimboka. Mpaka leo dunia nzima inajua ubabe wao, na hili bado linaendelea kuiva jikoni
- Wakamuua Mwangosi: Mpaka leo hili swala linaichemsha serikali.
- Wakamnyang'anya Lema Ubunge kwa miezi kadhaa. Mwisho Lema akashinda rufaa na kuifanya Chadema
- iwe na nguvu mara dufu zaidi.
- Mabilioni ya Uswiss, n.k.
- Sasa wanaendelea kukandamiza demokrasia Bungeni. Wananchi wanazidi kufumbuliwa macho.
Ninachoweza tu kusema ni kuwa, wanatumia nguvu kubwa sana kunyamazisha upinzani. Lakini badala ya nguvu hiyo kuua upinzani, imeendelea kuuimarisha na kuupa umaarufu zaidi.
Yapo mambo mengi sana. Unaweza kuongeza mengine mengi tu, mimi naishieni hapa.