ona janja ya chazbaba.

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
MWIMBAJI wa zamani wa bendi ya African Stars maarufu kwa mtindo wa Twanga Pepeta, Chalz Baba inasemekana tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na bendi ya Mashujaa kwa kupata donge nono.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa mwimbaji huyo amepewa sh. Milioni 15 kwa mkupuo na atakuwa analipwa mshahara wa sh. 400,000 kila mwezi.

Mbali ya malipo hayo, pia Chalz atakuwa analipwa sh. 200,000 ya kodi ya nyumba na shs. 50,000 kwa kila wiki (jumla sh. 200,000 kwa mwezi) na kupokea jumla ya sh. 800,000 kwa mwezi.

Aidha uchunguzi umebaini kuwa mwimbaji huyo kwa sasa anazuga tu kama anatafuta bendi wakati tayari amemalizana na bendi hiyo ya Mashujaa huku ikisemekana kuwa anatarajiwa kutua Jukwaa la Extra Bongo ambapo atakaa kwa muda mchache kabla kutangazwa rasmi kujiunga na Mashujaa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mwimbaji huyo atakuwa chini ya sheria kali (Mkataba) ya Mshujaa.

Moja ya masharti hayo ni kutakiwa kushiriki bila kukosa shughuli za bendi hiyo na kutakiwa kutopanda jukwaa la bendi yoyote hata kama bendi yake haitakuwa kazini isipokuwa kwa kibali cha maandishi kutoka kwa mkurugenzi mtendaji.

Pia mkataba huo umeonyesha kuwa endapo mwajiriwa atavunja mkataba huo, basi hatoruhusiwa kufanya kazi katika kampuni nyingine inayomiliki bendi Tanzania ila tu kwa kibali maalum cha maandishi kutoka kwa mwajiri kitakachotolewa na maombi ya mwajiriwa.
Mbali ya masharti hayo, pia mwanamuziki huyo anatakiwa kutotumia kazi za bendi yake katika sherehe au shughuli za aina yoyote bila ya ridhaa ya uongozi.
wadau wa karibu wa mwanamuziki huyo ambao hawakupenda kuandikwa majina yao hewani, walisema kuwa, Chalz, amejiengua katika kundi hilo la Twanga akiwa na nia ya kutua Bendi ya Mashujaa.

Aidha walisema kuwa Chalz anatarajia kutua jukwaa la Bendi ya Extra Bongo ambapo atakuwa akipita tu huku akijiandaa kukamilisha safari yake ambayo itaishia Bendi ya Mashujaa.

Kwa kauli hiyo inaendana na kauli iliyotolewa siku za hivi karibuni na Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, aliyesema kuwa anatarajia kufanya usajiri wa nguvu na wa aina yake kwa kusajiri wanamuziki mahiri kutoka katika bendi mahiri za jijini ambazo ni mahasimu wake.mia
 
Safi sana fedha kwanza
siyo kwa wasanii wa bongo!!!!wao jina kwanza pesa baadae!!kama anaenda huko naamini atarudi twanga kwani kule hawezi kupata jina kama akiwa twanga!...asha baraka fitina za mziki anazijua na hata akiondoka twanga haitotetereka!wameondoka wangapi lakini watu wanapepeta kama kawa!
 
maneno tu hayo....twanga ya sasa sio ile bwana hovyooo
 
siyo kwa wasanii wa bongo!!!!wao jina kwanza pesa baadae!!kama anaenda huko naamini atarudi twanga kwani kule hawezi kupata jina kama akiwa twanga!...asha baraka fitina za mziki anazijua na hata akiondoka twanga haitotetereka!wameondoka wangapi lakini watu wanapepeta kama kawa!

Umeona eeh..
 
twanga pepeta ni mtakuja, usishangae keshokutwa utawaona kina choki wameudi. ivi wapi msafiri diof siku izi?
 
Hakuna jema machoni pa wabongo kijana amekwenda kutafuta angali bado ana nguvu anaonekena mbaya,tatizo la watu wanataka aishi maisha ya kuganga njaa wakutane nae mtaani wampige madongo na kumcheka, apewe sapoti jamani suala la yeye na Twanga kule hajafukuzwa ukifika wakati nao wakimlipa fedha anazohitaji bado atakwenda kufanya kazi kumbukeni anatumia nguvu zake mwenyewe. Mimi nadhani ni hatua nzuri katika kujitafutia maisha, na hakuondoka Twanga pepeta ili bendi iyumbe kaondoka kwenda kutafuta maslahi tu.
Mimi sijui analipwa kiasi gani huko aendako kwani ni mambo ya ndani zaidi ila kama kweli zitafika hizo laki nane ukijumlisha fedha zake zote kwa mwezi naomba nikujibu wewe unayesema Laki 8 ndogo kwamba unakosea sasa mshahara wa Laki 8 ni mkubwa ndugu yangu hebu kuwa mmkweli ni ma graduate wangapi wanapokea kiasi hicho kwa mwezi.

Mpeni nafasi kijana atafute.
 
....Tumia kipaji chako vizuri maana vipaji vya muziki na mpira ni kama barafu Somalia.....
 
Twanga kuna nini wakuu? naona watu wanakimbia kama vichaa vile kha!!
 
800.000 kwa mwezi..hela ndogo sana!

Laki Nane kwa MWEZI ni ndogo? Kweli BASI gap kwa wenye nacho na tusiokuwa nacho ni Kubwa saana 800,000 ni mshahara wa miezi miwili ya mwalimu wa sekondari mwenye elimu ya Chou kikuu
 
Laki Nane kwa MWEZI ni ndogo? Kweli BASI gap kwa wenye nacho na tusiokuwa nacho ni Kubwa saana 800,000 ni mshahara wa miezi miwili ya mwalimu wa sekondari mwenye elimu ya Chou kikuu

bora ata hilo umeliona maana inasikitisha..
 
Back
Top Bottom