ombwe la uongozi Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ombwe la uongozi Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ngoshwe, Sep 29, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kupitia magazeti ya jana tarehe 28 Septemba, 2011 Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ilijibu makala hii ya Deusdedit Jovin ambayo kimsingi ina mantiki kubwa. Bodi imonyesha kumbeza na kumtuhumu mwandishi huyu kuwa ni Mbinafsi, asie na uzalendo, asiefanya utafiti kabal ya kuandika nk. Lakini kwa undani, Bodi imeshindwa kujibu hoja za msingi zilizotolewa na mwandishi ikiwemo vigezo vinavyotumika kukokotoa mikpo na msingi halisi wa kukadiria mikopo kwa walengwa.

  Kwa hivi sasa Bodi inatoa mikopo kwa kuzingatia taarifa za kwenye makaratasi tu (Paper work) na mbaya zaidi inasema inaangalia pia "background" za gharama ambazo mwambaji amekuwa akitumia katika shule za awali..hizi eti ndo zinapima kiwango cha utajiri au umaskini wa mwombaji??. Hivi inawezekana kweli mtu akaishi katika mfumo huo huo wa maisha bila kuteteleka? Ni wangapi wanakuwa na maisha mazuri mwanzoni na baadae kuporomoka na kuwa maskini wa kutupwa??
  Ikiwa watanzania wote ni maskini kwa mujibu wa takwimu, na ikiwa fedha zinazotumika kutoa mikpo ni kodin za watanzania wote bila kujali umaskini au utajiri alionao kila mmoja wetu, kwa nini pasiwe na "uniform approach" katika kutoa uamuzi wa wanaostaili kupata mikopo??..kwa mfano katika nchi nyingine, utaratibu ni kupitia benki za kawaida ila Serikali ndio inatoa udhamini tu.

  Katika majibu yake, Bodi inasema imeshindwa kuwahudumia waombaji wote wa mwaka 2011/2012 kutokana na ufinyu wa Bajeti, lakini cha kushangaza, Bodi haikuwahi kutangaza kabla ya Tuhuma zailizoandikwa katika Gazeti la Raia Mwema, ni kiasi gani imepewa kwa mwaka huu wa Bajeti kwa ajili ya mikopo na kiasi gani ingehitaji. Bodi INA USIRI MKUBWA, imekuwa ikiibuka na kujibu hoja tu pale inapotuhumiwa, lakini katika hali ya kawaida haijui kuwa inapaswa kuwapa wadau taarifa za nini kinaendelea. Kwa mfano, imezungumzia kuwa utartaibu mzima wa ukokotoaji unapaswa kutanghazwa na Waziri anayehusika katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Sheria inayoanzisha Chombo hicho, lakini haijabainisha ni Gazeti lipi (Government Notice Number - GN) ambalo wamewahi kutoa tokea chombo hicho kuanzishwa. Achilia Gazeti hilo la Serikali ambalo linaweza kuwa ni taratibu ndefu na lisiwafikie wengi, Bodi haijawahi hata kutoa katika magazeti ya kawaida mfumo huo wa ukokotoaji wala majina ya walioidhionihsiwa, kukataliwa au lah...pengine inadhani watanzania wote wanaweza kuingia kwenye tovuti yao na kusoma habari zao, lakini haijui kuwa sio maeneo yote ya nchi hii yanafikiwa na huduma ya intaneti...(nao wanaishi dunia ya kusadikika)!!. Ikumbukwe Bodi hii ni ile iel iliyowahi kuwajia juu vijana wa UVCCM kwakiwatuhumu kuwa ni "Wazushi" ( Rejea: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/105881-bodi-ya-mikopo-vijana-ccm-ni-wazushi.html...). Lakini katika majibu waliyotoa kwa mwandishi Jovin wa Raia Mwema, wanarejea tena kwa kumtuhumu kuwa naye ni mchochezi, hana takwimu na hajui analoandika... Bodi imesahau kuwa, Mwandishi kama huyu Mzalendo aliyepaswa kuelimishwa ili atumike kuelimisha watanzania wengine kuhusu Bodi hiyo, na asiandike haya ambayo wao wanaona ni "Uwongo na Uchonganishi".

  Walitarajia mwandishi aandike nini kama wao wameficha taarifa muhimu za yale wanayofanya??


  imekuwa na usiri Mkubwa katika utendaji wake mpaka ituhumiwe ndipo ijibu hoja
  .
  Raia Mwema
   
 2. B

  Bukijo Senior Member

  #2
  Sep 29, 2011
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Magazet yap mkuu,ningependa nifuatilie nione pumba zao jins walivyojibu hoja hiyo.
   
 3. Eshacky

  Eshacky JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 966
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Enyi watawala tusikilizeni kilio chetu!
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii bodi ya mikopo iliyo chini ya ukurugenzi wa nyatega na akina lubambula machunda haijawahi kukidhi haja ya kuwepo kwake tangu ilipoanzishwa.

  Hawajui namna ya kufanya means testing na wala hawana formula maalum ya kukokotoa mahesabu kwa ajili ya waombaji.

  Wamegeuka kupiga propaganda kupitia vyombo vya habari badala ya kutumia muda wao vizuri kujifunza namna ya kuboresha utendaji wao.

   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni pampoja na Gazeti la Majira Mkuu la tarehe 29/09/2011. Imetolewa Kama taarifa kwa UMMA
   
 6. B

  Bukijo Senior Member

  #6
  Sep 29, 2011
  Joined: Jul 28, 2010
  Messages: 166
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Aksante ngoja nikalicheck!
  Hawa jamaa taarifa zao sio sahihi kuna jamaa zangu weng tu majina hayaonekani kotekote,waliopata hawamo waliokosa hawamo wala sehemu yoyote ile majina hayaonekani.
  Je,tuseme bodi haijapata maombi yao?.EMS nayo ilichelewesha barua?.Au hata online applications zilichelewa!
  Wa release majina yote ya waliomba mikopo waoneshe makosa yaliyofanywa ili wayatambue na wasiyarudie au wapewe nafasi ya kufanya marekebisho!
  Imagine waliokosa kwa mjibu wao ni 13,382 nimejumlisha wale wenye matatizo mbalimbali kwa mjibu wao- Name differene,Contract problems,Not eligible, not need etc.
  Sasa fanya 13382*30000= 401,460,000/- hizo pesa zote wamegawana!
  Bado wale wasioonekana kotekote idad yao haijajulikana.Ni Wizi mtupu!

  [TABLE]
  [TR]
  [TD="width: 86"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="width: 86"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. N

  NIMIMI Senior Member

  #7
  Sep 29, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vile vile VITISHO wanavyovitoa kupitia Vyombo vya Habari juu ya watakaoandamana kudai haki zao za msingi ninaviita ni Ulimbukeni. Vitisho havitufikishi popote.
   
Loading...