Ombi oja tu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi oja tu....

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Bushbaby, Jun 21, 2011.

 1. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Jamaa mmoja alikuwa anatembea pwani ya bahari ya Hindi..... huku anasali kimoyomoyo, akasema kwa sauti Mungu natamani unifanyie kitu kimoja.....ikasikika sauti kutoka mbinguni ikisema "Kwa kuwa umejitahidi kuwa waaminifu mimi nitakufanyia..." jamaa akasema nataka ufanye daraja hapa na Zanzibar ili niende tu kwa gari kirahisi..."

  Bwana alijibu, "ombi lako ni gumu sana... fikiria vifaa vinavyotakiwa.....zinatakiwa nguzo, zitakazofika chini ya bahari....inatakiwa cement na chuma nyingi....sitaweza kufanya hilo kwani ni siwezi kukubali ombi lako la kimwili...fikiri kitu kingine...kitakachonitukuza.... .

  Jamaa akafikiri kwa muda kisha akasema..."Bwana, nataka nipate kumwelewa mwanamke!!,.... ..Nataka kujua mawazo yao...anaponipa jibu la kimya...kwa nini hulia...anaponyamaza kimya....anaponijibu kuwa ..hakuna kitu/shida... na jinsi nitakavyoweza kumfanya mwanamke afurahi....

  ......Mungu akatulia kwa muda ....akamwambia, Hivi lile daraja ulisema unataka lianzia wapi...... ?.......
   
 2. KIGENE

  KIGENE JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  Translated from english and reposted.
   
 3. a

  allydou JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,486
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  nadhani atakuwa alipewa kitabu kileeeeeeee akisome, kama unakikumbuka kiliwekwa hapa.sijui kama aliweza kuelewa au laaa.
   
Loading...