Ombi/Msamaha kwa kupiga magoti....Imekaaje hii???

Asprin

Platinum Member
Joined
Mar 8, 2008
Posts
68,487
Reaction score
96,976
Naamini jamboni iko. Swaumu ya Kwaresma si mchezo.

Unajua bana mimi babu yenu jana kwa bahati mbaya sana nikajikuta badala ya kugida mtungi na walipa kodi wenzangu nikawa naangalia Sinema na kafamilia kangu (furaha ilioje kwao na kwa malaika mbinguni). Shem AshaDii asisome hapa.

Ilikuwa sinema ya kinaijeria bana. Mojawapo ya matukio katika lile movie ni jamaa mmoja alipokuwa anaomba kumuoa binti flani. (Mambo ya kizungu flani ya "Will you marry me?") iliyoambatana na jamaa kushika pete huku akipiga goti.....OMG!

Tukio jingine ni wanandoa wawili walikorofishana kwa kosa la jidume (kama kawaida, kosa lazima liwe la mwanaume). Katika kuomba msamaha (mambo flani ya kizungu ya "Am sorry") nayo pia ikaambatana na njemba kupiga magoti kwa mkewe....Damn!

Mashemeji zangu wawili mabinti watanashati (Washapata wachumba, Mentor, Nicas Mtei Arushaone na mabachela wengine msiniombe namba zao za simu tafazali) wakawa wanazodoana. Mmoja akisema mwanaume akimpigia goti mwanamke anaonyesha heshima na kujali wakati binti mwingine akisema mwanaume kumpigia goti mwanamke ni unyonge, ushamba na kujishusha thamani (Ofkozi huyu alipata sapoti yangu kubwa tuuuu, ya kisirisiri lakini wife asije akanilabua).

Sasa nyie vijana wa siku hizi (Hapa wazee wenzangu Dark City, Kaizer na KakaKiiza wasiposema lolote najua wanamaanisha nini) hebu niambieni..... Huu ujuha, sorry hii tabia ya mwanaume kumpigia magoti mwanamke akiomba kitu ndio fasheni ya kisasa tuliyokubali kuikopa kwa wazungu au ni mimi babu yenu nimekomazwa na mfumo dume?

Walimu wangu snowhite, gfsonwin na machizi wenzangu King'asti, Kaunga na Kongosho hebu saidieni ODM asije kuwa anafanya makosa kutowapigia magoti wakeze BADILI TABIA na cacico (Yummy kishakula talaka)

Baada ya kusema hayo, naoma kuwafahamisheni rasmi kuwa leo ni Alhamisi, Kesho ni ijumaa, kesho kutwa ni Jumamosi, Mtondo ni Jumapili na Mtondogoo ni Jumatatu..... Serikali itapata makusanyo mazuri sana ya kodi zetu walipa kodi wa kujitolea.... Mbon safo Klemeeeee.....

Karibuni Kaunta Ya Juu.
Hivi kale kamodereta kangu pendwa Roulette nani kanionea kalipo? Nakamisije sasa?
 
Last edited by a moderator:
Asprin hubby ukinipigia goti najua unanilaghai......

Jishushe tu kwa maneno....ukiwa unanyenyekea najua ukiwa unafanya usanii nitajua....

halafu unajua wanaume wanaoliaga mpaka kupiga magoti kuomba huwa mara zote wasanii......
 
Natamani nikuoe mara ya pili. Vijana wa siku hizi bana.....Mtu kajilambia msuti wake afu eti anakupigia goti "Will you mary me".... Waambie shenzy zao eti.

BTW umenionea wapi Paloma na Raiza? Nataka kuongeza mke miongoni mwao.
 
Last edited by a moderator:
Asprin, tukio kama hili pia uliliona kwa Watanzania au ni kwenye hiyo movie ya ki-nigeria pakee? Nina wasiwasi isije kuwa ndiyo utamaduni wao watu wa huko nigeria wakifanya makosa kama hayo.

Katika hali ya kawaida, sioni sababu ya mtu wa jinsia yoyote ile kuomba msamaha kwa kupiga magoti. sidhani kama kuna kitu kitaongezeka kwa kupiga magoti kama mtu huyo hakumaanisha kuomba msamaha toka moyoni. Unaweza kuomba msamaha bila hata kupiga magoti, kwa unyenyekevu tu na kuonyesha kujutia kosa lako na kumaanisha kuacha kurudia kosa lile na ukaeleweka vizuri. Kwa kesi ya mwanaume kuomba msamaha kwa kupiga magoti, kwangu naona kama ni uzoba tu!
 
Nimeona kwenye sinema bana. Ila mdahalo wa mabinti mashemeji zangu ndo ulinistua. Mmoja anafagilia huo -----.
 
Ukipigiwa goti na mwanamme zaidi ya miaka 40 jua ana malaria imepanda kichwani wala suala la msamaha halihusiki hapo.
Kati ya miaka 30 - 39, jua ni usanii zaidi ya densel au lawrence
Chini ya 30 jua ni mkanganyiko wa mawazo ya kufulia na nguvu kubwa ya utandawazi.

Tanabahi: Ukipigiwa goti kaangalie historia ya ukoo wameishi wapi, labda ngozi nyeusi imekulia London School of Mental Hygiene.
 
Nimezoea kupiga goti wakti namwamkia mtu mzima au mwanamme, nikimpelekea mtu maji ya kunywa, au nikimkaribisha chakula(vya aina yote:-*)

Sasa mwanamme anipigie goti anaomba msamaha, kosa lenyewe kwanza lipi? Kuchit? Imesemwa mwanamme na awe na wanawake wengi ili wasaidiane kupika chakula cha mchungaji na kuchota maji.
 
Hapa siajelewa kitu kwa kweli......

Yaani msamaha magoti au proposal ya namna hiyo?

hii haipandi kabisa!

Babu DC!
 
Kudadadadadadeki...
Sousi: Lusinde, CCM
Nimezoea kupiga goti wakti namwamkia mtu mzima au mwanamme, nikimpelekea mtu maji ya kunywa, au nikimkaribisha chakula(vya aina yote:-*)

Sasa mwanamme anipigie goti anaomba msamaha, kosa lenyewe kwanza lipi? Kuchit? Imesemwa mwanamme na awe na wanawake wengi ili wasaidiane kupika chakula cha mchungaji na kuchota maji.
Kweli nimekubali kwaresma inaishia hivyoooooo

BTW leo una nafasi tukutane Fyatanga?
 
Mie nawapenda sana wasukuma kwa style ya proposal zao kama hizi

Anakubaka(kupondya), afu anakuja kwenu kujitambulisha
Anakutorosha(Kulehya) anakuja kwenu kujitambulisha
Anakuja tu kwenu from nowhere, humjui kumbe anakujua
Mme anachaguliwa na wazazi huko kilabuni
Na mara chache, mnakutana wenyewe kisimani, gulioni, mashineni, kilimoni, mnakubaliana anakuja kwenu

Goti la kupropose linatoka wapi?? Wanamme nao magoti yana grisi hadi wajikunje?

Hapa siajelewa kitu kwa kweli......

Yaani msamaha magoti au proposal ya namna hiyo?

hii haipandi kabisa!

Babu DC!
 
He he he he, wavae mara ngapi??

Nilikutana na mzungu mmoja akawana anashangaa wamasai wanavyovaa viatu vyeupe afu wanajiita 'worriors'

Akaniambia 'viatu vyeupe kwa mwanamme viko kama kishoga zaidi"

Vijana wanaiga mambo ya ulaya mzee mwenzangu.... si unaona wanavaa hereni? Muda si mrefu watavaa shanga
 
Mie nawapenda sana wasukuma kwa style ya proposal zao kama hizi

Anakubaka(kupondya), afu anakuja kwenu kujitambulisha
Anakutorosha(Kulehya) anakuja kwenu kujitambulisha
Anakuja tu kwenu from nowhere, humjui kumbe anakujua
Mme anachaguliwa na wazazi huko kilabuni
Na mara chache, mnakutana wenyewe kisimani, gulioni, mashineni, kilimoni, mnakubaliana anakuja kwenu

Goti la kupropose linatoka wapi?? Wanamme nao magoti yana grisi hadi wajikunje?
Kule kwetu uchagani kudadadeki kipindi cha Krismasi watu wanavizia misa ya usiku. Binti akitoka cvhurch (ofkoz anakuwa kishapanga na bwana wake) Njemba zinavizia rodini. Akikatiza (ofkozi anajipitisha makusudikale) wanamdaka...inaitwa "kutakura" na kumpeleka binti kwa njemba. (Ofkozi binti anajifanya kama hataki vile). Njemba inajilia vyake usiku kucha. Na kule binti asiporudi nyumbani ndo harudi tena.

Kesho yake watu wanaenda kulipa faini na mahari.

Biashara ya "Will you marry me" na goti juu wapi na wapi?
 
Mie nawapenda sana wasukuma kwa style ya proposal zao kama hizi

Anakubaka(kupondya), afu anakuja kwenu kujitambulisha
Anakutorosha(Kulehya) anakuja kwenu kujitambulisha
Anakuja tu kwenu from nowhere, humjui kumbe anakujua
Mme anachaguliwa na wazazi huko kilabuni
Na mara chache, mnakutana wenyewe kisimani, gulioni, mashineni, kilimoni, mnakubaliana anakuja kwenu

Goti la kupropose linatoka wapi?? Wanamme nao magoti yana grisi hadi wajikunje?

Wazee wetu walikuwa na akili sana aisee!!!!

Ndiyo maana ndoa ilikuwa ni taasisi yenye nguvu na imara sana.

Natamani wataalamu Wa socio-anthropology wagetufanyia tafiti na kuonesha jinsi copy & paste zilivyoharibu ndoa zetu za kileo.

Babu DC!!
 
He he he he, wavae mara ngapi??

Nilikutana na mzungu mmoja akawana anashangaa wamasai wanavyovaa viatu vyeupe afu wanajiita 'worriors'

Akaniambia 'viatu vyeupe kwa mwanamme viko kama kishoga zaidi"
Nakumbuka nilivaa kiatu cheupe (cha kuazima) wakati nikiwa fom foo. Tunaenda cheza muziki na Kibosho geloz, nisitinge mokasini nyeupe nichekwe? Kwenye soli imetiwa kichuma basi ni full kooo, kooo, kooo.

Sijawahi tena kuvaa kiatu cheupe, suruali ya njano na nyekundu na ndugu zao.
 
Wazee wetu walikuwa na akili sana aisee!!!!

Ndiyo maana ndoa ilikuwa ni taasisi yenye nguvu na imara sana.

Natamani wataalamu Wa socio-anthropology wagetufanyia tafiti na kuonesha jinsi copy & paste zilivyoharibu ndoa zetu za kileo.

Babu DC!!
Mkuu umenena. Ila waweza kuta na wataalam hao wenyewe pia ni wahanga wa hii makitu. Juzi kati hapa binamu yangu mmoja alinialika kwenye tukio la kuvishana pete na eti mchumba wake ambaye hata hajawahi kufahamika nyumbani. Kwa kuwa mi ni mstaaranu sikumkatalia direct bali nilijipangia ovataimu kazini.... ofkoz isiyo na malipo.
 
Naamini bado wapo ambao wanafikiria kama sisi.

Ngoja nimwite MwanajamiiOne atusaidie,

Babu DC!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom