Ombi Maalum Kwa JK!

Ombi Maalum Kwa JK!

LordJustice1

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
2,263
Reaction score
533
Mheshimiwa JK,
Wewe ni mtu mkubwa sana na kila unaloongea linapewa uzito unaostahili! Jana umedai kuwa "Mwanasheria maarufu, Tundu Lissu anachanganya Sheria na anawachanganya na wengina nao wanamwamini!"
Ombi: naomba Mhashimiwa JK utuambie ni Sheria ipi ambayo TL alichanganya na kuwachanganya wengine!

Nahofia kwamba inawezekana uliyejichanganya ni wewe kwa kutokujua Sheria!
Au unaposikia akina Jaji Werema anaporusha madongo huko Bungeni unaamini kuwa madongo hayo yana ukweli wowote! Hata hivyo ulituambia kuwa akili za kuambiwa changanya na za kwako! Kwa hiyo nilikuwa natarajia kuwa angalau za kuambiwa/kusikia ungechanganya na za kwako! Otherwise unajidhalilisha sana kuponda mtu ambaye ana-Practice fani ambayo hujui lolote au unajua kidogo kuhusu fani hiyo!
 
Ungeanza wewe kueleza hayo ambayo ame practise TL ambayo wewe unayaona muhimu, kama sivyo nawe ni kama JK kwa maana hoja yako haitoshelezi kutoa hukumu.
 
unapost angalau na wewe uonekane umepost. kinatusaidia nini hiki ulichopost?
 
Baada kuanza kuelewa huoni siku hizi hawatoki bungeni ??? Maana walikuwa wanatoka. Wanaomba kwenda ikulu !!
 
Shida tuliyonayo hapa Tz ni pamoja na kukosa washauri wakisheria waliobobea, ambao wanapaswa kumshauri Rais mambo ya kisheria, ndiyo maana anakurupuka kubishana na mtaalamu wa sheria aliyebobea.Huko ni kujidhalilisha mtu mzima,weka basi hicho ambacho unafikiri kimepotoshwa ama nawewe hukijui umeamua kuzungumza tu kwa vile Tundu lissu anawaharibia mambo yenu ya kupindisha sheria.Prezda kuwa muangalifu usipumbazwe na wanasheria wako uchwara,maliza muda wako ukapumzike kwa amani.
 
Ungeanza wewe kueleza hayo ambayo ame practise TL ambayo wewe unayaona muhimu, kama sivyo nawe ni kama JK kwa maana hoja yako haitoshelezi kutoa hukumu.

Mkuu ni kweli hujui mchango wa Tundu Lissu kwenye masuala ya kisheria au unafanana na mkubwa wako aliyetoa kali ya mwaka kuwa hajui kwa nini Tz ni maskini!

Kwa kifupi hii hoja inajitosheleza kumtaka JK atueleze yale aliyochanganya Mheshimiwa Tundu Lissu (sio kumhukumu kama ulivyodai wewe!)
 
unapost angalau na wewe uonekane umepost. kinatusaidia nini hiki ulichopost?

Wewe huoni kuwa JK huwa ana kinyongo kisichoisha na Tundu Lissu utafikiri kuna hidden agenda? Rejea kauli ya kwanza kabisa kuwa ni afadhali Dr Slaa kuingia Ikulu kuliko Tundu Lissu kuingia Bungeni! This is too low for our President kufanya personal attacks na mtu binafsi!
 
"Watanzania kunaogopa wabunge kupigana kwenye vikao vya bunge ni ushamba" hayo alisema Mwanasheria mkuu wa Chadema wakati alipohojiwa na mtangazaji wa Star TV wakati alipowasili mjini Dodoma tayari kwa kikao cha bunge.
 
Lissu ni reactionist, Much know ambaye 2015 asahau kurudi bungeni, wananchi wa Singida wamechoka naye hili analifahamu vizuri!
 
Mheshimiwa JK unajidhalilisha sana kuponda mtu ambaye ana-Practice fani ambayo hujui lolote au unajua kidogo kuhusu fani hiyo!

Na wewe mtoa maada unajidhalilisha sana kumponda raisi ambaye ana-practice uraisi ambao hujui lolote au unajua kidogo sana kuhusu uraisi sababu hujawahi kuwa raisi.
 
Mheshimiwa JK,
Wewe ni mtu mkubwa sana na kila unaloongea linapewa uzito unaostahili! Jana umedai kuwa "Mwanasheria maarufu, Tundu Lissu anachanganya Sheria na anawachanganya na wengina nao wanamwamini!"
Ombi: naomba Mhashimiwa JK utuambie ni Sheria ipi ambayo TL alichanganya na kuwachanganya wengine!

Nahofia kwamba inawezekana uliyejichanganya ni wewe kwa kutokujua Sheria!
Au unaposikia akina Jaji Werema anaporusha madongo huko Bungeni unaamini kuwa madongo hayo yana ukweli wowote! Hata hivyo ulituambia kuwa akili za kuambiwa changanya na za kwako! Kwa hiyo nilikuwa natarajia kuwa angalau za kuambiwa/kusikia ungechanganya na za kwako! Otherwise unajidhalilisha sana kuponda mtu ambaye ana-Practice fani ambayo hujui lolote au unajua kidogo kuhusu fani hiyo!
Si unamjua tena mzee wa mipasho? Naona kila aKilala lazima amuote TL
 
mipasho kwa jk ni jadi hatushangai wengi wa watu wa pwani ni maneno tu
 
Binafsi nilisikia raisi alipokuwa anasema hayo, kusema ukweli hata mie nilishangaa kwa maneno yake, Ni aibu kidogo kwa mtizamo wangu au angesema ni wapi ambapo TL aliwachanganya wengine lkn awe tayari kumpa nafasi ya 'kumwaga' vituzzz!
 
Wewe huoni kuwa JK huwa ana kinyongo kisichoisha na Tundu Lissu utafikiri kuna hidden agenda? Rejea kauli ya kwanza kabisa kuwa ni afadhali Dr Slaa kuingia Ikulu kuliko Tundu Lissu kuingia Bungeni! This is too low for our President kufanya personal attacks na mtu binafsi!
mkuu labda nikuulize, hii thead yako inatusaidia nini?
 
Back
Top Bottom