nyamalagala
JF-Expert Member
- Jun 5, 2016
- 744
- 673
Wana JF amani iwe kwenu wote.
Mimi ni kijana wa kitanzania,mwanafunzi wa Chuo Kikuu mwaka wa pili shahada ya elimu ambaye pamoja na mambo mengine nina ndoto ya kuwa mwandishi mahiri wa kazi za kufasihi ya Kiswahili.
Ikumbukwe kuwa wandishi wakongwe kama Ben R Mtobwa,Mulokozi,Kezilahabi ,Shafi A Shafi na wengineo waliitendea haki Jamii ya watanzania katika ulingo wa fasihi na tanzu zake hivyo nami ninawiwa kuendeleza dhima za fasihi na mwanafasihi kwa Jamii.
Katika kulitekeleza hilo nimetunga miswada kadhaa ya fasihi ya kiswahili na sasa mswada uliotayari kuchapishwa ni mmoja.Ili niweze kutimiza azma hii nahitaji pesa ya kugharamia uchapaji wa mswada huo.Tatizo kwangu ni pesa ya kugharimia uchapaji.Nimejikongoja kulingana na uwezo wangu nimemudu gharama za uhariri na kupata ISBN.Hatua iliyobaki ni kuanza uchapaji lkn mfuko hauruhusu.
Ombi langu kwenu wadau wa JF na wapenda fasihi ya kiswahili ni ufadhili ama msaada wa namna yoyote ili kufanikisha ndoto yangu.Chondechonde wadau niko mbele yenu kuomba msaada mtakaoona utanifaa ili kutimiza azma hiyo.Yawezekana kukawa na mtu anayejihusisha na uchapaji ama anamiliki kampuni ya uchapaji na nitakuwa tayari kushirikiana nae kwa makubaliano baina yangu na wao ili kufanikisha ndoto yangu.
Naomba kuwasilisha ombi langu kwenu.Asante.