Ombi kwa mwanakijiji "Hadithi zako" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ombi kwa mwanakijiji "Hadithi zako"

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Buswelu, Sep 21, 2008.

 1. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Habari za jioni Wana JF

  Kwa wale ambao hamfahamu mwanakijiji zaidi ya kuandika mambo mengi ya kisiasa na kiuchumu ni mtunzi mzuri wa hadithi,mashairi..yanayo wenza kuwekwa kwenye Jukwaa la mahusiano na kuwa funzo na faraja kwa wasomaji...Tena anataja sehemu ambazo ukiwa unasoma unapata picha kamili ya eneo lile...

  Mwaka 2006 ndio nilianza soma hadithi zake lakini kwa sasa sizioni tena kama ziko mpya..kama unaweza mwanakijiji please naomba uwe unatuwekea jamvini au tuwekee link ya moja kwa moja kwenye KLH new tuweze kuzi access ile ya awali ya pic & doc sasa naona haifanyi kazi..s

  Sehemu ya member log in nayo haionekani..
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Sep 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  bila ya shaka Buswelu, sijakusahau ndugu yangu. kuna kazi karibu tatu ziko mbioni pamoja na maendelezo ya riwaya wa "Ufalme wa Tandu". So, natumaini mwishoni mwa juma hili mojawapo itakuwa tayari. Thank you for your support.
   
 3. C

  Choveki JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2008
  Joined: Apr 16, 2006
  Messages: 448
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ndugu Buswelu kama utakumbuka humu ukumbini kulikuwa na kona maalum ya Kiswahili. Hapo mengi yalikuwa yakiandikwa, kutungwa, kuulizana na kuelimishana kuhusu LULU yetu ya taifa yaani Kiswahili chetu. Ila, kwa sababu ambazo hadi leo sijazielewa na nadhani sitazielewa waungwana wenyewe waliamua ati ile kona ya kiswahili na zile hadithi, mashairi na kufahamishana vizuri kiswahili hakukuwa na umuhimu wa kutosha hivyo ikapigwa panga!. Kwa sasa ukihitaji vitu vya kiswahili, kama mashairi, hadithi, nk inabidi kwanza utafute darubini halafu ndo uingie huko kwenye kona ya elimu. Kama una bahati na ni mvumilivu wa kutosha utaambulia utunzi mmoja au tenzi mbili ama kiji hadithi, kama si mvumilivu utatoka kapa.

  Nakumbuka wengi wetu tulilalama sana na kuomba huo ukumbi urudishwe. Nakumbuka hata Mwanakijiji alikuwa kati ya wanaharakati wa kuomba ukumbi urudishwe ilakwabahati mbaya haukurudishwa na hutukuambiwa sababu, hii iliniacha nikumbuke forum za miaka ya nyuma na ambazo vitu kama hivi vilikuwa vinatokea bila ya wadau kujulishwa au kupewa sababu.


  Ahsante.
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Nadhani Buswelu.. utarudi sasa..!
   
 5. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mzee, hili ombi bado lina maana yake yote leo, miaka tatu baada ya buswelu kulitoa. sijui bado uko busy na "maendeleo ya riwaya ya ufalme wa tandu" au ndio umeamua kutunyima kabisa... Nadhani wanajamiiforum wengi watakubaliana na mimi nikisema we miss it all.
  wengine tuna furahia sana tukisoma creations zako, hata za zamani, ila sasa tumezisoma hadi tumezi-memorize. Kama kuna ka blog, au ka site unako zipost, tunaomba utupe link tafadhali.
  Asante sana.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Nitawaomba support yenu very soon; niko natafuta publishers.. editors wangu ndio wamepitia draft ya kwanza ya hadithiya kusisimua ya ambayo kwa wakati huu jina lake sitoweka wazi; siku ikiwa tayari kiwandani (kwa ajili ya uchapishaji) nitaweka sehemu yake hapa kuonjesha. Ni matumaini yangu wapenzi wa hadithi zangu pote duniani hawatosita kununua kuunga mkono ili hatimaye masimulizi karibu hamsini ambayo hayajawahi kuchapishwa niweze kuyaleta kwenu na hatuwezi kujua yumkini twaweza hata kuingia katika filamu. Wanasema subira yavuta kheri, wengi mmesubiria sana inshallah subira hiyo italipa.

  Asanteni kwa uvumilivu.
   
 7. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Asante mzee, tunasubiti kwa hamu...
   
Loading...