Ombi kwa Mhe. Rais: Ikikupendeza mkoa wa Mtwara uongozwe na Mwanajeshi

Jasusi Mbobezi

Senior Member
May 17, 2020
195
851
Kwanza nakupongeza kwa namna unavyojituma kuitumikia nchi kwa moyo wa dhati na nakupa pole kwa matusi unayolipwa na baadhi ya Watanzania. Hata Yesu alijitoa kwaajili ya wanadamu na hawakusita kumsulubisha kwa aibu, ndivyo tulivyo mzee wangu ila we fanya kazi, Mungu atakulipa.

Nirudi kwenye mada, ninapendekeza ikikupendeza, mkuu wa mkoa wa Mtwara pamoja na wakuu wa wilaya watoke kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, sina maana kuwa waliopo hawafai, ila napendekeza ikiwezekana wahamishiwe sehemu nyingine.

Pia, napendekeza mkoa mzima wa Mtwara iwe ni lazima kila anayepokea mgeni kwenda naye kwa mjumbe na kumtambulisha na yeyote atakayekiuka achukuliwe hatua kali za kisheria.

Pia, napendekeza uwachunguze viongozi wote kuanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka juu kabisa mkoani Mtwara, naamini hakuna mgeni anayeweza kuja na kutekeleza uhalifu bila kuongozwa na mwenyeji.

Mwisho nasikitika sana kuona baadhi ya watu hapa JamiiForums wanafurahia vitendo hivi wakishabikia kuwa haviwezi kukomeshwa, nakusihi hata usijibishane nao, Mungu alietusaidia katika kipindi cha CORONA atusaidie katika hili, aviongoze vikosi vya askari wetu kushinda kwa kishindo kama alivyo washindia watu wake katika nyakati zote.

Mungu akubariki sana mzee wangu, watakusaliti wote ila kamwe Mungu hatakusaliti. Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe juu yako, sasa na hata milele Amen.
 
Shida unatoa maoni bila kujiridhisha hao viongozi ni kinani na status zao ni zipi hata kabla hawajafika hapo unapowaona.

Bwana mdogo utulie tu,ama jipatie home work utakuja kufuta uzi wako.

Huko mtwara hata uweke raia wake wawe wanajeshi bado hakuondoi tatizo.

Kimsingi IGP amekuwepo huko achilia mbali vikosi vingine,naamini wanafanya kazi zao kwa weledi kudhiti hao waharifu.
 
Back
Top Bottom