Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Taarifa ya kutoonekana kwa mfanyabishara aliyekuja kubainika kuwa ameuawa ilichukua muda mrefu Sana. Ndugu kwa maelezo Yao walifuatilia suala la ndugu yao ngazi tofauti. Zipo kamati mbili ambazo ni muhimu sana kuwa na updates za matukio yanayotokea. Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Mtwara Mjini ambayo ipo chini ya Mkuu wa Wilaya na Mmoja na Mmoja wa watuhumiwa ambaye ni OCD ni mjumbe Kwenye hiyo kamati. Je kamati DC na wajumbe wake walipata Lini taarifa ya tukio hili? Waliwajibika au walipuuza? Kama awakufanya kazi Yao kamati ya Mhe. Waziri Mkuu itawaacha salama?
Kamati ya pili ni kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa ambayo RPC ni mjumbe na Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti. Je hapa mkuu wa mkoa anawezaje kuchomoka mahojiano? Kama kamati yake haikuwa na taarifa aiwezi kutoa doa ufanisi wa kamati Hii? Je, zipo athari zinazoweza kumpata RC Kwa sakata hili?
Nauliza haya maswali Kwa maana uzoefu wa tume za kijaji Huwa na wigo mpana sana Kwenye uchunguzi. Tungekuwa na Tum ya kijaji maana yake kila aliyepaswa kuchukua hatau angewajibika.
Mwisho, kamati anaweza kuwahoji watuhumiwa ambao tayari wamefikishwa Mahakamani? Ushahidi wa tume una nafasi Gani kisheria Mahakamani au umejikita Kwenye madhaifu ya Watumishi wa Umma pekee?Tukumbuke tume inatumwa wakati timu ya wapelelezi imeshapita Kila Kona na hata askari aliyejinyonga tayari Polisi wameshaconclude Kwamba amejiua na hivyo kwao hakuna Cha Zaidi Cha kufanya.
Je, fedha zilizoporwa Kwa marehemu zimerejeshwa au ndizo zinatumiwa na watuhumiwa kugharamia mawakili wao? Kama zimerejeshwa means watuhumiwa walikiri?
Tuishi ndugu zangu, tuache kutoa nafsi za watu Kwa lengo la fedha au madaraka. Tusifike mahali tukasimama kutetea wauaji maana ipo siku watanogewa na kuamua kuondoa nafsi za watu wa karibu