Ombi kwa Kikwete: Pangua timu yako ya usalama...

Mkuu MM JK hawezi kufanya hivyo kwani kuna watu wengi wako kwenye waiting list ya kung'olewa meno na kucha na si ajabu na wewe umo.

mkuu umeniwahi inshort next move ni kuthreat jf kwa kuwatenda wamiliki na wake wanaoneka vinara wa kuipinga serikali.let cross our finger that not to happen.coz itakuwa disaster.guys we are not safe anymore
 
Upo umuhimu mkubwa kuvifanyia marekebisho vyombo hivi ili viwe vya kisasa, pia kuchagua viongozi wenye sifa, sifa siyo vyeti tuu bali na uwezo na record zilizotukuka...pili tunaweza kuwa na shida ya mawasiliano bora na ya haraka kati ya vyombo hivi, utoaji wa taarifa zisizo sahihi, UWEZO wa wakuu wa usalama kumshauri rais bila kumuongopea/kumuogopa...wanasiasa waache kuvitumia vyombo hivi vibaya..chaguzi mbalimbali nyuma ccm wamekuwa wakitumia udini kama 'turufu' ya kushinda, walianza na cuf na leo wako na chadema 'mfumo Kristo', bila kupima matamshi haya yatachukuliwaje na wenye dini yao.. Vyombo vya usalama vipime ukubwa wa athari na vichukue hatua kuiondoa kabla...na njia rahisi ni JK kukiri kutumia dini 2010, watz tutamwelewa ndiyoo mbona aliki kutumi police
 
mheshimiwa ,umeandika vzr saana lengo likiwa kuitakia mema Tanzania na watanzania. kwangu mimi tatizo ninaloliona ni USALAMA[TISS] kuacha kufanya kazi zake kitaalamu[weledi] na kuamua kujigeuza kuwa POLISI, kwa kuwa wao wako karibu saana na rais, wamewezeshwa kupewa kila kitu kihusucho USALAMA hususani shughuli za POLISI huku wale wenye jukumu na utaalam wa kutekeleza majukumu ya usalama wa raia na mali zao, wakiachwa bila kuwa na zana bora na mafunzo ya mara kwa mara kwa ajiri ya kukabiliana na teknolojia inayobadilika mara kwa mara. polisi wametekwa na TISS kwa kilemba cha NGUVU YA PAMOJA yaani kufanya kazi kwa kushirikiana , hapa ndipo kosa la kiutendaji linapoanzia, ni bora TISS wafanye kazi zao kwa utaalam wao na zile wananzoona zinapaswa kuwasilishwa POLISI waziwasilishe kwa ufuatiliaji wa kina na kiuweledi. POLISI wapatiwe mafunzo ya mara kwa mara , motisha na dhana bora za kazi kulingana na maeneo yao ya kazi . mf; Dar es salaam imepanuka saaana kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na golf gari ndogo za doria maeneo mbalimbali ya jiji kama zamani, mbwa wa kisasa kwenye magari, farasi , vtuo vya polisi kulingana na ukubwa wa jiji hivi sasa ,yote haya yanawezekana endapo tu TISS watakaa pembeni na kujipanga na nini?wao kama wao wanahitaji nawapongeza saaana TPDF wao wamekataa kuingiliwa na idara hii , vinginevyo nao mambo yangewaharibikia .
 
kupangua hakusaidii kikubwa arudishe mfumo uliokuwepo.. usalama ilikuwa idara huru ila yy kaifanya mali yake na majambaz

Siku hizi hao wadudu sitaki hata kuwasikia ....nimekuwa nikijiuliza sheria za usalama zimebadirika lini.....sheri iliyounda hiyo idara inavyo-state ni tofauti na yanayoendelea ....nitarudi kwa mifano ya some proviso za hiyo sheria
 
Kwa taifa ambalo ni ambitious,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kiakanda(regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi.TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni more sophisticated katika kufanya information sharing wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama Mkakati waq ulinzi na usalama wa Marekani,Uingereza,Pakistan,Is rael,Afrika Kusini,China,India na Canada

Ingawa miakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekua sensitive zaidi kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa(Power Interests) lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe ambitious na kwa kuanzia ni lazima tungeanza na kanda yetu ya Maziwa makuu,Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na power struggle hapa east afica ambao ni Kenya.Hatujaweza vya kutosha kwenye Economic intelligence kule Kenya inagawa wao wamewekeza hapa kwetu.Leo hii Kenya ina-export TANZANITE,Wana-Export gold n.k.Balance of trade kati ya Tanzania na Kenya ni subject of Economic intelligence.tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiinteligesnsia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie possible scenarios na move za washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi hapa EAC au ukanda kupitia economic power house(Kenya) katika ukanda huu?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu yetu.Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekua zikinunuliwa kwa wingi na kuwa smuggled kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi wetu na ku-frustrate fisical na monetary policy zetu?
Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe modern zaidi
Malengo ya TISS kulingana na trend ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri(si utabiri wa majini/tunguri bali utabiri wa kisayansi),Kupenya,na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu,na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye Nyanja za kimataifa(jamii nyingine)

Malengo makuu yanatakiwa kujikita katika

Mosi,Kuongeza nafasi na umuhimu wa idara ya mahakama na vyombo vya kutoa haki.Lengo hapa linatakiwa kuwa juu ya kuunganisha idara za mahakama,wizara ya mambo ya ndani na vitengo vyake kwa kuzingatia upeanaji wa taarifa huku haki za msingi za kiraia zikilindwa pamoja na uhuru wake tofauti na ilivyo sasa ambako TISS inatuhumiwa kutumika kuhujumu haki za kiraia kwa visingizio lukuki.Lengo kuu liwe kulinda haki na uhuru wa watu bila kuathiri maslahi ya jumla.Hili linahitaji ushirikiano kuanzia serikali kuu,mikoa,wilaya,majimbo ya uchaguzi,kata na hata ngazi ya mitaa pamoja na sekta binafsi

Pili,Utengenezwe utamaduni mpya wa kuahamasisha mawazo mbadala na matumizi ya weledi(professionalism/expertise):Kubadili utamaduni ndani ya TISS ni muhimu sana ili kuepuka mimosa ya kimkakati. It is necessary to create an intellectual culture that promotes discussion as well as dissenting opinion. It will require the use of collaborative technology, where subject expertise is maximized, increased cross-agency communication, and the exploration of alternative analysis

Tatu,Kurahisisha zaidi ukusanyaji wa taarifa za kintelijensia:TISS haina budi kuwa mbele katika matumizi ya teknolojia na pia ku-update wataalamu wake kitaaluma na katika matumizi ya zana za kisasa zaidi ili kurahisisha ukusanyaji huo kutoka Open-sources na kutoka Human-sources

Nne,Kuajiri watu kulingana na uwezo na taaluma zao na pia kuajiri watu ambao tayari wana ajira kwenye vitengo vingine lakini walipwe vizuri kwa ajili ya kazi ya usalama ili kupunguza gharama za kupachika watu wapya katika idara,mashirika na taasisi nyeti nchini.Pamoja na hili kitu cha muhimu watu hawa ni lazima wawe na sifa zinazofanana (common attributes) katika ujanja,uwezo wa hali ya juu na haraka katika utendaji huku maadili ya juu kabisa katika vigezo vya utendaji katika idara hii vikizingatiwa

Tano,TISS ibadili utamaduni wa kuhitaji-kujua kwenda Kuhitaji-kutoa taarifa(changing from the culture of need-to-Know to need-to-share):Ili kuongeza ushirikiano na ufanisi katika kila ngazi ni lazima mtazamo wa idara hii ubadilike na suala la kutoa taarifa liwe ndiyo njia kuu ya kufanikisha malengo ya idara katika ngazi zote kwa hiyo kuna haja ya kuangalia jinsi taarifa zinavyofika kwa ubora unaotakiwa,kwa usahihi na kwa muda muafaka na hili ni muhimu na litasaidia zaidi kuwa karibu na watunga sera(policy makers)

Sita,Kuimarisha na kupanua zaidi uhusiano kati ya TISS na washirika wa ndani ya nchi na vitengo vingine vya kijasusi vya mataifa ya nje:Hii ni kwa kuwa tunaweza kuwa na common threats kwenye uchumi,kiitikadi,kiutamaduni,k iulinzi n.kHata hivyo taarifa za kijasusi kutoaka kwa washirika wetu ni lazima ziangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na pia tuwe na taarifa zetu ambazo tunaweza kulinganisha na taarifa za washrika wetu.Hizi kwa kijasusi zinaitwa 'Corroboration codification'
Saba,kitengo kidogo kabisa cha mwisho ndichokinachotakiwa kuwa na acces ya taarifa nyeti lakini kitengo hicho kiwe scrutinized kwa hali na mali.Hata hivyo nitajadili kuhusu juu ya mfumo wetu mbovu wa counterintelligence

Nane,Kujenga mfumo ambao ni uniform zaidi katika utekelazi kisayansi na kiteknolojia,Ni lazima sasa idara iwe centralized katika kutoa maelekezo na iwe more decentaliced katika utekelezaji kwa mtindo ambao unaitwa 'pyramid execution'.unified research itumike ili kuongeza ushirikiano na idara mbali mbali

Tisa,Mfumo wa kupongeza na kuzawadia utumike kuongeza performance

Kumi,mtindo wa kutumia miongo utumike lakini zaidi kwa haraka mtindo wa kutumia siku utumike badala ya miaka.Kwa mfano 720 days plan itumike badala ya miaka 2,180 days pla itumike badala ya 6 months plan kwa ajili ya monitoring na kuepuka urasimu na uvivu usio wa lazima

Pia ni vyema kutokana na power struggle ya ukanda tuunde vitengo vya ujasusi vya nje.kitengo hiki kifanane kwa muundo ingawa kutakua na marekebisho kidogo lakini kifanane na kitengo cha RAW cha india ambacho kiliundwa baada ya vita ya India na China.kabla ya hapo kulikua na kitengo cha IB ambacho kilikua na miaka 120 lakini hicho kilitumika kuchunguza watu zaidi na taasisi za kisaiasa.waingereza walikitumia kuwachunguza akina Mahatma Gandhi,Azad na Nehru zaidi.Kitengo cha RAW kinatumika kwa ajili ya military Intelligence na financial intelligence.Kuna haja ya kupima maofisa ubalozi wetu wanaopelekwa nje pamoja na Mwambata wa jeshi katika balozi zetu(defence attaché) kulingana na sera yetu.

Kwa bahati mbaya sera yetu ya mambo ya nje tumeipigia kelele sana ifumuliwe.Naamini Mungu akitupa uhai CHADEMA itakuja na sera bora zaidi ya mambo ya nje specifically kwa regions na strategic partners
 
Nimeipenda michango yenu MMM, Lufungulo na Ben Saanane.

Ipo hoja nzito katika mada hii. Hatuwezi tukazungumzia uimara wa nchi katika eneo lolote kama hakuna usalama wa raia au hakikisho wazi la usalama wa raia.
 
Mkuu Mwanakijiji,

So far according to my knowledge naamini katika viongozi wa ngazi za uraisi hapa nchini; ambao wameongoza kwa kupangua na kupanga Rais J.K. anaongoza; So far haijasaidia kitu katika entities husika... Kupangua siyo suluhisho kama bado watakaopangwa wana sifa zile zile za waliopanguliwa tena chini ya uongozi ule ule. He should definitely do something... But kupangua ain't the answer from the looks of things.

Inawezekana; lakini mara ya mwisho Kikwete kupangua uongozi wa Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa ilikuwa lini?
 
Much respect mzee mwanakijiji kwa idea zako but ujue tu kua hivi ilivyo ameshapangua na kuiweka vile yeye anaona inamfaa.. una mawazo mazuri kama watanzania wengi walivyo but mawazo mazuri kwa serikali kwa sasa ni yale tu yanayoisaidia kupunguza critics na kuficha uozo wote.
 
Inawezekana; lakini mara ya mwisho Kikwete kupangua uongozi wa Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa ilikuwa lini?

Kwa vyombo hivyo viwili haondolewi mtu hapo kwani hao ni mahsusi kwa ajili yake binafsi na siyo kwa usalama wa nchi na raia wake, kuwagusa hao ni sawa na kuigusa mboni ya jicho lake, wakosoaji wengi wa himaya ya JK wajiandae kukutana na madhila kama yalyowakuta Dr. Ulimboka, Mwangosi, Kubenea na sasa Kibanda.Tanzania kuna uhasama wa taifa badala ya Usalama wa Taifa.
 
Inawezekana; lakini mara ya mwisho Kikwete kupangua uongozi wa Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa ilikuwa lini?

Kwa mtazamo wangu... Siamini kuwa inajalisha ni lini Kikwete alipangua uongozi wa Jeshi la Polisi na usalama wa Taifa. Hapa inachojalisha ni kuwa tokana na viashiria vya utendaji wake - kupangua siyo suluhisho. I bet kabisa with confidence hata akipangua; hao atakao wapanga na wale waliopanguliwa watatofautiana majina tu ila utendaji utakuwa ule ule.
 
Ili uwezekutatua tatizo kwanza unatakiwa kujua source.sio kupangua tu huyu juha aliye kuwa ikulu hajui hata kwanini nchi yetu ni masikini. Na hakika hajui kwanini ualifu unaongezeka
 
watu bwana wanachekesha kweli, mara hivi mara vile. wengi wenu hamuijui TISS mnagusagusa na kubahatishabahatisha tu!. ukiwa hujui jambo nyamaza. mwanakijiji hujui lolote kaa kimya!
 
Nakushukuru sana mkuu MM kwa maoni yako mazuri lakini naamini kabisa muhusika wa kufanya mabadiliko hayo unayoyaongelea hawezi fanya hivyo kabisa kwa sasa kwa sababu kadha wa kadha. Mimi nilishawahi wauliza viongozi wa CDM kuwa wamejiandaaje na kubadilisha mfumo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama pindi tu watakapopewa ridhaa na wananchi ya kuongoza (sikutegemea majibu yao kuwekwa hadharani kwani najua ulinzi na usalama ni swala nyeti na si la kuliongelea ama kuliweka wazi hovyo hovyo hasa mfumo unaotegemea kuutumia,ila mimi nilikuwa na wakumbusha na ntaendelea kuwakumbusha juu ya kujiandaa katika swala hili kwani bila kulifanyia kazi kwa maandalizi mazuri ambayo naamini yanachukua muda mrefu sana katika suala hili. Na mwito huu napenda hata kuutoa kwa wale wote amba wanasaka kupewa ridhaa na wananchi ya kuwaongoza kuanza kujipanga mapema kuhusu suala la mfumo wetu wa idara za ulinzi na usalama. Bla ya kuwa na mfumo bora na wa kisasa ambao utapelekea idara hizi kutenda kazi kwa ufanisi mkubwa,basi tusitegemee maendeleo yoyote kwa nchi yetu.
Huyu jamaa wa sasa hawezi kukimbia kivuli chake mwenyewe hasa kwa huu muda wa miaka miwili na ushee,sasa kilichobaki ni kwa wale wanaojiandaa kupokea kijiti kufanya maandalizi ya kuwa na ulinzi na usalama wa taifa halisi,thabiti na madhubuti kwa ustawi wa Tanzania yetu.
 
Seems like vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania vina-operate kama bado viko kwenye zama za Cold War, havijabadilika kwendana na threats/mahitaji ya karne ya 21.
 
Nimeandika mara nyingi sana katika miaka hii karibu sana juu ya tatizo la Usalama wa Taifa na haja ya kufanyia mabadiliko makubwa muundo wa Jeshi la Polisi. Baadhi ya mapendekezo yamewahi kufanyiwa kazi (kugawa Dar katika Kanda za Kipolisi mfano mmoja).

Hata hivyo kinachoendelea sasa hivi nchini ni ushahidi kuwa uongozi wa sasa wa vyombo vya usalama umeshindwa kuhakikisha usalama; ni dhaifu na unatishia hali ya usalama wa taifa. Naweza kutoa mifano ya mambo kadha wa kadha lakini nitakuwa narudia yale ambayo tayari watu wanayajua.

Kuchelewa kwa Rais Kikwete kupangua vyombo vya usalama na kuleta watu wapya wenye maono na mawazo mapya na wenye uelewa sahihi wa changamoto za taifa ni kujaribu kusubiri majanga makubwa zaidi mbeleni. Kuibuka kwa mauaji ya Albino tena na kuendelea kwa vitendo vya utekaji nyara na mauaji ya watu mashuhuri au yale ya kisiasa ni dalili kuwa tulipofika ni pabaya na tusipoangalia itakuwa vigumu sana kurudi kutoka hapa.

Pangua vyombo vyako vya usalama Rais Kikwete; SASA. Vinginevyo taifa litalia zaidi ya sasa.

MMM
hawezi kuipangua yanayo tekelezwa ni matakwa ya rais na chama!
 
Mkuu Mkjj, huyu hata apangue timu mara ngapi hakutakuwa na jipya lolote maana kama walivyosema waswahili "la kuvunda halina ubani" kashinikizwa na Bunge kupangua safu yake ya Baraza la Mawaziri na kuwatema akina Mkullo, Ngeleja na wengineo lakini utendaji wa Baraza lake hilo hauna tofauti yoyote ukilinganisha na kabla ya kulipangua. Tatizo ni DHAIFU anaweza kupangua timu kila mwezi lakini kama mwenyewe ni DHAIFU basi Watanzania hatutaona ahueni yoyote ile. Kumbuka maneno ya Dr Slaa, "Kumchagua Kikwete katika uchaguzi wa 2010 ni janga la Taifa" Dr Slaa hakukosea na sasa tunaliona janga la Taifa kila kukicha.

Nimeandika mara nyingi sana katika miaka hii karibu sana juu ya tatizo la Usalama wa Taifa na haja ya kufanyia mabadiliko makubwa muundo wa Jeshi la Polisi. Baadhi ya mapendekezo yamewahi kufanyiwa kazi (kugawa Dar katika Kanda za Kipolisi mfano mmoja).

Hata hivyo kinachoendelea sasa hivi nchini ni ushahidi kuwa uongozi wa sasa wa vyombo vya usalama umeshindwa kuhakikisha usalama; ni dhaifu na unatishia hali ya usalama wa taifa. Naweza kutoa mifano ya mambo kadha wa kadha lakini nitakuwa narudia yale ambayo tayari watu wanayajua.

Kuchelewa kwa Rais Kikwete kupangua vyombo vya usalama na kuleta watu wapya wenye maono na mawazo mapya na wenye uelewa sahihi wa changamoto za taifa ni kujaribu kusubiri majanga makubwa zaidi mbeleni. Kuibuka kwa mauaji ya Albino tena na kuendelea kwa vitendo vya utekaji nyara na mauaji ya watu mashuhuri au yale ya kisiasa ni dalili kuwa tulipofika ni pabaya na tusipoangalia itakuwa vigumu sana kurudi kutoka hapa.

Pangua vyombo vyako vya usalama Rais Kikwete; SASA. Vinginevyo taifa litalia zaidi ya sasa.

MMM
 
Mkuu unadhani akiwapangua hao usalama,watu wanaoikorofisha serikali hawataendelea "kushughulikiwa"?
 
Back
Top Bottom