Ombi kwa Gen Davis Mwamunyange: Acha kulitia aibu Jeshi letu (JWTZ)

Status
Not open for further replies.

HNIC

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
1,898
2,195
Kila siku humu tunamsema JK na mawaziri wake na wanasiasa wetu lakini naona leo tugeukie hawa jamaa wetu wa ulinzi na usalama. Kuna hali ambayo inanipa wasi wasi sana na sijui kinachoendelea pale Upanga (makao makuu ya jeshi) lakini I do not like what I see. Na naamini mpaka sisi wengine tumeona inamaana kuwa kuna tatizo la kikazi na uwajibikaji na inaonekana kuwa kuna tatizo kubwa zaidi hapo kwa Ndugu Mwamunyage.

Tulipokuwa wadogo ilikuwa huishi kuona ham ya kuwatazama wanajeshi wetu kwenye ceremonial parades. Nchi za wenzetu wameendelea zaidi kwani pale wanajua dunia nzima itakuwa inatazama hivyo watadiplay kila kitu kuanzia vifaa vya kijeshi mpaka nidhamu ya wanajeshi kwenye kutemebea, kukimbia na kila kitu. Leo hii nimeshangazwa sana kuona wanajeshi wetu kuvalishwa nguo OVERSIZE, viatu OVERSIZE, KOFIA OVERSIZE na kwa kuwatazama body language yao wanaonekana wanajeshi wetu wako demoralized na wako out of place kabisa. Wanaonekana hawana afya na hawapendezi hata kidogo.

Is this the best we can do? Nijuavyo wanajeshi ndio wanatakiwa kungoza kwa nidhamu ya kila kitu including kuvaaa...

Nimesikitishwa sana na aibu hiii na nasema wazi kama kuna institution naiheshimu ni JWTZ lakini kwenye hili siko pamoja na mkuu wa Mjeshi Gen Mwamunyange. Hii inamaana huko jeshini hakuna nidhamu na hakuna accountability na kila mmoja anamdharau mwenzake

Labda JWTZ wangekuwa wazi (YES JESHI WANATAKIWA KUTEKELEZA OPEN GOVT INITIATIVE YA KUWEKA WAZI NANI ANALIPWA KWA KUFANYA NINI BILA KU COMPROMISE NATIONAL SECURITY) na kuweza wazi nani wamepewa hizi tenda za UNIFORM ambazo ziko oversize na mavatu ambavyo hayaendani kabisa na nguo zao

IMG_7941.jpg


IMG_7949.jpg



This is un acceptable kijeshi na ki nchi

Heads must roll huko Jeshini.

tazama wenzetu walivyosmart:

1557559_968398643188689_161705344295554902_n.jpg



size0.jpg



_47371021_china_afp766.jpg
 
Dah Ee bwana ehh! Utadhani enzi za mkoloni.Buti limevimba hilo,na kofia zimewavaa.

Hii ni kuonyesha sasa serikali ya CCM imeamua kulidharau hata jeshi letu kuwa wape tuu hayo manguo watafanya nini? Sio ajabu hivyo viatu walipewa magazeti ya zamani wajaze huko mbele ili visichomoke wakati wa gwaride.
Hizi dharau hizi! Sijui siku wakielewa kuwa wanadharauliwa wata amuaje!
 
Kwani ww ni mwanajeshi? Si hawa wanajeshi ndo wanatumwa na ccm km mbwa kupiga raia wasio na hatia? Sasa hbt za mavazi yao zinatuhusu nn wkt wazee wetu huko vijijini hawana mavazi wanategemea mashati na fulana za ccm kila baada ya miaka mitano
 
Labda waliazima sare tu mkuu, utakuta ni size kubwa ya wadachi au jerumani. ni shida ya kuazima maana kama unatengeneza iweje utengeneza kubwa kuliko wavaaji
 
Kweli hata mmoja nimemuona katika gwaride kiatu kilikuwa oversize kabisa.
 
Hii ni kweli.....JWTZ ndio taasisi pekee tunayoiamini.....ibaki hivyo.....
 
Good observation!! Nakubaliana na mleta mada. Hili jeshi wanaofaidi ni wakubwa. Wao wanapimwa nguo na viatu. Kwani kiwanda cha pale chang'ombe kilicho chini ya 511kj kimeacha kushona sare za jeshi?

Waliobaki wanatupiwa tu kama CCM inavyowatupia ma-tshirt wasio na akili ili wawape kura.
Hahahahaaa!
Lilishadharaulika zamani kwa kutokusimama kiume wakati watu wakigawana rasilimali zao.
 
Good observation!! Nakubaliana na mleta mada. Hili jeshi wanaofaidi ni wakubwa. Wao wanapimwa nguo na viatu. Kwani kiwanda cha pale chang'ombe kilicho chini ya 511kj kimeacha kushona sare za jeshi?


KUna uwezekano mkubwa hiko kiwanda watu washagawana Vyerehani na vifaa vingine na kwa sasa UNIFORM zote zinatoka CHINA, na tenda kashapewa SINGASINGA.

Hizo tunaita NYELA HUMO HUMO!
 
Hao askari wenyewe nao nikama ma-reject halafu wanaonekana wana hali ngumu sana hao hata panya akitokea apo watakimbia wote!
 
duuu well said mkuu and.hongera kwa kuliona hili hope watalifanyia kaZ
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom