Ombi: Ile barabara ipitayo baharini nyuma ilipokuwa Ikulu Dar ifunguliwe tupate kupita Wananchi kama zamani kuepusha mzunguko

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kwanza naipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuhamia Dodoma.

Hivyo naimani Ikulu ya Dar Itabaki kuwa Ikulu ndogo kama zilivyo Ikulu zingine za kila mkoa.

Kwahiyo tunaomba wenye mamlaka; endapo itawapendeza jaribuni kutufungulia ile barabara sisi wananchi angalau kama ilivyokuwa awali.

Sote ni binadam! Sioni sababu ya kuendelea kuifunga hiyo njia kwasababu kama kuna magaidi wanaweza Fanya ambushi kupitia hata upande wa ocean road au upande wa chuo cha magogoni!
Hakuna sababu ya kufunga upande mmoja na kufungua upande mwingine! Kama ni walinzi wekeni doria huko baharini ikiwezekana jengeni mnara wa walinzi au boat ya walinzi ikae baharini! Lakini hiyo barabara waachieni RAIA wapite!
 
Ila wangeifungua tu. Tangu Jerumani, mwingereza, Nyerere, mwingine, nkapa, Jakaya haikuwahi fungwa. Hivyo kwa vile sasa ikulu kuu ipo Dodoma ni Vema serikali ikaifungua tu
 
Kwanza naipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuhamia DODOMA.

Hivyo naimani IKULU YA DAR Itabaki kuwa IKULU NDOGO kama zilivyo Ikulu zingine za kila mkoa.

Kwahiyo tunaomba wenye mamlaka; endapo itawapendeza jaribuni kutufungulia ile barabara sisi wananchi angalau masaa 12 ya mchana kama ilivyokuwa awali.
Ile imeshakua private road, sahau kuitumia. Hiyo barabara, hata mabeach boy hawasogei kipande hicho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom