Riwaya: Paspoti ya Gaidi

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,830
Riwaya: Pasipoti ya Gaidi part 1
Mtunzi: Richard Mwambe

Pasipoti ya Gaidi: Hujuma na Uzandiki

Sura ya I
Ikulu – Dar es Salaam

Saa 10:30 Alfajiri

Wakati giza likijiandaa kutoweka na kuipisha nuru ya asubuhi, miti yote ilikuwa imetulia kana kwamba kuna aliyeiambia ifanye hivyo. ni tausi mmoja mmoja aliyekuwa akilia alfajiri hii tena kwa nyakati tofauti. hawakuwa na zamu ya kufanya hivyo isipokuwa ilitokea tu, ndivyo walivyoumbwa. hawakuwa wakijua lolote linaloendelea katika maisha ya mwanadamu wakati huo, zaidi walisubiri kukuche waendelee kupendezesha mandhari ya eneo hilo. hawa walikuwa kivutio kikubwa sana katika eneo hilo kwa wapiti njia.

Hekaheka katika jengo hilo la makao makuu ya rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ilikuwa kubwa. vijana wa jeshi la polisi, kikosi maalum cha kutuliza ghasia, walikuwepo wakiwa kimejiweka tayari kwa lolote, ijapokuwa huwa hapo kwa lindo kila siku lakini leo hii walikuwa kivingine kabisa. mbali na wao, eneo hilo, afajiri hiyo lilizungukwa pia na vijana wa jeshi la wananchi waliovalia kombati zao za mabakamabaka, wakiwa na silaha nzitonzito mikononi mwao, kila mmoja akionekana kutingwa na shughuli inayompasa kufanya kwa muda huo. magari ya wagonjwa kutoka jeshi la wananchi yalikuwa yikifanya kazi ya kubeba majeruhi na maiti zilizokutwa ndani ya jengo hilo, hekaheka.

msemaji wa ikulu alikuwa kasimama katikati ya ukumbi mkubwa ndani ya jengo hilo, alikuwa kimya bila kusema lolote, macho yake yalijawa na machozi, midomo yake ilimwemwesa bila kutoa neno.

“samahani mzee!” sauti ilisikika kutoka nyuma yake, alishtuka kama mtu aliyekutana ghafla na mtoa roho, akageuka na kumtazama kijana aliyemwita. mzee huyo alijikuta anashindwa hata kuitikia ile salamu au kuuliza anamwitia nini, badala yake alimfuata yule kijana pindi alipoondoka eneo lile. moja kwa moja walifika kwenye ukumbi mdogo ambao ulikuwa na watu wasiozidi sita, yaani wale wenye vyeo vya juu, wenye dhamana ya ulinzi na usalama wa nchi, pamoja nao kulikuwa na wasaidizi wengine ambao ni maofisa wachache wa ikulu. akaketi katika kiti kilichokuwa wazi, akiwatazama watu hawa kwa zamu, pamoja nao alikuwapo mtu mwenye cheo cha pili kutoka kile cha mkuu wa nchi.

“kama mnavyoona… maofisa kadhaa na wafanyakazi wa ikulu wameuawa,” makamu wa rais aliliambia jopo, “kilichotokea hapa hakieleweki, hakuna anayejua nini kimetokea, ila mke wa rais yaani first lady ametoweka, nafikiri, kwa uwazi kabisa kuwa huu ni uvamizi lakini sijui ni nani au siwezi kuhusisha na kikundi gani kwani uchunguzi ndio kwanza umeanza,” akatulia kimya bila kusema lolote. macho yake yalionekana wazi kutona kwa machozi ambayo hayakutaka kumwagika.

“bila shaka, inawezekana walidhamiria kumteka au kumdhuru rais mwenyewe, walipoona hayupo basi wameondoka na mkewe, first lady. kumbukeni, ikulu ya tanzania ni kati ya majengo machache duniani yanbayolindwa kwa mitambo ya hali ya juu na wanausalama waliokomaa kwenye fani yao, lakini kama tumevamiwa, bila shaka, waliyovamia ni kundi lenye weledi wa juu zaidi katika medani hii ya usalama,” waziri wa ulinzi aliongezea na wajumbe wote wakatikisa vichwa.

“tumepoteza vijana wetu makini kabisa ambao waliaminiwa sana na mkuu. taarifa nimeshamfikishia, na amekatisha ziara yake, anarudi nyumbani kwani hali hii si ya kuvumilika, tunategemea neno la mwisho kutoka kwake,” makamu akalieleza baraza na wote wakaunga mkono.

“mheshimiwa makamu, naomba utoe tamko la wazi kwa sasa juu ya hali hii, maana, tusipoangalia, waandishi wa magazeti kama kawaida yao wataanza kutoa habari zisizothibitishwa,” msemaji wa ikulu alimwambia makamu wa rais.

“ok, naomba ieleweke hivi, ikulu imevamiwa na kundi la kigaidi, walinzi kadhaa wameuawa na bado kuna hali ya sintofahamu. vyombo vya usalama viko katika harakati za kuhakikisha vinategua kitendawili hiki ndani ya saa chache. tunaomba wananchi kuwa watulivu na pia kutoa taarifa polisi pindi unapoona mtu unayemhofia katika maeneo yenu,” makamu wa rais akazungumza. punde tu taarifa ile ikachapwa katika mashine na kusainiwa akakabidhiwa huyo bwana, msemaji wa ikulu ili kuwafikishia wanahabari waliofika alfajiri hiyo katika ukumbi mdogo wa maelezo ulio ndani ya jengo hilo.

***
ikulu ilikuwa haiingiliki mpaka uwe na kibali maalumu, vijana wa jeshi la wananchi waliegesha magari yao upande wa baharini na mengine mawili upande wa hospitali ya ocean road na nyingine zilisimama karibu na ofisi ya hazina. barabara ya magogoni ilifungwa haikuruhusiwa gari wala mtembea kwa miguu kupita eneo lile. juu angani helkopta ya jeshi na polisi zilikuwa zikifanya doria zikishirikiana na zile za jeshi la wananchi.

kwa ujumla jiji la dar es salaam lilikuwa katika misukosuko ya hapa na pale. majira ya saa sita mchana barabara kubwa na ya muhimu zaidi katika jiji hilo ilifungwa kwa muda, ile inayotoka uwanja wa ndege kuelekea mjini. ving’ora vikasikika na gari kama saba hivi zilipita kwa kasi ya ajabu kuelekea mjini. na dakika kumi na mbili tua gari hizo ziliingia katika lango kuu la ikulu na kuegeshwa mahala pake wakati tayari mkuu wa nchi alikuwa amekwishashuka na kuingia ndani ya jengo hilo, moja kwa moja akiwa na walinzi wake alipitiliza na kuteremka ngazi iliyompeleka katika chumba maalum ambacho hufanyia mikutano yake ya siri kilichopewa jina la ‘kilimanjaro square’.

“nimesikitishwa na kilichotokea, hii haiwezekaniki kuivumilia, ni uvamizi,” rais aling’aka huku akizunguka chumba badala ya kuketi chini. watu watano waliokuwa naye ndani ya chumba hicho walibaki kimya kabisa. mkuu wa nchi akarudi na kuketi mezani kwake, akakamata kalamu yake na kutaka kuandika kitu lakini mkono ulikuwa mzito.

“tulikuwa tunakusubiri wewe mheshimiwa rais ili utoe neno lako vijana waingie kazini mara moja,” makamu wa rais alitamka.

“oh! shiiit, come on, hii ni cold war! let me say cold war, na ntaipigana mpaka mwisho. mtu kukuvamia ndani ya chumba chako na kumchukua mkeo ni matusi, matusi yasiyovumilika!” akang’aka huku akisimama wima kwa hasira, “ni jengo gani au taasisi gani afrika ina ulinzi mkali na makini kama hili jengo hapa? hakuna, ninyi mnajua na dunia inajua. sasa hawa waliokuja na kufanikiwa kufanya madhara haya ina maana wamejuaje njia za kuingia humu na njia za kutokea kama si hujuma?” aliendelea kung’aka kwa sauti. kisha akatulia kidogo huku kijasho kikimtiririka, mwili wake ulimtetemeka kama mtu asikiaye baridi kali. akasimama na kutazamana na mkuu wa majeshi “nataka vijana wako waliobobea kweye michezo hii wahakikishe wanampata first lady ndani ya saas12.
“umesomeka amiri jeshi mkuu,” akajibu mkuu wa majeshi na kusimama akatoa saluti ya utii.
“na ninyi wengine muwe katika kazi zenu za kawaida lakini nyote muangaze macho katika sakata hilo,” akatoa maagizo kwa viongozi wa vikosi vingine. nao wakaitikia wito huo na kila mmoja akaondoka katika jengo hilo lililotukuka. ni dakika hiyohiyo tu ambapo ule ukumbi ulikuwa na watu wawili tu yaani rais na makamu wake.

“inaniuma sana mheshimiwa!” rais alimwambia makamu wake huku mikono yake ikiwa haitulii sehemu moja.

“mimi pia, ukizingatia tumepoteza vijana wenye ujuzi wa hali ya juu sana katika maswala ya usalama,” makamu naye alijibu.

“nina uhakika kwa vijana wetu hawa wa jw, hao wahalifu watapatikana tu,” rais akajibu.

“sawasawa kabisa, lakini unafikiri wao peke yao wataweza kulibaini kundi hilo lililofanya kadhia hii?”

“kwa nini unasema hivyo?”

“kwa sababu kutokana taaluma yao nahisi kama kazi hii inaweza kuwa ngumu,” makamu alikazia.

“hapana! hata mimi nilikuwa mwanajeshi, najua, tuna idara ya upelelezi ya jeshi, na kutokana na uzito wa jambo hili, wao ndio watu muafaka.” akameza mate kisha akaendelea,

“unajua hawa lazima wapambane na mtu anayelingana nao kwa sababu bila shaka ni magaidi sasa gaidi ni levo nyingine, lazima apambane na mtu wa levo yake na hao si wengine ni vijana wa jeshi,” mheshimiwa rais alamwelekeza makamu wake juu ya mpango huo. kikao cha wawili hao kilipomalizika, makamu wa rais akaondoka na kumwacha mkuu wake peke yake ndani ya ofisi hiyo. kitendo tu cha makamu wa rais kutoka na kumwacha mheshimiwa peke yake, simu ya mezani ilianza kuita kwa nguvu na fujo. mheshimiwa rais akaingalia kwa tuo kabla hajaamua kama ainyanyue na kuisikiliza au aiache, lakini tatizo ni kwamba hakujua simu hiyo ilikuwa inahusu nini au inamhusu nani. na mara nyingi simu ya chumba hicho ikiita basi huwa kunakuwa na jambo zito la kiofisi. kwa mkono wa kitetemeshi aliukwanyua mkono wa simu ile na kuiweka sikioni bila kuongea lolote.

“usijaribu kuchukua hatua yoyote kwa kumtafuta mkeo, tunajua unampenda na ndiyo maana tumemchukua, lakini ujue sisi tunachokitaka si fedha wala hatuna ugomvi na wewe. tunahitaji jambo moja tu, toa amri ya kuondoa majeshi yako ya kulinda amani katika kusini mwa nchi ya ngoko. ukilitekeleza hilo, mkeo utampata, na husipotekeleza tutateka na watu wa familia yako waliobakia, na wewe utakuwa wa mwisho…”

“ninyi ni nani? enh! ni nani?” alikatisha simu ile na kurusha swali ambalo halikujibiwa na simu ile ikakatika. rais alibaki amesimama bila kufanya lolote huku simu ile bado ikiwa sikioni, akili ilipomrudia akateremsha mkono taratibu na kuipachika mahala pake. akajitupa kitini nacho kikampokea bila hiyana huku kikinesanesa. mlango wa chumba hicho uliwaka taa ya kijani kwa ndani, akabonyeza swichi iliyo chini ya meza na kijiluninga kidogo kikaonesha mtu aliye upande wa pili.

“chakula kipo mezani mkuu!” akakribishwa lakini alipojitafakari aliona hata njaa hana, akanyanyuka na kutoka nje ya chumba hicho ambapo mlinsi wake namba moja kutoka idara ya usalama wa taifa alimpokea na kumwongoza kuelekea katika ukumbi wa chakula. ndani ya ukumbi huo kulikuwa na watu watatu tu ambao daima alipenda kula nao, hawa ni watu wa karibu sana nay eye, yaani watoto wake, mmoja wa kike na mwingine wa kiume. aliwaangalia watoto wake lakini alijikuta anashindwa kula chakula kile, badala yake aliamua kuondoka na kurudi ofisini, mara hii aliingia ofisi yake ya kawaida, akamwita katibu wake na kumwomba amwitie mkuu wa usalama wa ikulu.

“pole kwa kupoteza vijana wako!” alimpa pole.

“siwezi kupoa mpaka nipate ukweli wa hili,” yule mkuu wa usalama alijibu huku chozi likimdondoka.

“umefika olduvai?” akamwuliza.

“ndiyo mkuu!”

“hakuna madhara yoyote?”

“hakuna mkuu, kule hawajafika kabisa,” yule mkuu wa usalama akampa jibu lililomfanya yule rais kutabasamu kwa mbali.

“sikiliza othman, hili swala si dogo, ni gumu, nimetoa kazi kwa vijana wa jw walikamilishe, lakini nataka na wewe hapa unifanyie uchunguzi juu ya hili, hawa jamaa wamewezaje kuingia hapa ndani pasi na kuonekana?” rais alionesha wasiwasi wa wazi.

“mheshimiwa rais! hicho kitu kinanishangaza mpaka sasa, bado naumiza kichwa kujua ni vipi hawa watu wameweza kuipenya hii ngome ya chuma, sipati jibu. nafikiri inabidi tuwashirikishe wanaintelijensia wa juu kabisa katika hii nyanja,” othman, mkuu wa usalama ikulu alimweleza rais.

“usemalo ni sahihi, je unataka tukodi vyombo vya nje?” akamwuliza mara baada ya kuiinua uso wake.

“inapobidi hatuna budi kufanya hivyo,”
mkuu wan chi akajiinamia tena kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama othman.

“sikia othman, ina maana sisi vyombo vyetu vimeshindwa? ni mapema mno kuomba msaada kutoka mataifa ya nje, ngoja tushindwe kabsa hapo hatutakuwa na budi lakini si sasa,” akamwambia.

“ngoja nikwambie kitu, mimi kama mwanausalama nakueleza tu hili swala linaweza kuwa gumu sisi kulitatua, kwa sababu hatujui nini na nini kimetukwamisha katika kugundua hao majahili. isitoshe pamoja na ulinzi mkali wa jengo hili ndio maana unaona vijana wetu wamekufa na kuumia, wavamizi hao wameingia moja kwa moja mpaka ndani ya nyumba yako ilipo ndani ya ikulu hii, hili si la kawaida na halijawahi kutokea popote katika karne hii,” othamn akaongea kwa uchungu sana.

maneno haya yaliifinya akili ya rais kwa muda huo, akatafakari jambo, akamtazama othman, “othman, kati ya vijana wangu wachache ninaoheshimu mawazo yao, wewe ni mmojawapo ndio maana nilikutoa kule ubalozini kukurudisha hapa ikulu, sawa nitalifanyia kazi leo hii, asante,” rais akamshukuru othman, wakaagana.
***
kusini mwa nchi ya ngoko

Mvua kubwa ilikuwa ikinyesha wanajeshi wa majeshi ya kulianda amani kutoka tanzania walikuwa wamejificha katika msitu huo mnene, wakiwa wamegawana makundi ya askari ishirini ishirini na kuuzungukla msitu huo unaokaliwa na waasi wa x65. waasi hao waliouvamia msitu huo miaka kadhaa nyuma walikuwa sugu na hawakutaka kuondoka kabisa kwa kuwa waliteka migodi ya dhahabu na almasi kwa manufaa yao na waliowatuma.

uamuzi wa tanzania kutoa batalioni moja ya wapiganaji wake mahiri wa jeshi la wananchi ulitokana na ombi la umoja wa nchi za afrika ili kukomesha kabisa uasi huo uliokuwa ukikiuka haki za binadamu kwa watu waishio katika maeneo hayo. mara kadhaa majeshi ya kujitolea yalikwenda huko lakini yalikutana na waasi wenye silaha nzito za kivita hivyo kupelekea kushindwa na kurudi nyumbani bila kutimiza azma yao.

baada ya muda mrefu wa kuwaacha waasi hao, maafikiano ya amani yalishindikana kwa njia ya kidiplomasia kati ya viongozi wa afrika na kiongozi wa wassi hao wa x65 waliokuwa wakipigana vita ya gorilla. vikao vilikaliwa miji mbalimbali ya afrika lakini ilikuwa ngumu kufikia muafaka, waasi hao hawakutaka kabisa kuuachia sit u msitu bali na eneo husika.

“hawa jamaa si wa kuwaonea huruma hata kidogo!” mmoja wa wanajeshi aliyekuwa katika ficho lake huko msituni aliwaambia wenzake.

“ila inaonekana sio tu waasi bali ni wanajeshi waasi kwa maana wanajua vyema mbinu za kivita.

“yeah ni kweli, maana kila tunapowazunguka nao wanakuwa makini, na kila tufanyalo inaonekana kama wanalijua,” askari mwingine wa mstari wa mbele alimjibu mwenzake huku akiweka bunduki yake sawia kifuani pake maana mapambano yangelipuka wakati wowote.

“kumbukeni wenzetu wameshindwa kazi hii na sisi tumeaminiwa kuifanikisha,” kiongozi wao akawaambia.

“aaaa sisi ni jeshi imara la tanzania, hawatuwezi, tunawapanga wadunguaji kisha tunamaliza kazi, hawa waasi ni kuwafutilia mbali tu, aliongea mwanajeshi mwingine aliyekuwa amebeba redio kubwa mgongoni mwake.

“chonjo wasiliana na makundi mengine waambie karibu tunaingia kijijini, hapo lazima tuzunguke kijiji kwa maana hatujui, labda wapo hapo” kiongozi wa kundi akampa maagizo mtaalamu huyo wa redio aliyejulikana kwa jina la chonjo.

***
kutoka katika makundi mengine yote walipata taarifa ile ya redio kupitia vyombo vyao vya kisasa kabisa ambavyo kila mmoja aliweza kusikia kwa wakati wake na aliweza kuongea na mwenzake. askari wale wakajiweka vyema kila mmoja akaiweka tayari bunduki yake kubwa (assault rifle) aina ya m4 carbine kifuani tayari kwa uvamizi. bunduki hii wanajeshi wote walipewa katika operesheni hiyo ukiachana na hiyo bunduki kila mmoja alikuwa na bastola mbili zenye nguvu kwa operesheni za dharula, mabomu ya kutupa kwa mkono ‘fragmentantion granade’, mabomu ya kutoa moshi ‘smoke granade’ kwa ajili ya kumchanganya adui. zaidi ya hapo kila kundi lilikuwa na mtu mwenye lpg, ‘anti-tank weapon’, silaha ya kujitwisha begani inayotumika kuvunja vizuizi wakati wa operesheni. kwa ujumla vijana hawa walitimia kila idara.

kutoka katika maficho walipita chini kwa chini kwenye vichaka vinene kwa minajiri ya kuzunguka kile kijiji cha mpumbutu, wengine wakaenda mlimani na wengine upande wa chini. iliwachukua kama dakika ishirini na tano kuzingira kijiji hicho ambacho mara nyingi waasi walipenda kujificha humo. kisha askari wawili walijitoa chambo kuingia kijijini ili kuwafanya waasi hao kujitokeza kirahisi.

katika moja ya vichaka kulilala watu wawili waliojifunga nyasi kavu na mbichi migongoni na kichwani kiasi kwamba wakilala kifudifudi huwezi kutambua kama ni binadamu, hawa walikuwa ni wadunguaji kitaaluma walikuwa na bunduki kubwa ya kudungulia ‘heavy sniper rifle’ m82a1. walijificha kimya kwenye kichaka kilicho juu ya kilima huku kwa chini wakikiona kile kijiji.
-------------------------------------------------------
epuka corona, waepushe wengine.
kaa nyumbani kama huna ulazima wa kutoka
nawa mikono yako kwa sanitizer au maji yenye dawa au sabuni
#stopcorona
----------------------------------------------------------------

kijiji cha mpumbutu

Shughuli za wanakijiji ziliendelea kama kawaida, watu walikuwa wakijpatia huduma ndogondogo katika maduka na vigenge, wengine wakipata vinywaji na kulewa ili kujisahaulisha shida zao. pembezoni mwa kijiji hicho, ukimaliza tu nyumba za wenyeji kulikuwapo na nyumba nyingine kubwa tu, nyumba hiyo ilikuwa ya tajiri mmoja mfanyabiashara aliyeuawa na waasi na kisha wao kuichukua na kuifanya maskani yao kila waingiapo kijijini hapo. hakuna mtu aliyekuwa akiisogelea nyumba hiyo kwa kuhofia kuuawa. waasi waliitumia zaidi ya kazi hiyo, waliitumia kama dangulo, pale mkubwa wa waasi anapojisikia ashki ya kufanya ngono vibaraka wake walikwenda kijijini na kukamata mwanamke yoyote na kumleta humo ndani. endapo atakataa aliuawa hadharani, hali hii iliwafanya watu wawafungia mabinti na wake zao ndani na wengine hata kukikimbia kijiji hicho.

“hiki ndiyo kijiji cha mpumbutu, wananchi wake hufanyiwa vitendo vya uzazalishwaji na hutendwa kinyume na haki za binadamu, serikali ya ngoko kama haiyaoni haya, tunataka kusafisha waasi kwa mashambulizi ya kimbunga, na si wananchi, hakikisha risasi yako inampiga muasi na shabaha yako isikosee,” sauti ya kiongozi wa vikosi vya ukombozi ilisikika sikioni mwa kila mmoja.

benson boko aliweka jicho lake katika lensi ya bunduki lake kutoka pale alipojificha na kuchungulia, akiangalia lile jumba waliloelekezwa kwenye ramani na kisha taratibu alielekeza kwenye vijia na njia zinazopita katikati ya kijiji hicho. akaondoa jicho na kuangalia saa yake, ilikuwa yapata saa 12 jioni. bado si wanakijiji wala waasi waliokuwa wakijua kuwa wamezingirwa, muda ulikuwa haujafika wa kufanya kazi yao.

tuonane jumamosi

ukiitaka yote ni tsh 4000 tu 0766974865a kuumia, wavamizi hao wameingia moja kwa moja mpaka ndani ya nyumba yako ilipo ndani ya Ikulu hii, hili si la kawaida na halijawahi kutokea popote katika karne hii,” Othamn akaongea kwa uchungu sana.

Maneno haya yaliifinya akili ya rais kwa muda huo, akatafakari jambo, akamtazama Othman, “Othman, kati ya vijana wangu wachache ninaoheshimu mawazo yao, wewe ni mmojawapo ndio maana nilikutoa kule ubalozini kukurudisha hapa Ikulu, sawa nitalifanyia kazi leo hii, asante,” rais akamshukuru Othman, wakaagana.
***
KUSINI MWA NCHI YA NGOKO

MVUA KUBWA ILIKUWA IKINYESHA wanajeshi wa majeshi ya kulianda amani kutoka Tanzania walikuwa wamejificha katika msitu huo mnene, wakiwa wamegawana makundi ya askari ishirini ishirini na kuuzungukla msitu huo unaokaliwa na waasi wa X65. Waasi hao waliouvamia msitu huo miaka kadhaa nyuma walikuwa sugu na hawakutaka kuondoka kabisa kwa kuwa waliteka migodi ya dhahabu na almasi kwa manufaa yao na waliowatuma.
Uamuzi wa Tanzania kutoa batalioni moja ya wapiganaji wake mahiri wa Jeshi la Wananchi ulitokana na ombi la Umoja wa nchi za Afrika ili kukomesha kabisa uasi huo uliokuwa ukikiuka haki za binadamu kwa watu waishio katika maeneo hayo. Mara kadhaa majeshi ya kujitolea yalikwenda huko lakini yalikutana na waasi wenye silaha nzito za kivita hivyo kupelekea kushindwa na kurudi nyumbani bila kutimiza azma yao.

Baada ya muda mrefu wa kuwaacha waasi hao, maafikiano ya amani yalishindikana kwa njia ya kidiplomasia kati ya viongozi wa Afrika na kiongozi wa wassi hao wa X65 waliokuwa wakipigana vita ya gorilla. Vikao vilikaliwa miji mbalimbali ya Afrika lakini ilikuwa ngumu kufikia muafaka, waasi hao hawakutaka kabisa kuuachia sit u msitu bali na eneo husika.

“Hawa jamaa si wa kuwaonea huruma hata kidogo!” mmoja wa wanajeshi aliyekuwa katika ficho lake huko msituni aliwaambia wenzake.

“Ila inaonekana sio tu waasi bali ni wanajeshi waasi kwa maana wanajua vyema mbinu za kivita.

“Yeah ni kweli, maana kila tunapowazunguka nao wanakuwa makini, na kila tufanyalo inaonekana kama wanalijua,” askari mwingine wa mstari wa mbele alimjibu mwenzake huku akiweka bunduki yake sawia kifuani pake maana mapambano yangelipuka wakati wowote.

“Kumbukeni wenzetu wameshindwa kazi hii na sisi tumeaminiwa kuifanikisha,” kiongozi wao akawaambia.

“Aaaa sisi ni jeshi imara la Tanzania, hawatuwezi, tunawapanga wadunguaji kisha tunamaliza kazi, hawa waasi ni kuwafutilia mbali tu, aliongea mwanajeshi mwingine aliyekuwa amebeba redio kubwa mgongoni mwake.

“Chonjo wasiliana na makundi mengine waambie karibu tunaingia kijijini, hapo lazima tuzunguke kijiji kwa maana hatujui, labda wapo hapo” kiongozi wa kundi akampa maagizo mtaalamu huyo wa redio aliyejulikana kwa jina la Chonjo.

***
Kutoka katika makundi mengine yote walipata taarifa ile ya redio kupitia vyombo vyao vya kisasa kabisa ambavyo kila mmoja aliweza kusikia kwa wakati wake na aliweza kuongea na mwenzake. Askari wale wakajiweka vyema kila mmoja akaiweka tayari bunduki yake kubwa (assault rifle) aina ya M4 Carbine kifuani tayari kwa uvamizi. Bunduki hii wanajeshi wote walipewa katika operesheni hiyo ukiachana na hiyo bunduki kila mmoja alikuwa na bastola mbili zenye nguvu kwa operesheni za dharula, mabomu ya kutupa kwa mkono ‘fragmentantion granade’, mabomu ya kutoa moshi ‘smoke granade’ kwa ajili ya kumchanganya adui. Zaidi ya hapo kila kundi lilikuwa na mtu mwenye LPG, ‘anti-tank weapon’, silaha ya kujitwisha begani inayotumika kuvunja vizuizi wakati wa operesheni. Kwa ujumla vijana hawa walitimia kila idara.

Kutoka katika maficho walipita chini kwa chini kwenye vichaka vinene kwa minajiri ya kuzunguka kile kijiji cha Mpumbutu, wengine wakaenda mlimani na wengine upande wa chini. Iliwachukua kama dakika ishirini na tano kuzingira kijiji hicho ambacho mara nyingi waasi walipenda kujificha humo. Kisha askari wawili walijitoa chambo kuingia kijijini ili kuwafanya waasi hao kujitokeza kirahisi.

Katika moja ya vichaka kulilala watu wawili waliojifunga nyasi kavu na mbichi migongoni na kichwani kiasi kwamba wakilala kifudifudi huwezi kutambua kama ni binadamu, hawa walikuwa ni wadunguaji kitaaluma walikuwa na bunduki kubwa ya kudungulia ‘Heavy Sniper Rifle’ M82A1. Walijificha kimya kwenye kichaka kilicho juu ya kilima huku kwa chini wakikiona kile kijiji.
-------------------------------------------------------
Epuka Corona, waepushe wengine.
Kaa nyumbani kama huna ulazima wa kutoka
Nawa mikono yako kwa Sanitizer au maji yenye dawa au sabuni
#StopCorona
----------------------------------------------------------------

KIJIJI CHA MPUMBUTU

Shughuli za wanakijiji ziliendelea kama kawaida, watu walikuwa wakijpatia huduma ndogondogo katika maduka na vigenge, wengine wakipata vinywaji na kulewa ili kujisahaulisha shida zao. Pembezoni mwa kijiji hicho, ukimaliza tu nyumba za wenyeji kulikuwapo na nyumba nyingine kubwa tu, nyumba hiyo ilikuwa ya tajiri mmoja mfanyabiashara aliyeuawa na waasi na kisha wao kuichukua na kuifanya maskani yao kila waingiapo kijijini hapo. Hakuna mtu aliyekuwa akiisogelea nyumba hiyo kwa kuhofia kuuawa. Waasi waliitumia zaidi ya kazi hiyo, waliitumia kama dangulo, pale mkubwa wa waasi anapojisikia ashki ya kufanya ngono vibaraka wake walikwenda kijijini na kukamata mwanamke yoyote na kumleta humo ndani. Endapo atakataa aliuawa hadharani, hali hii iliwafanya watu wawafungia mabinti na wake zao ndani na wengine hata kukikimbia kijiji hicho.

“Hiki ndiyo kijiji cha Mpumbutu, wananchi wake hufanyiwa vitendo vya uzazalishwaji na hutendwa kinyume na haki za binadamu, serikali ya Ngoko kama haiyaoni haya, tunataka kusafisha waasi kwa mashambulizi ya kimbunga, na si wananchi, hakikisha risasi yako inampiga muasi na shabaha yako isikosee,” sauti ya kiongozi wa vikosi vya ukombozi ilisikika sikioni mwa kila mmoja.

Benson Boko aliweka jicho lake katika lensi ya bunduki lake kutoka pale alipojificha na kuchungulia, akiangalia lile jumba waliloelekezwa kwenye ramani na kisha taratibu alielekeza kwenye vijia na njia zinazopita katikati ya kijiji hicho. Akaondoa jicho na kuangalia saa yake, ilikuwa yapata saa 12 jioni. Bado si wanakijiji wala waasi waliokuwa wakijua kuwa wamezingirwa, muda ulikuwa haujafika wa kufanya kazi yao.

Itaendelea....
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI I - hujuma na uzandiki
MTUNZI: richard MWAMBE
Simu; 0766974865

Benson Boko aliweka jicho lake katika lensi ya bunduki lake kutoka pale alipojificha na kuchungulia, akiangalia lile jumba waliloelekezwa kwenye ramani na kisha taratibu alielekeza kwenye vijia na njia zinazopita katikati ya kijiji hicho. Akaondoa jicho na kuangalia saa yake, ilikuwa yapata saa 12 jioni. Bado si wanakijiji wala waasi waliokuwa wakijua kuwa wamezingirwa, muda ulikuwa haujafika wa kufanya kazi yao.
***

SEHEMU YA II

Bensoir Banginyana alikuwa juu ya kiti chake akipendacho huku wasichana wawili warembo walikuwa wakimkanda mwili wake. Kinywani mwake kulikuwa na siga kubwa kila akipiga pafu mbili hulitoa na kukung’uta jivu kibwetani.

Mlango mkubwa wa mbele wa jumba hilo la kifahari ulifunguliwa ghafla na kijana mmoja aliyevalia kijeshi akasimama mbele ya Bensoir Banginyana, akapiga saluti na kutulia kiutulivu wa kiaskari.

“Mkuu nahisi tuna wageni katika himaya yetu,” yule askari akaongea kwa ukakamavu bila hata kutikisika.

“Nani aliyekwambia mpiganaji huwa anahisi, sema vizuri, sema kitu chenye uhakika na si kuhisi,” Bensoir akang’aka na kuinuka pale kitini huku akiwasukuma pembeni wale wasichana, akavuta jaketi lake la kijeshi na kulivaa, “Mmeona nini?” akauliza.

“Kuna sura mbili ngeni hapa kijijini zimeingia, kwa jinsi walivyo ni kama majasusi wanaopeleleza kitu fulani,” akajibu.

“Mmewaweka jichoni au ndiyo mmewaacha tu kama kawaida yenu?”

“Wako jichoni mkuu,”

“Waleteni sasa hivi tugawane nyama!”

Dakika tano baadae vijana wawili waliingizwa katika ile sebule kubwa ya Bensoir, wakaamuriwa wapige magoti. Miili yao walikuwa wameifunika kwa makoti marefu ya mvua, lakini miguu yao ilionekana dhahiri kuwa wamevaa buti za kisasa za jeshi.

“Ha! ha! ha! ha! Wenzenu waliotangulia walisalimu amri kwenye msitu huu wa shetani ninyi mmekuja sio, sasa tutawachinja na video yenu ataiona rais wenu.” Akakohoa kidogo, “ wavueni hayo makoti,” akaamuru.

Baada ya kuvuliwa makoti walibaki na kombati zao za kijeshi, kwenye mabega yao kulipachikwa kibaka cha mstatili kilichoonesha bendera ya Umoja wa Mataifa.

“Tuwaambie mara ngapi pumbavu ninyi? Sasa wakuu wenu wamewasaliti, kwa kuwa wanajua wazi maafikiano yetu na wao,” Bensoir akawaeleza. Wale askari wawili walikuwa wamejiinamia huku mikono yao ikiwa imefungwa kwa nyuma.

“Mnatoka wapi?” akawauliza lakini hawakujibu. “Kuna ujeuri huwa hausaidii, maana mjibu, msijibu lazima niwaue tu”.
Teke moja la kushtukiza lilitua shavuni mwa kijana mmoja akamgonga mwenzake na wote wawili wakaanguka chini sakafuni.

“Nipe bastola yangu,” akamwambia askari mwingine aliyekuwa akilinda sebuleni hapo. Akiwa anapokea bastola hiyo akasikia kishindo kizito kutokea nje, akahamaki kidogo.
“Nini hicho? Hebu angalia nje,” akimalizia kusema hayo akasikia kishindo kinginie upande wa pili na kingine tena, mara taa zikazimika giza likatawala mle ndani.

“Ambush !!!” akanong’ona na kila askari wake akachukua kona yake, wakawasahau wale wawili pale chini.

***
“Nimeshaangusha watatu, eneo liko salama mnaweza kuingia,” yule mdunguaji alisema kwenye kile chombo chao cha mawasiliano. Kutoka kule milimani vijana kama ishirini waliteremka kutoka pande tofauti kwa mwendo ambao huwezi kuwagundua hata siku moja, waliikaribia ile nyumba na kujificha kimya kwenye vichaka vidogo mita chache tu kabla ya lile jumba. Walishuhudia wale jamaa waliokuwa wakilinda jumba hilo kutokea upande wa juu wakidunguliwa kwa ustadi kabisa kilichofuatia ni kufuata amri ile ya wadunguaji kuwa sasa wanaweza kuvamia jumba hilo.

Kutokana na mafunzo waliyoyapata vijana wale waliivamia ile nyumba kwa mtindo ambao uliwashangaza adui zao, walikuwa wakiingia kwa mstari na kila walipofika kwenye kona yule wa kwanza alibaki pale na kuwapa ishara wa nyuma yake kuwa wapite na kusonga mbele. Mmajibizano ya risasi yalipamba moto ndani ya jumba hilo, iliwapa taabu sana wale waasi kuwadhibiti hao wanajeshi kutokana na giza lililokuwako ndani humo. Vijana wa jeshi JWTZ chini ya mwamvuli wa UN walikuwa ngangari, ndaani ya vifaa vyao vilivyokaa machoni badala ya miwani ambavyo vilikuwa vikiwawezesha kuona vizuri gizani.

Walihakikisha hawapotezi risasi hata moja kwani kila moja ilianguka na mtu, wengine waliwasaidia wale wenzao huku wengine wakiendelea na msako wa chumba kwa chumba.

“Vipi?” mmoja alimuuliza mwenzake baada ya kumuona anakuja sebuleni.

“Hayupo?” akajibu. Askari wote walikutana sebuleni mwa jumba hilo lakini walimkosa Colonel Bensoir Banginyana.

“Kakimbilia wapi mwanaharamu huyu?” kiongozi wa ile platuni aliuliza wenzake.

“Hatujamwona, walinzi wake wote na askari wa nyumbani tumewaangusha.” Yule askari akajibu kisha dakika hiyo wote wakaiacha ile nyumba pweke baada kusikia kikirikikiri za watu huko nje.

“Marc weka wapangaji ndani ya nyumba,” amri ikatoka kwa kiongozi. Marc akapachika mikono katika mifuko ya mkanda mkubwa aliouvaa na kutoa mabomu matatu madogomadogo lakini yaliyokuwa yakitumia saa, akayapachika sehemu tatu tofauti na kisha kuiacha ile nyumba huku nyuma yake risasi zikirindima kumfukuza, lakini bahati nzuri alikuwa amekwishakwea ukuta na kujitupa upande wa pili na risasi za waasi waliovamia nyumba hiyo zikachimba ukuta.

“Move around!! move around!!” ilisikika sauti iliyokuwa ikiwapa amri wale waasi kuzunguka nyuma ya nyumba.

“Comander!” Mark akaita huku akimwangalia mkubwa wake hatua kama mia mbili mbali na ile nyumba.
Kutoka pale walipo walishuhudia mlipuko mkubwa ukiitawanya ile nyumba vipande vipande, mbao na vitu kama hivyo vikiruka hewani na kutawanyika kila upande..

“Sangalamanda mchuzi wa dagaa!” yule commander wa kikosi akatoa tusi la ajabu huku akiwasha sigara yake na kuipachika kinywani.

“Return to zero! Return to zero!” maelekezo yalisikika kutoka katika chombo cha kila mmoja na wote wakaondoka eneo hilo kwa njia ya siri, wakajificha tena msituni huku wakisikiliza matokeo ya operesheni yao hiyo.

MWAKA MMOJA ULIOPITA
Ikulu ya Dar es salaam

MKUTANO WA WATU WANNE ulifanyika katika ofisi ya Rais wa Tanzania ndani ya jengo la Ikulu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU) mwenyekiti wa kamati ya usalama ya umoja huo, mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama na Amirijeshi Mkuu wa Tanzania walikutana asubuhi hiyo kwa kikao kizito.

“Tunaelekea kushindwa na waasi hawa!” yule Katibu wa AU aliwaambia wajumbe, “Kwa sababu majeshi kutoa SADC yameelemewa na waasi, hapa hatuna jinsi tumeona ikiwezekan nchi yako itusaidie jeshi lako japo Batalioni moja nina uhakika na vijana wako,” akamwambia rais wa Tanzania ambaye ndiye alikuwa Amri Jeshi Mkuu, akamkabidhi na waraka wa kiofisi wa ombi hilo.

“Nalijua hilo!” rais akajibu, “kama majeshi ya muungano ya SADC yanaelekea kushindwa, mimi jeshi langu ni moja tu litaweza?” akaongeza.

“Oh, Sikia Mheshimiwa, wale waasi wapo msituni wanapigana vita ya ardhini, tulipokaa na kuchambua tumeona katika Afrika ni Tanzania yenye jeshi linaloweza vita hiyo tena kwa weledi mkubwa. Tumerejea vita ya Uganda, tumerejea ukombozi wa kisiwa cha Anzuan kule Comoro alkadhalika jeshi lako ndiyo limekuwa mwalimu mzuri wa mazoezi ya vita hii katika ukanda wa Afrika na hata nje ya Afrika, Ufaransa walikuja hapa kubadilishana uzoefu, India na nchi nyingine. Kiukweli tumeona jeshi lako litamaliza hii kazi,” akamaliza kusema na kuketi kitini.

“Nimekusikia na waraka huu tulishaupata, sasa kuna mambo ambayo tuliyazungumza” akampa waraka mwingine kutoka upande wa Tanzania, “bunge lilikubaliana hayo, kama yatatekelezwa sisi hatuna tabu. Opersheni yetu haitakuwa ya kulinda amani, sisi tunaenda kusafisha waasi, na lazima waondoke ndani ya kipindi kifupi,” akamaliza kusema.
Mwafaka ukafikiwa, na JWTZ wakapewa kazi chini ya kofia ya AU kutimiza kazi hiyo, miezi miwili baadae, batalioni moja ya wanajeshi wa miguu (Infantry) waliondoka Dar es salaam kueleke huko katika nchi ya Ngoko.

UPANDE MWINGINE WA AFRIKA

NDANI YA JENGO MOJA refu sana ambalo kwa juu kabisa lina kitu kama kisahani cha chai kinachojizungusha kwenye mhimili wake walikutana watu watatu waliotofautiana hata kimaumbile. Mwenye mwili mdogo kuliko wote ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikao hicho kisicho rasmi lakini wenyewe walikiita cha dharula. Majadiliano makubwa yalikuwa ni kusimamisha mtazamo wao na kuufanya kuwa kinyume na matakwa ya wengine.

“Huyu jamaa anatuharibia! Sisi tumeshweka msimamo wetu wa siri na mataifa mengi yanajua hata Rais wa Ngoko mwenyewe anajua hilo. Ina maana wao hawashangai kwa nini jeshi la Ngoko halifiki kule Kusini mwa nchi yao? Sasa huyu ni nani hata yeye kama yeye atoe jeshi la nchi yake tu kupambana na wale vijana wa X65?” yule kiongozi wao aliyekuwa na kauli yenye nguvu akawaambia wajumbe wake hao wawili juu ya swala hilo.

“Mimi nilipinga sana muswada huo pale Addis Ababba, kwa kuwa nilijua madhara yake, lakini nchi nyingi zikang’ang’ania tu, ikapita kauli ya ‘wengi wape’, basi, lakini sijui tufanyeje Comrade!” mwingine alichangia.

“Hakuna jinsi huyu lazima tumkomeshe, nilifanya hila mpaka nchi yangu ikaingia katika umoja wenu huu lengo langu mimi nataka nitawale hapa pote, na ninaweza kwa sababu nina akili japo nina mwili mdogo, we unafikiri pesa itatoka wapi? Lazima tuchukue madini kule Ngoko kwa nguvu tuwauzie huko dunia ya kwanza ili nipate pesa ya kuweka watu wangu. Ninyi nyote nimewaweka madarakani kasoro hawa wawili hawa, na huyu mwingine ananivuruga kabisa yaani,” yule Kiongozi aliongea mpaka akaona miwani nzito haimtoshi.

“Comrade, hapa ni mapinduzi tu, mi nakuaminia sana wewe, kama uliwatungua wale kipindi kile ukachukua nchi utawashindwaje hawa wawili?” akaongea mjumbe aliyevaa pama kichwani mwake. Wote hawa watatu walikuwa ni marais kutoka nchi tatu tofauti, walijitenga na kufanya mambo yao katika umoja wao usiotambulika popote.

“Msijali, wajumbe tukutane kikao kama hiki wiki tatu zijazo nitawajuza nini nimefikiria kufanya juu ya hili,” akamaliza. Kikao kikaahirishwa na wale wajumbe kila mmoja akaondoka kuelekea atokako.


2
UJERUMANI MASHARIKI

KAMANDA AMATA kama alivyojulikana, aliteremka kwenye gari ya kifahari aina ya BMW X5 liling’aa kwa rangi ya kimetaliki, ilimfikisha katika jengo hilo kubwa ambalo kwa juu liliandikwa kwa maandishi makubwa na ya kupendeza yaliyosomeka IN DIAMOND WE TRUST. Kwa hatua za haraka haraka alitembea kuelekea jengo hilo, zaidi ya suti ya gharama aliyoivaa mkononi mwake alikuwa na briefcase kubwa na ya kitajiri sana, kiatu chake kilionekana wazi kuwa hakijawahi kukanyaga udongo tangu kinunuliwe. Pamoja naye aliongozana na mwanamama mtu mzima,

Theresia Schurman, aliyekuwa ni mmoja wa maajenti wa kampuni hiyo iliyokuwa ikisifika kwa ununuaji wa madini hayo ya almasi.

“Karibu sana!” alikaribishwa ndani ya ofisi nadhifu sana, akiwa na yule mama waliongoza mpaka kwenye mlango mwingine mdogo ambako walifunguliwa na kuingia ndani ya ofisi hiyo. Kulikuwa na mtu mmoja wa makamo, si mnene sana lakini alikuwa na nyama za kutosha. Juu ya meza yake kulikuwa na jina lake lililochongwa vyema kwa mwandiko mlalo, Stephen Mc Donald.
-----------------------------------------------------------------------
Usisahau kunawa mikono kwa sanitizer au maji tiririka yenye dawa au na sabuni.
Corona inaua..... walinde wapendwa wako kwa kuwataka wakae nyumbani
#StopCorona
-------------------------------------------------------------------------

“Mc Donald kama tulivyoongea kwenye simu, huyu ni Mr. Spark kutoka Afrika yeye ni mfanyabiashara wa madini na anapenda kufanya kazi na sisi,” yule mama akamaliza na bwana Stephen akanyanyuka na kumpa mkono Mr. Spark kisha wakaketi.

“Ndiyo Mr. Spark!” akaanzisha mazungumzo.

“Yeah, kama alivyokwambia Bi. Theresia Schurmann, natokea Afrika, mimi ni mnunuzi na muuzaji wa madini haya na dhahabu pia, lakini kuja kwangu ni kutafuta masoko ya almasi hii mpya, sijui kama umepata kuiona kabla,” Mr Spark akazungumza na kufungua ile briefcase yake akampa huyo bwana kipande cha almasi. Mc Donald akakichukua na kukitazama kwa makini sana, akaonekana kama kapatwa mshituko hivi lakini baadae akakaa sawa.

“Unasema almasi hii umeitoa wapi?” Mc Donald akauliza.
“Inatoka Afrika, mimi ni biashara ya kukusanya madini haya, na nimefanya kazi na makampuni mbalimbali, safari hii nikapenda kuja kwenye kampuni yako…” Kamanda Amata au Mr Spark kwa jina la kificho alimwambia yule bwana ambaye sasa alikuwa kachuku kitu kama koleo na kubana kile kipande cha ng’walu, akikiangalia kwenye mwanga wa taa.

“Unajua kwa nini nakuuliza umeipata wapi?”
“Najua; ni kwa sababu unataka ujue kitu bora kama hiki kinatoka wapi, ni Afrika tu mzee, hakuna kwingine duniani,” Amata akamjibu huku akikunja nne na kujiweka sawa .

“Mr Spark! Hii sampuli haiuzwi wala haifanyiwi biashara yoyote kwa sababu ni ‘conflict diamond’, hata uende kwa nani Ulaya hii hawezi kununua,” akameza mate na kisha akanywa maji kidogo, uso wa Mc Donald ulionekana kutona kwa matone madogomadogo ya jasho, “Huwa tunaogopa sana watu wanaokuja na hii sampuli ya almasi,” akamalizia.

“McDonald, hii ni almasi ghali sana, kwa nini hamuitaki?”

“Sio hatuitaki, labda ninachoweza kukusaidi ni kukukutanisha na mtu anayeweza kufanya biashara ya sampuli hii na wewe,” Mc Donald akamweleza Amata.

“Ok, wazo zuri, basi kama utanikutanisha naye, itakuwa vyema name nitakupa sampuli ingine labda hiyo utaikubali,”

“Bila shaka!” akakohoa kidogo kwa sababu alionekana kuathiriwa sana na tumbaku, “Nitakupigia simu mara baada ya kumpata mtu huyo,” akamalizia na kuagana na Amata.
Conflict Diamond, Kamanda Amata akawaza wakati akiwa ndani ya gari hiyo kuelekea hotelini kwake ndani ya jiji hilo la Berlin. Kichwani mwake hakuwa na shaka na bishara hiyo anayojaribu kuifanya na nchi hizo za Ulaya kwani hata yeye anajua kuwa inalipa. Baada ya kupita mitaa kadhaa yenye mabarabara ya kutisha kwa uzuri aliwasili katika hoteli aliyofikia, Paradox Hotel.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI - hujuma na uzandiki
MTUNZI: richard MWAMBE
Simu :0766974865

“Bila shaka!” akakohoa kidogo kwa sababu alionekana kuathiriwa sana na tumbaku, “Nitakupigia simu mara baada ya kumpata mtu huyo,” akamalizia na kuagana na Amata.
Conflict Diamond, Kamanda Amata akawaza wakati akiwa ndani ya gari hiyo kuelekea hotelini kwake ndani ya jiji hilo la Berlin. Kichwani mwake hakuwa na shaka na bishara hiyo anayojaribu kuifanya na nchi hizo za Ulaya kwani hata yeye anajua kuwa inalipa. Baada ya kupita mitaa kadhaa yenye mabarabara ya kutisha kwa uzuri aliwasili katika hoteli aliyofikia, Paradox Hotel.

SEHEMU YA III

T S A MAKAO MAKUU

CHIBA WA CHIBA alikuwa ametingwa kwenye kompyuta zake akiangalia mambo mbalimbali katika mtandao, akifuatilia hiki na kile huku kwenye luninga kadhaa akitazama mienendo ya jiji la Dar es salaam sehemu nyeti nyeti kwa ajili ya usalama. Mlango ukafunguliwa na Madam S akaingia huku mkononi akiwa na kikombe cha kahawa.

“Bibi kweli umezeeka, jua lote hili na kahawa?” Chiba akaanza kumchokoza.

“Hivi hata humu ndani kuna jua? Na hilo air conditioner uliloliwasha unategeme nini, hata hivyo hiki ni kinywaji kama vinywaji vingine,” akajibu huku akivuta kiti na kuketi, jicho lake likipita kwenye zile luninga.

“Hivi ilikuwaje tukio la majuzi lile kutukia ilhali tuna vifaa kama hivi kwa usalama?” akauliza Madam.

“Hivi unawajua magaidi au unawasikia? Usijiulize imekuwaje au imewezekanaje, kuna watu hata wakiamua kwenda kukiiba kiti cha enzi kule mbinguni wanaweza, sasa sembuse hapa kwetu?” Chiba akajibu huku akigeuza kile kiti na kukigeuzia kwa Madam.

“Hapo unafanya nini?” akamwuliza.

“Aaah nilikuwa nachambua habari za watu tishio Afrika zaidi zaidi huyu kiongozi wa X65 ndiye ambaye namsoma zaidi na kuchukua vitu fulani Fulani,” Chiba akajibu huku akiurudi tena kwenye kompyuta yake.

“Enhe, nani mwingine uliyemdadavua?”

“Wengi, kuna Joseph Konyi naye nilikuwa namcheki hapa, kuna huyu kiongozi wa Al-Shabab na hawa Boko Haram wote nilikuwa nawapitia ila nimestak zaidi kwa huyu Bensoir Banginyana kwa sababu yeye ni hot cake,” akaeleza.

“Enhe nini kipya zaidi ya kuwa kiongozi wa juu wa X65?” Madam akazidi kuhoji.

“Eh, madam una maswali ka’ mtoto wa miaka minne! Bensoir Banginyana ni mzaliwa wan chi ya Nduruta, amesoma na kukulia huko Ngoko miaka mingi nyuma, baadae wazazi wake wakarudi Nduruta pamoja naye na kuanza maisha mapya. Huyu bwana alijinga na jeshi miaka ya 1985 na kwa sababu ya elimu yake alipata cheo cha juu sana cha Kanali akiwa na umri mdogo. Ameliongoza jeshi la Ndyryta kwenye operesheni mbalimbali na zote zimefanikiwa. Alikwenda USA kwa kujifunza zaidi maswala ya Military Intelligency kwa miaka minne, inasemekana alishiriki katika moja ya operersheni kubwa iliyofanywa na jeshi la Marekani katika jangwa la Afghanistan lakini hawajasema hapa ni operersheni gani…”

“We unasoma katika mtandao gani hizo habari mbona kwenye weekpedia hayo hayajaandikwa?” Madam S alimkatisha Chiba.

“Madam S! Mkuu wa TSA, mimi kuwa TSA 2 haikuwa makosa na ni wewe mwenyewe uliona nafaa au siyo. Hapa nimevunja codes za mtandao wa CIA, nimechukua faili kisha nimerudisha kama ilivyo. Hili tunaliweza watu wachache sana duniani, hapa ningekaa na code yao kwa dakika tatu tu wangegundua na wangejua ni wapi imevunjwa hiyo code, lakini nilijiandaa nikafanya kwa kasi ya ajabu bahati nzuri nikalipata, nikachukua faili hilo tu basi…”

“Umelipakua au?” Madam akamkatisha tena.

“Kama kawaida!”

“Endelea!”
“Bensoir Banginyana alirudi na kuendelea na wajibu wake katika jeshi la nchi yake kama awali. Baada ya mapinduzi ndipo huyu kanali alipohasi jeshi na kuingia msituni, huko aliwafundisha vijana kadhaa na kuanzisha kikundi kidogo cha uasi kilichosumbua sana nchi ya Nduruta. Faili hili linasema kwamba Banginyana aliongoza mapinduzi ya pili ya kumtoa Rais Sabinus wa Nduruta na kumtangaza Brigedia Kadanse Sebutunva kuwa rais na ndye huyu mbabe mpaka sasa, hataki kuachia madaraka…”

“Doh, hiyo habari mpya kabisaaa, niliwahi kufikiri lakini kwa kuwa sikuona haja ya kumfikiri mtu huyo. Sasa hapo kuna vitu vinanichanganya Chiba,” akasigeza kiti chake mpaka pale kwenye kompyuta ya Chiba, “kwa nini baada ya mapinduzi kufanikiwa na kumweka madarakani huyo Sebutunva yeye ameingia tena msituni?” akauliza.

“Sasa hapa ndipo pa kufanyia kazi kwa sababu mchunguzi kasema tu kuwa ‘miezi michache baadae Banginyana na vijana wake wakarudi msituni…’ hii taarifa imeishia hivyo, sasa hapa mawili, kama kuna mtu alikuwa anachunguza taarifa hii basi aliuawa bila shaka au kwa nini aliacha? Mi najua CIA aking’ang’ania kitu hata kama ni miaka mia atakimaliza tu” Chiba akamaliza.

“Ndiyo imeishia hapo?”
“Yes Sir!” akajibu.
“Na we kaka yako Amata anakuharibu. Haya hebu tafuta ‘Black Page’ angalia mwaka huo ni nani aliingia kwenye hiyo kurasa nyeusi CIA,” Madam akamwambia Chiba.
Chiba akafunga lile faili kutoka katika mtandao nyeti wa usalama ambao umeunganisha karibu mashirika mengi ya kijasusi ikiwamo TSA.

“Yeah ni watu watatu tu! Mmoja Amerika kwa ugonjwa wa kansa, mwingine Afghanistan haijaandika alipigwa risasi na nani, ila imeandikwa tu alishambuliwa kwa risasi ndani ya gari yake, na huyu niiii… ok… ok huyu ni Afrika katika mlipuko uliotokea katika hoteli ya Kijelos katika mji mdogo wa Ntukuta…”

“…katika nchi ya Ndurata, sivyo?” Madam akadakia na kumalizia. Chiba alibaki akitikisa kichwa juu chini huku akisukuma kiti chake nyuma.

“Blamack Laideoff…” Chiba akataja jina hilo.
“Alikufa katika hoteli ya Kijelos, mwaka 1998 kwa bomu lililotegwa katika mkoba wa mwanamke aliyekuwa naye chumbani humo…” Madam S alieleza habari nyingi sana juu ya mtu huyo na zote hizo zilitoka kichwani hakuwa anasoma popote.

“Ebo! Madam umemeza mafaili, unatisha!” akampa sifa inayomstahili. Madam S akanyanyuka na kuchukua rimoti akawasha televisheni iliyokuwa imebandikwa ukutani. Aliitazama saa yake ilikuwa ni saa saba mchana.

‘…vikosi hivyo vya jeshi la Umoja wa Mataifa viliivamia kambi hiyo jioni ya jana na kuisambaratisha, lakini taarifa zinasema kuwa kiongozi wa waasi hao kanali Bensoir Banginyana hajapatikana.’

Ilikuwa sauti ya Charles Hilal ikitoa taarifa hiyo kupitia kituo cha BBC . Chiba na Madam S walikuwa macho kodo wakikodolea luninga hiyo.
“Dah! Kumbe wamemkosa!” Chiba akashangaa.
“Wamemkosa, unajua yule jamaa ni mpiganaji huwezi kumpata kilaini namna hiyo,” Madam S aliongezea huku akivuta kiti na kuketi.

“Kamanda lini anatua?” Chiba akauliza.
“Aaaa Kamanda anafanya biashara ya madini huko Ujerumani, hawezi kurudi mpaka apate mteja na soko la kudumu,” Madam akaeleza, “Vipi umemmiss?” akauliza.
“Hii ishu ya Ikulu inanitia uchungu sana, yaani tumedharaulika kiasi hiki? Tuingie kazini Mama tufunge mchezo,” Chiba alisema.

“Sikia Chiba, haya mambo hayana haja kuyashobokea, kazi wamepewa MI, nafikiri watafanya vizuri kwa sababu ni levo yao, siyo yetu. Unapenda sana mateso ee? Mi kwangu naona ni poa tu maana saa hizi vichwa vingekuwa vinatuzunguka, tunakimbizana huku na kule,” madam alieleza wakati huo akiuelekea mlango tayari kwa kuondoka.

“Ngoja nikwambie Madam, MI wao moja kwa moja wataanza kuwasaka hao jamaa, lakini watasahau kuchunguza hao watu wameingiaje Ikulu, kwa sababu ukichunguza wameingiaje ndipo utajua ni akaina nani, kwa mtazamo wangu mimi asilimia 60, adui yuko miongozi mwetu, na huyu adui si rahisi kumpata kama akili yako haifanyi kazi sawasawa,” Chiba akaunguruma huku akipigapiga meza yake kwa ngumi hafifu. Madam S alisimama mlangoni akimsikiliza Chiba kwa makini.

“Unachosema ni sahihi kabisa, lakini kila watu wana mbinu zao, sisi TSA tuna mbinu zetu na wao kama MI wana mbinu zao, hivyo nafikiri wataweza si unaona wanavyofanya vizuri kule Ngoko,” madam alimwambia Chiba.
“Ina maana Ngoko MI wamekwenda?”
“Chiba, Chiba, uko wapi wewe? Wakati majeshi ya SADC yamekwenda tuliombwa kupeleka baadhi ya wanajeshi katika kuunda jeshi hilo, kilichofanyika waliochanguliwa wote ni Military Intelligency, walikuwa wane, wakaenda kule lakini lengo lilikuwa pia wakafanye uchunguzi wa kujua hawa waasi wamejipanga vipi, kwa hiyo lilipokuja swala hili imekuwa rahisi kwani ramani yote ya Kusini mwa Ngoko tunayo,” Madam alieleza huku akifungua mlango tayari kutoka nje.
“Aisee!” Chiba akapiga kofi la mshangao, “Hii ndiyo nchi yetu, Mungu ibariki Tanzania. Na hao waasi watauona moto, wamuulize Nduli Idd Amin Dada atawaambia kwa nini alikimbilia Saudia,” akamaliza na kugeuza kiti chake kuendelea na kazi zake.

***
UJERUMANI MASHARIKI
SIMU YA KAMANDA AMATA ikaita kwa vurugu pale ndani ya kijikapu kidogo kilichokuwa katika stuli ndogo pembeni tu mwa kitanda. Juu ya kitanda hicho kikubwa chenye kila aina ya starehe, Amata Ric alikuwa na mwanadada mrembo wakipeana raha za dunia.
“You are so sweet buddy!” mrembo alitoa sifa kwa Amata baada ya kushughulikiwa ipasavyo.

“Mmm kawaida tu,” akajibu huku mkono wake ukikifikia kile kikapu na kuinyakuwa ile simu, akaitazama kwenye kioo na kukunja sura kidogo, akatoka pale kitandani na kumwacha Precious akiwa anagalagala.
“Yes Sir!” akaitikia ile simu.
“Bwana Spark, yule mtu niliyekwambia anasema mnaweza kuonana leo jioni saa kumi ofisini kwake,” ilikuwa sauti ya Mc Donald iliyoongea Kijerumani safi.
“Ok, niko tayari, labda ni saa ngapi na ninakwendaje?” Amata akauliza.
“Nimewapa kadi yako ya biashara, watakupigia na kukujulisha jinsi gani mtaonana,” Mac Donald akamaliza.
“Ok, asante!” Amata akakta simu. Akavuta hatua chache na kuiweka ile mezani kisha akarudi kitandani na kumkumbatia yule binti wa kizungu, Precious Nancy Heibelghen, ndimi zao zikakutana na shughuli hiyuo ikaanza upya kwa amau nyingine. Wakiwa katikati ya mchezo ambapo kila mmoja alijikuta kwenye sayari yake anayoijua yeye, simu ile ya Amata ikaita tena kwa fujo, akataka kuipuuzia lakini akakumbuka kitu, akainyakuwa na kutazama, ilikuwa ‘private call’.

“Yes, hello!”
“Unaongea na Jirack Peterson, nusu saa ijayo kutoka sasa, teremka hapo nje ya hoteli yako, utamwona mtu mmoja mwenye nywele ndefu akisoma gazeti huku kaegemea gari aina ya Jeep Cherokee nyeusi, mfuate umwombe sigara, yeye atakuonesha kiberiti. Mfuate akulete tufanye biashara,” ile simu ikakatika.
Mwili wa Kamanda Amata ukasisimka kwa ujumbe huo, akakurupuka na kuliendea dirisha, akachukua darubini yake ndogo na kutazama nje lakini hakuona jipya. Akaingia bafuni na kujiswafi.

“Wapi unaenda mya black dog, uje tuendelee,” Precious aliendelea kumbembeleza Amata.
“Kuna kazi kidogo, tuonane jioni nitakupigia simu,” Amata akajibu wakati akijitupia koti lake mwilini, akavaa saa yake yenye uwezo wa kufanya mambo mengi, kunasa sauti kupiga picha. Ndani ya saa hiyo kulikuwa na bomu dogo lenye ukubwa wa kidonge cha pirton, chini yake kulikuwa na kijibomba kidogo ambaco kwa kutumia nguvu ya mkono kama utabetua kiganja kuja juu, kinatoa risasi ndogo kama kishale na sumu yake inaweza kukuua kwa dakika tatu tu, akaivaa na kuifunga. Kisha akachukua briefcase yake na kutoka taratibu huku akimwacha yule mwanamke bado akiwa bafuni.
Nje ya hoteli hiyo, shughuli mbalimbali zilikuwa zikiendelea, maji yaliyokuwa yakiruka huku na huko yaliwafanya watoto kufurahia hali hiyo, akavuta hatua chache na kumwona yule mtu kama alivyoelekezwa, akamwendea.

“Sigara tafadhali,” akamwambia, na yule mtu akamtazama Amata kisha akaingiza mkono mfukoni akatoa kiberiti cha gesi na kukiwasha, alipozima alifungua mlango wa ile Jeep na kumtaka Amata kuingia ndani, akafanya hivyo na mlango ukafungungwa.

“Mr. Spark, utanisamehe kwa hili, hutakiwi kujua mwenyeji wako anapatikana wapi,” yule jamaa akamvalisha sox nyeusi na kuuficha uso wako, watu wengine wawili zaidi wakaingia upande huu na huu naye akawa katikati.
Gari iliendeshwa kwa takribani nusu saa mpaka ilipoegeshwa kwenye moja ya majumba makubwa nay a kifahari sana nje kabisa na mjini. Amata akahisi kuwa wamesimama getini kisha akjua kuwa gari imeegeshwa ndani ya kitu kama chumba kutokana na muungurumo wake kuwa na mwangwi, akilini mwake alikuwa akihesabu kona zote walizokuwa wakipind naye akapata kona tatu na alijaribu kuhesabu kila kona moja na nyingine walitembea dakika ngapi na kumbukumbu hiyi yote akaiweka kichwani. Akatshushwa garini na kushikwa mkono mpaka ndani kabisa, akahisi kaingizwa kwenye lifti kwani alihisi ile hali ya chombo hicho kikiwa kinaelekea juu. Wakamtoa na kumwongiza chumba kingine kisha akakalishwa kitini. Ukimya ukatawala ile sox bado ilikuwa kichwani mwake kabla ya kuondolewa na mtu aliyekuwa mbele yake.

Amata akafikicha macho na kujiweka sawa, akamtazama watu wawili walio mbele yake, mmoja alikuwa ameketi kitini na mwingine alikuwa amesimama ndani ya suti ya gharama sana, zaidi ya hapo ule ukumbi ulikuwa mkubwa sana usio na kitu ndani yake.

“Mr. Spark, karibu sana,” ilsikika sauti ya tule bwana aliyekuwa ameketi kitini, uso wake ulionekana ni mtu wa makamo huku madevu aliyoyafuga yalikizunguka kinywa chake, alikuwa ndani ya vazi la kawaida lakini ukiliangalia utajua tu gharama ya vazi hilo unaweza kununulia gari moja ya wagonjwa.
“Asante sana Mr…”

“Jirack Peterson!” akadakia na kumalizia yeye mwenyewe.
“Nina dakika kumi tu za kuzungumza, sasa twende kwenye lililotukutanisha,” yule bwana akamwambia Amata. Amata akafungua briefcase yake na kutoa sampuli moja ya alamasi akampatia yule bwana, naye akaipokea na kuwasha kijitochi chake kidogo, akaiangalia kwa makini, kisha akaiweka mezani na kutikisa kichwa.

“Hii ni sampuli hadimu sana, umeipata wapi?” akauliza.
“Mimi ni mfanya biashara, sampuli hii nimepata huko kwetu Afrika katika, katika machimbo ya Bagon,” akajibu.
“Bagon, Bagon, ha! Ha! Ha! Naijua sana sehemu hiyo. Sawa, mimi niko tayari kufanya biashara na wewe, lakini sijajua biashara yetu mi na wewe tunafanyaje. Kwa sababu hapa ninafanya biashara na watu wengi sana, biashara za cash, na pia zile za kubadilishana vitu, unanipa almasi name nakupa ndege,” Jirack alieleza. Amata akameza mate baada ya kuona koo limemkauka, akainua na glass ya maji akajijiminia kinywani.

“Sawa nimekuelewa bwana Jirack, nina mzigo huo na mwingine huu hapa,” Amata akatoa sampuli nyingine akampa. Jirack akaichuykua na kufanya vilevile, akaiangalia na kubaki kakodoa macho.
“Na hii, umepata wapi? Maana ni almasi hadimu sana, nina mtu mmoja tu anayeniuzian kutoka Afrika nay eye mgodi wa almasi hii ni wake,” Jirack akaeleza huku akiiweka mezani ile sampuli.
“Ni nani huwa anakuletea na anasema mgodi huo ni wake?” Amata akeleza.

“Aaa Mr. Spark biashara hizi zina usiri mkubwa sana, siwezi kukueleza juu ya mteja wangu, na wala simwezi kumweleza mwingine juu yako. Kitu ambacho tutafanya mimi na wewe, kwanza tuiache hii sampuli ya pili, na tufanye biashara ya hii sampuli ya kwanza. Kwa sababu hii sampuli ya pili inaweza kuleta matatizo,” Jirack akaeleza.
“Sawa Mr. Jirack, kwa kifupi sampuli hii ya pili nimeepata huko Afrika, Magharibi mwa Tanzania, kuna machimbo makubwa ya almasi,” Amata akaeleza.
“Ok, tutaizungumza hilo. Sasa hiyo sampuli ya kwanza ya Bagon niko tayari kufanya kazi na wewe, je utaileta mwenyewe au nitume vijana wangu waje kuichukua kadiri ya biashara yetu?”

“Utakaponipigia simu tutapanga biashara nzima,” Amata akamwambia Jirack. Vijana watatu wakatokezea mbele yake kupitia milango tofauti. Na mara hiyo mwanadada mmoja alitokea katika ukumbi ule mkubwa na moja kwa moja alimfikia Mr. Jirack na kumnong’oneza jambo. Kamanda Amata akaikutanisha mikono yake na sekunde hiyo hiyo alipiga picha takribani ishirini za yule mwanamke kwa kutumia saa yake pasi na mtu yeyote kujua. Wale vijana wakamfunika lile sox na kuondoka naye kwa mtindo uleule....
------------------------------------------------------------------
Ikinge familia yako dhidi ya Corona Pasaka hii... Kaeni nyumbani kama hakuna haja ya kutka nje

#StopCorona
--------------------------------------------------------------------

Kamanda Amata alitulia chumbani kwake peke yake, akaivua ile saa na kuchukuwa waya wa USB akaunganisha kisha akauchomeka kwenye simu yake kubwa na kupakua zile picha pamoja na sauti ya mazungumzo aliyokuwa akiirekodi kati yake na Mc Donald na kati yake na Jirack Peterson, alipohakikisha zimeingia zote sawasawa, akazituma kwa Chiba moja kwa moja ili kuhakikisha kila kitu kipo salama, kishapo akaweka vitu vyake vizuri tayari kwa kazi ya pili ya kibiashara.

Usiku wa siku hiyo ukamkuta Kamanda Amata ndani ya Cassino la kisasa katika moja ya hoteli kubwa hapo Berlini. Akiwa katikati ya kaunta akiendelea kupata kinywaji chake Couvosier alihisi kuguswa begani, alipogeuka akagongana macho na mwanadada aliyevalia gauni refu la kumetameta. Amata alimtazama mwanamke huyo, sura yake kama aliijua lakini hakukumbuka wapi ameiona.
“Habari ya jioni!” yule mwanamke akamsalimu Amata.
“Nzuri, u mwanmke mrembo sana,” akamsifia na kumwangalia kutoka juu mpaka chini, mkono wake mmoja ukampapasa kalio.

“Tafadhali, sio wa aina hiyo,” aksindikiza na sonyo refu.
“Oh samahani sana kwa hilo, karibu sana unatumia kinywaji gani?” akamwuliza lakini yule mwanamke hakujibu lolote badala yake alikuwa akimwangalia Amata bila hata ya kupepesa macho. Amata akashusha kinywaji chake na kumwangalia yule mwanadada wakati huohuo nyuma yake akahisi kushikwa mbavuni alipogeuka akutana na Precious Nancy.

“Yes my queen!” akamsalimu kwa namna hiyo, huku akimpa bilauri iliyo tupu na kummiminia kinywaji.
“Mr Spark!” yule mwanamke wa kwanza akaita kwa sauti ya upole.
“Sema mrembo, maana naona unaniangalia tu bila kusema lolote,”
“Nakupenda, u kijana mzuri mtanashati,” kisha akamwangalia tena kwa makini, “Njoo nje nina shida na wewe!” akaondoka.
Kamanda Amata akageuka kwa Precious Nancy, akamtazama kwa jicho la mahaba.
“Nisubiri mpenzi!” akamwambia.
“Mpenzi wako nani, unafikiri mi naweza kushare mapenzi na mwanamke mwingine! Na tunakwenda wote hukohuko,” Precious akawa mkali mpaka watu waliokuwa jirani kwenye kaunta ile walibaki kuwatazama. Kamanda Amata akaondoka na kukatisha katika makundi ya watu waliokuwa kwenye burudani mbalimbali, akatoka mlango mkubwa na kumkuta yule mwanamke akiwa amesimama ngazini.
“Jina lako tafadhali,” Amata akamwambia akiwa kasimama nyuma yake.

“Haina haja ya kujua jina langu, nimetoroka kuja kukwambia jambo moja tu…”
“Umetoroka wapi? Mbona sikuelewi. Kwanza we ni nani?” Amata akang’aka huku akimshika began a kumgeuza, mara hii wakawa wanatazamana. Yule mwanamke akateremka ngazi mpaka kwenye maegesho ya cassino hiyo, Amata naye akamfuata hukohuko.
“Sikia, wewe si Mr. Spark, wewe ni Amata Ric, taarifa zako zimefika katika mtandao wa baba yangu, na najua nini kitafuata kwani wao hawana mchezo katika kazi yao. Wewe ni spy umegundulika, nakuomba uondoke haraka sana kwani hata mimi nitakuwa mashakani ikigundulika nimekwambia hili,” yule mwanamke alipomaliza kusema hayo, akaondoka zake na kuingia kwenye moja ya gari za kifahari zilizokuwa zimeegeshwa hapo na kuondoka nayo.

“Shiiiiiit!” akajisemea kwa sauti ndogo huku akibana meno yake, akageuka kurudi kule kwenye casino, alipogeuka tu akagongana kikumbo na Precious Nancy. Kamanda haukuongea kitu isipokuwa kumwangalia tu mrembo yule mwenye macho ya buluu, alikuwa mazungu haswa!
“Hey my buddy! Vipi?” akaongea kwa lugha ya kiingereza.
“Fine fine,” akavuta mkono na kurudi naye ndani, mara hii akaenda kujiunga na kundi la wacheza kamali kwenye mchezo aina ya Poker.

Itaendelea...
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI -I- hujuma na uzandiki
MTUNZI: richard MWAMBE
Simu 0766 974865

“Shiiiiiit!” akajisemea kwa sauti ndogo huku akibana meno yake, akageuka kurudi kule kwenye casino, alipogeuka tu akagongana kikumbo na Precious Nancy. Kamanda haukuongea kitu isipokuwa kumwangalia tu mrembo yule mwenye macho ya buluu, alikuwa mazungu haswa!
“Hey my buddy! Vipi?” akaongea kwa lugha ya kiingereza.
“Fine fine,” akavuta mkono na kurudi naye ndani, mara hii akaenda kujiunga na kundi la wacheza kamali kwenye mchezo aina ya Poker.

SEHEMU YA IV

3
BENSOIR BANGINYANA aliketi na makamanda wake wa juu kabisa katika kikosi chake cha X65. Hakuna ambaye aliruhusiwa kuongea mbele ya kanali huyo. Hakuna asiyemjua kwa ukatilia wake pindi tu unapombishia jambo ambalo yeye anaamini likiwa hivyo ndipo mafanikio yatakuja.
“Jamani hapa tuna jeshi lililojipanga haswa! Lazima tuwe makini na kila mmoja apange watu wake vyema!” aliwaambia makamanda wake waliokuwa wamemzunguka, “Tayari wameisambaratisha ngome yetu ya Mpumbutu, na najua ni wale vijana wawili watakuwa walifanya uchunguzi kuijua ilipo au watu wa Mpumbutu wamewaonesha,” akaongeza.

“Mkuu, nina uhakika watu wa Mpumbutu watakuwa wamewaonesha kambi ilipo, na kama ni huvyo, tupe ruhusa tukawafunze adabu,” kamanda mmoja akasema na wazo lake likaiutikiwa na Banginyana.

“Lakini tukumbuke kulinda migodi yetu, hii ndiyo migodi inayotoa almasi yenye thamani sana duniani, ni vipi kama watu hawa wakiivamia si tutakosa kila kitu!” kamanda mwingine akadakiaza maneno.
Banginyana akaonesha ishara ya kuwa wote wanyamaze, na walipotulia akainua simu yake ya mezani na kupiga mahala Fulani.

“Mkuu wa wakuu, ni jeshi gani lililopo huku msituni linatusumbua hivi, yaani ni kama mashetani kwa sababu ukiwasaka hawaonekanai walipo, wamesambaratisha ngome ya Mpumbutu na sasa nina wasiwasi wasije kufika migodini kule Lugombesi maana si mbali kutokam hapa…” aliongea kwenye simu.

“Kwanini mnashindwa kuwakabili nanyi ni magorilla mliobobea? Kanali Banginyana, uwezo wako wa upiganaji unauficha wapi?...” sauti ya upande wa pili ikamwambia. Ukimya ukatawala kati ya watu hao kisha Banginyana akajibu.

“Sikia Mkuu wa wakuu, kiukweli hapa tunahitaji silaha za kisasa sana kuweza kuwakabili hawa wendawazimu, tukiwa na silaha kama zao tutawadhibiti vyema na tutafutilia mbali uwepo wao, kwanza ni nani aliyewatuma wakati kila mmoja tuna mkataba naye?”

“Sikiliza Banginyana, hilo usiliwaze, hao wanajeshi sio wa Umoja wa Mataifa, ni kutoka Jeshi la Tanzania. Sasa naomba uje huku Nduruta ili tuweke mambo sawa, askari wote waambie wahakikishe ulinzi wa eneo,” ile sauti ya upande wa pili ikamwelekeza, kisha simu ikakatika.

Banginyana akawaangalia watu wake, “Sikilizeni, nakwenda Nduruta nitarudi ndani ya saa kumi tu, hivyo hakikisheni usalama wa eneo nyeti, na kikosi kimoja kiende Mpumbutu kikawatie adabu watu wa pale,” akamaliza kusema na kunyanyuka, vijana wake akampigia saluti za ukakamavu wakati kanali huyo akitoka ndani ya jengo hilo huku mlinzi wake akimsindikiza.

NCHI YA NDURUTA

KATIKA MAKAO MAKUU ya nchi ya Nduruta, kikao cha watu wawili tu kilikuwa kikiendelea. Rais wa Nduruta Brigedia Kadanse Sebutunva na Kanali Bensoir Banginyana walikutana kwenye chumba Fulani ndani ya jengo hilo, Banginyana aliingia hapo kwa siri na hakuna hata mtu mmoja aliyembaini.

“Mkuu, tunahitaji silaha nzito sana!” Banginyana akamwambia Rais Sebutunva.
“Usijali, wiki hii natakiwa nipeleke madini kule kwa wale matajiri wetu ili waendelee kutupatia pesa kwa ajili ya operesheni hii, unajua nchi yetu sasa hivi ni tajiri sana japokuwa ni kanchi kadogo tofauti na hiyo Tanzania inayojidai kimbelembele. Kwanza swala la huko Tanzania niachie mimi, najua cha kufanya na mpaka watakapokuja kugundua tayari nitakuwa nimeshawamaliza the! the! the! the!” rais aliongea na kuangusha cheko.

“Mimi nilifikiri tufanye juu chini tuwazibe midomo!”
“Aaaaaaa! Hawazibiki, kwanza Rais wao ni jeuri si unajua kuwa alikuwa mwanajeshi pia hivyo ana ile jeuri ya kijeshi ijapokuwa yeye aliishia kwenye vyeo vya chinichini. Mimi ni Brigedia na kule Tanzania nimeshapandikiza watu wangu katika kila idara nyeti, hivyo ile nchi yote iko hapa. Lakini nayamezea mate sana madini yao, yaani ipo siku nitayatia mkononi,” Rais Sebutunva akamwambia Banginyana.

“Sasa mkuu wa wakuu, unajua ile ndoto yako ya kuinua himaya yako ya Paramado itatimia kama tukiyapata na haya machimbo ya huko Tanzania. Kama vipi tugawe wale gorilla wengine waende huku wakavamie na kuanza kazi kama tulivyofanya huko Mpumbutu,” Banginyana alipendekeza.

“Aaaaah! Banginyana, hiyo siyo mbinu hata kidogo. Katika swala la usalama Tanzania usiiguse, wale inabidi kuwavamia kidiplomasia tu, kuweka mapandikizi yetu kama ambavyo nimefanya. Tutayapata yale madini kwa kuwekeza na wao kuwaminya, lakinikwa kutumia mtutu pale sahau, usione wapole vile, wabaya sana wale. Tuyaache hayo! Kesho kutwa mzigo wa almasi unatakiwa uende Amerika na Ulaya kwa wale wateja wetu, yule mteja wa Ujerumani atatupatia silaha za kisasa badala ya pesa, hizo zikija ndiyo utakuwa mwisho wa hao wanaojiita wanajeshi wa nini sijui, kwa hiyo kapange watu wako waweke ulinzi. Wewe utatakiwa uende mwenyewe Ujerumani ili ukaone vifaa vinavyofaa kwa kazi yetu ya msituni, nazani nimeeleweka sivyo?” Rais Sebutunva alimaliza, wakakubaliana na kuweka mipango sawa, kisha banginyana akarudi msituni kwa njia ileile ailiyokuja nayo.

--------------------------------------------------
Corona inazuilika... Fuata maelekezo ya Wizara ya Afya

Kaa nyumbani...

#StopCorna
-------------------------------------------------------------

DAR ES SALAAM-TANZANIA

RAIS WA TANZANIA, Mheshimiwa Robert Sekawa alikuwa kimya akisikiliza taarifa za kiintelijensia kutoka kwa kiongozi wa kitengo cha MI kutoka Jeshi la Wananchi.
“Tafiti zetu zinaonesha kuwa watu waliovamia hapa na kufanya unyama ule ni watu kutoka Nduruta kwa kuwa mpaka sasa ni rais wa nchi hiyo ambaye hatuna uhusino mzuri kidiplomasia,” yule kijana aliyevaa kombati zilizochafuka kwa vyeo alikuwa akimwambia rais Sekawa. Umakini wa rais huyo katika kusikiliza ulimkumbusha ile simu aliyopigiwa siku tatu zilizopita.

“Umenikumbusha! Hilo usemalo lina ukweli, juzi nilipigiwa simu na watu nisiowajua wakidai kuwa nisichukue hatua yoyote ya kumtafuta mke wangu isipokuwa niondoe majeshi kule Kusini mwa Ngoko,” rais akaeleza.
“Nafikiri hapo utathibitisha uchunguzi wetu wa awali, kwa hiyo bila shaka Nduruta ndiyo adui yetu mkubwa,” yule mwanajeshi kijana akaeleza.

“Ok, bila shaka hawa waasi kule Kusini mwa Ngoko ni watu wake, au ninyi mnaonaje?” akauliza.
“Kwa simu uliyopigiwa mheshimiwa ambayo sasa inabidi tuifanyie kazi kabla hatujasema ndiyo au hapana. Kama hiyo simu tukiipata na kuisikia upya bila shaka tutasema ndiyo wale waasi ni watu wake,” yule kijana aliongeza. Rais Robert Sekawa alikunja sura na kuonekana kuwa na hasira za wazi kabisa.

“Endeleeni kuchunguza na mkibaini ni wao waliyofanya haya, lazima tuwavamie kijeshi na tutahakikisha tunafagia takataka zote, asanteni sana. Mkuu wa majeshi naomba uwaongezee nguvu vijana kule Kusini mwa Ngoko kwa kuwapelekea silaha nzito, naona sasa kazi inaanza,” rais Sekawa akamaliza na kuwapa mikono kisha wakaagana naye akabaki peke yake ofisini. Macho yake yalionekana wazi kushikwa na hasira ya wazi, alivuta moja ya faili lake na kulipekua pekua kurasa hii na ile, akashika ukurasa fulani na kuutazama vizuri. Juu kabisa ya ukurasa huo kuliandikwa The DEAD Line kisha ukapigiwa mstari mwekundu pale chini, akasoma kurasa ile na kuchukua kalamu yake, akataka kuandika kitu fulani, alipoanza tu mlango wake ukafunguliwa, akalifunga lile faili na kuliweka kwenye sefu ya chini kabisa akalifungia humo.

“Mheshimiwa kuna ugeni unakusubili kama ilivyo ratiba yako ya leo!” kiongozi wa usalama wa rais alimpa taarifa hiyo na kumruhusu kupita mlangoni. Katika sebue kubwa iliyopangwa samani zake vyema na nyingine zilionekana kuwa ni mpya ambazo ziliwekwa badala ya zile nyingine kuvunjika. Wale wageni walisimama mara tu walipomuona kiongozi huyo akiingia katika sebule hiyo pana akiongozana na watu wengine wawili akiwamo katibu na mwandishi wake. Wakasimama na kupeana mikono huku wakimpa pole kwa kila lililotokea, wageni hao walikuwa maofisa wakubwa wa kibalozi. Mmoja alikuwa ni balozi kutoka Umoja wan chi za Ulaya akisindikizwa na msaidizi wake, lengo na madhumuni ya safari yao ilikuwa ni kutoa salamu za pole kwa serikali ya Tanzania baada ya tukio hilo lililoitwa la kigaidi.

“Pamoja na hayo yote, tuliona tukupe msaada wa vyombo vya uchunguzi kutoka nje, tulifikiri FBI wangekusaidia sana katika hili,” yule balozi alimwambia Rais Sekawa.
“Nashukuru, lakini ni mapema mno kuamua hilo, vyombo vyetu viko kazini na vinaendelea vyema kabisa katika kazi zao,” alijibu. Mazungumzo mengine yakaendelea na kukubaliana kuwa itakapofika muda wa kuhitaji msaada huo basi wangewapa taarifa hiyo. Lakini hata hivyo ofisi ya balozi huyo iliaahidi kuleta wanausalama kadhaa kwa ajili ya uchunguzi wa hapa na pale. Ijapokuwa ilikuwa ngumu kwa serikali kukubali lakini libidi kuwa hivyo.

***
UJERUMANI

KANALI BENSOIR BANGINYANA alipokelewa uwanja wa ndege wa Berlini na kuchukuliwa moja kwa moja mpaka nje ya jiji hilo na huko akapakiwa kwenye helikopta iliyompeleka mbali zaidi karibu na mpaka wa Ujerumani na Luxembourg. Akiwa na watu wawili katika msafara wake waliwasili kwa mwenyeji wao jioni ya siku hiyo na kikao cha biashara kilichoambatana na kula na kunywa kati yao na Jirack Paterson kilichukua nafasi.

“Safari hii naona umeleta mzigo mkubwa zaidi!” Jirack akamwambia Banginyana
“Unajua kule sshamba tuna tatizo jipya, si unakumbuka tuliyatoa yale majeshi ya SADC, sasa kuna jeshi la Tanzania limewekwa kule kwa ajili ya kukomesha waasi. Kiukweli bwana Jirack lile jeshi ni mwiba mkali tena wa sumu, siku tano zilizopoita almanusura waniondoe, kama si mbinu zangu za kikomandoo kuondoka eneo lile, aaaaaaaa, redio na televisheni za ughaibuni zingeingiza hela kwa habari hiyo,” Banginyana akaeleza.

“Pole sana, hao inabidi washughulikiwe kama wale waliojifanya wajanja kule Sierra Leone, tuliwasafisha kabisa. Sisi tunataka madini na ili tuyapate tunaweka mbinu nyingi sasa we ni nani utuzuie wakati viongozi wenzako wote wanakula hapohapo,” Jirack akaonesha kuhuzunishwa na hali hiyo.

“Sasa nimekuja na mzigo mkubwa kama mlivyoongea na Mkuu wa wakuu, tunahitaji silaha nzito za kuwashughulikia wale manyang’au, wanaojiita Jeshi la Tanzania…”
“Jeshi la Tanzania, linajiita jeshi wakati hata vita waliyopigana ya maana hatuioni!” Jirack akamwita mwanadada mmoja aliyekuwa hapo, akamnong’oneza kitu kisha akatulia kitini na yule mwanadada akaelekea kwenye kijichumba Fulani na baada ya kama dakika moja hivi akatoka na simu kubwa mkononi, akamkabizi Jirack. Kwa kidole chake cha kati akabofya tarakimu fulani fulani kisha akaiweka sikioni. Ilipopokelewa akaongea kama dakika ishirini hivi kwa lugha ambayo Banginyana hakuielewa kabisa, alipomaliza akakata ile simu na kumtazama kanali huyo usoni.

“Umepata! Wadau wamesema silaha zipo tena za kisasa ambazo hakuna jeshi la nchi yoyote Afrika inalozimiliki,” Jirack akamwambia Banginyana huku akiinua bilauri yake ya pombe kali na kuipunga hewani kisha akapiga funda mbili nayo ikakauka.
“Nashukuru yaani unipe hata ‘kifaru’ ikibidi ….”
“Oh! No! No! Banginyana kifaru huwa tunatoa kwa majeshi ya serikali ambayo yana mkataba nasi tu, kwa makundi yenu ninyi hatuwapi vifaru kwa sababu kifaru bwana ni ishara ya vita, nyie yale yenu ni mapigano tu. Tutawapa bunduki za kisasa, mabomu ya kisasa, badala ya kifaru tutawapa LPG za kisasa kabisa. Mwenyewe utaziona na tutazileta kwa njia yetu ileile, we usijali, kutoka sasa ni saa ishirini na nne zitakuwa pale,” Jirack alimkatisha na kumwambia maneno hayo.

“Sawa, nashukuru sana!” Banginyana akamalizia.
“Sasa bwana Bensoir, mimi katika biashara yangu hii huwa sina ubinaadamu kabisa nafikiri hata wewe pia. Nilimuua mke wangu kwa sababu alikuwa anatoa siri zangu nje mpaka nikaingi matatizoni na watu Fulani, sikuona haja ya kumuacha awe tatizo kwangu, nikatuma vijana wakamuondoa. Sasa lazima ujue kuwa mtu yeyote anayetoa au kuniharibi biashara zangu kwangu hana haki ya kuwa na maisha au ya kuishi hapa duniani. Mimi nina jeshi kama ilivyo serikali nyingine, timu yetu tupo nane, tuna pesa kama matundu ya neti, pesa kwetu ni kila kitu na si uhai wa mtu.” Aliposema hayo akamwita yule mwanadada na kumnong’oneza kitu kisha yule mwanadada akaondoka.
Muda mfupi baadae yule mwanadada alirudi na nyuma yake alifuatiwa na bintiu mrembo sana mwenye nywele ndefu zenye rangi ya dhahabu.

“Ni binti yako?” Banginyana akauliza huku akijilamba ulimi kwa jinsi binti yule alivyokuwa mzuri wa sura na umbo.
“Yeah, ni binti yangu anaitwa Butterfly!” Jirack akajibu. Na mara hiyo yule binti akaketi kitini pamoja na watu hao wane waliokuwa wakila na kunywa. Baada ya kusabahiana na waliopo, Jirack akamtazama binti yake kwa jicho kali sana.
“Butterfly, ulichokifanya juzi sicho, kinaniuma mpaka kwenye uvungu wa moyo wangu,” akamweleza.
“Kitu gani baba?” yule binti akuliza kwa woga.
Jirack akawatazama Banginyana na vijana wake, “Kanali Bensoir Banginyana, tusipotumia akili ya ziada tutapata pigo. Kuna mtu anaitwa Mr. Spark, mmewahi kumsikia?” akauliza na wao wakajibu kwa vichwa kuwa hawamjui.
“Huyu bwana amekuja hapa kufanya biashara ya madini tena ya almasi, alikuja na sampuli mbili, moja ya Bagon na nyingine ya Mpumbutu!” akawaeleza.

“Ya Mpumbutu?” banginyana akashtuka na vijana wake nao wakabaki kukodoa macho.
“Ndiyo, ya Mpumbutu. Alielekezwa kwangu na Mc Donald. Nmeshtushwa sana ameipata wapi ile sampuli ilhali ni ninyi wenye ule mgodi? Ina maana kuna mtu kaingia ndani yenu na ninyi hamna habari, ulinzi wenu uko wapi?” Jirack akaeleza kwa uchungu, “baada ya kumchunguza huyu bwana kwa kuingia kwenye mitandao ya watu hatari tukampata kuwa si mfanya biashara ni spy kutoka Tanzania anaitwa Amata Ric au amezoeleka kwa jina la Kamanda Amata, Tanzania Secret Agent namba moja alikuwa ameketi hapa na mimi,” akaongeza.
Taarifa hiyo, ilimfanya Bensoir na vijana wake kutazamana huku kijasho chembamba kikiwatiririka kwa zamu, Banginyana alihisi ganzi mwili wote.

“Simjui mtu huyo,” Banginyana akaeleza.
“Ni mtu mmoja matata sana, huwa hashindwi kitu akiamua kukivuruga, mi mwenyewe sikumjua kabla lakini file lake nililolipata mtandaoni, ni mtu hatari, akili yake ni 3D…”
“Yuko wapi sasa tumshughulikie asije kuwa tatizo kwetu,” Banginyana akang’aka na sura yake ikabadilika na kuwa ya kiumbe kibaya kabisa. Yule binti pale jirani yake ailikuwa akitetemeka muda wote.
“Nilikuwa nimemweka vizuri iuli nimchunguze, na nikamjua lakini unamwona huyu binti, huyu binti yangu, sasa amemchezea samba sharubu. Juzi amkwenda kwa Spark, akamwambia habari zote kuwa tumemgundua, na sasa yule bwana haonekani kwa sababu huyu Butterfly alimwabia kuwa tunataka kumuua hivyo aondoke, na yule bwana ametoweka lakini najua yuko hapa Ujerumani kwani watu wangu kwenye kona zote za kutokea nje ya nchi hawajamwona mtu huyo iwe ka sura wala kwa jina, lakini nimefanya msako kila mahali sijagundua alipo, tazama mtu huyu alivyo hatari, katoweka mbele ya macho yangu ambayo si rahisi binadamu mwenye nyama kuyatoroka,” Jirack akaeleza kwa uchungu, “Lakini yote hayo ni huyu binti Malaya,” akamtazama binti yake, “rudi chumbani kwako nisikuone hapa, ala!” akamwambia yule binti naye akanyanyuka haraka huku akilia. Jirack akachomoa bahasha chini ya meza yake na kumpa Banginyana, ndani yake kulikuwa na picha za Kamanda Amata wakati anazungumza na Jirack. Banginyana akazitazama zile picha kwa makini sana na kuwapa vijana wake nao wakazikodolea macho kwa zamu.

“Kabla sijaondoka hapa, roho yake naihitaji,” Banginyana akamwambia Jirack.
“All the best, Bensoir!” tuwasiliane saa tatu kabla hujaondoka hapa Ujerumani, kwa lolote katika msako wako wasiliana na kijana wangu. Lakini uwe makini sana na huyu kiumbe maana hapa nilipo nashindwa kujua wapi yupo, ila nikijua tu alipo nitakujulisha ili umshughulikie,” Jirack akamaliza na kuagana na Banginyana na timu yake.

***
Katika viunga vya mji wa Mannheim, kilomita kadhaa kutoka mpaka wa Ujerumani na nchi ndogo ya Luxembourg ndiko kulikokuwako kasri kubwa sana la tajiri Jirack Peterson ukiacha lile jumba lake la kule Potsdam ambako Kamanda Amata ndiko alilokutana na tajiri huyu, bado alikuwa na majumba mengi sana ya kifahari ambapo kila jumba alikuwa na watu anaokutana nao na kuna wengine hata balikuwa hakutani nao ndani ya Ujerumani.
Kamanda Amata aliishusha darubini kutoka machoni pake alipokuwa akiiangalia ile helikopta ikitua taratibu ndani ya jumba hilo katika mji wa Potsdam. Akiwa ndani ya mavasi ya kizee, nywele nyeupe alizozigeuza haraka haraka na ngozi yake ya kihindi iliyopchoka, aliiweka ile darubini kwenye koba lake wakati ile helkopta imepotelea ndani ya wigo mkubwa wa lile jumba lililo peke yake pembezoni mwa jiji la Berlin. Akaanza kujivuta taratibu kwa mwendo wa kizee mpaka mbele ya jumba lile ambapo alishuhudia gari mbili zikitoka kasi kuelekea mjini. Kamanda Amata akavuta hatua nyingine za kutosha na kufika katika jengo fulani, akaingia na ndani yake kulikua na vyoo vingi. ndani ya choo kimojawapo akabadili baadhi ya mavazi, akaonekana si mzee tena bali ni mtu wa makamo, sharubu za kubandika alizozisokota vyema zilimpendeza kabisa, akatokea mlango wa pili na kuingia kwenye gari alilokuwa ameegesha huko nje pamoja na gari nyingine nyingi ambazo huwekwa kwa ajili ya kuharibiwa kwani zimepita muda wake.

Akaitekenya na kuiingiza barabarani kisha akakamata barabara kubwa ya kuelekea Berlin. Baada ya kukamata barabara ya mwendo kasi kabisa ilimchukua dakika kumi na tano tu kuzikuta zile gari mbili, alizipita kwa kuwa zenyewe zilikuwa katika barabara ya mwendo wa kawaida. Kilometa tano mbele kulikuwa na makutano makubwa ya barabara, Kamanda Amata alihama kutoka ile barabara na kuchukua nyingine kisha akatoka nje kabisa na kuegesha gari katikakituo kikubwa cha mafuta. Dakika kumi baadae zile gari zikapita naye akaingia tena barabarani na kuchukua njia ileile, sasa alikuwa akiwaona muda wote.

HOTEL LOUISA – BERLIN
ZILE GARI MBILI ziliwasili kwenye hoteli hii iliyowekwa kwenye majengo ya kizamani sana, Maghalibi mwa jiji la Berlin karibu kabisa na Wilmesdorf. Banginyana na vijana wake wakateremka na mizigo yao ikaingizwa ndani na wahudumu. Yote haya Kamanda Amata alikuwa akiyatazama kutoka kwenye gari yake aliyoiegesha pembezoni mwa hoteli hiyo. Dakika hiyo hiyo ile gari moja ikaondoka na kubaki moja. Biashara nzuri sana, kumbe, sasa nimepata jibu la kazi niliyopewa, Amata aliwaza huku akitikisa kichwa na kuandika kwenye kijitabu chake huku tayari akiwa na picha kadhaa alizozipiga kupitia katika darubini yake. Taratibu akaiondoa gari yake kuiweka maegeshoni kisha akashuka na kuchukua tax akarudi hotelini kwake. Hakupoteza muda aliingia maliwato na kuurudisha ule mwili wake uliozoeleka siku zote, alipomaliza akarudi chumbani na kujiweka mbele ya kioo akichonga vindevu vyake kwa namna ya kupendeza. Akiwa ametingwa na kioo mlango wake ukabishwa hodi ya fujo, akachukua bastola yake na kuiweka tayari, akauendea mlango na kuufuangua kwa ghafla akamshika mkono huyo aliyemwona na kumrusha kitandani, kisha akaufunga mlngo kwa mguu wake huku bastola ikielekea pale kitandani.

“Usiniue, usniue Mr Spark!” ilikuwa sauti ya Butterfly, sauti nyembaba nzuri ambapo akiongea utafikiri anaimba.
“Kwa nini unakuja bila taarifa nyakati mbaya kama hizi?” Amata akauliza.
“Ukiona hivi ujue kuna sababu, Spark kwa nini hujaondoka? Watakuua, hakika watakuua, na sasa wamejua kuwa bado upo ijapokuwa uliwatoroka.” Yule binti akasimama na kumwendea Amata, “Sikiliza, mi nakupenda sana japo nimekuona leo mara ya tatu tu, nyumbani kwetu huwa wanakuja watu wengi sana kufanya biashara na mzee, biashara za kidhalimu zinazogharimu maisha ya watu wengi sana huko katika nchi za dunia ya tatu. Sikuona hilo juu yako, nilijua una nia ya biashara lakini wao wangekuzunguka. Upo hatarini, ondoka Spark, kama huwezi mi nitakutorosha kwa njia yoyote ile,” Butterfly alimwambia Amata.

Akairudisha bastola yake mahala pake na kumkumbatia yule binti, kisha nyuso zao zikakutana, “Kwa nini unitoroshe? Kwa nini usinihifadhi?” akamwuliza huku akimtomasatomasa mbavuni, Butterfly alijitahidi kujitoa kwenye mikono ya Amata lakini alijikuta hawezi, taratibu akaanza kulegea.
“Nitakuhifadhi wapi?” akauliza, “mimi ninaweza kukutorosha tu bila kujulikana,” akaongeza.
“Nihifadhi moyoni mwako…”
“Oooh please Spark,” yule binti alijikuta akipewa mabusu kutoka kwa Amata, alilalamika lakini alishindwa kuchomoka kwenye ile himaya. Kamanda Amata akakutanisha ulimi wake na wa yule binti mrembo mtoto wa tajiri, kisha wakaangukia kitandani nacho kikawapokea bila kinyongo.
Zilikuwa saa mbili za shughuli nzito juu ya kitanda hicho, Butterfly alikutana na jogoo la kiafrika lililompa raha za ajabu, alilalamika kimahaba, akashughulika vya kutosha, alihakikisha anakwanguliwa mpaka tone la mwisho. Simu ya Amata ikakatisha raha walizokuwa wakipena bila kuchoka, kila Amata alipotaka kutoka, yule binti alihitaji tena na tena. Amata akainyakua ile simu kwa taabu sana na kuiangalia kwenye kioo, ‘private call’, akaifyatua na kuweka sikioni.

“…Mr. Spark… naona sasa biashara yetu imechukua sura mpya. Baada ya kunionesha sampuli za almasi sasa naona unanionesha sampuli nyingine ya utaalamu wako wa kufanya mapenzi na binti yangu, umenitukana, sasa nimeamua kukufungisha ndoa na huyo Butterfly, muishi pamoja mpaka kifo kiwatenganishe…” ile simu ikakatika. Kamanda Amata akakurupuka na kusimama pembeni akiwa kama alivyo, akavuta taulo na kujifunga haraka haraka, akaliendea dirisha na kutazama nje, akarudi ndani na kufungua mlango, akaangaza huku na huko ndani ya kile chumba.
“Mr. Spark! Kuna nini mbona unahangaika…” binti akauliza.
“Wewe ndiyo Butterfly?”
“Ndiyo mimi, unasemaje Spark?”
“Chukua nguo zako uende, hapa tayari pameharibika!”
“Kitu gani Spark?”
“Fanya hivyo haraka!” akamwambia huku yeye akiingia bafuni, dakika moja tu zilimtosha kukamilisha shughuli yake akatoka kurudi chumbani.
“We Butterfly, mbona hivyo, nimekwambia uondoke hapa hapafai ndiyo kwanza umelala!” akabwata, “Butterfly! Butterfly! Butterfly!” akaita mara tatu lakini yile binti alitulia vilevile, akamwendea na kutaka kumtikisa lakini alipomkaribia alisimama ghafla.
“Shiiit!” akang’aka kwa hasira. Butterfly alikuwa amelala kimya, uchi wa mnyama juu ya shuka jeupe, macho yake yalikuwa yakitazama bila kupoteza uzuri wake, katikati ya paji la uso palikuwa na tundu dogo lililotiririka damu kidogo tu, alikuwa ameuawa. Amata akainua macho kueleka dirishani akakuta tundu la zaizi ileile limetoboa kioo na kuacha nyufa kadhaa pembeni mwake.

Mbisho wa hodi ukamstua kutoka katika wimbi la mawazo, huku mkono wake ukiwa umeshika kifua cha Butterfly pale kitandani, chozi la uchungu likamdondoka huku ile hodi ikiwa inamletea makelele kichwani mwake. Kwa hasira zilizojawa uchungu akashusha ngumi nzito juu ya meza ya kioo na kuitawanya vipande vipande huku ile hodi ikizidi kupigwa kwa fujo. Akainuka na bastola mkononi taulo kiunoni, akauendea mlango na kuufungua kwa ghafla.
“Oooh Mr Spark!” sauti ya Preciuos Nancy ikapenya kwenye masikio huku ye mwenyewe akijipenyeza ndani ya chumba hicho, “Samahani kumbe ulikuwa na mwanamwali humu ndani, nimekuharibia starehe, mwanaume gani wewe kila siku kubadilisha wanawake kama nguo za ndani…” akaongeza nkukiendea kitanda, akakamata shuka ambalo Amata alimfunika Butterfly.
“Noooo!” Amata lipiga kelele lakini alichelewa, Precious alikuwa tayari kaondoa shuka lote na kumwacha marehemu kama alivyo, ukimya ukapasua anga la chumba hicho. Kamanda Amata akasogea na kuufunika tena ule mwili, yule mwanamke akageuka na kumtazama Amata. Kama Amata alitarajia sura ya gadhabu kutoka kwa Precious Nancy basi haikuwa hivyo, sura ya tabasamu ilimpokea, Precious akamkubatia Amata.

“Wonderfull, Mr Spark. Kweli unanipenda, umemuua hasimu wangu wa mapenzi, usijali nitakusaidia kuzika huu mwili,” maneno ya Precious Nancy yaliuchanachana moyo wa Amata. Hakusema kitu, alimwangalia tu kisha akamsukumia pembeni na kuchukua pochi ya Butterfly akaikagua ndani na kukuta vipodozi na bastola moja ndogo, akaichukua na kuikamata mkononi mwake, kisha akaziendea nguo zake na kuzipekua huku na kule, hakukuta kipya zaidi ya hela tu kwenye baadhi ya mifuko ya siri, mfuko mmoja. Akasogea kando na kuvaa suruali yake, shati huku macho yake yakiwa kiooni yakimwangalia Precious Nancy, akikikagua kiatu cha Butterfly, akakivuta kisigino na kukirudisha tena. Kisha akakiweka pale chini.
“Unachukua simu ya nini?” Precous akamwuliza Amata.
“Nawataarifu polisi juu ya hili…”
“Ooh! No! no! no! usifanye hilo, utaingia matatizoni sasa hivi mya dear Spark. Subiri jioni ifike, nimekwambia nitakusaidia kuuzika huu mwili na mtu yeyote asijue kilichotokea, tuondoke,” akamwambia. Amata akaitazama saa yake ilikuwa saa kumi na moja jioni. Akachukua vitu vichache pamoja na ile bastola ya marehemu akavitia kwenye begi lake. Bastola yake moja aina ya PPK akaipachika kiunoni na kuondoka na Precious.
“Unanipeleka wapi leo?” Amata akamwuliza Preciuos wakati akiondoa gari yake pale hotelini.
“Usijali nakupeleka sehemu nzuri sana ambayo utainjoi na kumsahau huyo marehemu wako, tukacheze muziki, kamali, tule tunywe kisha tuje tufanye ila kazi yetu,” akajibu yyule mwanamke huku akibadili gia ya gari lake kuongeza mwendo.

ITAENDELEA.......
 
PASIPOTI YA GAIDI

MTUNZI: richard MWAMBE

SIMU; 0766974865

“Ooh! No! no! no! usifanye hilo, utaingia matatizoni sasa hivi mya dear Spark. Subiri jioni ifike, nimekwambia nitakusaidia kuuzika huu mwili na mtu yeyote asijue kilichotokea, tuondoke,” akamwambia. Amata akaitazama saa yake ilikuwa saa kumi na moja jioni. Akachukua vitu vichache pamoja na ile bastola ya marehemu akavitia kwenye begi lake. Bastola yake moja aina ya PPK akaipachika kiunoni na kuondoka na Precious.
“Unanipeleka wapi leo?” Amata akamwuliza Preciuos wakati akiondoa gari yake pale hotelini.
“Usijali nakupeleka sehemu nzuri sana ambayo utainjoi na kumsahau huyo marehemu wako, tukacheze muziki, kamali, tule tunywe kisha tuje tufanye ila kazi yetu,” akajibu yyule mwanamke huku akibadili gia ya gari lake kuongeza mwendo.

SEHEMU YA V

SPIELBANK POTSDAMER PLATZ
Berlin Casino

PRECIUOS NANCY aliegesha gari yake nje ya jengo hilo kubwa lililozungukwa na vioo kila upande na kufanya mandali ya kuvutia kutokana na kuakisi kwa mianga ya taa mbalimbali zinazowaka barabarani. Giza lililkuwa likianza kulifunika jiji hilo. Magari mazuri ya kifahari yalikuwa yakiegeshwa huku na huko na watu walioonekana wenye pesa walikuwa wakiingia ndani ya jumba hili la kuvutia.

“Berlin Casino, hii ndiyo casino bora yenye chat Ujerumani, karibu sana Spark; leo hapa kuna kamali zawadi ya kwanza ni Range Rover ya kisasa mpya kabisa brand new, ukitaka kuwaona matajiri wa Berlin leo hii,” Preciuos alimwambia Amata.

“Sawa!” Amata akajibu kwa mkato kisha wote wakateremka na kuongoza kwenye jengo hilo. Kila alipokuwa akivuta hatua moja na nyingine Amata alihisi uzito miubwa na nywele zikimsisimka. Ndani ya jengo hilo kulikuwa na casino kubwa tatu, moja wapo ilikuwa ya wacheza kamali, hapop kulikuwa na michezo kama Poker, blackjack na mingine kama hiyo na pembeni yake kwa juu kulikuwa na sehemu ya mazungumzo kulikuwa na meza zenye viti viwili, vitatu, vine na kuendelea, kulikuwa na kaunta kubwa ya pombe za kila aina kali, tamu kwa chungu. Muziki laini uliokuwa ukipigwa na Tori Amos alikuwa akifanya eneo hilo kuwa la kipekee sana.
Ghorofa ya pili kulikuwa na casino nyingine huko kulijaa mashine za bahati (slots machine) nyingi kupita maelezo na ghorofa ya tatu huko kulikuwa na disko zito, vijana wengi walijaa huko.

“Unapenda kuangalia Poker? Au Blackjack?” akauliza Precious.

“Napenda kunywa pombe, twende tukaketi kule juu,” wakapita na kupanda ngazi chache, wakakaa kwenye moja ya meza ambazo zilikuwa na viti viwili tu, vinywaji vikaletwa na burudani zikaendelea.

Wakiwa wamezama kwenye mazungumzo ya hapa na pale huku pombe ikizidi kuwachukua, simu ya Precious ikaita, akanyanyuka na kwenda kuipokea pembeni ambako Amata hakumwona sawasawa, akainua bilauri yake iliyojaa pombe ile aina ya Couvosier, akaimiminia kinyani na alipoitua akakuta hayupo peke yake. Kiti kile alichoketi Precious kulikuwa na mtu mwingine mweusi kama yeye, aliyevaa suruali nyeusi, shati jeupe lenye tai ya kipepeo ya rangi ya buluu na kujifunika kwa koti jeusi, mkononi mwake alikuwa na bastola Magnum 22 iliyofungwa kizuia sauti ikimtazama. Sura ya mtu huyu haikuonesha hata kama alikuwa na masihara au vipi, ilitulia na katika paji lake la uso kulifanya mawimbi machache ya kunyanzi la ngozi, ndita. Hakutabasamu wala hakununa alikuwa katikati lakini mkono wake uliokakamaa na kushika ile bastola ambayo tayari ilikuwa haina usalama, ulipambwa kwa kovu moja kubwa lililoanzia kwenye kiwiko na kuzunguka mpaka karibu na kiganja upande wa juu.
Kamanda Amata akataka kuchukua ile chupa ili ajimiminie kinywaji.

“Usilete ujanja! Tulia kama ulivyo na ufuate amri yangu,” yule bwana aliongea kisawahili safi kisicho na hila.

“Sawa! Unataka nini?”

“Nataka kujua almasi uliyoileta kuiuza, sampuli kutoka Mpumbutu umeipata wapi?”

“Unataka nikuuzie au? Maana biashara hiyo haikuhusu sasa wewe unaiulizia ya nini?” Amata akajibu kijeuri.

“Kamanda Amata!” yule jamaa akaita, “Ujue mkononi nina bastola iliyojaa risasi, ukijifanya jeuri sintosita kuitumia na kuyakatisha maisha yako,” akaongeza.

“Nimeipata Mpumbutu,” akajibu.

“Nimepewa kama zawadi,”

“Na nani?”

“Unataka umjue?” akauliza na yule bwana akajibu kwa kubetua kichwa.

“Nimepewa na bosi wako, Kanali Banginyana,” alipojibu hilo akajiegemeza kwenye kiti na mara akahisi kitu baridi kikigusa kisogo chake.

“Usigeuke, inuka hivyohivyo,” sauti ilimuamuru, akainuka,

“Ongoza njia hiyo moja kwa moja”. Hakuwa na ujanja akafuata na kutii hiyo amri, wale jamaa wakamwongoza mpaka kwenye eneo la vyoo, wakamwamuru aingie ndani ya jengo hilo la vyoo vya VIP. Ndani ya eneo hilo hakukuwa na mtu, ni ukimya tu ulitawala kila mahali.

“Geukia ukutani!” akaamuriwa naye akatii.

“Weka mikono kisogoni”. Akatii. Kamanda Amata alikuwa kawapa mgongo wale jamaa wote wawili wakiwa na bastola zao, mmoja akiwa kasimama karibu na mlango na mwingine karibu na Amata.

“Piga magoti!”

Anafasi hiyo ndiyo hasa aliyokuwa akiisubiri, alikwenda chini kana kwamba anapiga magoti, akajibiringisha kwa sarakasi ya kitoto miguu yake ikafika ukutani akajiinua kwa nguvu na yule jamaa akaachia risasi iliyopita milimita kama mbili hivi kwenye ngozi ya began a kuchimba ukutani. Amata alijisukuma kwanguvu kwa miguu yake na kuja kutua kwenye kifua cha huyo bwege, kabla hajakaa sawa akapamiana na mwenzie aliyemwacha mlangoni. Amata akaanguka chini na kujiviringa huku mguu mmoja kimchota ngwala yule jamaa na kumbwaga chini kama mzigo, alipojaribu kujinyanyua alikutana na ngumi nzito iliyo,rudisha chini, yule mwenzake alianza kuweweseka, akiiweka bastola yake vizuri, Amata tayari aliikamata bastola yake ya PPK mkononi na kuifyatua, ikabanja na kumvunja mguu yule wa pili, akaenda chini huku akitoa yowe la uchungu. Kabla hajajiweka vizuri, Amata akajikuta akipigwa teke la maana nyuma ya kisogo kutoka kwa yule jamaa aliyeanguka pale chini, akagumia kwa uchungu maana netweki ilipotea kidogo, akamgeukia na kumshushia kichwa kisha akamdaka kabali ya maana. Yule jamaa naye alikuwa mzuri si haba, akajikunja na kujigeuza akamnasa Amata kwa miguu yake shingoni na kuvuata kwa nguvu, mikono ya Amata ikaachia shingo na kudaka miguu ya yule bwege wote wakaenda sakafuni.

Yule jamaa wa pili hakuwa na uwezo wa kufanya lolote, alijivuta na kutambaa kuilekea bastola yake. Wakati mapigano ya wawili hao yakiendelea yule jamaa akaikamata bastola yake, hisia za Amata zikamshtua, akamwona jamaa kwa jicho upande akiiweka ile bastola sawia. Akatumia nguvu zake zote na kubingilika mara kadhaa na risasi zile zikawakosakosa. Amata kwa mikono yake yenye nguvu aliitanua miguu ya yule jamaa akafanikiwa kuitoa, akajigeuza na kumtwanga ngumi ya kwenye korodani, wakati anagalagala, Amata aliinuka na kusimama wima.

“Weka mikono yako juu!” yule jamaa aliyevunjika mguu akamwabia Amata huku akiwa kamwelekezea bastola, hakuweza kusimama kutokana na mguu wake. Mara mlango wa chooni ukaanza kugongwa kwa nguvu, yule jamaa akageuka kuangalia mlangoni akajikuta akipigwa teke la nguvu kifuani akaenda chini, Amata kwa bastola yake akamshindilia risasi mbili za kifua na kumkata ngebe. Sekunde hiyo hiyo mlango ulipigwa kikumbo ukafunguka, Amata akajirusha na kujibanza nyuma yake, vijana watatau waliovalia sare za kiaskarai, moja kwa moja Amata alijua walikuwa walinzi wa casino hiyo waliingia na nyuma yao walifuatiwa na Precious Nancy.

Precious Nancy alikuwa na bastola ndogo mkononi, Amata akaitazama ile bastola, ilifanana kabisa na ile ya marehemu Butterfly, akili yake ikagonga, alipoona wale jamaa watastuka alipo akapiga risasi tatu juu na zile kelele za bastola wote wakalala chini, akatoka ndani ya kile choo na kufunga mlango kwa nje kisha akavunja kitasa ili mtu wan je asiweze kufungua kiurahisi. Akaondoka eneo hilo na kujichanganya na watu wengine mpka nje kabisa, akaondoka zake.

***
Tax aliyochukua ilimfikisha Hoteli Louisa, akalipa na kuingia kwenye gari yake aliyoiacha hapo tangu mchana ule, akaketi kwa utulivu na kuangalia kinachoendelea. Gari moja nyeusi ikaingia pale kwa kasi na kuegeshwa, akashuka yule jamaa aliyepambana naye kule casino, mkononi mwake alikuwa amesika kitambaa na kuibana pua yake, aliingia ndani na ile gari ikabaki imesimama pale nje. Kijana mwingine wa kizungu akatoka kawney ile gari na kusimama nje, Amata akachukua darubini yake na kumtazama vyema alikuwa yule mwenye nywele ndefu aliyempokea kule hotelini na kumpeleka kwa Jirack. Timu moja! Akawaza. Dakika mbili baadae, watu wawili wakatoka mle hotelini, yule wa kwanza aliyepambana naye na mwingine aliyevalia suti nadhifu, walionekana kuwa na harakaharaka. Matukio yote hayo alikuwa akiyanasa kwa kutumia darubini yake ndogo ikiyrekodi kwa picha mjongeo, ila gari ikaondoka nay eye akasubiri sekunde thelathini akaondoka zake.

Amata aliwasili kwenye hoteli aliyofikia, akafungua mlango na kuusukuma taratibu huku jicho lake likitua kitandani alipouacha mwili wa Butterfly, haupo. Aliuacha mlango na kuingia ndani bastola mkononi. Kitanda kilitandikwa safi kabisa tena kwa shuka zenye chapa ya hoteli ile ile. Akanyata na kufungua mlango wa bafuni, hakuna mtu! Kila kona hakukuwa na mtu, alichoshangaa zaidi hadi kioo kilikuwa kimebadilishwa tayari, akafungua kabati na kukuta sanduku lake lipo vilevile, mkoba wa Butterfly haukuwepo, lakini ile bastola alikuwa ameiweka kwenye mkoba wake ilikuwepo. Amata akahisi kama akili yake inapata ganzi, akatoa na kuangalia namba ya mlango wa chumba, ileile. Aliporudi ndani akahisi mlango unafunguliwa nyuma yake, alipogeuka akamwona Preciousy Nancy. Kofi moja kali lilimpepesua Precious mpaka kitandani.

“Unanifanya mi bwege siyo? Unalala na mimi kumbe unanizunguka sivyo? Leo utaniambia nani unayemfanyia kazi,” Amata alilalama na kumtia kofi linguine na linguine.

“Spark, unathubutu kunipiga mimi? Sijawahi kupigwa tangu kuzaliwa kwangu, nguruwe mweusi we,” Precious naye akachacharuka, lakini kabla hajatulia alipokea konde moja zito toka kwa Amata, akarudi kitandani huku damu zikichuruzika puani. Amata akamkamata vizuri.

“Nani alikutuma kwangu, nani unamfanyia kazi?”

“Hakuna ninayemfanyia kazi, mimi nipo kwa biashara zangu mwenyewe za kuuza mwili,” alijibu huku akipambana na damu iliyokuwa inavuja puani kwa kasi.

“Najua, kifo cha Butterfly wewe unahusika!”

“Hapana Spark! Hapana!”

“Kwa nini umekifurahia kifo chake, kwa nini ulisema utanisaida kuuzika mwili wake na sasa sijaukuta? Utanieleza leo,” makofi mengine ya nguvu yalipita kwenye mashavu laini ya Precious.
“Unanionea Spark!”

“Nakuonea ee!” Amata akaingiza mkono kwenye paja la Precious na kuchomoa bastola ndogo iliyojaa kignjani kwake.
“Hii bastola ya nani?”

“Ya kwangu hiyo,” Amata akamwacha na kuingiza mkono wa pili mkobani kwake na kutoa bastola ya Butterfly.
“Na hii je? Kwa nini inafanana nay a kwako kwa kila kitu? Usiponambia nakuua,” Kamanda Amata alifyatua risasi iliyochimba kwenye godolo sentimeta chache kutoka kwenye paja la Preciuos.

“Nasema, nasema! Nafanya ka-ka-zi kwa ba-ba wa Butterfly”
“Kazi gani?”
“Inategemeana ninayopangiwa, kwa sa-sa nilita-ta-kiwa kuhaki-kisha nyendo za-ko zote zinajulikana” alijibu kwa kitetemeshi. Hasira za Amata zikawaka juu ya mwanadada huyo, akamzabua konde moja zito lilitua usawa wa sikio lake, Precious akaenda chini kaitandani na kupoteza fahamu. Haraka haraka alichukua mkoba wake na kufunga begi lake, akaondoka mpaka mapokezi.

“Nacheck out, nimepata dharula kuwa nyumbani kuna wagonjwa,” akamwambia yule mwanadada wa mapokezi.
“Ulikuwa umeomba kwa wiki mbili na sasa ni moja tu,”
“Usijali!”

***
Kamanda Amata akatoka ndani ya hoteli ile, akiwa katika ngazi za hoteli ile akaangaza macho na kuiona gari yake ikiwa kando, palepale alipoiacha imeegeshwa, kwa hatyua zisizo na shaka akaindea na kuufungua mlango kwa kifaa maalumu cha kielektroniki, akatupia begi lake katika siti ya nyuma nay eye akaketi nyuma ya usukani tayari kwa safari, akapachika ufunguo na kuwasha gari, haikuwaka, akajaribu tena, kimya. Kila lipozungusha funguo funguo ilizunguka tu lakini hakukuwa na jibu lolote, kwenye dashboard ya gari hiyo nako hakukuwa na dalili yoyote ya uhai.
Akateremka na kuelekea upande wa boneti la gari hiyo, akafungua na kuangalia ndani yake.

“Shiiiiit!” akang’aka kwa hasira baada ya kuona hakuna betri, nani kaondoa betri hapa? Akajiuliza pasi na jibu, akalibamiza lile funiko la boneti kwa hasira, wakati huohuo akahisi kupigwa na kitu kizito kisogoni, akakosa nguvu na kujibamiza garini akaanguka chini chali. Watu watatu waliovalia suti nyeusi walisimama, aliwatazama kwa maluweluwe na kuwaona zaidi ya kumi na tano, wamekuja wengi kweli, akawaza, aaa wameniua hawa sina ujanja, akalalama nafsini mwake. Amata akaanza kupoteza nuru taratibu, zile taa zilizokuwa ziking’aa akaziona kuwa nyekundu sana, masikio yake yakagubikwa na kelele nyingi sana, akainua mikono yake akajiziba masikio, giza likamtawala na ukimya mkuu. Alihisi anatumbukizwa kwenye shimo refu sana lisilo na mwisho.

4
MSITU WA MPUMBUTU

JESHI LA UMOJA WA MATAIFA lilikuwa katika operesheni yake iliyokuwa ikiongozwa na vikosi kutoka Tanzania. Ndani ya Msitu wa Mpumbutu, vijana hao hodari na wapiganaji waliotumainiwa walikuwa kwenye maficho yao ya kila siku. Wanakiji walipita kwenda poleni kutafuta kuni na mahitaji mengine lakini hawakuweza kabisa kugundua maficho ya askari hao, walikuwa wakitembea kwa nyakati maalum kusingambele kuelekea kambi kuu ya waasi wale. Wakati yote hayo yakiendelea hakuan hata mmoja wao aliyejua kuwa kiongozi wa waasi hayupo msituni hapo kwa zaidi ya saa arobaini na nane. Iyalikuwa mapambano ya kimyakimya, hii iliwapa waasi wakati mgumu sana wa kulidhibiti jeshi hilo kwa kuwa daima walishindwa kujua ni wapi wamejificha, walichomaua kufanya ili kuwachokoza walitoa askari watatu wapiti msituni kama chambo ili wakiuawa basi watajua ni ueleo gain wapeleke mashambulizi yao.
Kikosi namba moja kikiwa kimya kabisa msituni kiliwaona vijana wale waliovalia sare za kijeshi na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) wakirandaranda msituni. Wadunguaji kama kawaida yao waliashaanza kuwamezea mate vijana hao.

“Msifanye lolote, huo ni mtego!” sauti ya kiongozi wa mapambano mstari wa mbele iliyoa angalisho na wale askari wakatulia tuli kusubiri amri nyingine. Mmoja wa wale askari waasi akainua redio koli na kuibofya kinobu Fulani kisha akaongeza kidogo.
“Zone namba moja iko shwari, tunasonga mbele, ova!” ukafuata mlio Fulani kama wa kukoroma hivi.
“Songa mbele ova!”
“Roja! roja!” akaitua ile redio na kuitumbukiza mfukoni, wakaondoka mahala pale na kuendelea mbele bila kujua kuwa nyuma yao wanawaacha wanajeshi wa kutosha waliojificha kimya kwenye nyasi na mawe na mapango yaliyozunguka eneo hilo. Dakika moja baada ya wale askari kuondoka na kusonga mbele lilifuata kundi kubwa la waasi waliokuwa na silaha nzitonzito miilini mwao, mabomu ya kurusha kwa mkono na mabunduki makubwa yalikuwa miongozi mwa silaha hizo, wengine walikuwa bado ni vijana wadogo umri wa kwenda shule. Wakapita eneo lile kwa mstari mmoja.

Kepteni Chwaka aliyekuwa kikosi namba moja cha jeshi la UN aliwahesabu vijana wale walikuwa kama kumi na nane hivi.
“Waaceni wapiti!” akawaambia wengine. Dakika mbili baadae walipita wengine na wengine. Ulikuwa ni msafara uliokuwa ukielekea mahali Fulani ambako hawa wanajeshi hawakukujua. Dakika tani baadae hakuna waasi waliopita zaidi ya wale waliotangulia.

“Operesheni yetu si kulinda amani ni kusafisha waasi, sasa kikosi namba tano kiwashambulie kutoka nyuma wengine tulieni kama mlivyo,” amri ikatoka kwa Kepeteni Chwaka.
Kikosi namba tano kikatoka mafichoni na kuwavamia waasi hao kwa nyuma, milio ya risasi ilipoanza kusikika katika msitu huo wale waasi nao walitawanyika kwa jinsi ya kupendeza na kuanza kurushiana risasi na askari hao. Kutokana na utaalamu wa majeshi ya Tanzania yaliyokuwa huko msituni chini ya UN waliweza kuwaua waasi wengi, huku wao wakipata majeraha madogomadogo kwa maana walikuwa wakirusha risasi na kujikinga kwenye mawe makubwa na wengine kwenye miti huku wakijitokeza na kulindana kwa ufundi kabisa.

Wale waasi walipoona wanazidiwa nguvu na jeshi hilo waliamua kutoa taarifa kambini kwao. Na mara hiyo chopa moja yenye rangi nyeusi ikawasili na kuangusha mabomu na risasi nyingi kutoka kwenye Heavy Machine Gun iliyofungwa kwenye lango la chopa hiyo. Hili lilikuwa pigo zito sana kwa majeshi ya UN, iliwawia vigumu jinsi ya kujificha katika eneo hilo kwani wale waasi walio kwenye chopa walikuwa wanajua kulitumia mashine hilo vizuri kabisa. Mmoja wa vijana mahiri wa vikosi vya UN aliyekuwa na jukumu la kutumia RPG hakuaona haja ya kupoteza muda, aliiweka sawa bunduki hiyo kubwa ambayo hutumika badala ya ‘kifaru’, alipohakikisha ipo sawa akaipachika begani na kusimama nyuma ya jiwe ambako haikuwa rahisi kuonekana. Wenzake wa jirani naye wakapisha pembeni kuepa mlipuko unaotoka wakati wa kufyatua grenade hiyo ambayo ilikuwa na kasi ya mita 294 kwa sekunde. Akaipachika dole lake la shahada kasha akabana jicho kutafuta shabaha ya kulidungua chopa hilo. Huku akitoa matusoi ya nguoni kwa sauti ndogo, alikuwa akifuatisha mwendo ule wa ile chopa alipoona yuko sawa, bila kusita, akavuta nyuma dole lake, lile kombora likafyatuka na sekunde mbili tu mlipuko mkubwa ulitokea hewani, ile chopa ikakatika vipandevipande na kuanguka porini.

“Retreat retreat retreat!” sauti ya amri hiyo ikawafikia wanajeshi wote na wale waliokuwa kwenye uwanja wa mapambano wakarudi mafichoni mwao huku kikosi kingine kikijitokeza na kumalizia waasi waliokuwa bado wako hai, hii ililetwa na hasira baada ya kuona miili ya wenzao ikiwa chini. Dakika moja baadae msitu ulikuwa kimya na mioshi ya baruti ilitapakaa huku na kule. Wapiganaji watano wa jeshi la UN wakawa chini bila uhai. Kepteani Chwaka na wengine wakajitokeza kusaidia majeruhi na kuhifadhi zile maiti. Ilikuwa ni huzuni kubwa kwa wapiganaji wote hawa, wakavua kofia zao, wakainamisha chini bunduki zao kuonesha ishara ya huzuni kwa tukio hilo.

Chonjo aliweka redio lake chini na kubofya hapa na pale kutafuta mawasiliano na kambi yao iliyokuwa mpakani mwa Tanzania na Ngoko katika upande huo wa kusini.
Alipopata mawasiliano nao, akawapa taarifa hiyo na kuomba msaada wa haraka. Nusu saa baadae chopa la kijeshi lenye nembo ya UN uvunguni likawasili eneo hilo na kutafuta mahali penye uwezekano wa kutua likafanya hivyo, ile miili ya wanajeshi watano ikapakiwa na wale majeruhi kadhaa nao wakapakiwa kwenye chopa nyingine iliyokuwa na alama zaidi ya Msalaba Mwekundu zikaondoka eneo hilo na kuwaacha wale wengine wakiwa bado kule msituni.

Kepteni Chwaka akawatazama vijana wake, “Tumepungukiwa, kikosi namba tano kimepungukiwa wapiganaji watano, nina uchungu sana. Sasa tuhakikishe tunafika katika kambi yao huko machimboni na tusibakishe hata salio, sasa ni jino kwa jino, aluta continua,” akawaambia vijana wake na kuamuru wasonge mbele nao wakafanya hivyo.

ITAENDELEA...
 
PASIPOTI YA GAIDI

MTUNZI: richard MWAMBE

SIMU; 0766974865

Alipopata mawasiliano nao, akawapa taarifa hiyo na kuomba msaada wa haraka. Nusu saa baadae chopa la kijeshi lenye nembo ya UN uvunguni likawasili eneo hilo na kutafuta mahali penye uwezekano wa kutua likafanya hivyo, ile miili ya wanajeshi watano ikapakiwa na wale majeruhi kadhaa nao wakapakiwa kwenye chopa nyingine iliyokuwa na alama zaidi ya Msalaba Mwekundu zikaondoka eneo hilo na kuwaacha wale wengine wakiwa bado kule msituni.
Kepteni Chwaka akawatazama vijana wake, “Tumepungukiwa, kikosi namba tano kimepungukiwa wapiganaji watano, nina uchungu sana. Sasa tuhakikishe tunafika katika kambi yao huko machimboni na tusibakishe hata salio, sasa ni jino kwa jino, aluta continua,” akawaambia vijana wake na kuamuru wasonge mbele nao wakafanya hivyo.
***

SEHEMU YA VI

IKULU - DAR ES SALAAM
RAIS ROBERT SEKAWA alisikitishwa na taarifa ya vifo vya wapiganaji wake wa mstari wa mbele vilivyotokea huko Ngoko. Yeye kama maafisa wengine wa usalama walishikwa na wingu zito la sintofahamu ijapokuwa walikuwa wameridhishwa na taarifa ya kuwa waasi wote eneo lile waliuawa na chopa lao kudunguliwa bado vifo hivyo vilisumbua nyoyo za viongozi hao.
“Mpumbutu imekuwa kaburi la vijana wetu?” alimuuliza Mkuu wa Majeshi aliyekuwa amefika Ikulu kutoa taarifa hiyo.
“Hapana, mapambano bado yanaendelea, na tutahakikisha tunafutilia mbali hao waasi wa X65 bila huruma,” yule Mkuu wa Majeshi aliyechafuka vyeo mabegani kifuani aliongea kwa kujiamini. Wakiwa katika mazungumzo hayo, mmoja wa wale walinsi wake anaombatana nao daima ambaye huwa na nguo za kijeshi muda wote yaani ‘Aide de Camp’ (ADC) alimjia na kumnong’oneza kitu mara baada ya kutoa saluti ya utii, akamjibu kwa kumnong’oneza na yule jamaa akaondoka. Baada ya dakika tu akaja na bahasha na kumkabidhi, rais akaifungua na kuisoma. Ilikuwa nukushi iliyotumwa mchana huo.

…Tunarudia tena, ondoa majeshi yako katika msitu wa Mpumbutu ama la tutakalolifanya sio dogo kwa jeshi lako mnalolitumia kama jeshi la UN. Kumbuka hao waliokushauri kulituma jeshi lako huko wamekuingiza kwenye domo la mamba. Waliokufa leo ni patgazeti tu film inakuja, tutafanya kitu kibaya, tega sikio….
Baada ya kuisoma, akatulia kidogo na kutikisa kichwa, “Naomba yule kijana wako wa MI afike hapa mara moja!” akatoa oda na wakati huohuo taarifa ikafika makao makuu ya jeshi.
“Ninavyoona hii vita ni kubwa na imetuzunguka,” rais akaendelea kuongea.
“Ni kweli hatuna budi kuhusisha vikundi vingine vya kiintelijensia kutoka majeshi mengine kama polisi au Usalama wa Taifa ili sote tuweze kuchunguza kila mtu kwa nafasi yake, najua tutafanikiwa,” akashauriwa. Kikao kile kikaendelea kwa dakika kadhaa huku rais akiomba ile miili ya wanajeshi ifanyiwe utaratibu wa kurudi nyumbani kwa ajili ya kuzikwa kijeshi na kishujaa...

***
SIKU HIYOHIYO – SAA 8 MCHANA – IKULU

BMW NYEUSI ilifunguliwa geti na kuingia moja kwa moja mpaka kwenye maegesho ya wageni. Mvua ya rasharasha ilikuwa ikinyesha, milango yake haikufunguliwa na gari hiyo iliku imetulia palepale bila kwenda popote huku ikiunguruma. Dakika tano baadae, mlango wa upande wa dereva ukafunguliwa. Mwanamama mtu mzima, nywele zake zilizachakaa kwa mvi, alikuwa ndani ya miwani na suti safi ya kijivu, alikuwa na mwili wenye afya, kutoka mbali utamjua kuwa alikua akitembea kwa umakini wa hali ya juu. Akazikwea ngazi za jingo hilo na kupokelewa na wasaidizi wa Ikulu, moja kwa moja akaongozwa katika mlango mmojawapo ambapo alikuatana na Othman, mwana usalama namba moja wa Rais, akampokea na kuingia naye ndani ya ule mlango. Ndani yake wakateremka na lifti mpaka chini kama mita tatu hivi.
Kilimanjaro Square, maandishi yalisomeka mlangoni, yule mwanausalama akabofya tarakimu Fulani na ule mlango ukafunguka.
“Karibu ndani, karibu sana” akamkaribisa kasha yeye akarudi mahala pake pa kazi.
Madam S, mkuu wa kitengo cha TSA, idara nyeti ya Usalama wa Taifa inayofanya kazi moja kwamoja chini ya rais aliwasili ndani ya ofisi hiyo nyeti ambayo siyo rahisi kwa mtu wa kawaida kufika. Wakapeana mikono na Mheshimiwa kasha wakaketi katika mtindo wa kutazamana.
“Pole mheshimiwa kwa kupoteza wapiganaji watano huko Ngoko,” Madam S alivunja ukimya.

“Asante lakini hali ni mbaya sana, na wewe unajua bila shaka, Selina tunahitaji kuimaliza hali hii, bila kuyumbisha chochote nahitaji idara yako ichukue nafasi ya uchunguzi wa uvamizi wa Ikulu na watakaobainika wafanyiwe kazi bila huruma,” rais akamwambia Madam S aliyetulia kimya akisikiliza maagizo ya kazi hiyo mpya, “najua unavijana makini, wenye weledi wa hali ya juu na wanaweza kufanya kazi hii kwa muda mfupi sana,” akamaliza na kujiegemeza kwa nguvu kwenye kiti chake.
“Bila shaka mkuu tutaifanya kwa kuwa ni kazi yetu, na kiapo chetu ni kukilinda kiti cha rais, nakuhakikishia kazi hii itamalizika haraka,” akamjibu.
“Patakapohitajika msaada wowote usisite kuwasiliana na mimi moja kwa moja kwa ile namba ya Alpha,” akamwambia. Madam S akasimama nakuanza kuuelekea mlango.
“Oooh Sellina, hakikisha katika kazi hii Yule kijana wako machachari Yule nani anaitwa Yule…”
“Amata Ric au Kamanda Amata…” Madam akasaidia kujibu.
“Enheee huyohuyo asikose kwenye hiyo operesheni,” akaagiza.

“Oh, mheshimiwa Kamanda Amata yuko Ujerumani,”
“Kuna nini Ujerumani?” akauliza kwa wahka.
“Anafanya uchunguzi kujua ni wapi waasi wa Ngoko wanapata silaha, hii kazi tuliombwa kuifanya na Umoja wa Afrika,” akamweleza kwa usahihi.
“Oh ok, sasa hilo tuliache, huyo kijana arudi hapa mara moja na kazi yake naomba idara impe mtu mwingine akaanzie yeye atakapoishia, right?” Mheshimiwa rais aliongea huku kijasho kikimtiririka na kutoa maagizo hayo kuwa Kamanda arudi nchini.
“Right Sir!”
“Ok!”
Madam S akatoka ndani y ofisi hiyo huku kichwa kikianza kumzunguka kama kawaida yake, jambo la kwanza alilolifanya ni kutuma taarifa kwa njia yao ileile.
…fika nyumbani haraka, mama ni mgonjwa sana. Tena sana aisee…
Ujumbe huo uliwafikia kila mtu kwa muda uleule na mara nyingi walijua wazi wakiapewa taarifa hiyo basi nyumbani ni wapi na mama ni nani.

***
Akiwa amegubikwa na usingizi wenye ndoto nzitonzito Gina aligutushwa na kijimuziki kilichokuwa kikisikika kutoka ndani ya pochi yake, akainua mkono na kuivuta, akaifungua na ndani ya pochi hiyo ndogo kulikuwa na kijitaa chekundu kikiwaka waka, akakibonyeza na kusikiliza.

‘…fika nyumbani haraka, mama ni mgonjwa sana, tena sana aisee…’

“Ujumbe umefika na unafanyiwa kazi!” akajibu kasha akaifunga ile pochi na kukurupuka kutoka kitandani. Jicho lake likatua kwenye saa ya ukutani, saa tisa za alasiri, akaingia maliwatoni na kujiweka sawa, akachukua bastola yake na kuijaza risasi, akaibana mahala pake ndani ya nguo alizovaa, akainua pingu yake na kuipachika kiunoni katika suruali yake. Gina alipenda kutembea na pingu kutokana na mazoea ya kazi yake ya awali kabla Amata na Madam S hawajafanya longolongo kumhamishia TSA. Akajitazama kwenye kioo na kuinua rangi ya midomo akajipakaa vyema na kuibanabana midomo hiyo, alipohakikisha ana kila itu tayari, akatoka na kuufunga mlango kasha akajitupa ndani ya gari yake Peugeot 405, akaingia barabarani na kuondoka.

***
Ndani ya mgahawa wa Steers, Daktari Jasmine alikuwa ameandamwa na kijana mmoja shababy aliyekuwa akimtaka kimapenzi. Ijapokuwa Jasmine alionesha kukataa muda mrefu lakini kijana huyo hakukata tama.
“Hivi nikwambie mara ngapi ili unielewe kuwa sikutaki?”
“Aaaa dokta, unaniumiza moyo, hebu tazama ni muda mrefu kiasi gani nakufuatilia lakini unanikataa, au kwa sababu sina hela, lo jamani masikini sisi tutakosa vingi vitamu,” Yule kijana alikuwa akilalamika huku macho yake yakitoka machozi. Sekunde hiyohiyo wakati Jasmine akiendelea kunywa juice yake alihisi kitu kama pini kikimchoma kwenye kidole chake cha shahada, alipoiangalia pete yake aliona lile jiwe likibadilika rangi, akajua kuna ujumbe nyeti umefika. Akainuka haraka na kutoka kwenye ile meza.

“Wapi tena sweetie?”
“Unikome…!” akajibu huku akiteremka ngazi chache kisha akavuka barabara na kuifikia gari yake ndipo alipogundua uwa kuna mtu nyuma yake, akageuka kumtazama ni Yule kijana.
“Hivi wewe unanielewa, najua kuwa unanipenda, lakini kwa sasa sina muda huo, nitafute siku nyingine,” Jasmine akamwambia huku kamkazia macho. Akafungua mlango wa gari na kuingia kasha akajifungia. Akainua mkono wake na kukifunua kile kifuniko cha pete ambacho juu yake kuna lile jiwe la urembo akasogeza sikioni na kuupata ule ujumbe sawia kabisa.
“Ujumbe umefika na unafanyiwa kazi,” akajibu huku akiwasha gari na kuondoka eneo lile akimwacha Yule jamaa kazubaa pale. Mijitu mingine bwana yaani inawaza mapenzi na ngono muda wote mpaka inasahau kazi, akajisemea moyoni na kusindikiza kwa sonyo refu, akaingia barabara ya Samora na kukunja kushoto akapotelea mitaani.

SHAMBA
NI WATU WANNE tu walikuwa wamekutana kwenye meza yao ya umbo la yai ambalo daima hukutana na kupanga mambo mazito yanayolikabili taifa. Wawili hawakuwepo, Kamanda Amata na Scoba hawa walikuwa kwenye misheni maalum za kiofisi kila mmoja na jukumu lake.
“Scoba nampata kwenye signal, lakini kamanda Amata haonekani kabisa,” Chiba alimweleza Madam S huku akiendelea kubofyabofya kompyuta kompyuta yake.
“Signal hamna kabisa kabisa yaani?” Madam S aliuliza huku kwa mbali akianza kupatwa na hofu.
“Oh, kamanda!” akajikuta akijisemea kwa sauti ya chini.
“Mpigie Scoba, anaweza kujua nini kinaendelea?” Madam akamwambia Chiba, naye kwa kutumia kifaa kilekile akabonya sehemu fulani kasha akabonya kinobu chenye namba 3 akainua mkonga wa simu uliopachikwa pembeni tu kompyuta hilo na kuuweka sikioni. Sekunde kama thelathini hivi zilipita.

“…TSA 2 nakupata!” Sauti ya Scoba ikasikika kupitia simu ile ya satellite ambayo Chiba alikuwa ameifunga ili isiweze kudakwa na watu na kusikiliza mazungumzo yao.
“TSA 3 nashindwa kumpata TSA 1 nipe ripoti…” akabonyeza kitufe Fulani na kusubiri kidogo kama sekunde tano hivi.
“TSA 1 yuko shimoni, najaribu kuwatafuta panya waliompeleka shimoni lakini naona wako undercover siwapati kabisa, nimefika pangoni mwake nimekuta mzimio wa mwanamke. Sasa nipo katikati ya jiji la Berlin najaribu kutafuta njia ya kujua liliko shimo hilo, roja!”
“Nimekupata, nitakuja kwako tena,” Chiba akamaliza na kukata ile simu.
Gina akashusha pumzi ndefu na kujiweka sawa kitini, macho yake yalianza kuonesha huzuni ya wazi, yakaanza kutona kwa machozi ya mbali. Madam S akamkazia macho makali, Gina akaelewa nini maana yake akatoa kitambaa mfukoni na na kujifuta.

“Hii kazi wewe, unatakiwa kuwa mwanamke wa chuma sio kitu kidogo kulialia tu” Madam S akamwambia Gina.
“Samahani,” akanyamaza na kuruhusu kikao kuendelea.
“Nimewaiteni hapa, najua wazi mnafahamu kilichotokea siku tano zilizopita pale Ikulu,”
“Ndiyo!” wote wakaitikia.
“Sasa basi tumepewa kazi ya kuingia kazini, kutafuta na kujua nani ni nani na First Lady apatikane ndani saa chache,” Madam S akaunguruma kikazi.
“Bila Amata?” Gina akalopoka.
“Kama amekufa je? Hujui kwamba wewe ndiyo upo katika kitengo chake? Tulikupeleka mafunzo miezi mitatu ulifikiri nini, safari hii we ndiyo unaanzia pale mpaka Kamanda atakapopatikana. Nimepanga hivi, Gina utakuwa mstari wa mbele kwa mapambano ya ana kwa ana itakapobidi, Chiba utabaki nafasi yako ileile ya uchunguzi wa kimtandao lakini nakuongezea utauchunga mkia wa Gina mara zote, Dr. Jasmine utabaki katika utabibu pale watu wanapopata majeraha lakini safari hii utachukua nafasi ya Scoba pia kwa uokoaji, usafiri na kadhalika. Mimi nashughulika na swalka la huko Ujerumani kwani kuna kazi nyeti ambayo Amata alienda kuifanya,” akamaliza.

Ukimya ukawa dhahiri shahiri kati ya watu hao, kila mmoja alitafakari kazi yake na jukumu alilopewa.
“Chiba uwe masterplan wa mchezo mzima, na tunaanza sasa kila mtu aingie kitengoni, na Mungu awatangulie. Gina mtu tunayemtaka akiwa na uhai wake ni Mke wa Rais tu hao wengine usiwape nafasi, shoot on the spot, uno trabajo!” akamaliza na kuondoka ndani ya chumba hicho kuelekea ofisini kwake huku akionekana wazi sura yake jinsi ilivyosawajika kwa habari ya Kamanda Amata. Gina alimkumbatia Jasmine wakaangusha machozi ya maana.
Kufanya kazi na wanawake shida tupu, sijui tutafanikiwa maana niko peke yangu, Chiba aliwaza huku akiwaangalia wale wananwake wanavyojililia kama wana msiba.

“Jasmine, naomba unipeleke Ikulu kazi yote lazima ianzie pale, kuna mambo ya kuchunguza tukiyamaliza pale ndipo tutapata jambo la pili,” Chiba alimwambia Jasmine. Wakaachana na Gina kila mmoja akajiweka sawa kwa kuchukua kifaa hiki na kile na kuvijaribu kama vinafanya kazi.
“Point of reference namba moja?” Jasmine akauliza.
“Chiba wa Chiba, kama kawaida,” Gina akajibu.
“Point of reference namba mbili,” akauliza tena
“Dr. Jasmine kwani muda mwingi utakuwa garini,” Gina akajibu.
Kutoka kwenye lile kabati lao la chuma, walipakua vifaa vya mawasiliano vya aina mbili wakimaanisha kuwa mawasiliano nya kwanza yatakuwa yakipitia kwa Chiba ndiyo ‘point of reference namba moja’ hayo yakishindwa kwa njia yoyote ile basi watatumia laini ya pili ambayo mtambio wake mdogo atakuwa nao Jasmine. Walipohakikisha sasa wako tayari wakapeana mikono na kukumbatiana kwa pamoja.
“Mama ni mgonjwa lazima asaidiwe, sisi ndiyo tiba haswa ya mama huyu, tutakieni mkono wa heri katika kazi,” Chiba aliwaambia kasha wakapeana mikono na kila mmoja akamalizia mambo yake machache.

5
MANNHEIM – UJERUMANI

KATIKA JUMBA MOJA KUBWA lililojulikana kama jumba la shetani kwa kuwa halionekani mtu kuingia wala kutoka, tukio hilo kwenye jumba hilo huwa ni kama kupatwa kwa jua. Ndani ya chumba kimoja kikubwa kilichooneka hakikumaliziwa kujengwa kwani chini hakikusakafiwa bali kilikuwa kimemwagiwa sementi iliyochanganyika na mawe, kuta zake nazo hazikuwa na rangi bali ni plasta iliyoachwa hivyo na makolokolo mengine mengi yalikuwa yamelundikana pembezoni mwa kuta hizo.
“Na utasema ni nani aliyekutuma kuja kuchunguza kazi za watu!” sauti nzito nene ya kikatili ilisikika ikiwa na mwangwi wa kutosha. Amata Ric akiwa juu ya kiti cha chuma kilichokuwa na tundu katikati. Alivuliwa nguo zote na kukalishwa hapo huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma kwenye vyuma vya kiti hicho na miguu imefungwa kwa nyuma ya miguu ya mbele ya kiti kilekile. Damu zilikuwa zikimvuja maeneo mbalimbali ya mwili.

“Hautaki kujibu siyo? Kweli wewe jasusi sasa nakukata korodani zako ili ujue kwamba kufanya mapenzi na motto wangu lilikuwa kosa kubwa sana,” Jirack Paterson, alifungua kitu kama bakuli kubwa la chuma ndani yake kulikuwa na vifaa mbalimbali vya kutesea, kulikuwa na vifaa vya kukata ulimi, kubana korodani, pini za umeme na vingine vingi. Akachukua kifaa kama mkasi ambacho kwa mbele kilikuwa na meno yaliyokaa nusu duara kila upande, nyuma ya kifaa hicho kulikuwa na kijichuma kido kilichotokeza ambacho ukikibana yale meno kule mbele nayo yanabana na kupasua korodani.
“Aaaaa aaaa aa please, please!” Amata alilalamika alipokuwa akiletewa kile kifaa.

“Ah! Ah! Ah! Kumbe na wewe unalia, Ah! Ah! Ah!” Jirack akacheka sana kasha akamgeukia Bensoir.
“Nampasua korodani kisha, nakuachia kazi yako,” Jirack akamwambia Bensoir aliyeonekana kujawa na hasira kali. Kwa kasi akakipiga kiti kikaanguka chini kwa nguvu.
“Aaaaaaaiiighhh! Aaaaaaaah! Mnaniua jamani, mnajua mkiniua mimi mtapata tabu sana,” kamanda alipiga kelele huku akiwa chini na kiti kile. Jirack akakamata kile kifaa na kukiendea kile kiti kilichoanguka na Kurusu korodani za Amata kuwa huru upande huu wa chini ya kile kiti.
“Noooooooooooo! Nasema nasema nasema, aaaaaiiigh nasema!” Amata alilia baada ya kilekifaa kuanza kubana zile korodani.
“Sema haraka, nani bosi wako, serikali au kundi gani limekutuma?” Bensoir akabwata.
“Mimi sio jasusi, aaaaaaiiigghh! Koh! koh! koh!” akaeleza huku akilia.

“Sasa kwa nini umemuua kijana wangu?” Bensoir akahoji.
“Yule nimemuua kwa sababu aliniuzia almasi kutoka Mpumbutu, nika-nika- aaaaaaiiighhh, mnaniumiza…”
“Sema uka- ukanini?”
“Nikamhurumia dhidi ya mkono wako, ndiyo maana huyu nikamwacha, mi sio jasusi mi mfanyabiashara,” akjitetea.
“Kadanganye mbwa wewe sio mimi! We ni TSA namba 1 wa serikali ya Tanzania nani asiyejua, ninyi mmepeleka majeshi kule Ngoko dhidi ya waasi kukomesha biashara za wakubwa, na tunajua umekuja huku kujua mambo mengine mengi. Basi kabla hujayajua utakuwa umeshafika kuzimu, pumbavu wewe, waliokutuma wamekusaliti na wanajeshi wenu watano jana wameshauawa na sasa tunapeleka silaha mpya za kisasa na kuwafutilia mbali hilo jeshi la UN wakati ni la Tanzania…” Bensoir aliunguruma huku macho yamemtoka, akampiga Amata teke kali la kwenye korodani.

“Ah!” Amata alitoa ukulele huo mmoja na kunyamaza ghafla, akafinya macho yake na kasha akayalegeza, akawa kama anayetaka kuinama lakini alishindwa kutokana na kamba alizofungwa, akanyamaza kimya.
Kijana wa Bensoir akamwende pale chini na vijana wengine waliokuwa na silaha mabegani mwao, wakamgeuza na kufungua macho.
“Vipi?” Jirack akauliza.
“Naona amezimia huyu! Lile pigo lilikuwa kali sana. Mkuu tummalizie kwa risasi ya kichwa,” mmoja wa wale vijana wa kizungu alimwambi Jirack.
“Hapana, huyo bado, kuna siri nyingi sana anazo lazima azitaje zote kwa faida yetu na wenzetu, mtoeni hapo mwekeni kwenye kile chumba cha pili, mumlinde mpaka atakapoamka. Akiamka tu mniite kuna watu wengine wanakuja kuonana naye,” Jirack akawaambia wale vijana kasha yeye na Bensoir pamoja na Yule kijana wa Bensoir wakaondoka zao.
“Sasa huyu kijana wako mwingine tunafanyaje? Maana familia yake lazima itahitaji kumzika,” Jirack akamwambia Bensoir.
“Hana familia, Yule kisa cha kuingia jeshini ni kisasi familia yake ilichomwa moto ikiwa ndani usikuu wamelala, kwa hiyo tusubiri mambo haya yatakapotulia tutatuma watu kuja kuchukua mwili,” akajibu.

Saa mbili baadae Kanali Bensoir Banginyana, alikuwa uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurudi huku akiwa na hasira za kumpoteza kijana wake.
“Hakikisha Yule mshenzi anakufa,” alimwambia mmoja wa vijana wa Jirack kasha yeye akaondoka zake.
“Count on me!” yule jamaa akajibu.

***
Katika lile jumba ambamo Amata alilazwa kwenye kitanda cha chuma kisicho na godoro uchi wa mnyama huku akiwa kafungwa kwa pingu mikono kila mmoja upande wake na miguu vivyo hivyo, kulikuwamoi na vijana watatu wenye silaha, wawili mlangoni kwa nje na mwingine alikuwa ndani. Wote watatu walikuwa na shotgun zilizojaa risasi. Yule jamaa wa ndani akaangaza angaza na kuvuta nguo za Amata zilizokuwa juu ya meza shaghalabaghala. Hawa jamaa huwa wana vitu vya ajabu sana, ngoja nipekuwe nijipatie changu, akajisemea huku akipekua mifuko ya suruali ya Amata. Katika mmoja wa mfuko akatoa kitu kama saa lakini kisicho na mikanda, akakitazama na kukigeuza geuza, mh! Nini hiki? Akajiuliza. Katikati ya kidubwasha kile kulikuwa na kinobu chekundu, Yule bwege akakiangalia na kusogeza dole gumba lake tayari kwa kukibonyeza, mh! Kama bomu je! Akajiwazia. Haiwezi kuwa bomu hii ni saa hii, akabonyeza na kushikilia kwa muda kuona nini kinatokea, hakuna kitu, akabaki kaduwaa. Sasa hiki kitu gani? Akajuliza, akakigeuzageuza tena huku na huku, na kukiweka juu ya meza ndogo.

‘Piiiip! Piiiip! Piiip!’ kile kidubwasha kilianza kutoa sauti kali iliyokuwa ikiumiza masikio, Yule mjinga mle ndani alijiziba masikio na kuanza kuhangaika, ile sauti kali ya kile kidubwasha ilikuwa ikimsumbua sana masikio, akaanza kugonga mlango. Wale vijana waliokuwa nje wakasikia kelele za ule mlango, wakafungua na kuingia wakamkuta mwenzao kajiziba masikio huku kakunja sura. Wale jamaa nao wakaanza kutaabika na ule mlio mkali sana lakini mlio ule ulikuwa haufiki mbali zaidi ya kile chumba. Kamanda Amata kutoka katika usingizi mzito alianza kuusikia ule mlio, akili yake ikarudi taratibu, akajitikisa mkono umefungwa, akatikisa miguu imefungwa, kwa mbali akaona wale jamaa wanavyohangaika. Mmoja wao akakinyanyua kile kidubwasha, na kujaribu kukizima, alipobonyeza katikati kikalipuka, moshi mzito wa kahawia ukatoka kwenye kile kidude na kuwafanya wale jamaa wasionane. Vikohozi vya dharula vilitokea huku na huko. Amata alihisi kitu kinamwangukia jirani yake, ukimya wa vikoozi ukatawala na ule moshi taratibu ukaanza kupungua. Pumbavu wakubwa nyie! Akawatukana kimoyomoyo lakini bado alikuwa hawezi kujitoa pale kitandani, kutokana na alivyofungwa Amata alijinyanyua na kuketi huku akihisi kizunguzungu kwani ule moshi kama hujaujua sawasawa lazima usimie ila kama unaujua unachotakiwa ni kutompumua kwa nguvu na kutumia muda mwingi kubana pumzi.

Akatazama wale jamaa wamelala pale chini huyu mmoja alikuwa jirani kabisa na yeye, akajipinda kwa tabu na kuung’ata mkanda wa bunduki kasha akaivuta taratabu kwa kutumia kinywa na meno yake akaukamata kwa mkono akausogeza kwa vidole, mpaka akaikamata ile shotgun, alipohakikisha ameishika vyema akajaribu kutafuta shabaha ya zile pingu za miguuni, lakini ilimuwia ngumu kutokana na nguvu ya mkono uliofungwa, alipohakikisha hapo yuko sawa bila kuhofia lolote, akafyatu na ile risasi haikufanya mzaha. Pingu ya mguu wa kulia ikatawanyika na kuuwacha mguu huo huru. Katika harakati zile mmoja wa wale jamaa akatikisika, akapiga chafya na kufumbua macho, alipoona hali aliyokuwa nayo akakurupuka na kusimama huku akiiweka sawa bunduki yake. Lakini kabla hajakaa sawa, Amata akiwa na ile bunduki mkononi kwa vidole vyake vitano akaikamata sawasawa.

“Tulia hivyo hivyo!” sauti hafifu isiyo na nguvu ya Amata ilimwamuru kijana huyo, naye akatulia, “Tupa bunduki yako kabla sijakumaliza,” akatupa. “Haya nifungue nitoke,” akamwamuru.
“Nikikufungua boss ataniua,”
“Atakuua vipi wakati ushatoroka, fungua!” akaongea kwa nguvu kidogo, Yule jamaa kwa kutetemeka akatoa funguo na kufungu pingu moja ya mkono wa pili kisha akafungua ya mguu uliobaki, Amata akanyosha mkono ule uliofunguliwa na kuchukua ile shotgun kutoka mkono wa pili, yule kijana akaufungua ule wa pili huku akitetemeka.

ITAENDELEA
------
 
PASIPOTI YA GAIDI
MTUNZI: richard MWAMBE
SIMU; 0766974865

“Tulia hivyo hivyo!” sauti hafifu isiyo na nguvu ya Amata ilimwamuru kijana huyo, naye akatulia, “Tupa bunduki yako kabla sijakumaliza,” akatupa. “Haya nifungue nitoke,” akamwamuru.
“Nikikufungua boss ataniua,”
“Atakuua vipi wakati ushatoroka, fungua!” akaongea kwa nguvu kidogo, Yule jamaa kwa kutetemeka akatoa funguo na kufungu pingu moja ya mkono wa pili kisha akafungua ya mguu uliobaki, Amata akanyosha mkono ule uliofunguliwa na kuchukua ile shotgun kutoka mkono wa pili, yule kijana akaufungua ule wa pili huku akitetemeka.

SEHEMU YA VII
***
Simu ya Scoba aliyokuwa kaivaa mkononi na kuifunika na mkono wa suti yake ilitoa ukulele mdogo, haraka, akavuta ule mkono wa koti nyuma na kuitazama, juu ya kioo ilionesha tarakimu nyinginyingi kama kumi hivi, alipozisoma akaelewa kuwa hiyo ni namba ya kumtambulisha TSA 1 kwa njia ya satellite. Akabofya hapa na pale na kuiomba impe uelekeo, kwenye kile kioo ikatokea tufe la dunia likajizungusha na kuleta bara la Ulaya, ikajisogeza karibu na kulieta ramani ya Ujerumani, mji wa Mannheim, ikamwonesha na nmba Fulani za eneo lakini haikuonesha kama mtu huyo yupo hapo au alikuwa hapo. Kutokana na umbali wa hapo alipo mpaka huko Mannheim ilimpasa kama ni gari kuendesha kwa saa zizizopungua nne.

Shittt! Akang’aka huku akiondoa gari haraka pale alipo na kuelekea stesheni ya treni iendayo kasi. Dakika mbili tu alikuwa tayari stesheni na bahati akaikuta ndiyo inaingia, akaegesha gari haraka na kuteremka huku akifunga mlango nyuma yake. Bastola zake mbili zilikuwa tayari kwenye makwapa yake na visu vidoko kama kumi na tano alikuwa kavipanga kwenye ubavu huu na huu, akaiwahi ile treni na kuondoka.
“Unaelekea wapi?” mtu mmoja aliyevalia sare nadhifu alimwuliza, moja kwa moja Scoba akajua kuwa huyo ni mfanyakazi wa treni hiyo.
“Mannheim! Ni muda gani tutachukua?” akauliza.
“Dakika thelethini tu,” akajibiwa. Scuba akaketi huku akiitazama ile sa yake na wakati huo bado ilikuwa inaonesha kitu kilekile.

***
Amata alinyanyuka ghafla na kumpiga ngumi moja nzito yule jamaa, akayumba na kujigonga vibaya ukutani, akapoteza fahamu kwa mara ya pili. Kutoka pale kitandani, akajiinua na kusimama wima, mwili wake ukiwa umechoka nab ado damu zilikuwa zimemganda huku na kule, akajinyoosha viungo na kujiweka sawa. Kutoka nje ya chumba hicho alikuwa akisikia watu wakitembea kuja sehemu hiyo, akaufunga mlango kwa ndani. Mara ukimya ukatawala, kisha hodi ikafuatia kugongwa baada ya hodi hiyo kutokuwa na mafanikio, Amata akajua kinachofuata, akajificha nyuma ya mlango, kitasa kikanyongwa na ule mlango ukafunguliwa ghafla, wale jamaa waliingia kwa kasi na kukuta wenzao wakiwa chini.

“Katoroka! Toa taarifa!” mmoja akamwambia mwenzake. Kutoka kwenye kona ya mlango, Amata alijitokeza, konde moja lililotua nyuma ya shingo ya huyu aliyempa mgongo lilimfanya ampamie mwenzake na wote wakaenda chini. Mmoja aliyekuwa juu akajigeuza na kujiinua kiufundi kabisa, lakini aliposimama tu alikutana na pigo linguine baya zaidi la karate lililotu kwenye kifua na kuufanya moyo ushindwe kufanya kazi sawasawa, akajibwaga chini kama mzigo, huku akiwa kakodoa macho. Yule mwingine akasimama wima na kutaka kukimbia, lakini hakuweza kwani ngwala aliyopigwa ilimpaisha juu na uso wake ukatua katika mpango.
“Mh!” akaguna, akajigeuza chali na kujiinua, teke la pili la Amata likadakwa, Yule jamaa akauzungusha ule mguu kwa minajiri ya kuuvunja lakini alikose sana kwani TSA 1 alifanya vitu vywake kwa kujiinua na kujizungusha kisha mguu wa pili ukatua kwenye shavu la Yule bwega akamwachi Amata kisha naye akaenda chini, na alipoanguka aliikamata redio call.

“…Ame-to-roka! Msaada tafadh…” kabla hajamaliza kusema alijikuta amekanyagwa shingoni.
“Bismark …. Bismark ….!” Ile redio ilikuwa inaita, Amata akainyanyua na kusikiliza wanachoongea, “Andre… mateka ametoroka paleka msaada haraka,” ile sauti kwenye redio ikawa inatoa taarifa upande mwingine. Kwa haraka, akamvua suruali kijana mmoja aliyeonekana kushahabiana naye kimwili akaivaa na nguo ya juu nayo akaivaa, akachukua ile shotgun na kuikamata mkono huu na nyingine mkono ule, akatoka ndani ya kile chumba, alipoangaza jicho akakutana na kamera ya usalama ikimtazama, akaifumua kwa risasi kisha akapita eneo lile na kujibana kwenye ngazi za kuelekea chini, akawaona wale jamaa wamefika na wananyata kuingia kwenye kile chumba.
“Hayupo! Kuna wenzetu tu, aiyaaaaa wamekufa!” sauti moja ilisikika ikisema. Kamanda Amata akacheka kimoyomoyo, akatazama zile ngazi hakujua zinaelekea wapi. Akazifuata akajionee hukohuko...

***
Dakika thelathini kama alivyoambiwa, ile treni ilisimama katika stesheni ya Mannheim, Scoba akashuka na kuingia mtaa kama wan ne hivi huko huegeshwa magari, pikipiki au baiskeli ambazo watu wamechoka kuzitumia na hapo husubiri kuchukuliwa kwenda kuyeyushwa na kutengeneza bidhaa nyingine.

Akapepesa macho huku na kule akakutana na pikipiki kubwa limeegeshwa mahali hapo, akaliendea akajaribu kuliwasha halikuwaka, huku na kule aliona kituo cha mafuta, akalikokota mpaka pale akajaza lita kumi na kuliwasha likakaubali, akatua juu yake na kuondoka kwa kasi huku kila mtu akimtazama mwafrika huyo.
Jumba la Jirack Peterson lilionekana kwa mbali, Scoba alipoitazama ile GPS yake pale mkononi limuonesha kuwa yuko jirani zaidi, kutokana na eneo hilo kuwa wazi bila makazi na jumba pekee lililoonekana na ni hilo akajua hana budi kulikabili. Akapita na kuegesha pikipiki yake kwenye vichaka vya mizabibu, akalifuata kwa miguu kupitia mashambani. Ukuta wa jumba hilo ulikuwa na nyaya za umeme juu yake ambazo hutumika kuzuia wezi, aliutazama na kuuona unawezekana kabisa kupandika au kuuruka kama mtu una mazoezi ya kutosha ya kuruka viunzi. Scoba alijua kwa vyovyote vile akijaribu tendo hilo hajui anapotua kuna nini, akaambaa na ukuta mpaka mbele ya jingo hilo kulikuwa na geti kubwa na kamera mbili huku na huku, nimekamatika, akawaza. Hatua tatu akalifikia lango kuu na kubofya kengele bila woga, mlango mdogo ukafunguka, kijana mmoja akajitokeza lakini Scoba tayari alikuwa na bastola mkononi na kuingia ndani, ule mlango ukajifunga nyuma.

“Mtu wangu yuko wapi?” akauliza. Yule jamaa hakujibu akabaki katumbua macho, Scoba alimuona Yule jamaa akirudi nyuma na mkono wake kubonyeza swichi moja nyekundu, akajua kuwa swichi hiyo ni swichi ya hatari, alipotaka kumvamia ili kumpa kichapo, Yule jamaa alikuwa tayari kabonyeza ile swichi. Scuba akamtandika ngumi tatu na kumwacha chini hoi, akachuku bastola. Alipojitokeza, nje akakutana na vijana wawili wakija getini, Scoba akachomoa visu viwali na kuvirusha kwa ustadi kabisa, kila kimoja kikakwama kwenye kolomeo la mmoja, wakaanguka chini na kugalagala, bastola yake ikawatungua wengine waliokuwa juu nao wakajiachia hadi chini. Scoba akapita na kuingia mlango mdogo waliotokea wale jamaa.
“Weka mikono kichwani!” akamwamuru kijana aliyekuwa mbele yake. “Nipeleke alipo rafiki yangu, haraka!” Yule kijana akaanza kuongoza njia huku Scoba akifuata nyuma yake kwa tahadhari, wakateremka ngazi na kufika eneo linguine upande huo wa chini. Mbele yao walitokea vijana wawili wenye silaha.
“Nimetekwaaaa!” Yule bwege akapiga kelele huku akiwakimbilia wale wenzake lakini kabla hajawafikia alikula risasi ya mgongo iliyompaisha na kuwaangukia wenzake, Scoba hakufikiri mara mbili alitawanya risasi na kuwamwaga wale jamaa sakafuni.

***
Kamanda Amata alisikia mlio ule wa bastola, Beretta! Akajisemea moyoni mwake na jinsi risasi zile zilivyopigwa akajua kuwa huyo ni Scoba kwa maana wao walikuwa na mtindo wao wa kufyatua risasi endapo unapiga zidi ya mbili ili kufahamaina kwa haraka. Ukimya ukatawala jumba hilo, maiti kama kumi natano hivi zilikuwa katika vibarabara vya hilo jumba, Amata akajitokeza kwa tahadhari katika moja ya zile korido, na upande wa pili akajitokeza Scoba na bastola mkononi.
“Upige!” Amata akpiga kelele, na Scoba akauma meno na kushusha ile bastola chini, akatikisa kichwa. Amata akaongeza hatua mpaka kwa Scoba, wakakumbatiana na kupeana pole.
“Ilikuwa ngumu kutoka kwa kuwa sijui hata watu hawa wako wangapi na wapi njia ya kutokea, ahsante braza umekuja!” Amata akamwambia Scoba.
“Usijali, nilipata shida sana kutambua ulipo mpaka nilipopata signal ya smoke star, ndio nikaanza kukutafuta, nilikuwa Berlin,” Scoba akamwambia huku akianza kuondoka na Amata akimfuata.
Walipofika karibu na mlango wan je waliona geti likifunguka lenyewe na gari tatu nyeusi zikaingia, wakajificha mmoja upande huu na mwingine ule wa mlango.

Zile gari zikasimama, Peter Jirack akateremka, sura yake haikuwa ya furaha hata kidogo, na katika gari zingine walishuka vijana tofauti walikuwa na silaha nzito mikononi mwao wakalizunguka lile jumba huku watatu kati yao wakiongozana na Jirack kuingia ndani. Wakapita palepale pasi na kuwaona Amata na SCoba kutokana na haraka zao za kwenda kule kwenye chumba walichomfunga Amata. Huku nyuma wawili hawa wakatoka na kulivuka geti mpaka nje.
“Una usafiri?” Amata akauliza.
“Kuna pikpiki moja kuleee!” akamwonesha huku akielekea upande huo.
“Piga namba hizi tafadhali,” Amata alimwambia Scoba naye akazibonyeza zile namba kadiri alivyotajia kwenye ile simu yake pale mkononi.
“Hizi namba za nini?” akauliza.
“We ukimaliza bonyeza ok, hizo ni namba za mpenzi wangu,” Amata akajibu huku akikaa nyuma ya pikipiki lile na mbele akiwa Scoba tayari kukamatia usukani. Kwa mbali waliona gari mojawapo ikitoka pale getini. Scoba akabonyeza ok kwenye ile simu yake. Ni sekunde ileile mlipuko mkubwa ukatokea, lile jumba la Jirack likalipuka vibaya, ardhi ya eneo lile ikatetemeka kwa nukata kadhaa. Scoba akamtazama Amata.

“Ulitega bomu saa ngapi?”
“Usijali, hilo bomu lilikuwa kwenye viatu, tuondoke!”
Scoba akaliwasha lile pikipiki na kuondoka kwa kasi, alipopita mbele ya lile jumba lililokuwa likiendelea kuwaka moto, gari moja ilijitokeza kwenye ujia uliokuwa pembezoni na kuanza kuwafukuza.
“Scoba, tuna marafiki huku nyuma!”
“Wataisoma namba!” Scoba akajibu wakati akibadili gia na kuongeza mwendo wa pikipiki hilo kubwa linalotumia propeller shaft badala ya mnyororo. Akiwa barabarani alikuwa anayapita magari kwa mitindo ya ajabu huku ile gari nayo ikifuatia vivo hivyo. Risasi kutoka katika ile gari zilikuwa zikiwaandama lakini Scoba alihakikisha anawasumbua wale jamaa.
“Hauna silaha?” Amata akauliza kwa sauti kali kutokana na upepo uliokuwa ukiwasumbua.
“Kwe nye koti,” Aakajibu Scoba huku akililaza lile pikipiki na kuzipita gari kama tatu hivi kwa wakati mmoja na kusababisha ajali za hapa na pale. Amata akachomoa bastla kwenye koti la Scoba.

“Niletete niwamalize, wapumbavu hawa!” Amata aling’aka huku akijiweka sawia. Scoba alipofika mbele kabisa hakukuwa na magari mengi, ile ya wale wapumbavu ilikuwa inakaribia kabisa kuwafikia, akasopgeza pikipiki karibu na ukuta wa kutenganisha barabara, akaishtua ikanyanyuka na kupita juu ya kile kiukuta. Amata akageuka nyuma na kuiona ile gari ikifunga breki, akainua bastola yake na kufyatua risasi mfululizo, vioo vya gari hiyo vikatawanyika na moja ya risasi ikapata mdomo wa tanki ya mafuta. Moto ukalipuka, kile Kigali kikapaishwa juu na kutua chini huku kikisababisha ajali kubwa kwa magari mengine.
Scoba alitua barabara ya upande wa pili na lile pikipiki, walikuwa tayari kwenye daraja kubwa sana, na chini yake kulikuwa na mto mkubwa unapita.
“Scoba, acha pikipiki!” Kamanda akamwambia na Scoba akasimamisha hiyo pikipiki pembeni huku ving’ora vya polisi vikiwa vimewakaribia, wakakimbia na kupanda kingo za daraja kisha wakajirusha kuelekea majini. Polisi walikuja kasi na bunduki zao lakini walishuhudia tu maji yakitawanyika huku na huko.

***
IKULU – DAR ES SALAAM
NDANI YA JENGO HILO tukufu, jingo jeupe, Chiba alikuwa ameketi katika chumba maalum chenye luninga nyingi zinazopiga picha kila pembe ya nje na ndani ya jingo. Alijaribu kurudisha nyuma matukio ili aone nini hasa ilitukia siku hiyo, usiku wa manane. Picha zile zilimchanganya kidogo, zilikuwa zikionesha hali ya utulivu kabisa muda wote lakini ilipofika saa nane kama na dakika arobaini na tano hivi, kamera zote zikazimika na zile luninga zilionesha chenga chenga na dakika moja tu baadae ikarudi ile picha ya awali. Hakukuwa na wa kumuuliza kwani aliyekuwa zamu huko aliuawa usiku huo baada ya kiujaribu kuilinda kazi yake. Siku hii alikuwa na vijana wengine kabisa. Alirudiarudia ile picha ili kuitazama vizuri kisha akaipeleka mbele mpaka ilipoanza kufanya kazi sawasawa, akarudisha tena nyuma na kutazama pale ilipokuwa inasoma saa nane na dakika arobaini na tano. Aliangalia kamera moja baada ya nyingine, katika kamera ya upande wa baharini ndipo alipoona kitu kigeni kidogo.

Palionekana bomba refu la maji taka lililoingia huko baharini, kisha akaona lile bomba linakuwa jeusi kutoka kule mwanzoni yaani ndani ya maji mpaka lilipoishia ambapo barabara ya lami alkatiza kabla ya kuufikia ukuta, akatikisa kichwa na kurudiosha tena picha hiyo, akaitazama kwa makini, hakika kwa mtu wa kawaida hasingeweza kugundua tofauti hiyo.
Akachukua kijitabu chake na kuandika vitu Fulani.
“Umegundua nini? Maana mi naona maruweruwe tu!” Gina akamwuliza Chiba
“Nitakupa tathmini baadae, lakini kwa sasa subiri kwanza,” Chiba akajibu kisha akahamia luninga nyingine na nyingine. Ilimchukua kama saa tatu hivi kukaa kwenye chumba hicho, akarekodi matukio yote ya siku hiyo aliyoyaona kwenye zile runinga na kuyahifadhi kwenye hard disc yake akaitia mkobani.
“Sasa twende nje ya uzio kuna kitu nataka kukiangalia,” akamwambia Gina, wakatoka pamoja na kuagana na Yule kijana aliyekuwa ndani ya ofisi ile. Nje ya uzio, upande wa baharini, usawa wa lile bomba, Chiba akasimama na kuutazama ule ukuta. Kutokana na weupe wa ule ukuta aligundua alama za kiatu zilizo hafifu. Mpandaji alikanyaga pale, akafikiri kisha akavuta hatua na kuuendea ule ukuta, akachukua kamera yake ndogo akapiga picha na kuhifadhi alama ile ya soli ya kiatu kisha wakarudi ndani.

Kwa upande wa ndani katika eneo sawa na lile ambalo ameona ile alama ya soli ya kiatu alikuta mchimbiko wa mtuo wa miguu ya mwanadamu, walitua hapa! Akawaza na kustikisa kichwa. Kutoka pale aliposimama Chiba aliinua uso juu na kuangalia kushoto na kulia na kuiona ile kamera ya jirani kabisa, akaomba msaada na kupanda pale juu kuitazama kwa makini.
“Gina!” akaita kutoka pale juu ya ule ukuta.
“Sema!” Gina akabetua kichwa chake na kutazama juu alipo Chiba ambaye alikuwa akiioneshea ile kamera kwa kidole chake, akatoa taarifa chumba cha mawasiliano kuwa anaizima kamera hiyo na kuiondoa kwa muda. Chiba alilifanya zoezi hilo na baadae akaweka kamera nyingine yeye akabaki na ile aliyoing’oa pale juu. Wakatoka na Gina mpaka chumba cha watu wa Usalama wa Taifa, pale akakutana na maofisa mbalimbali, wengi walikuwa wamemzidi umri, akaawamki na kuvuta siti moja kati yanyingi zilizokuwa hapo, Gina naye akafanya vilevile.

“Tunakusikiliza kijana maana tunajua utatupa lolote juu ya shida ‘etu,” mmoja wazee wale alivunja ukimya huo ghafla.
“Bado sina jibu la kuwapa, uchunguzi unaendelea, samahani nahitaji kuona maeneo yote yenye milango ya siri ya kutokea ndani ya jingo hili,” Chiba akaomba.
“Wewe umeambiwa, kila tafutishi yako utujulishe ofisi hii sasa unasemaje kuwa ‘uchunguzi unaendelea’?” mmoja aliyeonekana mzee kuliko wote lakini alikuwa na tambo kubwa hivi, alimkoromea Chiba.
“Naomba npatiwe msaada ninaoutaka na siyo kelele!” Chiba naye akawa mkali, wakati huo wote Gina alikuwa ametulia akiwasikiliza.
“Kijana nashindwa kujua ilikuwaje ukaajiriwa na kupewa kazi nyeti kama hii, maana kila unapoelekezwa huelekezeki, ningekuwa bosi wako ningekufaya auti,” Yule mzee aliongea huku amesimama na kuruhusu kuonekana ukubwa wa mwili wake.

“Ndiyo maana hukuwa bosi wangu, mbona wenzio wote wametulia na kuelewa kwa nini wewe usielewe?” Chiba akauliza, “Mtu yeyote anayehitaji na kung’ang’ania jibu la swali ujue jibu hilo analijua sasa anataka kuoanisha na la kwako. Nimekuweka alama we mzee,” Chiba akamaliza na kutoka huku Gina akimfuata.
“First Lady alichukuliwa kutokea chumbani mwake usiku huo, vitendo vyote vilifanyika kimya kimya kwa kuwa hatuna hata sauti iliyorekodiwa na mitambo yetu. Kwenye mitambo utasikia tu vitu vidogovidogo lakini si watu wakiongea,” Othman alikuwa akiwaeleza Chiba na Gina, baada ya maelezo marefu waliliridhika na kuondoka zao ndani ya jengo hilo jeupe.
***
OFISI NDOGO

NDANI YA ofisi ndogo ya Madam S, jopo la TSA lilikutana kujadili kile walichokiita uchunguzi wa awali. Madam S, Chiba, Jasmine na Gina walijifungia na kupanga awamu ya pili ya kazi yao.
“Hawa jamaa kwanza walikuwa na mavazi meusi, na waliivamia Ikulu kupitia upande wa baharini kwa kutambaa juu ya bomba la maji machafu ili kuhadaa wanausalama walio kazini. Kwenye ukuta wa upande huo nimekuta kitu hiki,” akawaonesha zile picha za ile soli ya kiatu.
“Chiba!” Madam S akaita kwa mshtuko.
“Nini Madam?”
“Endelea nitakwambia kitu,” akamruhusu.
“Sasa hawa wavamizi, naomba niwaite magaidi, walianza kazi yao kwa kuichokonoa hii kamera ya CCTV, waliilubuni hii kamera kitaalam kiasi kwamba ikazisimamisha kamera zote za upande huu kusafirisha still picture ya saa 8:45 usiku wa manane”.
“Sasa Chiba, hiyo kamera wameilubuni vipi, hapo umenichanganya asee ijapokuwa tulikuwa wote!” Gina aliuliza na wengine wakatikisa vichwa.

“Hizi ni tekniko za kiufundi jamani, sio kila kitu muelewe, kwa kifupi, aina hii ya CCTV tunayotumia pale Ikulu zinatumia kadi maalum kwa ajilki ya usafirishaji wa picha zake kwenda kwenye monitor, sasa hawa jamaa ina maana wanazijua hivyo wakabadilisha kadi, na kadi hiyo siyo rahisi kwa fundi wa kawaida kugundua. Hivyo ni vitu ambavyo sisi tunajifunza kwa sababu maalum,” Chiba akaeleza na wakati huo huo simu ya mezani kwa Madam S ikaunguruma, akawap ishara ya kunyamaza kisha akinyanyua na kuiweka sikioni.
“Hello!”
“…TSA1 online…”
“Copy! Endelea…” Madam S alijibu kwa furaha.
“…mwanaume bado anapumua, niko njiani kuja nyumbani, uno trabajo!” ile simu ikakatika.
“Kamanda Amata yuko njiani…!” akaliambia jopo na wote wakalipuka kwa furaha kushangilia taarifa hii.
“Kazi imekwisha, nilikuwa nawaza mimi, maana Madam ulinipa kazi nzito sana,” Gina akasema huku akienda kwenye jokofu na kuchukua mvinyo mlipuko, akaifungua na kuwapatia kila mmoja kwenye bilauri yake.

MAKAO MAKUU YA NCHI YA NDURUTA

KANALI BENSOIR BANGINYANA alikuwa katika kikao kifupi na rais wa nchi ya Nduruta au Mkuu wa wakuu kama alivyopenda kumwita. Kikao hiki kilifanyika mara tu baada ya kutoka Uwanja wa Ndege na kabla hajaenda Mpumbutu.
“Mkuu, kijana wangu ameuawa huko Ujerumani kama nilivyokutumia taarifa, na mtu aliyemuua ni huyu,” akampa picha ya Amata, Yule rais akaiangaliaa na kusonya.
“Huyu ni nani?”

“Anaitwa Amata Ric au kamanda Amata,” Bensoir akajibu. Yule Rais akafinya macho na kuibana pua yake kisha akaiweka miwani yake ya duara vizuri katika macho yake na kumtazama Banginyana huku akiichana ile picha na kuitumbukiza kwenye pango la kukokea moto.
“Nimeshamjua, huyu bwana ndiye tulimpendekeza kumaliza lile swala la kule Afrika Kusini, ndiye aliyemuua Sir Robinson Quebec,” akasimama na kulielekea dirisha.
Baada ya dakika kama tatu hivi alaimgeukia banginyana, “Sikiliza Banginyana, hii nchi ya Tanzania isijifanye ndiyo yenye nguvu katika ukanda wa Maziwa Makuu, tupo wenye nguvu na tutazidhihirisha muda si mrefu. Nasema hivi, huyu ajenti wao namuua…”
“Mkuu, mbona yupo mikononi mwa Jirack…”
“Eeeeeee, ishia hapo hapo!” akamsogelea, “Ametoroka, na lile jumba kule Manheim amelilipua lote, na sasa hajulikani alipo,” Rais Kadanse Sebutunva alimwambia Banginyana ambaye alionekana kushtuka maan hakujua kilichoendelea.

“Kanipigia simu Jirack na amesema yuko tayari kufadhili kila aina ya ufadhili ili huyo anayejiita Amata afutiliwe mbali katika uso wa dunia. Huko Ujerumani haonekani alipo na wanamsaka kila kona,” rais akaeleza, “Tuyaache hayo, silaha zitashushwa kesho Mpumbutu, uwe pale, hakikisha ndani ya siku nne umesafisha hicho kijeshi chao, hii operesheni nyingine niachie mimi nitakwambia mambo yanaendeleaje,” akamaliza na kuondoka kwenda zake ofisini kwake. Kichwa kilimzunguka hakujua nini anatakiwa kufanya, huyu rais wa Tanzania hanijui mimi, sasa namtangazia vita, naamsha watu wangu wote niliowapachika waanze kumhujumu, kuanzia kwenye idara yake ya usalama mpaka Jeshi analolitegemea laity angejua kuwa kuna watu wangu asingeleta nyodo, sasa nammaliza, akawaza na kupiga ngumi mezani. Akainua simu na kuitisha kikao cha dharula cha vibaraka wake kutoka nchi jirani, na ni siku hiyohiyo usiku wa manane. Na wao kutokana na kutawaliwa bila wao kujijua walikutana usiku huo huo katika mji mkuu wa Nduruta na kufanya kikao hicho cha siri.
Akawasimulia kila jambo lililotukia huko ughaibuni na jinsi alivyokasirika na mipango aliyoamua.

“Huyu sio mwenzetu kabisa, unajua wao wana linchi likubwa lakini uchumi wao umedorola kila siku, mi nataka ile nchi iwe chini yangu,” akaeleza hisia zake.
“Iwe chini yako kivipi? Utaingiaje pale?” swahiba wake ambaye hupenda kuvaa pama mara nyingi aliuliza huku akigusagusa mustachi wake pale chini ya tundu za pua.
“Sikia sasa tutampa pigo la kwanza la kisaikolojia, hili ni pigo la kiuchumi, unajua nchi yangu, Ngoko na nyingine kama ile kule Lamawi zote tunategemea bandari kwake nah ii inamnufaisha sana…”
“Sasa unataka kufanyaje?” mjumbe aliyekuwa kimya muda wote akauliza.
“Nataka tujenge reli itakayotokea nchini kwako, ipite kwa huyu bwana ije mpaka hapa Nduruta kisha mizigo yetu yote itapita kwenye bandari yako hiyohiyo na kusafirishwa kwa reli mpaka hapa, kwisha habari…”
“Mi nilifikiri unataka tumvamie kijeshi,” Yule mwenye pama akasema.

“Hata kama ni kijeshi, hana kitu Yule, unajua mipango yake yote ya kiusalama ninayo hapa, silaha zake zote za kijeshi ninazo hapa, kila wanachofikiria juu yetu ninakijua kwa hiyo wala hanibabasihi, najua mpaka leo saa ngapi ataenda kuoga, sasa kazi inaanza, sikilizeni redio,” akamaliza akiwa anatokwa na jasho la pua.
“Mi nafikiri ili tuwe vizuri, kwanza ni kuanzisha umoja wa nchi hizi nne halafu yeye mwenyewe atajiona anatengwa mpaka hapo tayari atajua kuana jambo,” Yule mjumbe mkimya akatoa wazo lake na wote wakaliafiki, wakapanga kukutana baada ya wiki moja na vyombo vya habari vitangaze mkutano huo.

ITAENDELEA
 
Haya wadau kwa leo zinatosha hizo tutaendelea badae.
 
RIWAYA: PASIPOOTI YA GAIDI
MTUNZI: richard MWAMBE

“Hata kama ni kijeshi, hana kitu Yule, unajua mipango yake yote ya kiusalama ninayo hapa, silaha zake zote za kijeshi ninazo hapa, kila wanachofikiria juu yetu ninakijua kwa hiyo wala hanibabasihi, najua mpaka leo saa ngapi ataenda kuoga, sasa kazi inaanza, sikilizeni redio,” akamaliza akiwa anatokwa na jasho la pua.
“Mi nafikiri ili tuwe vizuri, kwanza ni kuanzisha umoja wa nchi hizi nne halafu yeye mwenyewe atajiona anatengwa mpaka hapo tayari atajua kuana jambo,” Yule mjumbe mkimya akatoa wazo lake na wote wakaliafiki, wakapanga kukutana baada ya wiki moja na vyombo vya habari vitangaze mkutano huo.

SEHEMU YA VIII

MSITU WA MPUMBUTU

JESHI LA TANZANIA lililokuwa chini ya mwamvuli wa UN lilisonga mbele ndani yam situ huo, walishangaa hakukuwa na upinzani wowote katika harakati hizo mpaka wamekaribia kabisa eneo wanalolihitaji, kwa mbaaaaali chini ya milima waliona kambi ya waasi iliyokjengwa kwa mahema mengi sana. George Kolongo, mtaalamu wa kusoma ramani wa jeshi hilo, aliigua karatasi yake kubwa na kuitazama akishirikiana na wenzake watatau.
“Hii ndiyo kambi kuu ya waasi, ndiyo ile paleeeee chini ya milima, ahalafu huku nyuma yam lima Busese ndipo kwenye machimbo ya almasi hadimu ya Mpumbutu inayosababisha haya yote” Kolongo aliwaambia wenzake.
“Sasa hawa tuwavamie kwa mtindo wa ‘mtu kati’, tuwazunguke kisha tukiteremka tunawamaliza,” Kapteni Ngauya alitoa wazo huku akionesha maeneo ya kuingilia kwa kutumia vidole vyake juu ya hiyo karatasi.
“Mshapata mbinu ya jinsi ya kuwavamia?” akauliza kiongozi wa vikosi vyote aliyekuwa mstari wa mbele ambaye kwa amri yake wangefanya vile alivyosema.

“Tayari, hapa ni kupiga ring attack kama mnavyojua ni mbinu yetu ambayo tumeitumia sana kwa hawa watu na tumeona matunda yake, tukishakuwa tayari tuna kamilisha kazi,” Yule kiongozi aliyekuwa na cheo kikubwa begani mwake aliwaambia vijana wake, kisha kwa kutumia kifaa chake cha mawasiliano alivipanga vikosi vyote kuzunguka ile himaya na wakati huo akiwatuma nyoka wake wateremke chini na kuingia kambini ili kupata habari mbili tatu kabla hawajaangusha timbwili ambalo wao waliliita ‘parapanda’.
“Kumbukeni tunaenda kusafisha waasi, naomba vikosi vyote tasa vipite kushoto na vile vya shufwa vipite kulia, wadunguaji pia mtatawanyika kwa mtindo huo huo lakini ninyi hamtashuka, bali mtabaki juu mita 500 ili kuua nguvu za waasi,” kisha akateua vikosi vitano vilivyoshiba na kuvipanga kudhibiti machimbo ya almasi kwani walishakubaliana kuwa baada ya kuiteka kambi ya waasi watoa taarifa ili majeshi zaidi yaje kukalia eneo hilo.
“Tunawachapa kwanza kuwatia adabu kisha ndiyo tunawaita hao wengine waje kudhibiti eneo,” akawaelekeaza na kila mmoja akachukua kona yake tayari kwa kazi. Mbinu ya kusogea eneo husika ilikuwa ni ileile ya kujificha na kutembea, mbinu hii iliwafanya wasionekane kabisa.

“Kila mtu awe na hasira na ndugu zetu watano waliokufa na wengine waliojeruhiwa ambao hatujui kama watapona au la,” Yule kiongozai aliwapa mori vijana wake na kuwaondoa woga kwa kutumia misemo mbalimbali ya kijeshi ambayo daima huwapa hamasa wapiganaji kufanya kazi yao. Wapiganaji wale waliitikia wito wa kiongozi wao, wakaanza kuizunguka ile ngome kama walivyoelekezwa, ndani ya saa moja tayari walifanikisha zoezi hilo la kuizunguka ile ngome, wadunguaji walijiweka vizuri kwenye engo walizoona zinawafaa huku wakitupia macho yao katika lenzi zilizokuwa zikiwaonesha kwa ukaribu kabisa kila kitu kinachoendelea. Kila mdunguaji alikuwa na msaidizi mwenye darubini kubwa yenye nguvu ambaye alitoa maelekezo muda na nani wa kupiga. Nyoka waliopewa kazi ya kuingia kambini nao tayari kwa mwendo usio na papara kama ule wa nyoka waliteremka vilima hivyo huku wakipewa maelekezo wa pi pa kuingilia.
***
HOTEL NEW AFRIKA
JUA LA MAGAHARIBI lilikuwa likipotelea katika katika kona zake za jiji la Dar es salaam. Rangi nzuri ya dhahabu ilikuwa ikilipendezesha jiji hilo wakati gari moja land Cruizer nyeusi iliposimama mbele ya mlango mkubwa wa hoteli hiyo.
Hakuwa mzee aliyeshuka ndaniye bali kijana wa makamo tu, kadirio la miaka 35 hivi, ana mwili wa wastani na sura iliyoonekana haina usawa kwani ilikuwa na aina Fulani ya mabonde ya tabu na matataizo. Hakuwa mweusi wala hakuwa mweupe, huyu alikuwa wa rangi ya udongo lakini udongo uliopigishwa jua kwa nguvu na nyuma ya rangi hiyo basi kulikiuwa na rangi halisi ya mtu huyu mfupi ila aliyeonekana ana mazoezi ya mara kwa mara. Mashavu yake yalijaa kana kwamba anatafuna kitu lakini sivyo bali misuli ya mashavu yake ilikuwa ngangari.

Anaitwa Kubra Kaleb, aliufunga mlango nyuma yake na ile gari ikaondoka kisha yeye kwa hatua fupifupi lakini za haraka haraka akapotelea ndani ya hoteli hiyo, moja kwa moja mpaka kwenye lifti na kupanda mpaka ghorofa ya nane, akaingia kwenye chumba namba 806 na kumkuta mwenyeji wake, mtu mzima, Briston Kalangila.
“Kwema?” akauliza.
“Kwema kidogo, kuna sampuli inabidi kuondolewa sokoni haraka sana, mimi nina moja na Mkuu wa wakuu ana nyingine,” Briston Kalangila akamwambia huku akiketi chini na kufungua pombe kali ya Captain Morgan na kujimiminia kwenye bilauri kisha akaipunga hewani na kuinywa.
Kubra Kaleb naye akavuta kiti na kuketi juu yake, akachukua Coca cola na kuchanganya na Konyagi ya kiroba akainusa na kupiga funda moja.
“Malkia yupo salama?” Briston akauliza.
“Yupo salama anakula na kulala,” Kaleb akajibu.
“Good! Jamaa atasalenda tu, maana kwa sasa namwona yuko kimya sana,”
“Huyu ni jeuri sana, lakini hata wafanye nini hawawezi kugundua chochote, tulivyoingia wala tulivyotoka,” Kaleb akaeleza huku ile bilauri ikiwa bado mkononi mwake.
“Najua, najua kazi yenu, na hapa lazima wapate tabu,” Briston akaongeza.
“Mmemweka kulekule kilindini?”
“Ndiyo! Hakuna sehemu salama na isiyoweza kugundulika kirahisi kama ile”.

“Ah! Ah! Ah! Ah! Safi sana, Kubra Kaleb, Mkuu wa wakuu hakupoteza pesa yake,” Briston akacheka na kusifia.
“Sasa sikiliza, una vijana wangapi mafichoni?”
“Sita, na wote ni komandoo watoro”.
“Safi sana, tazama hii picha…” Briston akamwambia na kumwonesha picha mbili.
“Unamwona huyu?”
“Ndiyo!” kaleb akajibu.
“Huyu kijana leo asubuhi alikuwa anafanya uchunguzi wa kamera za usalama pale Ikulu, anaonekana mkorofi sana, mimi nataka ashughulikiwe mara moja,” Bristona akamwambia kisha akajikohoza wakati Kaleb akiinua ile picha na kutabasamu, “Na nyingine ni hii hapa,” akampa picha nyingine, “Hii imetumwa kwa email na Mkuu leo mchana, sikiliza kwa makini, huyu kijana na ni mtu hatari sana ni Mtanzania alikuwa Ujerumani akichunguza ni akina nani wanaoleta silaha kwa waasi…”
“Amefanikiwa…?”
“Ndiyo amefanikiwa, na amefanya uharibifu mkubwa kwenye ngome ya Yule tajiri, ameua mfuasi wa Banginyana katika ile casino kubwa pale Berlin, wanasema ana weledi mkubwa sana wa kupigana na kuwakwepa maadui. Ametoroka ndani ya ngome ile ngumu ya Jirack, huyu si wa kawaida. Mkuu anaitaka roho yake kabla hajaleta madhara kwani ni mwiba, anasema huyu akifika hapa anaweza kuharibu mpango wote,” Briston akamwambia Kaleb.

“Sawa! Kazi hiyo itafanyika leo hii, cha muhimu ni kumtafuta kujua yuko wapi,” Khaleb alieleza huku zile picha akizitia katika mfuko wake wa shati.
“Bado yuko Ujerumani, ila muda wowote atatua hapa Dar,” Briston akaleza huku akiendelea kupiga funda lingine na lingine kisha akaitua ile bilauri mezani.
“Kikao chetu kitakuwa hapahapa kila mara,” Briston akamaliza na kuagana na Khaleb.
“Sawa hakuna tabu, ila sasa lazima niweke watu pale uwanja wa ndege wa Dar ili akitua tu amalizwe, hafai kuishi. Unajua Briston kuna watu hawatakiwi kuishi duniani; wambea, wachawi, wezi, wanga na watu kama hawa, nakuhakikishia hatoikanyaga ardhi ya nchi yake akiwa hai, lazima wapokee mwiliwa marehemu,” akaitoa ile picha na kuichana vipande viwili kisha akaichoma kwa kiberiti chake cha gesi, na kuufungua mlango tayari kwa kuondoka.
“Khaleb! Be careful” Briston akamwambia kisha wakaagana kwa macho.

Khaleb akaiacha hoteli hiyo ya New Africa na kuingia katika gari hiyo, ndani ya gari aliifungua kompyuta yake na kuwasiliana na watu anaowajua yeye kuwa wanaweza kumsaidia kazi yake, akapekua hapa na pale na kumpata kijana mmoja anayemwamini sana ambaye kishawahi kumfanyia kazi ngumu na za haraka na akafanikiwa pasi na kushtukiwa na mtu yeyote au mamlaka husika. Baada ya kumpata mtu huyo, akawasiliana na vijana wengine wa huko Ujerumani kuhakikisha Amata ni ndege ya shirika gani anaondoka nayo, akawapa maagizo wasimdhuru bali wahakikishe usalama wake mpaka atakapoingia ndegeni...

HEIDELBERG – UJERUMANI
KAMANDA AMATA akiwa na Scoba waliwasili kwenye moja ya hoteli ndogo za jijini Heidelberg, mjia ambao haukuwa mbali kutoka Mannheim. Walifika katika jiji hilo baada ya hapa nap le kupanda katika magari ya wakulima watokao mashambani na kuwasili alfajiri ya siku iliyofuata.
“Sasa hapa tusipoteze muda, inabidi turudi Berlin ili nikachukue vifaa vyangu,” kamanda akamwambia Scoba wakati wakitembea kwa miguu na kukatiza viunga vya jiji hilo. Bado watu walikuwa hawajaamka lakini baadhi ya magari tayari yalikuwa barabarani kuelekea huku na kule, baridi ilikuwa kali miezi hiyo ya mwisho wa mwaka lakini Amata na Scoba waliivumilia huku wakijikunyata hapa na pale.
“Nafikir hapa patatufaa kwa dakika chache kabla hatujaliacha jiji hili maana lazima ubadilike Kamanda,” Scoba akamwambia huku akikata barabara moja kuelekea kwenye hoteli ndogo iliyo upande huo.
“Ndiyo Scoba, na inabidi tuanze kutafuta usafiri sasa wa kuondoka Berlin haraka,” kamanda akaisistiza.
“Usijali, niko hapa kwa ajili yako, lakini Berlini hapakufai kwa sasa maana hujui adui yako anakusubiri wapi,” Scoba akamwambia.

“Usijali wakati mwingine huna budi kujionesha kwa adui ili upate dondoo za kuendelea mbele,” akiwa katika kuzungumza hilo, tayari waliwasili katika moja ya hoteli ndogo za hapo Heidelberg, Hoteli Kohler. Moja kwa moja wakaingia na kufikia mapokezi ambapo walipokelewa na kuchukua vyumba viwili kwa kujibadili kidogo kimavazi. Scoba akauliza kama anaweza kupata huduma za manunuzi ya nguo na vitu kadhaa, wakampatia kitabu maalumu akajaza na kuingiaza namba za kadi zake za benki kisha Yule mwanadada akachukua ile kadini na kuichanja kwenye kimashine Fulani kisha akamrudishia na kumpa funguo ya chumba.
Scoba na Amata wakapanda ghorofa ya pili na kila mmoja akaingia katika chumba chake. Ndani ya chumba cha kila mmoja kulikuwa na kila kitu, vinywaji mashati ya kubadilisha. Amata alivuta hatua mpaka kwenye kabati na kufungu akakutana na suti pea nne za kisasa na za gharama, akachagua ile yenye namba inayomtosha na baada ya kujiswafi maliwato akaivaa nguo hiyo iliyomsitiri vizuri na kuonesha ushababi wake wazi wazi.

Nusu saa iliwatosha watu hao kujibadili kabisa na kuonekana wengine kutokana na utanashati wa mavazi hayo, wakatoka na kusaini kwenye vitabu kisha wakaondoka zao majira kama ya saa tatu asubuhi. Tax waliyokodi ikawafikisha katika stesheni ya treni iendayo kasi, wakakata tiketi ya kuelekea Berlini na dakika tano zilizofuatia walikua njiani kulikabili jiji hilo.
“Tutafika kwanza hotelini kwangu, na wewe ndiye utakwenda kunichukulia vitu vyote,” Kamanda alimwambia Scoba.
“Kamanda Amata, kila kitu nilishakihamisha, sasa hivi ni kufika na kunyanyua begi lilipo na kuondoka,” Scoba akajibu.
“Waoh, ulishafanya hilo?”
“Muda mrefu sana, nilipoona tu signal yako imepotea name nikafanya hilo,”
“Ulikuta nini chumbani kwangu?”
“Kwani we uliacha nini zaidi ya kukuru kakara zako tu?” Scoba akauliza.
“Nilimwacha msichana mrembo kalala kitandani,” Amata akajibu huku akiendelea kunywa kahawa katika chumba hicho walichoketi wao wawili tu huku wakiangalia madhali ya ya miji waipitayo kasi kuelekea Berlin. Wakiwa katikati ya maongezi, mlango wao ukagongwa na kisha kufunguliwa, vijana wawili waliovalia mavazi ya kiaskari lakini hawakuwa askari walijitokeza, hawakuongea chochote, waliwatazama tu kisha wakafunga ule mlango na kuondoka. Scoba na Amata wakatazamana kisha wakacheka bila kutoa sauti.
“Sikumkuta huyo mrembo,” Scoba alianzisha tena mazungumzo. Hapo Amata akili yake ikakimbia kwa kasi na kugundua kuwa Precious Nancy yuko hai, ndiyo maana Scoba hakumkuta chumbani alikomwacha amezimia.

“Vipi kaka mbona hivyo? Maana we nakujua damu ikishaanza kukuchemka unakuwaje…”
“Ni kweli Scoba, nilimwacha mrembo mmoja akiwa amezimia kitandani kabla mi sijatekwa na hawa majahili. Kama hujamkuta ina maana yuko hai na anaweza kuwa tatizo kwangu.”
Asubuhi ya saa tano waliwasili Berlini, wakajiweka sawa kwa kuteremka kwenye treni ile.
“Uko tayari?” Amata akauliza.
“Ndiyo!” Scoba akajibu kisha wakatoka ndani ya kile chumba. Amata akatazama huku na huku kisha akakunja kushoto na kuufuata mlango uliokuwa tayari umefunguka automatiki ukisubiri watu kushuka. Alitangulia Amata kukanyaga ardhi ya jiji hilo kwa mlango wa upande mmoja na Scoba akashuka kwa mlango wa upande wa pili. Kamanda Amata akaitazama saa yake na kurudihsa mkono chini, alipoinua kichwa kutazama upande wa pili wa treni hiyo ambapo aliweza kuona japo kwa nusu kutokana na ukubwa wa vioo, moyo wake ulipiga chogochemba kwani hakuamni kama anayemwona ni Precious. Kajuaje kama nitakuwa hapa sasa? Akajiuliza huku akihakikisha mwanamke huyo hapotei machoni pake. Akiwa katika mshangao huo akahisi kitu kikimpiga mgongoni.
“This way!” kikafuatiwa na sauti hiyo, alipogeuka akamwona Scoba kishapita hatua mbili tatu mbele, aliporudisha macho hakumuona Precious. Amata akamfuata Scoba mp[aka kwenye maegesho, hapo Scoba akaikuta ile gari imetulia kama alivyoiacha jana yake. Akaminya saa yake, ikawaka mwanga wa kijani tu.
“Usalama upo?” Kamanda akauliza.
“Upo!” wakaingia na kuketi kisha akawasha na kuliondoa eneo hilo.

UWANJA WA NDEGE WA TEGEL
BERLIN, UJERUMANI

SCOBA ALIEGESHA gari panapohusika, akateremka na kufungua buti, kila kitu kilikuwa salama wakateremsha mizigo tayari kwa kuondoka. Mbele yao ikapita gari moja BMW kwa kasi sana kisha ikasimama umbali wa kama mita ishirini na kurudi nyuma mpaka pale walipoa Scoba na Amata ikasimama, kioo kikataremka na uso mrembo wa Precious ukajitokeza, akamtazama Amata kisha akasonya.
“Wasalimie kuzimu!” akamwambia huku kioo kikipanda na ile gari ikiondoka. Scoba na Amata wakatazamana tena, kisha wakavuta mabegi yao kuelekea ndani ya uwanja huo.

***
Kubra Khaleb alivivutavuta vindevu vyake vichache huku akiiweka simu masikioni mwake tayari kuongea na mtu wa upande wa pili.
“Yes, anaondoka na ndege ya shirika la Qatar, atapitia Doha, hakikisha unapata usafiri na kumaliza kazi. Huyo mtu hatakiwi kuteremka akiwa hai bali mwili wake tu ili uzikwe na wengine,” akamaliza na kukata simu. Kisha akarudi na kuingia katika gari.
“Sikilizeni, baada ya saa saba, wewe na wewe mtakuja hapa uwanja wa ndege muhakikishe huyu mtu ameshuka akiwa marehemu na si vinginevyo,” akawaambia vijana wake huku ile gari ikiondolewa, “Na vilevile kijana wetu atakuwa kava shati la maua maua mumpokee na kumleta hoteli ya New Africa,” akaongeza kusema wakati ile gari ikichanganya mwendo. Ukimya uliotawala ndani ya gari hiyo ulikatishwa na kelele ya simu ya Kubra, akainyakuwa na kuiweka sikioni.
“… sawa! Sawa kabisa, basi nategemea kazi itakuwa sawa,” akakata simu na kuwageukia watu wake, “Amepata…”

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA
DOHA – QATAR

RAJAN KADAH aliwasili uwanja wandege wa Doha dakika arobaini na tano kabla ndege ile haijafika, akakamilisha taratibu zote za safari ikiwamo ukaguzi wa tiketi na hati yake ya kusafiria. Alipohakikisha kila kitu kipo sawa alisubiri safari hiyo huku moyo wake akiwa keishaupanga kwa kazi moja tu. Muda ulipofika ndege ile iliwasili Doha na abiri walitakiwa kubadili ndege baada ya nusu saa kwa safari za Dar es salaam na miji mingine mikubwa ya ulimwenguni. Kamanda Amata na Scoba waliteremka lakini kila mmoja alikuwa na hamsini zake kiasi kwamba ilikuwa ngumu kujua kuwa watu hao wako pamoja, kila mmoja kati yao alikuwa na simu mkononi na kupachika vifaa vya kusikilizia masikioni. Lakini kwa vifaa hivyo waliweza kuwasiliana kwa siri juu ya kile ambacho walikuwa wakikitilia shaka.
Kama kawaida ya Amata, nusu saa ya kusubiri kwake ni kubwa sana, akajipenyeza na kuibukia kwenye duka la vinywaji vikali ndani ya uwanja huo, akaagiza kile anachohitaji kutumia na kuketi katika moja ya viti vilivyopo hapo. Scoba aliendelea kuketi palepale kwenye viti na abriria wengine huku akiendelea kusikiliza muziki lakini pia jukumu la usalama lilikuwa palepale.

Scoba aligongana macho na kijana huyo wa Kihabeshi katika harakati zake za kutazama huku na kule, kutokana na utaalamu wake kama kachero wa kumsoma na kumtambua mhalifu, akili ya Scoba ilitua kwa kijana huyo umakini wake ukayasoma macho. TSA 4 akauona wazi uhalifu wa kijana huyo ndani ya mboni za macho yake mawili. Akampa ishara Amata ambaye bado alikuwa akipombeka pale kwenye kile kiduka. Amata alipopata taarifa hiyo ya kumhofia huyo kijana alihitaji kujiridhisha kama anaweza kuwa na madhara. Amevaa shati la dhambarau, akawaza huku akiteremka kutoka pale kitini maana tangazo tayari liliwataka kuingia ndegeni.
Rajan Kadah alikuwa akimwangalia Scoba kwa wizi, kisha mara kwa mara alikuwa akiangalia picha ndogo aliyonayao na kuona haifanani na mtu huyo, lakini kila alipopepesa macho kwa abiria wengine hakuona mtu ambaye haswa anamtaka. Akanyanyuka kutoka pale alipokuwapo, na kujiunga katika foleni ya kuingia katika mlango maalum ambao ungemfikisha katika ndege hiyo. Rajan akasubiri Scoba aende kwenye foleni hiyo na Scoba alilijua hilo, bila kufikiri akaenda zake na Yule kijana akaja nyuma yake. Muda huohuo, Amata aliwasili kwenye foleni na kusimama nyuma ya Rajan. Katika harakati za kuingia ndegeni kijana huyo akageuka nyuma na kukutana macho na Amata, mshtuko wa wazi uliyashika macho yake, Amata hakutetereka alimkazia macho yake na kisha wakaendelea kwenda.

Ndani ya ndege hiyo waliketi viti tofauti huku Rajan akiwa kiti cha nyuma ya Amata, Scoba yeye alikuwa kiti kama cha tatu lakini katika safu ya upande mwingine, hivyo aliweza kuwaona wote yaani Amata na Rajan. Ndege ilipokuwa angani, Rajan alionekana wazi kukosa utulivu, mara ajishike hapa mara pale ilimradi tu alikuwa hajui anapaswa kufanya nini. Dakika moja mbele Kamanda Amata aliinuka na kufuata ujia uliokuwa ukielekea nyuma ambako kulikuwa na huduma ya maliwato. Nyuma yake na Rajan aliinuka na kuelekea upande uleule, alipofika kwenye mlango wa choo kile akakuta kitasa kimejiandika ‘vacant’ ikimaanisha kuwa mlango huo haujafungwa au ndani yake hakuna mtu anayetumia choo hicho, akatulia kama sekunde tano hivi kisha akakamata kile kitasa na kukinyonga taratibu, alipohakikisha kuwa kimeshafayatuka akauvuta mlango na kuingia ghafla lakini hakukuwa na mtu, akabaki kapigwa na butwaa. Kaenda wapi mshenzi huyu? Akajiuliza huku akitazama juu na chini ndani ya kijichumba hicho, akasonya na kugeuka tayari kwa kutoka. Hamad, alipofika mlangoni alikutana uso kwa uso na yule anayemtafuta, Rajan alihisi ganzi mwili mzima, akamtazama Amata aliyesimama bila kuonesha hata tabasamu. Amata alivuta hatua kuingia ndani na kijana huyo alirudisha hatu kurudi ndani kisha Amata akaufunga mlango.

“Kwa nini unanifuata fuata?” akamwuliza.
“Wewe unajua kwa nini nakufuata, au unataka kujua aliyenituma?” Rajani akarudisha jibu ksha akapiga swali.
“Sina haja ya kumjua mpumbavu yeyote aliyekutuma kwa kuwa kama uliona anakutuma basi ujue amekuua,” Amata akamwambia kwa sauti ndogo.
“Never!, huwezi kunikua wewe mbwa mweusi. Inelekea hujawahi kukutana na Rajan Kadah! basi leo utabaki histori,” Rajan akamkazia macho Amata ambaye naye alikuwa amesimama bila kupepesa macho hata kidogo, “Kwanza utaniuaje?” Rajana akauliza.
“Kwanza nitakuvunja mfupa Clavicle, kisha nitakuuliza maswali mawili tu yenye vipengele na mwisho nitakuvunja shingo,” Amata akamwambia. Rajan akacheka sana aliposikia maneno hayo. Kamanda Amata alimtazama kijana huyo anayejigamba kuwa hawezi kuuawa na mbwa mweusi. Kwa kasi ya umeme, Kamanda Amata akapiga pigo moja kali la karate likatua begani karibu kidogo na shingo akavunja clavicle kisha kwa kichwa chake alimpiga Rajan naye akajibamiza ukutani na kuanguka chini akigugumia maumivu. Kamanda akamkanyaga shingoni kwa nguvu na kutazamana naye.

“Nani unamfanyia kazi?” akamwuliza lakini Rajan hakuweza kujibu, maumivu ya lile pigo kwa namna Fulani yalimpa wakati mgumu. Rajani kutoka pale alipo, aliinuka ghafla na mkono wake ukakamata korodani za Amata. Kwa pigo moja la nguvu Amata aliivunja shingo ya kijana huyo, naye akaanguka chini bila ubishi.
“Vipi?” Scoba aliuliza kutokea nyuma.
“Kwisha kazi!” Amata akajibu, huku akimpekua hapa na pale na kutoa vitu mbalimbali mfukoni mwa yule jamaa, miongoni mwa vitu hivyo kulikuwa na kadi za benki, hata ya kusafiria yaani pasipoti, simu na pesa tasilim. Kamanda hakuchukua pesa hizo alimwachia marehemunna yeye akachukua vinavyomhusu.
“Sasa hapa itakuwaje, si watagundua!” Scoba akamwambia Amata.
“Shauri zao!” akatoka na kuufunga mlango kisha akakwanyua kitasa na kukivunja ili iwe ngumu kwa mtu kutoka nje kuingia kisha akarudi katika kiti chake na kuketi.
***
Gina aliegesha gari uwanja wa ndege majira ya saa kumi na mbili jioni hivi, hakuteremka bali alifyatua kiti chake na kujilaza akiruhusu sauti ya muziki laini kuyapenya masikio yake, akiwa katika starehe hiyo akapitiwa na usingizi.
Nyuma yake ilikuja Land Cruiser moja na kuegeshwa katika mstari uleule lakini kati ya gari hiyo na ile ya Gina kulikuwa na nyingine kama nne hivi. Hisia za Gina akiwa usingizini zilifanya kazi, akafumbua macho taratibu na kuinuka huku akikiacha kiti bado kipo katika mtindo uleule wa kulala. Alipogeuka huku na huku akawaona wale jamaa wawili walioshiba wakiwa wanelekea kule uwanjani, akili yake ikamsihi atie umakini juu ya watu hao, naye akatii. Akateremka na kuifunga gari kisha akawafuata kwa nyuma huku akihakikisha kuwa silaha yake aliyo nayo iko tayari kwa kazi endapo italazimu.
Wale jamaa wakatafuta nafasi ambayo iliwawezesha kuona vyema kule ile ndege itakaposimama na kutoka hapoi wangeweza kuona kila anayeshuka, mikononi mwao walikuwa na picha ya Amata kuwa endapo akishuka hai basi wamfungie kazi.

Saa kumi na mbili kamili jioni, ile ndege ikawasili pale JNIA na kuchukua eneo lake la kuegesha, kisha ngazi kubwa kabisa ikasogezwa na kupachikwa mlangoni, dakika moja iliyofuata watu wakateremka na kuteremka lakini hakuoneka Yule mwenzao wala hawakumwona Amata. Wakati wale jamaa wakihamaki kutomwona mwenzao na Gina alihamaki kutomwona Amata wala Scoba.
Wale jamaa wakapiga simu kwa Khaleb na kumweleza hali halisi.
“Ina maana hakuwamo katika ndege?” wakaulizwa.
“Hatujui kwa sababu abiria ndiyo wameshaisha nay eye hatumwoni, wala huyu mjinga uliyetupa picha yake naye haonekani,” kiongozi wa operesheni hiyo akajibu.
“Fanyeni kila mnachoweza mhakikishe mnapata habari zote juu ya jambo hilo kabla hamjauacha huo uwanja, mgawane, mwingine apeleleze kujua kama Rajan alikuwamo na mwingine apeleleze kujua huyo Amata sijui Amanda yuko wapi kisha mnipe taarifa moja kwa moja, nasubiri”. Ile simu ikakatwa na wale jamaa wakabaki kutazamana wakiwa hawajui la kufanya.

ITAENDELEA ..
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI

MTUNZI: richard MWAMBE

“Nafikiri tumepata picha na tumejua pa kuanzia, asante Kamanda kwa uwepo wako, yaani Jirak angekuua ningemla nyama…”
“Na nilimwambia kuwa ungeenda kumnasa vibao…” kamanda akamkatisha Madam S kwa maneno yake ya utani.
“Ok, sasa ipo hivi, Gina unajua wajibu wako sijabadilisha, ila Kamanda fanya unaloona linafaa kwa sasa, Scoba utakuwa na mimi kuna kazi maalum leo, naomba tukutane ofisi ndogo kesho saa kumi n ambili jioni, asanteni na kwaherini,” Madam akamaliza kikao hicho na kila mtu akainuka tayari kwa kazi.

SEHEMU YA IX

rejea.... MPUMBUTU

USIKU WA SAA NANE waasi wote walikutana katika uwanja mdogo na kiongozi wao Kanali Bensoir Banginyana alijitokeza kati yao na wote wakaanza kupiga makofi na kuimba nyimbo za kijeshi za kusifia kundi lao na kumtukuza kiongozi wao huku wakimpa sifa za kutosha Mkuu wa Wakuu yaani Rais wa Nduruta.
“Nimewaamsha usiku huu makusudi, nyote mnajua kuwa hapa tulipo tunawindwa na majeshi ya Tanzania yakiwa chini ya mwamvuli wa UN. Hatuyaogopi na nasema tena hatuyaogopi na tutayasambaratisha kama yale mengine yaliyokuja hapa. Sisi ni wanyama wabaya kuliko wanyama wenyewe,” alipotamka hayo wale waasi wakashangilia na kupiga risasi hewani kisha wakanyamaza.

“Nawaambia hivi kwa sababu, juu hapo ya milima majeshi hayo ya adui yamezunguka hivyo sasa ni kwenda kuwasambaratisha, wanajifanya wajanja kumbe sisi ni wajanja zaidi, mafunzo mliyopewa na wale jamaa wa Khazakhistan myatumie vyema, tunatoka sasa kwenda kufagia, kama jana wamezika watano basi wiki iajyo wazike mia tano, na tuna silaha mpya kabisa kutoka Bolivia, na tuzitumie ili zijue kuwa zimeletwa zifanye kazi na si kutembeatembea migongoni na mikononi ka za Wartanzania,” kisha akachukua bastola yake na kupiga hewani mara tatu akiashiri sasa kila mmoja aanze kazi ya kusaka adui.
Juu ya milima ile vikosi vya UN vilitulia kimya kabisa kana kwamba hakukuwa na kiumbe katika msitu huo, walikuwa wakisikia hotuba yotye kupitia chombo cha Joru ambaye alikuwa katikati ya waasi hao nay eye ndiye alikuwa kiongozi wa kuanzisha mashangilio.
Joru katikati ya waasi aliikoki bundui yake kubwa tayari kuungana na waasi hao kulishambulia jeshi lake, mfukoni mwake alikuwa na chombo kidogo ambacho kiliunganisha mabomu yote yaliyotegwa kwenye yale magari, alisubiri amri tu ya kamanda wake ili afanye kazi hiyo kwa sekunde moja.
“Joru, Joru!” sauti ikaita kwenye kifaa chake kidogo alichokipachika sikioni.
“Nakupata kiongozi,” akajibu.
“Toa mkono kwenye sikio haraka, toa!!” Yule kiongozi akamkaripia Joru kwa kuwa alijua kwa kuweka kidole chake sikioni wangemgundua kuwa alikuwa katika mawasiliano na mtu mwingine.

“Unasemaje mkuu sikusikii vyema…”
“Hey, Stop, hapo ulipo simama!” sauti ikatokea nyuma yake, Joru akahisi ganzi kwani waasi wawili walikuwa wakimfuata pale alipo.
“Unaongea na nani?” mmoja akauliza kwa sauti kavu, wakamfikia na kumvua kofia.
“Ha! Bonsoli umeiona hii kofia, huyu ni nyoka, auawe!” mmoja wa wale waasi akmwambia mwenzake mara baada ya kuichukua ile kofi nyekundu lakini alipoigeuza kwa ndani ilikuwa ya buluu bahari na nembo ya majesji ya UN. Joru alipigwa konde zito, akapigwa ngwara akaanguka chini kwenye tope.
“Msaliti mkubwa, peleka kwa Banginyana akamshughulikie,” mwingine akatoa amri, Joru akainuliwa na kupewa kichapo kikali kisha akapelekwa hemani.

HOTELI-NEW AFRIKA DAR ES SALAAM
Usiku uo huo

KUBRA KHALEB aliegesha gari nje ya hoteli hiyo na kuteremka, moja kwa moja aliingia na kupanda lifti mpaka ghorofa ya juu aliyokuwa akiitaka, akaingia na kukutana na mwenyeji wake Bwana Briston Kalangila, ndani ya chumba kilekile namba 806.

“Yes Khaleb, unaonekana leo hauna raha vipi?” akauliza.
“Jaribio limefeli, Kalmat ameuawa,” Khaleb akamwambia Briston.
“What! Hii sasa balaa, Kalmat muuaji hatari aliyeshindikanika kote tulikomtumia, lo!” Briston alisikitika, “Ni nani huyu mshenzi? Nahitaji nikutane nae uso kwa uso nimjue,” akalalam huku kijasho cha kwapa kikimchurizika.
“Mbona nasikia ni mtu wenu wa usalama huko huko?” Khaleb akauliza.
“Hapana, simjui huyo, mimi ninajua watu wote wa usalama nchi hii na nimewaweka wakuu wote wa idara za miko na wilaya, lakini huyu mtu hapana labda kama yuko MI,” akajibu.
“Hapana, hayuko MI, huyu ni TSA,” Kheleb aktoa maelekezo.
“TSA?” Briston akauliza, “Hiyo idara mii siijui hakika,”
“Basi kama ni hivyo bado hujaweka mikononi idara zote, huyu jamaa ni mtu wenu, na ninahitaji kumuua kwa mkono wangu maaha kwa upiganaji huyu atakuwa ni shida, kumbuka Kalmat ni mpiganaji mzuri sana lakini kauawa,” Khaleb akaeleza.

“Ok nimekuelewa, nitapeleleza ili nimjue kisha nitakupa mbinu za kumtia mkononi, hilo niachie mimi tuonane hapa hapa kesho muda kama huu, kama kuna taarifa nyingine tutapeana,” Bristona alimaliza na kujiegeme
Za kwa nguvu kitini mpaka kile kiti kikalia ‘kwinyo’ huku akimshuhudi Khaleb akiondoka zake na kuubamiza mlango. Akainua simu na kupiga ofisi ya mapokezi na kuagiza kile anachotaka kije kwa wakati huo kwa mijiri ya kupunguza mawazo mintarafu kula raha. Dakika tano baadae mwanadada mrembo aliingia katika chumba hicho, na utuli aliokuwa amejifukiza ulikijaza kile chumba.
“Karibu mrembo!” akamkaribisha huku akiinuka kitini na kumwendea pale mlangoni, Yule mwanadada akaondoka na kwenda upande wa pili wa chumba, Briston aye akamfuata hukohuko Yule mwanadada akapanda kitandani na kukaa katikati huku akiachia gauni lake refu liangukie upande mmoja, ukizingatia fundi alisahahu kushona (mpasuo). Bristona naye akapanda na hapo Yule mwanadada akaanza shughuli yake ya kupapasa na kuminya mpaka jamaa likawa hoi kabisa, ndmbendembe.

***
Kubrah Khaleb aliteremka ngazi za hoteli hiyo na kutoka nje kabisa ya jingo hilo aliingia ndani ya gari yake na kuketi nyuma ya usukani, akaiwasha na kuondoka eneo hilo huku akili yake ikiwa inakimbia mara mbili kuliko kawaida. Kichwani mwake alimfikiria huyo adui aliyemuulia swahiba wake kama ndugu yake, alitamani kama aonane naye muda huohuo ili amchakaze ikiwezekana, lakini haikuwa hivyo kwani alichokuwa anakutana nacho ni madaladala tu na watu wenye shughuli zao nyingine kabisa. Akaendelea kuifuata barabara ya Azikiwe mpaka maktaba na kukunja kona kulia na kuifuata barabar ya Bibi Titi, alipofika makutano ya Barabara tatu; ya Bibi Titi, Ohio na Ally Hassan Mwinyi, taa zilimuamuru kusimama, akatii na gari yake ilikuwa ya kwanza kabisa. Kichwa chake kilikuwa kikiwaza mengi hata taa ziliporuhusu hakuwa na habari.

“Piii piiiiih!!! Piiiiii” honi za gari za nyuma zilimshtua Kubra akakanyaga krachi na kuingiza gia namba moja kisha akaachia krachi taratibu na kukandamiza kwa mguu wake ile akselereta mara tu baada ya kushusha breki ya mkono, ile Land Cruiser ikafuata barabara ya Ally Hassan Mwinyi kwa mwendo wa kasi. Kubrah akainua simu yake na kubofya kitufe kimoja tu kisha akaiweka sikioni.
“…naomba tuonane jengoni mara moja na haraka!” akasema hayo tu na kukata simu, akairudisha kwenye kidroo chake na kutoa gia namba tatu na kuweka nyingine. Dakika kumi baadaye alikuwa akikunja kona kulia kuelekea Slip way, nayo ilimchukua mpka amitaa ya Masaki, akakaunja kulia na kupiga honi kwenye moja ya majengo mapya yaliyokuwa yakiendelea kujengwa katika eneo hilo. Mlinzi wa kimasai akafungua na ile gari ikapita moja kwa moja mpka mwisho wa barabara ile, ikaingizwa chini ya jengo hilo na kuegeshwa. Punde si punde gari nyingine nne ziliingia eneo hilohilo na kusimama pembeni yake tu. Vijana wane tofauti wakateremka na kumzunguka Kubrah huku mikono yao ikiwa imeshikamanishwa vifuni mwao.

“Wote mmekuja?” akauliza huku akiwaangalia mmoja baada ya mwingine, “Nisikilizeni kwa makini, mwenzetu, ndugu yetu, kijana wetu, mpigania uhuru mwenzetu, ameuawa kwenye ndege, nataka aliyeua auawe, sina masihara hata kidogo,” akawaambia. Wale jamaa walibaki kimya wakimwangalia tu huku giza la eneo hilo chini ya jingo lisilokwisha ambalo bado liko matengezoni likiwapa shida kidogo kuonana.
“Sasa tutampata wapi huyo mtu na hatumjui?” mmoja aliuliza.
“Dakika chache baadae nitawatumia picha na mahali ambapo huyu jamaa hupenda kuonekana,” akawajibu.
“Kiongozi, na yule Malkia kule amegoma kula kabisa,” mwingine akaeleza.
“What? Anakataa kula? Mwacheni afe kwa njaa kwani si tuna undugu gani naye?”...

***
Ndani ya wigo wa Ikulu, Scoba aliegesha gari yake katika amegesho yake na kuzima injini. Kamanda Amata akateremka akifuatana na Madam S, moja kwa moja wakazipanda ngazi za jingo hilo na kupokelewa na Othman, afisa Usalama wa taifa anayefanya kazi karibu kabisa na Rais, moja kwa moja wakaelekea kwenye chumba ambacho walikuwa wakisubiriwa.

“Yule uliyemwulizia huyu hapa!” Madam akamwambia Rais.
“Kijana kwanza nafurahi umerudi, hapa kuna shida ngumu kutatuka kama ulivyokwisha aambiwa, nataka ufanye kazi tupate ufumbuzi haraka,” akaelezwa.
“Mheshimiwa Rais, tayari niko hatua kadhaa mbele na nakuhakikishia ndani ya saa arobaini na nane First Lady atakuwa hapa bila hata mkwaruzo wa kalamu. Lakini kuna mambo ambayo ningependa kujua kutoka kwako…”
“Sawa, sawa kijana uliza tu nitakujibu yote, ninachotaka mimi ni utatuzi wa jambo hili,” Rais akakubaliana na Amata huku Madam S akitikisa kichwa kuafikia hilo.
“Kwa nini hukwenda na mkeo katika ziara yako? Kwa maana tumezoea kuona hilo kila mara,” Amata akauliza huku kwa siri akiwa kaiwasha zimu yake na ilikuwa ikirekodi kila kitu ijapokuwa ndani ya chumba kile hakukutakiwa kurekodi kitu chochote wala kupiga picha.

“Safari hii yeye alikuwa ana mkutano na vongozi wa asasi ziziso za kiserikali, hivyo nikmwacha,” akajibu.
“Nani aliandaa mkutano huo na lini uliandaliwa?” akazidi kuchimba.
“Aaaaa huu mkutano haukuandaliwa muda mrefu ni kama wiki tatu zilizopita, that is why nikamwacha ili ashughulike na hilo lakini baada ya mkutano ule usiku wake ndiyo hayo yakatokea,” akaeleza huku akianza kusikitika.
Ukimya ukapita kati yao, hakuna aliyeongea kwa nukta kadhaa, kisha Amata akajikohoza tena na kuuvunja ukimya ule.

“Sasa Mheshimiwa, huoni kwamba aliyeandaa mkutano huo alikuwa amekula njama? Kwa nini aandae wiki tatu hizi ilhali ulikuwa na ziara ambayo ilikupasa kuondoka na mkeo?” swali hili lilimgutusha mheshimiwa.
“Unasema!” akatamka kwa mshangao.
Kamanda Amata akarudia sentensi yake ambayo iliiingia sawasawa katika masikio ya wawili hao yaani Mheshimiwa Rais na Madam S. Hali ya Mheshimiwa Rais ilikuwa kama inabadilika na kuonekana akipumua kwa nguvu.
“Hivi hili swalama linawezekana eti?” akauliza.
“Hapana, mi nilikuwa nauliza tu. Lakini mkuu labda kuna kundi unalolihisi katika hi….”

“Enheeee hapo hapo kijana umenikumbusha, nilipigiwa simu na watu nisiowajua, wakinitaka nisichukue hatua yoyote juu ya swala hili, ila nikitaka nimpate tena mke wangu basi niyaamuru majeshi ya Tanzania chini ya UN yarudi nyumbani,” Rais alimkatisha Amata na taarifa hiyo ilimvutia zaidi Amata na akajiweka vyema kitini.
“Unaweza kukumbuka ilipigwa lini?” akauliza.
“Siku ileile niliporudi, ndiyo nilipokea simu hiyo,” akaeleza.
“Na simu ipi kati ya hizi mezani iliyopigwa?” akauliza Amata na Mheshimiwa Rais akaonesha mara moja ni simu ipi siku hiyo ilipigwa, Hii simu imeunganishwa kutoka nje? Akajiuliza Amata, “Naomba fundi wangu aje kuichunguza kama inatoka nje au la, tukishajua hilo tu kazi imekwisha,” akaongeza kusema huku akiinua simu yake na kumpigia Chiba, akamwita afike hapo mara moja. Wakati wakimsubiri waliendelea kuongea ya hapa na pale hasa maendelea ya operesheni ile ya kijeshi inayoendelea huko Ngoko. Haikupita hata dakika kumi na tano Chiba alifikiswah katika ofisi hiyo na Yule afisa wa usalama, Othman.

“Chiba, naomba unitazamie hii simu kama laini yake inatoka nje ya hili jingo au la, hilo tu” Amata akamwambia Chiba naye mara moja akaanza kuifuatilia ile laini kuanzi pale na baada ya dakika tano alirudi na jibu kuwa laini ile ya simu ipo kwenye mfumo wa simu za ndani ‘Internal Telephone System’ ambayo simu zake upigwa toka ofisi moja kwenda nyingine ndani ya jingo moja na sin je ya hapo ingawaje unaweza kupiga au kupokea kutoka nje endapo una namba maalum ya kufanya hivyo. Kwa hiyo ina maana simu hii ilipigwa kutoka humuhumu ndani au? Amata alijiuliza.
“Chiba! Ina maana katika mfumo huu haiwezekani simu kutoka nje ikaingia?” aliuliza swalinhilo Amata baada ya Mheshimiwa Rais kuwaelekeza simu zote zilizokuwa mezani kuwa ipi anapokelea simu za mtindo gani.

“Inawezekana kwa sababu huu mfumo uziunganisha simu zote za ndani katika swichi moja inayoitwa PBX. Sasa kama unataka kupiga simu nje ya jingo hili kwa kutumia simu hii kuna namba maalumu unayoitanguliza kisha unapiga namba uitakayo na signal ile itafika kwenye swichi ya PBX kisha hiyo swichi itaitambua kuwa hiyo simu inatakiwa kutoka nje hivyo itakuunganisha na kitu kinaitwa PSTN yaani Public Switched Telephone Network nayo itafanya kazi ya kukuunganisha na unayemtaka, lakini si kila mtu anajua namba za utangulizi yaani jinsi ya kupiga kwenda nje, kwa sababu hii siri hukaa na System Administrator na wachache wanaoaminika kwa kazi maalum,” Chiba akadadavua na kuwaacha hao watatu vinywa wazi huku Mheshimiwa Rais akiwa haamini kila anachosikia.
“Kijana, unataka kuniambia kuwa hiyo simu itakuwa imepigwa kutoka humu ndani?” Rais akauliza kwa shauku.
“Siyo hivyo Mheshimiwa, simu inaweza kupigwa kutoka nje ya jingo hata Amerika na ikaingia katika mfumo huu, ina maana mtu atakuwa anajua anyempigia ni nani,” akamalizia huku akifunga kijimkoba chake. Kwa mara ya kwanza tangu wafike hapo Madam S alifungua kinywa chake.

“Chiba, nataka rekodi ya simu zote za siku ile aliporudi Mheshimiwa zilizopigwa kwenye namba hii, hii ni 603,” akamwambia.
“Sawa hakuna tabu nina uhakika itapatikana tu japo si kazi rahisi sana,” Chiba alieleza na kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana, wakaagana na Mheshimiwa ili wao waendelee na kazi nyingine. Wakatoka wote watatu kayika ofisi ile nyeti, Madam S akaingia katika ofisi nyingine huku Chiba na Amata nao wakielekea kwenye ofisi ya watu wa mawasiliano, pale wakamkuta kijana mmoja mtaalamu wa Tehama akifanya hili na lile katika kompyuta zake, huku akirekodi miito yote ya simu inayoingia na sauti za kila kinachofayika hata kama siyo simu. Kwa kuaminiwa kwake, alikuwa ni yeye tu mwenye funguo za kabati ambalo kumbukumbu zile hubakia na eneo ambalo server imehifadhiwa. Walipofika wakaonesha vitambulisho halisi vya kazi na kibali walichopewa kufanya hayo yote.

Chiba akaomba kuona miito ya siku hiyo ambayo Mheshimiwa Rais aliwasili Ikulu, lakini hakutaka kuona au kusikia iliyorekodiwa, ila alihitaji kuchambua kutoka katika kompyuta kile ambacho kiliingia, Yule kijana akisaidiana na Chiba waliweza kufikia codes za miito ya siku hiyo, Chiba akaipakua na kuihifadhi katika chombo chake maalum.
“Hivi miito inayoenda Kilimanjaro Square huwa inajirekodi au la?” Chiba akamwuliza Yule kijana.
“Ndiyo ila imefungwa kwa namba maalum ambazo bila hizo huwezi kuipata, na namba hizo wanazo watu watatu tu, hata mi sina kwani pale ndiyo mambo nyeti ya Mkuu huzungumzwa au hupangwa pale,” Yule kijana akajibu. Chiba akaitazama ile media yake mkononi ambayo alikuwa amechukua zile namba za code.

“Ok, nahitaji kuzipata kama mwana usalama kwa kuwa tupo kwenye uchunguzi wa tukio hilo la uvamizi,” Chiba akaeleza na Amata akatikisa kichwa. Yule kijanaakainua simu na kupiga mahala Fulani na dakika mbili tu aliingia bwana mmoja mwenye kitambi cha wastani, lakini mwili wake ulikuwa mkubwa kiasi na tambo lake lilimruhusu kuitwa giant. Yule kijana akaeleza vyema shida ya Chiba na Amata. Na Yule mtu akawatazama kwa makini sana, Chiba alimtambua mtu huyu mara moja kuwa ni Yule waliyobishana naye sana jana yake.
“Halafu wewe jana si ulikuja hapa? Nilikujibu nini?” akamwambia Chiba, Amata akawa akimwangalia mtu huyo bila usema neno.

“Tekeleza ninalotaka, niko hapa kwa amri ya Rais na siyo wewe, ingiza hizo namba hapo haraka watu tupo kazini,” Chiba akaunguruma na Yule bwana akasonya.
“Sasa hii nyie itawasaidia nini?” akawaambia huku akiingiza zile namba na lile faili ikafunguka, lilikuwa na michoro tu ajabu ajabu, Chiba akaipakua na kuweka kwenye chombo chake kisha akaaga na kuondoka. Amata alimtazama kwa makini sana Yule jamaa, akili yake ikakimbia huku na kule akamweka alama.

KAMBI YA WAASI – MPUMBUTU
JORU ALIFIKISHWA katika hema ya Banginyana, na kumkuta kiongozai huyo akiwa bado analizia mtemba wake alioubana vyema kinywani mwake.
“Huyu naye ni nani?” akuliza huku akiwa ameketi juu ya kiti na miguu yake kaitundika juu ya maeza kama kawaida. Wale askari waasi hawakujibu wakamvua Joru koti la juu la jeshi lao na ndani yake alikuwa na kombati ya jeshi la Tanzania.
“Anhaaaa, ha! Ha! Ha! Naona sasa mnamtafuta nyoka miguu, unajifanya jasusi wewe, tena nakukumbuka hata kule kijijini ni wewe ulikamatwa vivi hivi, leo huponi, mtieni adabu kwanza,” akaamuru. Joru alishikwa huku na huku na kupokea makonde mazito, mateke na mkong’oto wa aina mbalimbali, akawa hoi alipoachiwa akaanguka chini na ile swichi ya kufyatulia mabomu ikamtoa mfukoni mwake na kutu chini. Kanali Bensoir Banginyana akaiona ikiwa pale chini, macho yakamtoka pima.
“Mshenzi wewe! Yaani hii swichi ulitaka kutulipua? Ina maana … asee, mpigeni mpaka afe kisha waambie watu watafute ili bomu mpaka walipate lilipo,” aliposema hayo akaketi akiwa kalowa jasho katka uso wake, akaiweka ile swichi mezani na kuendelea kunyonya mtemba wake.

Joru alijua asipojiokoa basi itakuwa ndiyo mwisho wake kwani wenzake bado walikuwa kimywa huko nje na alishuhudia waasi wakiwa tayari wameanza msako juu ya adui zao kwa minajiri ya kuua kila wanapowakuta. Yule muasi wa mbele alirusha ngumi na Joru akainama ile ngumi ikaufikia uso wa jamaa wa nyuma akamwacha Joru na kuanguka kando. Joru alijitutumua na kuzuia teke kali kutoka kwa mwingine huku akimshuhudia Banginyana akinyanyuka na bastola mkononi, Joru aliruka hewani na kupiaga mateke mfululizo yaliyowatawanya wale jamaa huku risasi za Banginyana zikitoboia hema na kusababisha mtafaruku mkubwa. Joru alipotua moja kwa moja aliikanyaga ile swichi pale juu ya meza na kujirusha sama soti akatoka nje ya hema.
Milipuko mizito ikasikika huko nje, magari yalilipuka yakifuatiwa na mahema ya waasi, kizaazaa. Waasi wengi waliumia vibaya na milipuko hiyo iliyozunguka karibu kambi nzima. Banginyana akatahayari kwa hali hiyo, hata hakujua ni wakati gani aliziama au aliitupa sigara yake kubwa. Walinzi wake wakajiandaa umwondosha eneo hilo.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI

MTUNZI: richard MWAMBE

“Nafikiri tumepata picha na tumejua pa kuanzia, asante Kamanda kwa uwepo wako, yaani Jirak angekuua ningemla nyama…”
“Na nilimwambia kuwa ungeenda kumnasa vibao…” kamanda akamkatisha Madam S kwa maneno yake ya utani.
“Ok, sasa ipo hivi, Gina unajua wajibu wako sijabadilisha, ila Kamanda fanya unaloona linafaa kwa sasa, Scoba utakuwa na mimi kuna kazi maalum leo, naomba tukutane ofisi ndogo kesho saa kumi n ambili jioni, asanteni na kwaherini,” Madam akamaliza kikao hicho na kila mtu akainuka tayari kwa kazi.

SEHEMU YA IX

rejea.... MPUMBUTU

USIKU WA SAA NANE waasi wote walikutana katika uwanja mdogo na kiongozi wao Kanali Bensoir Banginyana alijitokeza kati yao na wote wakaanza kupiga makofi na kuimba nyimbo za kijeshi za kusifia kundi lao na kumtukuza kiongozi wao huku wakimpa sifa za kutosha Mkuu wa Wakuu yaani Rais wa Nduruta.
“Nimewaamsha usiku huu makusudi, nyote mnajua kuwa hapa tulipo tunawindwa na majeshi ya Tanzania yakiwa chini ya mwamvuli wa UN. Hatuyaogopi na nasema tena hatuyaogopi na tutayasambaratisha kama yale mengine yaliyokuja hapa. Sisi ni wanyama wabaya kuliko wanyama wenyewe,” alipotamka hayo wale waasi wakashangilia na kupiga risasi hewani kisha wakanyamaza.

“Nawaambia hivi kwa sababu, juu hapo ya milima majeshi hayo ya adui yamezunguka hivyo sasa ni kwenda kuwasambaratisha, wanajifanya wajanja kumbe sisi ni wajanja zaidi, mafunzo mliyopewa na wale jamaa wa Khazakhistan myatumie vyema, tunatoka sasa kwenda kufagia, kama jana wamezika watano basi wiki iajyo wazike mia tano, na tuna silaha mpya kabisa kutoka Bolivia, na tuzitumie ili zijue kuwa zimeletwa zifanye kazi na si kutembeatembea migongoni na mikononi ka za Wartanzania,” kisha akachukua bastola yake na kupiga hewani mara tatu akiashiri sasa kila mmoja aanze kazi ya kusaka adui.
Juu ya milima ile vikosi vya UN vilitulia kimya kabisa kana kwamba hakukuwa na kiumbe katika msitu huo, walikuwa wakisikia hotuba yotye kupitia chombo cha Joru ambaye alikuwa katikati ya waasi hao nay eye ndiye alikuwa kiongozi wa kuanzisha mashangilio.
Joru katikati ya waasi aliikoki bundui yake kubwa tayari kuungana na waasi hao kulishambulia jeshi lake, mfukoni mwake alikuwa na chombo kidogo ambacho kiliunganisha mabomu yote yaliyotegwa kwenye yale magari, alisubiri amri tu ya kamanda wake ili afanye kazi hiyo kwa sekunde moja.
“Joru, Joru!” sauti ikaita kwenye kifaa chake kidogo alichokipachika sikioni.
“Nakupata kiongozi,” akajibu.
“Toa mkono kwenye sikio haraka, toa!!” Yule kiongozi akamkaripia Joru kwa kuwa alijua kwa kuweka kidole chake sikioni wangemgundua kuwa alikuwa katika mawasiliano na mtu mwingine.

“Unasemaje mkuu sikusikii vyema…”
“Hey, Stop, hapo ulipo simama!” sauti ikatokea nyuma yake, Joru akahisi ganzi kwani waasi wawili walikuwa wakimfuata pale alipo.
“Unaongea na nani?” mmoja akauliza kwa sauti kavu, wakamfikia na kumvua kofia.
“Ha! Bonsoli umeiona hii kofia, huyu ni nyoka, auawe!” mmoja wa wale waasi akmwambia mwenzake mara baada ya kuichukua ile kofi nyekundu lakini alipoigeuza kwa ndani ilikuwa ya buluu bahari na nembo ya majesji ya UN. Joru alipigwa konde zito, akapigwa ngwara akaanguka chini kwenye tope.
“Msaliti mkubwa, peleka kwa Banginyana akamshughulikie,” mwingine akatoa amri, Joru akainuliwa na kupewa kichapo kikali kisha akapelekwa hemani.

HOTELI-NEW AFRIKA DAR ES SALAAM
Usiku uo huo

KUBRA KHALEB aliegesha gari nje ya hoteli hiyo na kuteremka, moja kwa moja aliingia na kupanda lifti mpaka ghorofa ya juu aliyokuwa akiitaka, akaingia na kukutana na mwenyeji wake Bwana Briston Kalangila, ndani ya chumba kilekile namba 806.

“Yes Khaleb, unaonekana leo hauna raha vipi?” akauliza.
“Jaribio limefeli, Kalmat ameuawa,” Khaleb akamwambia Briston.
“What! Hii sasa balaa, Kalmat muuaji hatari aliyeshindikanika kote tulikomtumia, lo!” Briston alisikitika, “Ni nani huyu mshenzi? Nahitaji nikutane nae uso kwa uso nimjue,” akalalam huku kijasho cha kwapa kikimchurizika.
“Mbona nasikia ni mtu wenu wa usalama huko huko?” Khaleb akauliza.
“Hapana, simjui huyo, mimi ninajua watu wote wa usalama nchi hii na nimewaweka wakuu wote wa idara za miko na wilaya, lakini huyu mtu hapana labda kama yuko MI,” akajibu.
“Hapana, hayuko MI, huyu ni TSA,” Kheleb aktoa maelekezo.
“TSA?” Briston akauliza, “Hiyo idara mii siijui hakika,”
“Basi kama ni hivyo bado hujaweka mikononi idara zote, huyu jamaa ni mtu wenu, na ninahitaji kumuua kwa mkono wangu maaha kwa upiganaji huyu atakuwa ni shida, kumbuka Kalmat ni mpiganaji mzuri sana lakini kauawa,” Khaleb akaeleza.

“Ok nimekuelewa, nitapeleleza ili nimjue kisha nitakupa mbinu za kumtia mkononi, hilo niachie mimi tuonane hapa hapa kesho muda kama huu, kama kuna taarifa nyingine tutapeana,” Bristona alimaliza na kujiegeme
Za kwa nguvu kitini mpaka kile kiti kikalia ‘kwinyo’ huku akimshuhudi Khaleb akiondoka zake na kuubamiza mlango. Akainua simu na kupiga ofisi ya mapokezi na kuagiza kile anachotaka kije kwa wakati huo kwa mijiri ya kupunguza mawazo mintarafu kula raha. Dakika tano baadae mwanadada mrembo aliingia katika chumba hicho, na utuli aliokuwa amejifukiza ulikijaza kile chumba.
“Karibu mrembo!” akamkaribisha huku akiinuka kitini na kumwendea pale mlangoni, Yule mwanadada akaondoka na kwenda upande wa pili wa chumba, Briston aye akamfuata hukohuko Yule mwanadada akapanda kitandani na kukaa katikati huku akiachia gauni lake refu liangukie upande mmoja, ukizingatia fundi alisahahu kushona (mpasuo). Bristona naye akapanda na hapo Yule mwanadada akaanza shughuli yake ya kupapasa na kuminya mpaka jamaa likawa hoi kabisa, ndmbendembe.

***
Kubrah Khaleb aliteremka ngazi za hoteli hiyo na kutoka nje kabisa ya jingo hilo aliingia ndani ya gari yake na kuketi nyuma ya usukani, akaiwasha na kuondoka eneo hilo huku akili yake ikiwa inakimbia mara mbili kuliko kawaida. Kichwani mwake alimfikiria huyo adui aliyemuulia swahiba wake kama ndugu yake, alitamani kama aonane naye muda huohuo ili amchakaze ikiwezekana, lakini haikuwa hivyo kwani alichokuwa anakutana nacho ni madaladala tu na watu wenye shughuli zao nyingine kabisa. Akaendelea kuifuata barabara ya Azikiwe mpaka maktaba na kukunja kona kulia na kuifuata barabar ya Bibi Titi, alipofika makutano ya Barabara tatu; ya Bibi Titi, Ohio na Ally Hassan Mwinyi, taa zilimuamuru kusimama, akatii na gari yake ilikuwa ya kwanza kabisa. Kichwa chake kilikuwa kikiwaza mengi hata taa ziliporuhusu hakuwa na habari.

“Piii piiiiih!!! Piiiiii” honi za gari za nyuma zilimshtua Kubra akakanyaga krachi na kuingiza gia namba moja kisha akaachia krachi taratibu na kukandamiza kwa mguu wake ile akselereta mara tu baada ya kushusha breki ya mkono, ile Land Cruiser ikafuata barabara ya Ally Hassan Mwinyi kwa mwendo wa kasi. Kubrah akainua simu yake na kubofya kitufe kimoja tu kisha akaiweka sikioni.
“…naomba tuonane jengoni mara moja na haraka!” akasema hayo tu na kukata simu, akairudisha kwenye kidroo chake na kutoa gia namba tatu na kuweka nyingine. Dakika kumi baadaye alikuwa akikunja kona kulia kuelekea Slip way, nayo ilimchukua mpka amitaa ya Masaki, akakaunja kulia na kupiga honi kwenye moja ya majengo mapya yaliyokuwa yakiendelea kujengwa katika eneo hilo. Mlinzi wa kimasai akafungua na ile gari ikapita moja kwa moja mpka mwisho wa barabara ile, ikaingizwa chini ya jengo hilo na kuegeshwa. Punde si punde gari nyingine nne ziliingia eneo hilohilo na kusimama pembeni yake tu. Vijana wane tofauti wakateremka na kumzunguka Kubrah huku mikono yao ikiwa imeshikamanishwa vifuni mwao.

“Wote mmekuja?” akauliza huku akiwaangalia mmoja baada ya mwingine, “Nisikilizeni kwa makini, mwenzetu, ndugu yetu, kijana wetu, mpigania uhuru mwenzetu, ameuawa kwenye ndege, nataka aliyeua auawe, sina masihara hata kidogo,” akawaambia. Wale jamaa walibaki kimya wakimwangalia tu huku giza la eneo hilo chini ya jingo lisilokwisha ambalo bado liko matengezoni likiwapa shida kidogo kuonana.
“Sasa tutampata wapi huyo mtu na hatumjui?” mmoja aliuliza.
“Dakika chache baadae nitawatumia picha na mahali ambapo huyu jamaa hupenda kuonekana,” akawajibu.
“Kiongozi, na yule Malkia kule amegoma kula kabisa,” mwingine akaeleza.
“What? Anakataa kula? Mwacheni afe kwa njaa kwani si tuna undugu gani naye?”...

***
Ndani ya wigo wa Ikulu, Scoba aliegesha gari yake katika amegesho yake na kuzima injini. Kamanda Amata akateremka akifuatana na Madam S, moja kwa moja wakazipanda ngazi za jingo hilo na kupokelewa na Othman, afisa Usalama wa taifa anayefanya kazi karibu kabisa na Rais, moja kwa moja wakaelekea kwenye chumba ambacho walikuwa wakisubiriwa.

“Yule uliyemwulizia huyu hapa!” Madam akamwambia Rais.
“Kijana kwanza nafurahi umerudi, hapa kuna shida ngumu kutatuka kama ulivyokwisha aambiwa, nataka ufanye kazi tupate ufumbuzi haraka,” akaelezwa.
“Mheshimiwa Rais, tayari niko hatua kadhaa mbele na nakuhakikishia ndani ya saa arobaini na nane First Lady atakuwa hapa bila hata mkwaruzo wa kalamu. Lakini kuna mambo ambayo ningependa kujua kutoka kwako…”
“Sawa, sawa kijana uliza tu nitakujibu yote, ninachotaka mimi ni utatuzi wa jambo hili,” Rais akakubaliana na Amata huku Madam S akitikisa kichwa kuafikia hilo.
“Kwa nini hukwenda na mkeo katika ziara yako? Kwa maana tumezoea kuona hilo kila mara,” Amata akauliza huku kwa siri akiwa kaiwasha zimu yake na ilikuwa ikirekodi kila kitu ijapokuwa ndani ya chumba kile hakukutakiwa kurekodi kitu chochote wala kupiga picha.

“Safari hii yeye alikuwa ana mkutano na vongozi wa asasi ziziso za kiserikali, hivyo nikmwacha,” akajibu.
“Nani aliandaa mkutano huo na lini uliandaliwa?” akazidi kuchimba.
“Aaaaa huu mkutano haukuandaliwa muda mrefu ni kama wiki tatu zilizopita, that is why nikamwacha ili ashughulike na hilo lakini baada ya mkutano ule usiku wake ndiyo hayo yakatokea,” akaeleza huku akianza kusikitika.
Ukimya ukapita kati yao, hakuna aliyeongea kwa nukta kadhaa, kisha Amata akajikohoza tena na kuuvunja ukimya ule.

“Sasa Mheshimiwa, huoni kwamba aliyeandaa mkutano huo alikuwa amekula njama? Kwa nini aandae wiki tatu hizi ilhali ulikuwa na ziara ambayo ilikupasa kuondoka na mkeo?” swali hili lilimgutusha mheshimiwa.
“Unasema!” akatamka kwa mshangao.
Kamanda Amata akarudia sentensi yake ambayo iliiingia sawasawa katika masikio ya wawili hao yaani Mheshimiwa Rais na Madam S. Hali ya Mheshimiwa Rais ilikuwa kama inabadilika na kuonekana akipumua kwa nguvu.
“Hivi hili swalama linawezekana eti?” akauliza.
“Hapana, mi nilikuwa nauliza tu. Lakini mkuu labda kuna kundi unalolihisi katika hi….”

“Enheeee hapo hapo kijana umenikumbusha, nilipigiwa simu na watu nisiowajua, wakinitaka nisichukue hatua yoyote juu ya swala hili, ila nikitaka nimpate tena mke wangu basi niyaamuru majeshi ya Tanzania chini ya UN yarudi nyumbani,” Rais alimkatisha Amata na taarifa hiyo ilimvutia zaidi Amata na akajiweka vyema kitini.
“Unaweza kukumbuka ilipigwa lini?” akauliza.
“Siku ileile niliporudi, ndiyo nilipokea simu hiyo,” akaeleza.
“Na simu ipi kati ya hizi mezani iliyopigwa?” akauliza Amata na Mheshimiwa Rais akaonesha mara moja ni simu ipi siku hiyo ilipigwa, Hii simu imeunganishwa kutoka nje? Akajiuliza Amata, “Naomba fundi wangu aje kuichunguza kama inatoka nje au la, tukishajua hilo tu kazi imekwisha,” akaongeza kusema huku akiinua simu yake na kumpigia Chiba, akamwita afike hapo mara moja. Wakati wakimsubiri waliendelea kuongea ya hapa na pale hasa maendelea ya operesheni ile ya kijeshi inayoendelea huko Ngoko. Haikupita hata dakika kumi na tano Chiba alifikiswah katika ofisi hiyo na Yule afisa wa usalama, Othman.

“Chiba, naomba unitazamie hii simu kama laini yake inatoka nje ya hili jingo au la, hilo tu” Amata akamwambia Chiba naye mara moja akaanza kuifuatilia ile laini kuanzi pale na baada ya dakika tano alirudi na jibu kuwa laini ile ya simu ipo kwenye mfumo wa simu za ndani ‘Internal Telephone System’ ambayo simu zake upigwa toka ofisi moja kwenda nyingine ndani ya jingo moja na sin je ya hapo ingawaje unaweza kupiga au kupokea kutoka nje endapo una namba maalum ya kufanya hivyo. Kwa hiyo ina maana simu hii ilipigwa kutoka humuhumu ndani au? Amata alijiuliza.
“Chiba! Ina maana katika mfumo huu haiwezekani simu kutoka nje ikaingia?” aliuliza swalinhilo Amata baada ya Mheshimiwa Rais kuwaelekeza simu zote zilizokuwa mezani kuwa ipi anapokelea simu za mtindo gani.

“Inawezekana kwa sababu huu mfumo uziunganisha simu zote za ndani katika swichi moja inayoitwa PBX. Sasa kama unataka kupiga simu nje ya jingo hili kwa kutumia simu hii kuna namba maalumu unayoitanguliza kisha unapiga namba uitakayo na signal ile itafika kwenye swichi ya PBX kisha hiyo swichi itaitambua kuwa hiyo simu inatakiwa kutoka nje hivyo itakuunganisha na kitu kinaitwa PSTN yaani Public Switched Telephone Network nayo itafanya kazi ya kukuunganisha na unayemtaka, lakini si kila mtu anajua namba za utangulizi yaani jinsi ya kupiga kwenda nje, kwa sababu hii siri hukaa na System Administrator na wachache wanaoaminika kwa kazi maalum,” Chiba akadadavua na kuwaacha hao watatu vinywa wazi huku Mheshimiwa Rais akiwa haamini kila anachosikia.
“Kijana, unataka kuniambia kuwa hiyo simu itakuwa imepigwa kutoka humu ndani?” Rais akauliza kwa shauku.
“Siyo hivyo Mheshimiwa, simu inaweza kupigwa kutoka nje ya jingo hata Amerika na ikaingia katika mfumo huu, ina maana mtu atakuwa anajua anyempigia ni nani,” akamalizia huku akifunga kijimkoba chake. Kwa mara ya kwanza tangu wafike hapo Madam S alifungua kinywa chake.

“Chiba, nataka rekodi ya simu zote za siku ile aliporudi Mheshimiwa zilizopigwa kwenye namba hii, hii ni 603,” akamwambia.
“Sawa hakuna tabu nina uhakika itapatikana tu japo si kazi rahisi sana,” Chiba alieleza na kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana, wakaagana na Mheshimiwa ili wao waendelee na kazi nyingine. Wakatoka wote watatu kayika ofisi ile nyeti, Madam S akaingia katika ofisi nyingine huku Chiba na Amata nao wakielekea kwenye ofisi ya watu wa mawasiliano, pale wakamkuta kijana mmoja mtaalamu wa Tehama akifanya hili na lile katika kompyuta zake, huku akirekodi miito yote ya simu inayoingia na sauti za kila kinachofayika hata kama siyo simu. Kwa kuaminiwa kwake, alikuwa ni yeye tu mwenye funguo za kabati ambalo kumbukumbu zile hubakia na eneo ambalo server imehifadhiwa. Walipofika wakaonesha vitambulisho halisi vya kazi na kibali walichopewa kufanya hayo yote.

Chiba akaomba kuona miito ya siku hiyo ambayo Mheshimiwa Rais aliwasili Ikulu, lakini hakutaka kuona au kusikia iliyorekodiwa, ila alihitaji kuchambua kutoka katika kompyuta kile ambacho kiliingia, Yule kijana akisaidiana na Chiba waliweza kufikia codes za miito ya siku hiyo, Chiba akaipakua na kuihifadhi katika chombo chake maalum.
“Hivi miito inayoenda Kilimanjaro Square huwa inajirekodi au la?” Chiba akamwuliza Yule kijana.
“Ndiyo ila imefungwa kwa namba maalum ambazo bila hizo huwezi kuipata, na namba hizo wanazo watu watatu tu, hata mi sina kwani pale ndiyo mambo nyeti ya Mkuu huzungumzwa au hupangwa pale,” Yule kijana akajibu. Chiba akaitazama ile media yake mkononi ambayo alikuwa amechukua zile namba za code.

“Ok, nahitaji kuzipata kama mwana usalama kwa kuwa tupo kwenye uchunguzi wa tukio hilo la uvamizi,” Chiba akaeleza na Amata akatikisa kichwa. Yule kijanaakainua simu na kupiga mahala Fulani na dakika mbili tu aliingia bwana mmoja mwenye kitambi cha wastani, lakini mwili wake ulikuwa mkubwa kiasi na tambo lake lilimruhusu kuitwa giant. Yule kijana akaeleza vyema shida ya Chiba na Amata. Na Yule mtu akawatazama kwa makini sana, Chiba alimtambua mtu huyu mara moja kuwa ni Yule waliyobishana naye sana jana yake.
“Halafu wewe jana si ulikuja hapa? Nilikujibu nini?” akamwambia Chiba, Amata akawa akimwangalia mtu huyo bila usema neno.

“Tekeleza ninalotaka, niko hapa kwa amri ya Rais na siyo wewe, ingiza hizo namba hapo haraka watu tupo kazini,” Chiba akaunguruma na Yule bwana akasonya.
“Sasa hii nyie itawasaidia nini?” akawaambia huku akiingiza zile namba na lile faili ikafunguka, lilikuwa na michoro tu ajabu ajabu, Chiba akaipakua na kuweka kwenye chombo chake kisha akaaga na kuondoka. Amata alimtazama kwa makini sana Yule jamaa, akili yake ikakimbia huku na kule akamweka alama.

KAMBI YA WAASI – MPUMBUTU
JORU ALIFIKISHWA katika hema ya Banginyana, na kumkuta kiongozai huyo akiwa bado analizia mtemba wake alioubana vyema kinywani mwake.
“Huyu naye ni nani?” akuliza huku akiwa ameketi juu ya kiti na miguu yake kaitundika juu ya maeza kama kawaida. Wale askari waasi hawakujibu wakamvua Joru koti la juu la jeshi lao na ndani yake alikuwa na kombati ya jeshi la Tanzania.
“Anhaaaa, ha! Ha! Ha! Naona sasa mnamtafuta nyoka miguu, unajifanya jasusi wewe, tena nakukumbuka hata kule kijijini ni wewe ulikamatwa vivi hivi, leo huponi, mtieni adabu kwanza,” akaamuru. Joru alishikwa huku na huku na kupokea makonde mazito, mateke na mkong’oto wa aina mbalimbali, akawa hoi alipoachiwa akaanguka chini na ile swichi ya kufyatulia mabomu ikamtoa mfukoni mwake na kutu chini. Kanali Bensoir Banginyana akaiona ikiwa pale chini, macho yakamtoka pima.
“Mshenzi wewe! Yaani hii swichi ulitaka kutulipua? Ina maana … asee, mpigeni mpaka afe kisha waambie watu watafute ili bomu mpaka walipate lilipo,” aliposema hayo akaketi akiwa kalowa jasho katka uso wake, akaiweka ile swichi mezani na kuendelea kunyonya mtemba wake.

Joru alijua asipojiokoa basi itakuwa ndiyo mwisho wake kwani wenzake bado walikuwa kimywa huko nje na alishuhudia waasi wakiwa tayari wameanza msako juu ya adui zao kwa minajiri ya kuua kila wanapowakuta. Yule muasi wa mbele alirusha ngumi na Joru akainama ile ngumi ikaufikia uso wa jamaa wa nyuma akamwacha Joru na kuanguka kando. Joru alijitutumua na kuzuia teke kali kutoka kwa mwingine huku akimshuhudia Banginyana akinyanyuka na bastola mkononi, Joru aliruka hewani na kupiaga mateke mfululizo yaliyowatawanya wale jamaa huku risasi za Banginyana zikitoboia hema na kusababisha mtafaruku mkubwa. Joru alipotua moja kwa moja aliikanyaga ile swichi pale juu ya meza na kujirusha sama soti akatoka nje ya hema.
Milipuko mizito ikasikika huko nje, magari yalilipuka yakifuatiwa na mahema ya waasi, kizaazaa. Waasi wengi waliumia vibaya na milipuko hiyo iliyozunguka karibu kambi nzima. Banginyana akatahayari kwa hali hiyo, hata hakujua ni wakati gani aliziama au aliitupa sigara yake kubwa. Walinzi wake wakajiandaa umwondosha eneo hilo.

ITAENDELEA

Nzuri sana mkuu. Mi msoma novel maarufu. Za kina David Baldacci and Tom Clancy to mention them but a few. You are good.
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI

MTUNZI: richard MWAMBE

Milipuko mizito ikasikika huko nje, magari yalilipuka yakifuatiwa na mahema ya waasi, kizaazaa. Waasi wengi waliumia vibaya na milipuko hiyo iliyozunguka karibu kambi nzima. Banginyana akatahayari kwa hali hiyo, hata hakujua ni wakati gani aliziama au aliitupa sigara yake kubwa. Walinzi wake wakajiandaa umwondosha eneo hilo.
***
SEHEMU YA X
Kiongozi wa vikosi vya UN alipohesabu milipuko akajua tayari imemalizika akawaamuru vijana wake wateremke chini sasa ni vita ya ana kwa ana. Kambi ya waasi ilidhibitiwa kwa kipigo kikali kutoka katika kila kona, hawakupata mahala pa kutokea, maana kama ni vyombo vya usafiri vilikwishalipuliwa tayari. Moto ulizagaa huku na huko, askari wa Tanzania chini ya UN walifanya yao na kulidhibiti eneo lote kabisa kila mahala walikuwa wao huku wakiwa wamewakamata mateka kadhaa lakini Banginyana hakupatikana. Hii ilimtia hasira sana kiongozi wa vikosi vya UN.

“Ningemtia mkononi, leo tungepambana ngumi kwa ngumi,” akasema huku akiwa haamini kama kiongozi huyo wa waasi ametoroka tena kwa mara ya pili. Vijana wa JW walitanda kila kona, wakiwa wamekalia kila mahala, sasa eneo hilo lilikuwa lao. Zaidi ya kupata maumizu madogomadogo hakuna aliyepoteza maisha. Joru alijikokota na kujiweka sawa kutoka nkwenye nyasi alizokuwa ameangukia, wakati wa mapambano alijua akisimama tu angekufa hivyo alitulia kimya kama mmoja wa wafu. Akainua mikono na kusimama wima. Askari wa UN walipomwona walimwinulia bunduki zao, na kiongozi wao akawaamuru kushusha.
“Huyo ni Joru,” akawaambia. Joru akasalimiana na kamanda wa kikosi na kuonesha wazi kusikitishwa kwake juuu ya kumkosa Banginyana.
“Wamekimbilia njia hii huku bondeni, kule kuna mto mkubwa sana wa maji,” Joru akaeleza na baadhi ya askari wakateremka huko kumsaka Banginyana kwa udi na uvumba. Walipita mapori na mapori lakini hawakumuona Banginyana wala kivuli chake, baada ya mwendo mrefu walisimama, katikati yam situ uliozungukwa na miti na ndege waliokuwa wakiimba nyimbo wazijuazo wao tu.
“Huyu jamaa keishatutoka tena,” mmoja wao akasema huku akiiweka vizuri bunduki yake.

“Ana bahati sana dhidi ya mkono wetu,” mwingine akadakia kisha akawaamuru wenzake kurudi. Joru alibaki kasimama nyuma wakati wenzake wakiondoka wakati wa giza nene.
“Joru twende, achana na huyo Mungu wake anampenda lakini ipo siku,” mwanajeshi mmoja akamwambia Joru naye akageuka na kuondoka mpaka kule walikowaacha wenzake.
Giza lilikuwa likiendelea kufika mwisho wakati vikosi vya JW chini ya UN vikiwa tayari vimekalia eneo lile la waasi huku baadhi yao wakiwa chini ya ulinzi, mateka na wengine wengi zaidi wakiwa tayari hawana uhai. Taarifa ya kumkosa Banginyana ilimsikitisha sana kamanda wa vikosi hivyo ambaye alimpania kwelikweli mtu huyo, alikubali tu afanyeje lakini bado moyo wake haukukata tamaa. Aliwatazama vijana wake waliokuwa tayari wamekaa kwenye kona mbalimbali za eneo lile kuanzi kwenye hema za waasi mpaka kwenye machimbo ya almasi ya Mpumbutu.

“Mnajua …” akawaambia kiongozi wa kikosi, “Banginyana hajakwenda mbali na tukimuwahi tutampata, nina uhakika atakuwa amekimbilia kule kijijini. Joru nakupa ukamanda, chukua vijana kumi na nane mnatosha kwa kazi kahakikisheni kile kijiji nacho kipo katika mikono yetu na si sjsbu huyo Banginyana atakuwa pale…”
“Tukimkuta…” Joru akamkatiza.
“Mnajua cha kufanya, nendeni,” akawaamuru. Joru akachukua vijana kumi na nane pamoja naye wote wakiwa na silaha nzito na kupotelea msituni usiku huo. Kijiji cha Mpumbutu hakikuwa mbali kutoka eneo hilo kama ukipanda na kushuka milima kadhaa ambayo ilivitenganisha kijiji na eneo hilo la machimbo. Mwendo wa saa moja tu ungeweza kuwafikisha kama wasingeizunguka milima hiyo. Kwa ari waliyokuwa nayo hiyo viijana hao walitiana moyo na kutembea kijeshi kufika katika kijiji hicho.

KIJIJI CHA MPUMBUTU
Kikosi kiliingia kijijini saa kumi na moja alfajiri, hali ya kijiji ilikuwa hai hai maana watu walikuwa nje wa,ekusanyana vikundi vikundi hasa baada ya kuona yale mashambulizi ya kule msituni. Akina mama walikusanya watoto wao na kujificha ilhali akina baba walionekana nje wakiweka ulinzi juu ya familia zao. Joru aliwapa ishara wenzake watawanyike kuzunguka eneo hilo, kisha wakateremka kijijini kila mmoja kupitia upande wake. Joru alikuwa wa kwanza kuingia kijijini, wale wanaume waliosimama vikundi walipoona wanajeshi wa UN wameingia pale walitoa ushirikiano kuonesha kila kona ambako waasi mabaki walijificha.
“Kajengo kaleeeee, wapo mle, inawezekana kabisa hata huyo mkubwa wao yupo pale, hawezi kuondoka usiku huu…” mmoja wa wazee alikuwa akimweleza Joru. Joru alilitazama lile jingo, lilikuwa jingo la kawaida ambalo nje yake lilizungukwa na ukuta, pembeni kama mita mia moja hivi kulikuwa na lile jingo waliloliangusha kwa uvamizi wiki moja iliyopita. Joru akawaita vijana wake na kuwapanga tayari kwa uvamizi, kisha akawaomba wale wanakijiji waendde mbali na eneo hilo kwani hawakujua uzito wa mapigano yatakayotokea. Wale wanakijiji wakafanya hivyo na dakika kama kumi na tano hivi utulivu ulichukua nafasi.

Baada ya vijana kujipanga tayari kwa kazi, kiongozi aliyepewa jukumu la operesheni hiyo ndogo akatoa amri ya kuvunjwa nyumba hiyo bila huruma. Mmoja wa vijana aliyekuwa kabeba RPG muda mrefu akaliweka begani sasa tayari kwa kazi. Dole lake la shahada likavuta kifyatulio kwa nyuma na grenade lililochomekwa mbele ya bunduki hilo likafyatuka. Nalo bila kukosea lilitua kwenye ukuta na kuuangusha kipande cha ukuta huo. Askari waliobaki nje tayari na bunduki zao kubwa mikononi waliingia ndani ya wigo ule. Nusu saa ya mabishano ya risasi yalitosha kuwazimishwa waasi wale. Joru alihakikisha usalama wa vijana wake waliokuwa na hasira juu ya visasi vya ndugu zao. Waasi nao japokuwa walikuwa wachache lakini walijua vyema mbinu za mapigano kwani mtafutano haukuwa mdogo. Mapigano yalikuwa ni ya kuviziana ilipooneakana muda unazidi kuyoyoma, Joru aliamuru grenade nyingine ipigwe, ikapigwa na kuangusha kipande kingine, ikapigwa nyingine na kuangusha tena sehemu kubwa ya ya ukuta wake.

“Aaaaaiiighh!” kelele ya Yule jamaa mwenye ile RPG ilisikika, Joru alipogeuka alikuta jamaa katupa ile mashine kajishika goti lake, risasi ilikuwa imevunja mfu[pa wa goti na jamaa alikuwa chini. Mwanajeshi mmoja aliyekuwa na taaluma ya uuguzi aliwahi eneo lile na wakati huohuo askari wawili wakawawekea ulinzi, Joru na waliobaki wakaivamia ile nyumba na kutembeza kipigo kisicho na huruma na kufanikiwa kuwadhibiti waasi wale. Dakika sitini za uongozi wa Joru zilisambaratisha eneo lile lakini Banginyana hakuwapo, baada ya kuwabana na kuwatesa wale waasi wakasema kuwa Kanali huyo alikwishatoroka. Wanakijiji walijitokeza na kushangilia hali hiyo maana waliona sasa wamekomboka kutoka katika mikono ya X65. Vijana wale wa jeshi wakakikalia kijiji kile na wengine zaidi wakaongezeka.
***
Taarifa ya habari kutoka BBC saa kumi na mbili asubuhi ilimkuta Kamanda Amata akiwa bado kitandani. Saa yake ilipomgutusha kumwonesha ni saa kumi na mbili, akachukua rimoti na kuwasha redio kubwa iliyo chumbani mwake.

“…Majeshi ya ukombozi ya Umoja wa Mataifa huko Mpumbutu Kusini mwa nchi ya Ngoko yameisambaratisha ngome ya waasi na kuyakalia maeneo yake, taarifa zinasema kuwa, majeshi hayo yalivamia mahali palipo na machimbo ya almasi usiku wa kuamkia leo na kusambaratisha waasi wote huku wakiteka eneo hilo na kijiji cha Mpumbutu. Wakazi wa eneo hilo wamefurahia zoezi hilo na wamelisifu jeshi hilo kwa hatua waliyoifikia, mwandishi wetu anaripoti….

…..ulikuwa usiku wa manane vikosi vya UN vilipoteremka katika kambi hiyo ya waasi na kuisambaratisha vibaya. Msemaji wa jeshi hilo Luteni Chongo Chongoli amethibitisha juu ya shambulizi hilo na kukiri kuwa kiongozi wa waasi hao Kanali Banginyana hajapatikana, lakini msako unaendelea…..”

Baada ya kumaliza kuripoti habari hiyo zilisikika sauti za wakazi wa Mpumbutu wakishangilia na kulisifu jeshi hilo kwa kuwakomboa dhidi ya X65.
“….Hii mutu hii imetutesa sana, imechukua batoto yetu na kupelekwa kwa jeshi…”
“….ilikuwa inbaka mabinti na wanamuke yetu, tunashukuru UN kwa kukomboa kipande hii…”
“…mengine yalijificha kwa fasi hii na sasa yote imekufa, ilikuwa kumi mbili na tatu…”
Kamanda Amata alisikiliza taarifa ile kwa makini sana, akamtumia ujumbe Madam S kisha akainuka kutoka kitandani na kuwasha televisheni channeli ya Al-Jazeera ambapo aliikuta habari ileile kwa picha.
Banginyana ametoroka tena? Akajiuliza na kutikisa kichwa kisha akasonya kwa hasira na kuingia maliwato kwa minajiri ya kujiandaa kwa kwenda kulijenga taifa.

NDURUTA

KANALI BENSOIR Banginyana aliketi kwa kujiinamia huku wasaidizi wake wawili wakiwa upande huu na upande ule. Dakika hiyohiyo Rais wa Nduruta Mheshimiwa Sebutunva aliingia katika chumba hicho na kuketi kwenye kiti cha mbele yake. Banginyana alisimama na kutoa saluti kisha akaketi tena.
“Nimesikitika sana,” akaanza kusema, “Imekuwaje Banginayana, mimi nakuamini wewe mpiganaji, umefanya mapinduzi hapa hakuna asiyejua weledi wako wa kivita au umezeeka?” akauliza.
“Mkuu wa Wakuu, mbinu waliyotumia wale jamaa kutuvamia hakika imeniacha kinywa wazi, maana tumekuja kushtuka tayari adui yuko ngomeni, na we unajua jeshini tunasema ‘adui mbaya ni yule aliye miongoni mwako’ hatukuwa na ujanja walituwahi kwa pigo moja tu…”
“Unasema?” akadakiza swali.

“Wametupiga kwa pigo moja tu, wamelipua magari na mashine zetu zote za kivita kwa sekunde moja tu, wakati natoa amri ya kuanza kuwasaka ni dakika na sekunde hiyohiyo wakafanya hilo,” banginyana akaeleza.
“Kwanza wamekiuka maagizo tuliyokubaliana ya UN kuwa hawakutakiwa kuwashambuli bali walitakiwa kulinda amani, na hili lazima nilifikishe kwenye baraza la usalama. Hawa Tanzania ni nani hasa, sasa watanikoma…” alisema huku akiuma meno. Wameua wapiganaji wangu! Nitaua wa kwake, akawaza na kuondoka kwenye kile chumba. Siku hiyo ilikuwa siku ngumu sana kwa Sebutunva, moyoni mwake aliona jinsi gani itamuwia ngumu kutimiza azma yake ya kukamata na kukalia nchi fulanifulani kwa nguvu. Aliwaza wapi sasa ataendelea kupata pesa za kuendesha mambo yake na kuweza kuwatawala wenzake kama alivyokuwa akifanya mwanzo. Kichwa kiliuma.
Sasa hapa, lazima nibadilishe katiba, niongeze muda wa kukaa tena madarakani ili nifikie lengo langu, akapitisha uamuzi na kuondoka zake.
Baada ya kikao hicho Banginyana aliondoka na kuelekea kusikojulikana huku wale vijana wasaidizi wakirudishwa jeshini kuendelea na majukumu mengine...

7

MBELE YA JENGO la Wizara ya Elimu, Kamanda Amata aliegesha gari yake na kuteremka huku akifuatiwa na Chiba na Gina.
“Hapa sasa ndipo tutapata jibu kamili juu ya huo uvamizi wa Ikulu,” Kamanda akawaambia wakati wakianza kupanda ngazi kwenda ghorofa ya juu kabisa.
“Kivipi Amata?” Chiba akauliza.
“Unajua hatukuwa na muda wa kutosha pamoja nanyi lakini kuna maeneo ambayo tuliyatazama kwa jicho la pekee, mtaona,” akawaambia na wakati huo tayari wakawa juu, ghorofa ya tano, kati ya milango mingi kulikuwa na mlango mmoja ambao kwa muonekano ulikuwa haufunguliwi kabisa.
“Du!” Gina akapiga kite kwa vumbi lililokuwa katika mlango huo ambao kabla ya kuufikia kulikuwa na maboksi kadhaa yaliyojaa makabrasha na mafaili mbalimbali. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na meza moja ndogo na kiti huku mezani hapo kukiwa na kompyuta ya kizamani, karibu na dirisha hilo ambalo ukisimama kulikuwa na mashine kubwa la kupoza hewa, ukiangalia dirisha lile moja kwa moja utaona lango kuu la Ikulu na ile barabara inayoongoza mpaka mbele ya jengo lile.

“Washa airconditioner!” Gina akamwambia Amata.
“Acha ushamba, hii siyo airconditioner,” akajibu na kuiendea ile kompyuta, “Chiba washa kompyuta hiyo, utakuta picha za tarehe hiyo tuangalie nini kilijiri,” Amata akamwambia Chiba. Vumbi lilitimka juu ya kiti kile baada ya Gina kukipiga kwa kitambaa. Chiba akaketi na kuiwasha kompyuta hiyo ya IBM, nayo ilipomaliza kuwaka ikadai nywila.
“Oya, nywila hapa!” Chiba akamwambia Amata.
“Ulichokalia na unachokitazama,” Amata akajibu huku akicheka, Chiba akaelewa na kuingiza, alipobofya kitufe cha Enter, ile kompyuta ikakaa kama sekunde kumi kisha ikawaka, moja kwa moja wakafungua app inayobeba kamera hiyo. Wote watatu walikusanyika nyuma ya chombo hicho na kuangalia kile ambacho kilitukia siku hiyo.

KILICHOJIRI…

Watu kumi waliovalia mavazi meusi, wakiwa wamekamilika kwa silaha nzito, walikuwa wamejioanga katika chombo kidogo mfano wa boti, kilichofungwa juu na chini. Chombo hicho kilichiokuwa kikisafiri chini ya maji kilisogea karibu kabisa na eneo lililotakiwa.

“Hapo hapo, kila mmoja awe tayari,” mmoja wao alitoa maelekezo. Wale watu wakachukua vidubwasha vidogo mfano wa mbilimbi na kuvipachika vinywani mwao, vidubwasha vile viliweza kuwapa hewa ya oksijeni kwa dakika tano. Kisha Yule nahodha akafungua mlango wa chini ya hiyo nyambizi yao nao wakatokea huko . dakika mbili ziliwatosha kuibuki katika bomba la maji taka lililokuwa likielekea kule wanakokutaka, wa kwanza kabisa akapanda juu ya loile bomba na wapili na wa tatu kisha wote wakawa juu ya lile bomba na kuanza kutambaa kama nyoka wakiwa katika mstari mmoja. Walipokaribia ufukweni, Yule aliyetangulia akawapa ishara wenzake watulie, kisha yeye akatoka pale alipo kwa kasi na moja kwa moja alidanda juu ya ukuta wa jingo lile na kutulia katika vyuma vilivyotengeneza maua mazuri kabisa. Juu ya ule ukuta kulikuwa na kamera ya CCTV, akapachika kidole chake kwa chini na kupachua kifuniko kidogo, ndani yake kulikuwa na kadi, akaibonya nayo ikachomoka, akachukua yak wake iliyokuwa kwenye kijifuko cha plastiki akaipachika na kisha akarudisha kile kifuniko. Mfukoni mwake akatoa kitu kama simu, akachukua waya mdogo na kuupachika kwenye moja ya matundu ya simu hiyo, na waya ule akaupachika pale kwenye kamera na kitazama nini kinaonekana, aliporidhika akaurudishia ule uliokuwapo, kisha akawapa ishara wale wenzake wakati yeye katulia palepale.

Mtu wa pili akachomoka na kuufikia ule ukuta, hakupanda, akainama pale chini kama mtu anayetafuta kitufulani, my wa wa tatu akafika na kuukanyaga mgongo wa Yule wa kwanza kisha akatulia juu huku mguu wake ukining’inia, wan ne alipokuja alikanyaga mgongo wa Yule wa kwanza, akaudaka mguu wa Yule wa pili kisha aruka na kutua ndani, alipofika tu mbele yake aliona askari wawili, akainua bunduki yake iliyofungwa kifaa cha kuzuia sauti na kuwaangusha kwa risasi moja moja kila mmoja, kimya kimya waliwainua na kuwaweka mahala kisha wao wakatawanyika na wale wa mwisho wakapitiliza na kuufikia mlango mkubwa. Yule aliyekuwa na kazi ya kuilaghai ile kamera akafika na kuingiza tarakimu fungushi na kuufungua mlango huo, wote wakiwa na shotgun mikononi mwao, waliingia ndani ya jingo hilo. Taa kubwa iliyofungwa katika ukumbi wa kwanza katika jingo hilo ikwaka na kuwamulika watu hao, taa hii ilikuwa imeunganishwa na chanzo mbadala na zile nyingine, mmoja wa wale magaidi akailipua kwa bastola yake na wakati huohuo wana-usalama ndani ya jingo hilo walianza kutoka kwenye kona zao mbalimbali na kufanya kazi yao. Ilikuwa kizaazaa kila kona, risasi zililindima huku na kule, wale magaidi walikuwa wamevaa nguo zisizopitisha risasi tofauti na wanausalama wa Ikulu ambao walivaa nguo zao za kawaida. Kutokana na silaha nzito walizokuwa nazo wale jamaa walifanikiwa kuwadhibiti wana usalama ambao walikuwa na silaha ndogondogo. Mapigano hayo yalikuwa magumu sana kwa watu wa usalama kutokana na giza lililotanda ndani ya jingo hilo.

Ndani ya nyumba maalumu ambayo imejengwa ndani ya Ikulu, nyumba hii ambayo huishi Mheshimiwa Rais na familia yake, wanausalama walikuwa mbioni kuufungua mlango ili kumnusuru mke wa Rais, wanausalama hao wa kike walikuwa wakisaidiwa na wanaume waliokuwa na funguo bandia katika kufanya hilo. Lakini kabla hawajafanikiwa walifikiwa na wale magaidi wakamimina risasi za kutosha na kuwaua wale wanausalama pale mlangoni kisha wakafungua mlango na kuvamia ndani ya ile nyumba, walitanda huku na huku na kukifikia chumba cha kulala ambako walimchukua mke wa Rais na kutoka nae huku wakiwa wamefunga gundi kinywani hasipige kelele.
Walipotoka nje ya nyumba hiyo walipewa maelelekezo wapi pa kutokea, mmoja wa wanausalama aliyekuwa sakafuni akivujwa damu, alikuwa akishuhudia yote hayo, alimwona mmoja wa watu wao aliyemjua kwa sura akiwaonesha njia wale wavamizi. Akakohoa ili aseme neno yule msaliti akageuka na kugundua kuwa mtu huyo hajafa, wakagongana macho.

“Ni we-we! Aaaaaaiiiiigggghhh…!” kabla hajamaliza kusema risasi moja ikamfumua kichwas naye akanyamaza kimya. Wale magaidi wakaongozwa na kuteremka chini ambko walikuta kitu kama mlango wa chuma, kufuli lake lilikuwa limeliwa na kutu, mmoja wao akalipiga risasi likafyatuka wakaingia ndani ya kitu kama bomba kubwa ambalo liliwezesha wao kupita bila taabu. Na walipofika mwisho wake wakakuta kuna maji, kila mmoja akapachika kifaa maalum cha hewa ya oxygen kinywani mwake na kingine wakamvalisha mateka wao, wakaingia majini na kuibukia baharini, huko walipiga mbizi mpaka chini ambako walikiacha kile chombo kikiwasubiri, wakaingia kupitia mlango wa siri kisha nahodha akaondoa maji chomboni na kukiondoa eneo lile.
***

rejea... CHUMBA CHA SIRI….

“Uhhhhhh!” Chiba alivuta pumzi ndefu na kuishusha, “Sasa hawa jamaa walitokea wapi? Maana hapa mlangoni sijawaona,” akauliza.
“Kwa vyovyote hawakutokea mlangoni, kuna njia nyingine ya siri ndani ya lile jingo, ziko njia tatu tofauti, sasa hawa lazima wametumia moja wapo, na kwa kuwa walikuja kutokea baharini basi wamerudi kutpiti baharini lakini kwa njia ya siri,” kamanda akawaeleza. Gina alibaki kimya kabisa bila kuongea lolote.
“Mnajua huu uvamizi inabidi tuufanyie uchunguzi wa hali ya juu sana, hebu tuonane na Madam mara moja,” Kamanda akaeleza na Chiba wakati huohuo akampigia simu Madam S nao wakamsubiri pale ndani.
Dakika tano tu zilimchukua kuwasilia katika jingo lile kwani halikuwa mbali na Ofisi Ndogo. Alipowasili walimwonesha zile picha walizokuwa wakitazama zilipkwisha nae akawatazama vijana wake.
Kamanda Amata akasogea kutoka aliposimamawakati huo na kusimama mahala pengine.

“Enhe, nipeni mpango,” Madam S alianzisha mazungumzo. Wote wakamwamngalia Amata aliyekuwa akichungulia dirishani, kisha akageuka na kuwatazama baada ya kauli ile ya Madam.
“Nahitaji turudie uchunguzi au tuone pia tafutishi za uchunguzi wa awali, hii ishu Madam ni ngumu hata ile ya ‘Olympus Has Fallen’ ilikuwa nyepesi,” akasema.
“Maswali gani?” Madam akatupa swali.
“Yeah, najua kabisa kuwa pale Ikulu kuna chumba cha kuhifadhi silaha, tena silaha za kivita, lakini sijaona kama zilitumika, sasa je ina maana wanausalama wa Ikulu hawajui silaha ziko wapi, au mwenye gunguo alikufa au ilikuwaje?” Amatab aliuliza.

“Kwa maelezo ya Othman, mtunza silaha alikutwa amekufa pale aple kwenye mlango wa chemba hiyo nyeti na hakuna silaha iliyochukuliwa,” akawaambia. Amata akatikisa kichwa kuonesha kuwa ameelewa kitu.
“Madam S, kama ni adui aliyemuua huyo bwana basi angechukua silaha, lakini kama hakuna silaha iliyochukuliwa basi huyo mtunza silaha aliyekuwa zamu kauawa na mtu wetu wenyewe, hii ni hujuma!” Amata akaongeza shaka. Kila mmoja akatikisa kichwa kuonesha kimeeleweka kitu.
“Lakini unaonaje tukikutana na watu waliofanya uchunguzi tunaweza kung’amua mambo zaidi hapa,” Gina alifunguka.
“Inspekta Simbeye alikuwapo katika lile jopo,” Chiba akaeleza.

***
Baada ya kumaliza uchunguzi wao pale chumba cha siri sasa walikutana na Inspekata Simbeye, mzee huyu aliyechoka na majukumu aliweka miwani yake vizuri na kumtazama Amata na Gina waliokuwa wameketi mbele yake.
“Yaani tatizo lako wewe Amata, ukiwa unakunywa pombe zako hunitafuti ila ukiwa na shida inayokutatiza ndiyo unanitafuta, utakua lini wewe?” Simbeye akamuuliza kwa utani.

“We mzee ukinywa bia utazirai endelea kugonga Chibuku tu!” kwa jibu hilo wote wakaangua kicheko.
“Ok tuyaache sema…” Simbeye akawaambia huku akijivuta kwa mbele na kuiegemea meza yake.
“Mzee, najua ulikuwapo katika jopo la uchucnguzi wa tukio lililotukia pale Ikulu wiki ileee…”
“Ndiyo!” akajibu.
“Sasa nina wasiwasi kuwa kati ya watu wetu waliouawa, watakuwa wameuawa na wasaliti, yaani ndani kwa ndani…”
“Kwa nini.mbona sisi hatuliona hilo?” Simbeye akauliza.
“Fikiria, mtunza silaha aliuawa sivyo?” Kamanda akauliza.
“Ndiyo, tena palepale kwenye chemba ya silaha,” akajibu Inspekta.
“Aliuawa kwa mikono au kwa risasi?” Gina akauliza.
“Risasi,” Simbeye akajibu. Amata akatikisa kichwa.
“Mlikusanya maganda yote ya risasi?” Amata akauliza.
“Tena yote hatukubakisha hata moja, wale jamaa walitumia risasi themanini na moja kufanya shambulizi lile,” Simbeye akajibu.

“Naweza kuona maganda yake au mmeshayatupa…”
“Huwa situpi vitu kama hivyo Amata, wao walishatupa lakini mimi nimeyachukua na kuyahifadhi,” akavuta droo na kiuwapatia ule mfuko wenye maganda ya risasi, hakika yalikuwa maganda themanini na moja.
“Simbeye… sasa jibu hili hapa!” Amata akasema na wote wakakodoa macho. Maganda haya sabini na tisa ni Heavy Shotgun, mtoto wa AK-47, ina maana hawa magaidi walitumia silaha hii haribifu kabisa kwa uvamizi huu, na nina wasiwasi sasa haya maganda mawili ambayo si yah ii silaha si ya hawa magaidi. Moja umesema mmelipata kwa huyo kijana mtunza stoo ya silaha, na la pili je?” Amata akaeleza na kisha akahoji.
“La pili; mlangoni mwa nyumba ya Mheshimiwa,” Simbeye akajibu.

“Inspekta Simbeye, kwa uzoefu wako wa kipolisi na ukachero unakubali kuwa risasi hizi zote ni za hao magaidi? Sabini na tisa zinafanana na mbili tu hazifanani, maana hizi mbili ni Mgnum 22,” Amata akaonesha wasiwasi wake.
Simbeye alibaki kimya, akavua miwani yake na kuiweka mezani akamkazia macho kijana huyo shababi na mrembo wake Gina waliokuwa kimya wakisubiri jibu la mzee huyo. Akajikuna kichwani na kufikicha masikio yake.

“Amata, Kamanda Amata, unanipa fikra mpya ya kuweza kufikiria mambo amabayo nilikwishayaweka kando, hilo unalosema linawezekana tena kwa asilimia sitini, na lazima lifanyiwe kazi,” Simbeye akajibu huku akikusanya yale maganda na kuyarudisha kwenye ule mfuko, Amata akachukua yale mawili yenye utata na kuyatia mfukoni.
“Vipi?” Gina akauliza.
“Naenda kumkamata muuaji na huyu ndiye mwenye jibu la nini kilitukia. Na nitamkamata leo hiihii,” Amata akaongea kwa hasira. Wakaagana na kuondoka zao huku wakimuacha Simbeye akiwa hoi kwa mawazo.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI

MTUNZI: richard MWAMBE

“Amata, Kamanda Amata, unanipa fikra mpya ya kuweza kufikiria mambo amabayo nilikwishayaweka kando, hilo unalosema linawezekana tena kwa asilimia sitini, na lazima lifanyiwe kazi,” Simbeye akajibu huku akikusanya yale maganda na kuyarudisha kwenye ule mfuko, Amata akachukua yale mawili yenye utata na kuyatia mfukoni.
“Vipi?” Gina akauliza.
“Naenda kumkamata muuaji na huyu ndiye mwenye jibu la nini kilitukia. Na nitamkamata leo hiihii,” Amata akaongea kwa hasira. Wakaagana na kuondoka zao huku wakimuacha Simbeye akiwa hoi kwa mawazo.

SEHEMU YA XI

***
“Amata! Hivi hii akili ya haraka unaipata wapi?” Gina akauliza wakati akiondoa gari pale kituo cha polisi cha kati na kuelekea mjini.
“Ukishakuwa katika kazi hizi inabidi uwe na akili ya juu sana, hata wewe baadaye utajikuta unakuwa hivyo,” Amata akaeleza, na wakati huo simu yake ikaita, daima simu hii ikiita alijua ni kutoka kwa Madam au mtu yeyote wa TSA kwa kuwa haikuwa simu ya kawaida.
“…yes Madam!” akaitika, “…ndiyo, tupo hatua moja kutoka katika ufumbuzi wa hii kitu, na naamini leo hii utafurahi huku hauamini (…) sawa Madam,” akamaliza kuongea na simu ile, akaikata na kuiweka mahala pake.

“Twende ofisi ya Kinondoni tukamwone Hosea,” Amata akamwambia Gina, na mara hiyo akawasha indiketa na kuisha barabara ya Samora akakunja kulia kuchukua ile ya Ohio na kuongoza mpaka barabara ya Hali Hassan Mwinyi. Nusu saa baadae walikua tayari katika jingo la ofisi za Usalama wa Taifa, Kinondoni. Jingo hilo lililoonekana kama limetelekezwa kwa nje, ndani kulikuwa na mambo mengi sana yaliyokuwa yakiendelea, mambo ya kiusalama. Wakazipanda ngazi na kuingianndani ya jingo hilo, moja kwa moja wakaongozwa mpaka ofisi ya mkuu huyo wa idara nyeti ya Usalama wa Taifa. Huyu bwana ndiye alikuwa na cheo cha juu kabisa katika kitengo hiki.

“Karibu sana bwana Amata, ni muda mrefu hujafika katika ofisi yangu najua utakuwa unahitaji msaada tu hakuna linguine,” Hosea alimwambia Amata huku wakipeana mikono.
“Bila shaka,” Amata akajibu huku akiketi.
“Ndiyo bwana!”
“Ndiyo, Bwana Hosea, nimekuja kweli nahitaji msaada, silaha zangu zimeibwa nyumbani mkuu unisamehe sana, na sasa sina silaha kabisa unisaidie,” akamwambia kwa kumzunguka.
“Hivi Amata mpaka unaibiwa silaha ulikuwa wapi?” Hosea akauliza.
“Mkuu, sikuwa nyumbani na wamevunja kitasa wamechukua zote. Nimeogopa kumwambia Selina najua maswali yatakuwa mengi, nitazirudisha naazima kwa sasa tu,” akamweleza. Hosea akatulia kimya akifikiria jambo kisha akatuliza mikono yake mezani.

“Kwa sababu ni wewe, nitakupa lakini saa sabini na mbili uwe umezirudisha,”
“Sawa, halafu kama una Magnum 22, ingenifaa sana,” Amata akasema. Dakika kumi zilizofuata akachukuliwa mpaka kwenye chumba maalum cha silaha, kule alikuwa na kijana ambaye kazi yake ilikuwa ni kutunza ghala hiyo ya silaha kwa ajili ya watu wa usalama.
“Magnun 22, hii hapa,” yule kijana akamwambia Amata huku akimkabidhi kikasha chenye silaha hiyo.
“Hii ndiyo silaha bwana, nani mwingine anayo kama hii? Najua wengi hawaipendi,” Amata akadodosa.
“Aaaa sikumbuki ngoja nitacheki kwenye kumbukumbu lakini ni kama wawili au watatu ndiyo maana unaziona zipo za kutosha maana siku hizi wengi hawataki hizi,” yule kijana aliendelea kuongea huku akimpa na risasi za bastola hiyo, kisha wakafuatana mpaka kwenye ofisi ndogo ambayo kulikuwa na kabrasha kadhaa mezani na kompyuta ndogo, ofisi hii ndiyo aliyokuwa akiitumia yule kijana kuweka kumbukumbu zake.

“Du, tuna watu kama kumi na mbili hivi wanaotumia silaha hiyo kiofisi ambao wamechukulia hapa,” yule kijana akamweleza Amata na kisha akataja namba za wale watu, hakuwajua kwa majina kwa kuwa ilikuwa ni siri za kiofisi. Kamanda Amata alikuwa akirekodi mazungumzo yote na kijana huyo alipojiridhisha akaagana naye na kuondoka kisha akapita ofisini kwa Mkurugenzi bwana Hosea na kuagana naye huku akitakiwa kuirudisha silaha hiyo ndani ya saa sabini na mbili.
“Umepata unachotaka?” Gina akauliza.
“Bila shaka!” akajibu na kutoa ile bastola mpya kabisa na kumweleza Gina mbinu aliyoitumia kupata anachotaka, “Hapa nina namba za wafanyakazi kumi na mbili wa idara ya Usalama wa Taifa, nitazichambua kujua nani ni nani na yuko wapi, najua katika hili yupo ambaye bundi litamfia na huyo ndiye tutaanza naye!” akaongeza kujibu huku Gina akiicaha barabara ya Kinondoni na kukamata ile ya Hali Hassan Mwinyi kuelekea mjini.

OFISI NDOGO

KATIKA OFISI hiyo ndogo ambayo Madam S aliitumia kama ofisi yake ya kazi, alikutana tena na vijana wake majira ya mchana. Kamanda Amata aliwasimulia yote aliyoyafanya huko alikotoka. Akampa Madam ile sauti iliyorekodiwa kati yake na yule kijana kule Kinondoni.
“Nahitaji kuzitambua hizo namba moja baada ya nyingine,” Amata akamwambia Madam S, katika idara ya usalama Madam S alaikuwa na nywila iliyomwezesha kuingia kwenye mtandao wa Usalama wa Taifa. Madam S akabofya kitufe Fulani uvunguni ma meza hiyo na juu ya ile meza pakafunguka na kujiinua kompyuta ya ukubwa wa wastani ikasimama mbele yake na kuwaka.
“Msije huku tafadhali!” akawaambia na wote wakatulia walipo. Amadam S alitaja namba moja moja na jina la mtu husika, huku Chiba akiendelea kuingiza majina hayo katika mtandao wake wa utambuzi. Jina namba 301 ambalo katika orodha hiyo lilikuwa la mwisho kabisa, lilimstua Chiba.
“Madam! Namba 301…” akamwambia wakati picha ya mtu huyo imejitokeza pale juu na taarifa zake zote, Chiba akahamaki kwa sauti.
“What!? Gina njoo hapa haraka…” Gina akawahi pale alipo Chiba na kutazama kwenye ile kompyuta, macho yakamtoka.
“Nini nyie? Mbona hivyo?” Amata akauliza huku akigeuza kiti chake kutoka kwa madam na kukutana uso kwa uso na picha ile.

Briston Kalangila, mwajiriwa wa serikali ya Tanzania tangu mwaka 1990 katika kitengo cha Usalama wa Taifa. Kabila Muha mwenye uchanyiko wa baba wa Kiha na mama mwenye asili ya Nduruta. Amepata elimu yake huko Nduruta na kisha kuja kumalizia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kabla ya kujiunga na Idara ya Uhamiaji na baadae kuingia Usalama wa Taifa, namba ya utambulisho wake wa kikazi ni TNS 301.
“Mimi nilisema huyu ana shida, nilishamhisi tangu siku ya kwanza nilipokutana naye!” Chiba akaeleza na Gina akaunga mkono. Amata akaitazama ile picha.
“Unamjua vyema?” Madam akamwuliza Amata.
“Namjua vizuri ila nilikuwa sijui kama ni yeye,” akamgeukia Madam, “ Madam S, huyu ni mtuhumiwa wetu namba moja na sasa hivi lazima ashughulikiwe, katika maganda ya risasi themanini na moja maganda mawili ni ya huyu Briston, Briston ameua wanausalama wetu wawili na lazima achunguzwe,” Amata akasema.
Madam S akajishika kichwa na kukitikisa kisha akawatazama vijana wake.

“Sasa nimeelewa, nimeelewa mengi sana vijana, mmenifungua macho na akili, sasa nimeelewa kitu,” Madam S akafunga kompyuta yake nayo ikarudi pale mezani na meza ile ikawa ya kawaida, akainuka na kuliendea jokofu akachukua pombe kali na kujanayo mezani na bilauri kadhaa akawamiminia vijana wake kwenye bilauri hizo huku akionekana wazi kuwa na hasira zisizojificha. Kamanda Amata akainuka pale kitini na kumwendea Madam pale dirishani aliposimama baada ya kuwamiminia kinywaji kile.
“Madam S, nakufahamu vyema kabisa miaka yote tuliyokaa pamoja, hebu niambie ni nini umekielewa hapo?” akauliza.
“Sikia Amata, kama TSN 301 Kalangila ameshiriki katika njama hii na ye kumbuka ni chotara wa Kitanzania na Kinduruta, basi hapa kuna mengi, hii njama ni ya wengi, lazima kuna mapandikizi mengi, mengi sana tena katika idara mbalimbali za serikali; jeshini, polisi, bungeni. Serikali inabidi kuwa makini hawa watu wa mchanganyiko wa damu si wa kuwapa vipaumbele kwenye vitengo nyeti hasa vya usalama kama hivi, wapo wengi sasa naanza kuwajua mmoja baada ya mwingine. Nahitaji kuonana na Rais…” akatoka na kumwacha Amata pale akaiendea meza yake na kuinua simu.
“Subiri Madam! Ngoja tumshughulikie huyu 301 kisha utafanya hiyo process, tafadhali,” Amata akamwambia Madam. Kisha akarudi kwa Chiba na Gina.
“Ok, jioni hii ni siku ya kumnasa Kalangila Briston, na hiyo kazi itafanywa nasi sote,” akawaambia.

***
Briston Kalangila alitoka taratibu na gari yake katika geti la Ikulu, akateremka barabara ya Magogoni na kukunja kulia pale katika soko la samaki na kupandisha kuelekea Posta. Moja kwa moja mpaka barabara ya Maktaba kisha akaegesha gari yake Hoteli ya New Afrika, akateremka na kushusha miwani yake huku akiangalia huko na huko.
Gina alitulia kimya katika tax ya Scoba akimwona mtu huyo aliyemfuatilia tangu pale Ikulu bila yeye kujua, akamtazama, akiingia ndani ya hoteli hiyo ya kimataifa. Gina akataka kushuka ile aelekee kule, lakini Scoba akamzuia.
“Usiende, subiri kidogo,” Scoba akamzuia, Gina akatulia lakini wakati huo tayari damu yake ilikuwa ikichemka. Nukta hiyo hiyo Land Cruiser moja ikaingia katika hoteli ile na kuegeshwa nje tu. Kijana mmoja aliyeshupaa misuli akateremka, Gina akamkodolea jicho. Nani Yule? Akajiuliza. Kwa kamera yake ndogo akachukua picha ya mtu huyo kisha wakatulia ndani ya gari ile. Nusu saa baadae Yule jamaa mfupi akatoka, Gina akachukua kamera yake na kuchukua picha kadhaa.
“Fuata hiyo gari,” akamwambia Scoba, naye akaingiza gari barabarani na kuifuata ile Cruiser. Mpaka Masaki ilipoingia katika yale majengo ambayo bado yalikuwa kwenye ujenzi. Picha zote Gina akazihifadhi vyema katika kamera yake, kisha taratibu wakaondoa gari yao na kuchukua barabara ya kwenda Cocobeach kisha moja kwa moja wakapita tena mbele ya Hoteli New Africa lakini hawakuiona gari ya Briston.
“Ameondoka” Gina akanong’ona huku Scoba akipita bila kusimama, akazunguka mzunguko wa askari na kuchukua barabara ya Samora kurudi Ofisi Ndogo.

CASINO LAS VEGAS
DAR ES SALAAM

Briston alipotoka pale New Africa moja kwa moja alielekea katika Casino kubwa ya Las Vegas kwenye makutano ya barabara ya Hali Hassan Mwinyi na ile inayoelekea Ocean Road. Ndani ya Casino ile jioni hiyo tayari watu walianza kumiminika kwa starehe mbalimbali. Miongoni mwa waliokuwa wakiingia, Briston Kalangila alikuwa mmoja wapo akiwa sasa ndani ya suruali ya jinzi ya bei mbaya na fulana ya pundamilia iliyomkaa sawasawa, tambo lake kubwa lilimfanya aonekane kama mnyanyua vitu vizito. Mkono mmoja mfukoni na mwingine ukining’inia alivuta hatua na kupishana na warembo kadhaa waliokuwa ndani humo wakiuza na kujiuza. Ndani ya casino hiyo muda huo wa saa kumi na moja ya nje kule tayri ulikuwa usiku kwani mataa ya rangi rangi yalikuwa yakipishana kuupendezesha, gizale lilikuwa dhahir shahir. Akajivuta mpaka kwenya meza moja ya duara iliyokuwa na viti vine na katikati ya meza hiyo kulikuwa na mchezo wa ‘gurudumi la bahati’, haukupita muda aliongezeaka mtu mwingine naye alionekana kujaa mwili, walishahabiana kwa nukta chache kana kwamba walikuwa mapacha, naye akaketi palepale, huyu alikuwa maji ya kunde ukiachana na ukubwa wa mwili wake alikuwa na sura ndefu kiasi yenye pua nyembamba.
Kamanda Amata alikuwa mmoja kati ya wateja wa casino hiyo jioni hiyo, baada ya kuingia nyuma kidogo ya Briston, aliketi kaunta akipata kinywaji na kumtanabahi kila aingiaye na atokaye, kutokana na ile sehemu aliyoketi aliweza kuona hayo yote. Alimwona anyemtaka, Briston.

Yule ni nani? Akajiuliza baada ya kumuona huyo aliyeongezeka, akapiga funda moja la kinywaji, kisha akashusha ile bilauri na kuendelea kuangalia upande ule kwa chati. Baadae zaidi akaja mtu mwingine kati yao, huyu alikuwa wa kawaida tu lakini alikuwa mrefu, mwembamba, aliketi kati yao, wakawa watatu. Katika meza hiyo kulionekana kuwa na mazungumzo mazito yaliyoleta shida ya muafaka. Yote hayo Amata alikuwa akiyatengeneza kadiri anavyoona hali ya waliyonayo watu hao. Alijitahidi kupata japo pizza za hao wengine lakini alishindwa kutokana na nyendo za watu ndani humo na pia. Akainua simu yake kubwa na kuandika ujumbe mfupi kwa Chiba akimtaka kuwapo nje ya casino hiyo haraka iwezekanavyo na kumwelekeza watu ambao anataka awajue ni akina nani.
Baada ya dakika kama arobaini na tano hivi, wale jamaa walionekana kumaliza mazungumzo yao, akatoka Yule mwembamba na kwenda zake huku Briston na Yule mwingine wakibakia. ya casino ile na moja kwa moja akaegesha gari yake mahala salama na ambapo angeweza kumwona kila atokaye ndani ya jumba hilo, akateremka na kuchukua lap-lap akaanza kuifuta gari yake kana kwamba anamsubiri mtu fulani.
Chiba aliwasili nje ya casino ile na moja kwa moja akaegesha gari yake mahala salama na ambapo angeweza kumwona kila atokaye ndani ya jumba hilo, akateremka na kuchukua lap-lap akaanza kuifuta gari yake kana kwamba anamsubiri mtu fulani.

“…mrefu, mwembamba, kava kofia ya pama,” ujumbe uliingia kwenye kifaa cha Chiba kilichopachikwa sikioni kwa ufundi kabisa, akaendelea kufuta gari yake mara hii upande wa nyuma ili apate nafasi ya kumwona mtu huyo. Lengo lake lilifanikiwa, alimwona mtu huyo akitoka ndani ya jengo hilo, akasimama ngazini na kuwasha sigara yake. Wakati huo Chiba alikuwa nyuma ya gari yake, akafanikiwa kupata picha ya mtu huyo kwa simu yake kubwa nay a kisasa. Picha tofauti kama kumi hivi mpaka kijana huyo alipokuwa akipanda gari yake na kuondoka, kilichomwacha Chiba kinywa wazi ni gari iliyokuja kumchukua, ilikuwa na namba za kibalozi. Namba zile Chiba alizitambua mara moja kuwa ni namba za ubalozi wa nchi ya Nduruta. Akatikisa kichwa na kisha akaendelea na shughuli yake. Mara akapokea ujumbe mwingine uliyomtaka kummulika anayetoka.
“…Ana tambo kubwa kava suti kijani juu mpaka chini,” ujumbe ulitoka ka Kamanda Amata. Mtu Yule alijitokeza nje, akapitiliza na kuteremka zile ngazi mpaka chini kabisa, na kuingia kwenye gari oja ya kisasa. Chiba alikamata picha zote alizozihitaji na kuzihifadhi kadiri alivyotaka, alipohakikisha zote amezipata, akaingia ndani ya gari yake na kujifungia kimya. akisubiri...

***
Baada ya wale watu kuondoka, Briston alibaki peke yake pale mezani, Kamanda Amata akateremka taratibu na kumwendea palepale alipo, akavuta kiti na kuketi. Briston akamtazama kijana huyu mwenye macho maangavu yanayoonesha kila aina ya udadisi.
“Mbona wajikaribisha mwenyewe, kijana huna adabu…”
“Haina haja ya kukuzungusha, naitwa Amata Ric au wengi huniita Kamanda Amata bila shaka umelisikia jina hili na kama la basi ndiyo mimi mbele yako,” Amata akamwambia Briston. Briston akajiweka sawa kitini na kumwangalia tena kijana huyu.

“Nikusaidie nini Kamanda sijui kidudu gani sijui, huna kinywaji?” akamwuliza kwa kejeli.
“Sina haja ya kinywaji maana ni vingi nyumbani kwangu. Briston Kalangila TNS 301,” Amata alipotamka namba ya kazi ya huyo mtu, Bristoni alihisi akili kumpaa kwa sababu raia wa kawaida hawajui namba hizo.
“U-u-mesema unaitwa nani?” akauliza tena, sasa kwa makini zaidi. Amata akaondoa miwani yake usoni, akabandua mustachi mzuzu wake bandia nay ale masharafa akabaki wa kawaida. Briston akashusha pumzi ndefu, “Umekuja kwa heri au kwa shari?” akauliza kwa hofu iliyoonekana wazi.
“Sijaja kwa shari, ni kwa heri tu maana wakati mwingine huwa tunapenda kufanya kazi katika mazingira kama haya, wanausalama saba na zaidi wameuawa ndani ya jingo la Ikulu na mke wa Rais ametekwa na wewe ulikuwapo lakini hukufanya lolote hili ndilo limenileta kutaka kujua,” Amata akamchokoza bila kumyumbisha.
“Hivi we una wazimu? Wale jamaa walivyovamia pale ulikuwepo, unajua waliingia na silaha gani au zenye uzito gani?”
“Mzee, hukuwa mtu wa kushindwa kuzuia uvamizi ule kwa jinsi unavyojua kuorganize watu, kumbuka Rais aliyepita alikuweka kwenye kitengo cha runners kwa sababu ya weledi wako wa kupanga na kutengeneza mambo,” Amata akaendelea.
“Narudia tena, unajua silaha walizokuwa nazo na uzito wake, ulitaka wote tufe halafu nini kitokee? Si ushukuru hao saba sijui wangapi waliokufa, kama huna la kuongea nitokee hapa!” akaongea huku jazba ikipanda.

“Najua, walikuwa na Assault Shotgun, shambulizi lao walitumia risasi sabini na tisa tu lakini zilizopatikana ni themanini na moja...”
“Kwa hiyo hizo mbili zimetoka wapi?” Bristona akadakiza swali.
“Ndiyo hicho nataka unijuze, risasi mbili ni za bastola ya Magnum 22 na katika katia ya wanausalama wanaomiliki silaha hiyo mmojawapo ni wewe, na ambaye upo pale Ikulu muda mwingi. Moja imeokotwa kwenye mlango wa chumba cha silaha pamoja na maiti ya mtunza stoo hiyo, na nyingine imeokotwa kwenye mlango wa kuingilia katika apartment ya Rais, ina maana katia ya watu wetu waliouawa, wewe kwa mkono wako umeuwa wawili, na ni hao nimekutajia…” Amata alieleza bila kusitasita na kumfanya Briston afure kwa hasira, macho yake yalibadilika.
Briston alikumbuka matukio hayo yakamrudiarudia kwenye kumbukumbu zake wakati huo, alijaribu kupingana nayo lakini ilishindikana, “Hivi umetumwa?” akauliza.

“Ndiyo,”
“Na nani?” akauliza.
“Na mama yako!” Amata akamjibu huku akirusharusha yale maganda ya risasi katika kiganja chake cha mkono, kisha akayatia mfukoni na kunyanyuka, “Kazi njema Briston kalangila,” akamuaga naye akatoka eneo lile.
Briston Kalangila, alimtyazama kijana Yule akiondoka pale mezani kwake kwa mwendo wa mikogo, akajichanganya na wateja wengine mpaka alipoishia kaunta. Kwa hasira akapiga ngumi mezani na kisha akainua simu yake na kuongea machache alipomaliza akatulia tuli, mara hii kile kinywaji kilikuwa hakipiti shingoni, mishipa ya kichwa ilimdinda na kijasgho chembembe kilitiririka ijapokuwa mashine za nguvu za kupoza hewa zilikuwa zikiwajibika kufanya hivyo.
“Yes boss!” sauti ya kike ikasikika mbele ya Kalangila, akainua uso wake na kumtazama binti huyo, mwembaba wa wastani mrefu mwenye shingo nyembamba, sura ndefu, meno yake meupe yalipangiliwa vyema na Malaika aliyesadifu kinywa hicho.
“Sikia Lulu, fanya unaloweza, umtie mkononi huyu mtu naujua ubembe wako hawezi kuchomoka kwani hakuna mwanaume ngangari mbele ya mwanamke mrembo labda awe hanithi,” muda huohuo akamtumia picha ya Amata kwenye simu na kumwacha Yule binti aende zake. Briston akanyanyuka na kutoka kwenye ile casino kuelekea nje.
***
Kamanda Amata alikuwa wa kwanza kuiacha casino hiyo na kutoka nje, moja kwa moja aliiendea gari aliokuja nayo Cjoba na kuingia siti ya mbele akaketi huku Chiba akiwa nyuma ya usukani. Kimya hakuna aliyeongea, wote macho yao yalikuwa yakiangalia kule kwenye lango la casino hiyo. Briston akatokezea na kuteremka ngazi taratibu akaelekea kwenye maegesho na kuingia ndani ya gari yake kisha akaiwasha tayari kuondoka.
“Sasa?” Chiba akauliza.
“Tunamfuatilia mguu kwa mguu, yaani usiku huu mpaka tujue nini anafanya na ikiwezekana nitakwenda kuikagua nyumba yake…”

“Nyumba yake? Vipi kama mkewe na watoto wapo huko?” Chiba akamkatisha na kumuuliza.
“Usijali, kila kitu kitajulikana papo hapo,” akiwa katika kusema hayo, ile gari ya Briston ikapita mbele yao na kupunguza mwendo, kioo cha upande ule waliokuwa akina Amata kikateremka taratibu kisha Briston akawaoneshea dole la kati na kile kioo kikapanda taratibu huku ile gari ikiselelereka barabarani kulifuata lango la kutokea. Chiba akaweka mkono katika katika funguo ya gari tayari kuwasha, Amata akamzuia huku akimwonesha ishara ya kidole kuangalia kule katika lango la kutoke casino. Chiba akainua macho na kumwona mrembo aliyesimama huku akichezea simu yake.
“Kaka tupo kazini kaka, achana na hayo, kila siku bibi yako anakuonya…”

“Aaaa bibi yako keshazeeka, ye mwenyewe enzi zake alikuwa hivihivi. Kazi na dawa; huyu lazima nimkamate leo hii, cheki mtoto Yule,” Amata akaongea.
“Kwa hiyo tunamfuata Briston au?” Chiba akauliza.
“Ameshatujua, tukisubutu tu tumeisha, Yule hafai kabisa. Sasa ipo hivi, kanifanyie utambuzi wa hizo picha za hao jamaa wawili, mi niache na huyu mrembo,” alimaliza kusema hayo akiwa tayari nje ya gari hiyo. Chiba akawasha na kuondoka eneo lile.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: PASIPOTI YA GAIDI – 1 –
Hujuma na uzandiki
MTUNZI: richard MWAMBE
“Aaaa bibi yako keshazeeka, ye mwenyewe enzi zake alikuwa hivihivi. Kazi na dawa; huyu lazima nimkamate leo hii, cheki mtoto Yule,” Amata akaongea.
“Kwa hiyo tunamfuata Briston au?” Chiba akauliza.
“Ameshatujua, tukisubutu tu tumeisha, Yule hafai kabisa. Sasa ipo hivi, kanifanyie utambuzi wa hizo picha za hao jamaa wawili, mi niache na huyu mrembo,” alimaliza kusema hayo akiwa tayari nje ya gari hiyo. Chiba akawasha na kuondoka eneo lile.
Sehemu ya 12
Briston usiku ule moja kwa moja alielekea hoteli ya New Africa ambako daima hukutana na kijana wake Kubra Khaleb. Wawili hao walikutana kwa dharula haikuwa imepangwa kuwa hivyo.
“Vipi comrade?” Kubra akauliza.
“Mpango umestukiwa?” Briston akajibu huku akilisaidia feni kumpepea.
“Unasema! Mpango upi?”
“Mcehzo wote wa Ikulu umegundulika…”
“Nani kagundua wakati kazi ile tumeifanya kwa umakini wa hali ya juu?” Kubra aliwasiwasika kwa hilo.
“Sikiliza Kubra! Tulifanya kwa weledi wetu wote, lakini kuna watu wana vichwa vya ajabu, huyu jamaa tusipomdhibiti sasa tumeumia na anatufuatilia nyayo kwa nyayo,” Briston akaeleza.
“Unafikiri atajua yote?”
“Kubrah! Kama kagundua kuwa silaha za waasi zilikuwa zinatoka Ujerumani na mpaka digala mwenye kamjua na kapambana naye, unafikiri hatojua kuwa mipango hii yote ina lengo moja? Sasa keshajua kilichotokea ndani ya Ikulu, keshanijua mimi, bila shaka keshakujua wewe. Na leo nimekutana na Kepteni Banzilahagi pamoja Kimosa Kabalege Yule afisa wa ubalozi katika idara ya usalama, sasa hapa sijui kama kawaona au vipi, maana baada tu ya kuondoka wale jamaa na ye akaja mezani kwangu…”
“Ha! Yaani kaja mpaka mezani kwako umemwachia? Huku na silaha?” Kubrah akang’aka kuuliza.
“Kubrah, nilikuwa nahitaji kujua nini anakijua juu ya hili, nimeona anajua lakini hasa ni swala la uvamizi zaidi ya hapo hakuna anachokijua,” akaeleza.
“Good! Sasa inabidi tumdhibiti usiku huu,” Kubrah akaeleza mpango.
“Ni sawa, kazi nimempa Lulu, nina uhakika atalifanikisha, akimpata atatupigia ili tukamalizie kazi,” akamwambia Kubrah.
“Oooh una jina zuri sana Lulu, yaani kitu chenye thamani sana ambacho kwanza hakipatikani kirahisi,” Amata alimwambia mrembo huyo wakati akiwa naye ndani ya gari.
“Mmmmmh maneno yenu tu hayo,” Lulu akajibu.
“Napenda nikapitishe usiku huu na wewe,”
“Waoh! Is it possible?” Lulu akatia shaka.
“Hauamini?”
“Siwezi kuamini moja kwa moja kwa sababu, umekaa pale ndani hata kumpapasa mwanamke yoyote hujajaribu…” Lulu akaeleza.
“Uliniona?”
“Aaaa sana, sisi huwa tuna macho mia…”
“Nyinyi na nani?” Amata akamkatisha.
“Ah we! Tuko wengi tunafanya shughuli zetu hapa,” Lulu akaeleza huku macho yake akiyapeleka nje.
“Nimekuchagua wewe, mrembo, unapenda tukamalizie usiku huu wapi? Nyumbani kwangu?” Amata akauliza huku mkono wake tayari ukipapasa paja la mrembo huyo, taratibu kutoka kwenye goti kuelakea pajani.
“Nyumbani kwako namwogopa mkeo,”
“Sina mke!”
“Basi mpenzio,”
“Ah… hapana sina mpenzi, nimekuchagua wewe leo…”
“Napenda New Africa,” Lulu akachagua. Amata akaondoa mkono wake pajani mwa Lulu, akakamata gia ya gari huku mkono wa kulia ukitekenya ufunguo na gari hiyo ikawaka, akaweka gia namba moja na kuondoka taratibu.
Iliwachukua takribani dakika kumi na sita tu kuwasili New Afrika, Kamanda Amata akangiza gari maegeshoni na kushuka na membo huyo akiwa mkono wake wa kuume kauzungusha kiunoni mwa mrembo huyo huku mabusu ya hapa na pale yakiendelea.
“603,” mwanadada wa mapokezi alimtajia namba ya chumba huku akimkabidhi kadi maalumu ya kufungulia mlango wa chumba hicho.
“Nahitaji whisky tafadhali…”
“Mmmmh na Amarula!” Lulu akaongeza huku wakiondoka pale mapokezi na kumwacha Yule mwanadada akishughulikia hilo.
Ndani ya chumba hicho Amata alimbwaga Lulu kitandani na kuanza kumpiga mabusu mazito ya kinywani huku Lulu naye akionesha ufundi wa hali ya juu katika kuumung’unya ulimi wa Amata. Kengele iliyogongwa mlangoni iliwaachanisha wawili hao na Amata akauendea mlango na kupokea vinywaji walivyoagiza. Lulu aliinuka na kpekua pochi lake, akatoa simu ndogo na kubofya haoa na pale na wakati huo Amata alikuwa amekwisha fika.
“Achana na simu dear!” akamwambia.
“Aaaa ndiyo nilikuwa nazima ili tule raha kwa raha, naomba nimalizie process basi,” Lulu akaongea kwa sauti ya kubana pua, Amata akamruhusu naye akabofya ‘send’ kisha akazima simu na kuitupa pembeni.
Madam S alibaki akizunguka zunguka huku na huko, kichwa chake kilionekana kuchanganyikiwa wazi kabisa.
“Chiba simaini unachoniambia kabisa, una uhakika na hilo jambo?” akauliza.
“Bila shaka Madam, Amata aliniita kufika pale Las Vegas name nikafanya hivyo, na akanipa hizo ishara nikakamata picha za hao watu, nimezicheki hapa kwenye mtandao wetu na majibu ndiyo hayo,” Chiba akaeleza.
“Banzilahagi, Kepteni wa Jeshi la Wananchi tena ana kitengo nyeti sana jeshini, kama atakuwa ndani ya mpango huu tumekwisha na katika hili lazima tuchukue hatua ya haraka sasa hivi, huyo Kimosa Kabalege naye pia!” Madam akazungumza huku akivuta kiti na kuketi, “Kamanda yuko wapi?” akauliza.
“Aaaaa nimemwacha viungani ana misheni nyingine,” Chiba akajibu huku akibana kicheko kilichojionesha wazi mashavuni mwake.
“Unacheka nini? Au unamfichia siri? Sema tu kama yuko na mwanamke, maana Yule sijui ana ugonjwa yaani sielewi…”
“Aaaa hayo umesema wewe Madam mi husiniweke hatiani,” Chiba akamaliza kusema huku akiifunga kompyuta yake.
Madam S akainua simu yake ya mkononi na kubofya namba Fulani kisha akaweka sikioni mwake kwa sekunde kadhaa, “Hapatikani…” akashusha simu hiyo na kupiga namba nyingine, akaweka tena sikioni.
“Gina! Hello!” Madam alipoita jina hilo Chiba akafumba kinywa chake kwa hofu, anaharibu lo! Akawaza.
“Uko wapi? (…) ok, sasa nataka uhakikishe unamchunga mtu anayeitwa Banzilahagi Yule kepteni wa jeshi, anaishi Makongo plot namba 703, nipe kila dondoo za nyendo zake,(…) ok vyema, fanya hivyo,” akamaliza na kukata ile simu. Chiba akashusha pumzi huku mikono sasa ikiwa kiunoni. Kisha akabofya namba ingine na kuweka sikioni.
“Scoba! Unasomeka wapi? (…) ok! Nimekupata, sasa ipo hivi, nataka uweke jicho katika nyumba ya Afisa Baalozi Kimosa Kabalege na unipe dondoo zote za nyendo zake usiku huu na mpaka nitakapokupa amri nyingine,(…) ok, ok!” akakta simu na kuketi.
“Naona mbananisho umeanza,” Chiba akamwambia Madam huku akiitazama saa yake.
“Inabidi tufanye kazi kwa mtindo huo kwa kuwa mpaka sasa hawa tunawashuku,” akajibu Madam S.
Lulu alimwonesha manjonjo ya kutosha Amata kitandani hapo, ilikuwa shughuli nzito ukizingatia walikuwa tayari wametanguliza kinywaji. Lakini ghafla, Amata alichomoka kutoka kitandani na kumwacha mwanamke Yule palepale, akaketi kiatandani.
“Vipi jamani, unanikatisha utamu!” Lulun akalalamika. Amata akamwoneshea kiganja chake cha mkono kumuashiria anyamaze. Akaingiza mkono wake chini yam to na kutoa bastola, akavuta slider yake na kuiachia, risasi moja ikakaa sawa, kwa haraka akavaa bukta na kusimama pembezoni mwa kabati.
“Kuna nini?” Lulu akauliza.
“Shhhhhhh!!!!” akamwaonesha kwa kukiweka kidole juu ya midomo yake. Kisha akanyata na kuliendea dirisha na kujibana sawia pembeni yake. Dirisha lile likavutwa polepole kufunguliwa na mkono wenye bastola ukajitokeza kule pale kitandani, Amata akaiweka bastola yake pembeni na kwa kasi ya ajabu akakukamata mkono wa Yule mtu na kuukunja.
“Aaaaaiiggghhh!” ule mkono ukateguka mifupa, akamvuta ndani kwa nguvu na yule jamaa akaingia na kioo cha dirisha, alipoingiza shingo akampa pigo moja kali la karate na yule jamaa akatua ndani kama mzigo na bastola ikimtoka mkononi na kuselereka mbali. Lulu akakurupuka kitandani na kupiga sarakasi moja maridadi akainyakua ile bastola. Amata hakutegemea kile kitendo alipogeuka tu, risasi moja ilipita karibu kabisa na uso wake na kufumua kioo cha dirisha. Akjitupa kwa nyuma na kukoswa na risasi nyingine kutoka kwa Lulu, Amata akainyakuwa bastola yake lakini kabla hajaishika vizuri, Lulu aliilenga kwa risasi na kuiondoa mahala pale, Amata akaikosa. Shabaha ya Lulu ilimshangaza Amata, akaona akizubaa na kudharau kwa kuwa mwanamke anaweza kuaibika. Aliinua taa ya mezani na kumrushia kwa nguvu, ikampiga usoni, Lulu akapoteza mwelekeo, wakati akijiandaa kufyatua risasi yake akajikuta akikutana na miguu mizito ya Amata iliyotua tumboni mwake na kumfanya ajibamize vibaya ukutani. Amata akajiinua lakini kabla hajawa wima, aliliona teke kali la mwanmke huyo likija usoni mwake, akaepa na mguu ule ukapita wakati huo na yeye akauzungusha wa kwake na kuupiga kwa chini wa yule mwanamke uliobaki wima sakafuni, akamchota ngwala maridadi na kumbwaga vibaya.
“Mhhhh! Aaagh! Mpenzi unaniua?” Lulu akalalama huku akijaribu kujiinua. Amata akamwahi na kumkamata night dress yake akampiga kichwa kimoja maridadi na Lulu akalegea na kusihiwa nguvu, Amata akamsukuma na kupigiza ukutani, akaanguka kando akiwa hana fahamu na damu zikitiririka katika tundu za pua yake. Amata akamwacha pale chini na kuiendea suruali yake, akaivaa haraka na fulana yake ikafuta juu yake, bastola yake akaibana sawia kiunoni mwamke kisha akamwendea Yule jamaa aliyemwacha pale usawa wa dirisha baada ya kipigo kile akampekua na kumkuta na simu tu mfukoni mwake, akaichukua na kubofya kidubwasha cha kupigia kisha akaitoa loki yake na kupekuwa kwenye boksi la ujumbe mfupi.
‘…hakikisheni huyo Malkia anahifadhiwa vyema, safari inakaribia alfajiri ya kesho…’
Baada ya ujumbe ule ukafuatiwa na mwingine ukisema…
‘…wapo chumba namba 603, muue mwanaume, mwanamke tuachie…’
Amata akatabasamu kwa ujumbe ule na alipouchunguza akagundua kuwa ulitumwa na mtu mmoja kwa tofauti ya muda wa saa moja, akaujibu ule wa pili kwa kutumia simu ileile, akajua wazi wakiupokea ujumbe huo lazima hao walioutuma wachanganyikiwe.
‘…nimekufa mimi…’
Kisha akautuma na kuitia ile simu mfukoni, akaunyakua mkoba wa Yule mwanamwali na kumwaga kila kilichopo, akakuta mashine ndogo ya kurekodi sauti, akaichukua zaidi ya hapo hakukuwa na kingine cha maana za ya kijitabu kidogo cha anwani za watu akakichukua na kutoka ndani ya chumba kile haraka, badala ya kutumia lifti kuteremka mara hii akatumia ngazi za kawaida tena isitoshe ngazi za dharula kwani alihofu kukutana na watu asiowatarajia, moja kwa moja akaiendea gari yake lakini kabla hajaifikia, alipojitokeza tu upande wa pili wa hoteli ile kutokea nyuma, alimwona kijana mmoja akiwa usawa wa tairi la mbele akifanya jambo Fulani kwenye gari hiyo. Amata akajificha na kuangalia kila kitu kwani alihofia hicho anachofanya kijana huyo. Baada kama ya dakika mbili hivi Yule kijana akatoka na kuliacha gari la Amata kisha akaingia kwenye gari kama ya tano hivi katika maegesho yale. Amata akafikiri moj na mbili, akapita kwa haraka nyuma ya gari zile, na kuiacha ile ya kwake, akiwa anakimbia huku kainama aliliifikia ile gari Toyota Mark II na kuchukua fungua yake yenye uwezo wa kufungua kila kitasa cha gari, akafungua buti na kujitia ndani kisha akafunga na kuacha nafasi ndogo ya kupata hewa, akatulia kimya.
Ndani ya gari hiyo kulikuwapo vijana watatu, nao walikuwa kimya muda wote hakuna aliyeongea ila tu mitikisiko ya gari kila walipojigeuza. Baadae akasikia mmoja akijikohoza na kufuataiwa na kauli.
“Asee huyu jamaa vipi hadi sasa!” mmoja akasema.
“Dakika kumi sasa, sio kawaida maana tunachelewa,” mwingine akajibu kisha ukimya ukatawala tena.
“Mpe taarifa Master juu ya hali hiii kisha yeye atatuambia la kufanya,” mtu wa tatu akatoa wazo na mara hiyo Amata akasikia mlio wa batani za simu akazisikiliza kwa makini sana ili aweze kugundua ni namba gani iliyopigwa, akatikisa kichwa baada ya kuona kasahau baadhi ya milio, hii anaweza Chiba, akajisemea moyoni. Lakini aktega sikio kusikiliza nini kitaongelewa.
“Ee Master, jamaa hajarudi hadi sasa tuchukue hatua gani?” akauliza. Kisha ukimya ukafuata, Kamanda Amata akajua kwa vyovyote mtu wa upande wa pili atakua akiongea.
“Sawa! Master,” kisha ukafuatwa mlio wa simu kukatwa. Amata akainua simu yake taratibu na kutuma ujumbe mfupi kwa kampani yake kuwajulisha kinachoendelea.
“Huyu jamaa naye mbona haji? Au bado anakula raha, mh! Leo Lulu anal oleo,” mmoja wao katika gari ile akawaambia wenzake mara Amata akasikia mlio wa simu inayoita.
“Yes! Ndio… he! Ok sawa!” Yule jamaa akaongea hayo katika simu kisha ile gari ikawashwa na kuondolewa mahala pale. Amata akaangalia kwenye uwazi mdogo wa buti hilo akaoana kuwa bado hawajaiacha hoteli ile na baadae wakaingia barabara ya Maktaba.
Briston alitikisa kichwa akamwangalia Kubrah.
“Ametuweza mshenzi huyu!” Bristona akasema.
“Na mimi nimemuweza, subiri usikie,” Kubrah akajibu na kumfanya Briston kumtazama, “Mbona unaniangalia?” akamuuliza.
“Umesema umemuweza?”
“Ndiyo, we sikiliza tu ndani ya saa moja lijalo, nimemuwekea motto katika gari yake akiingia tu puuuuuu!” Kubrah akasema kisha wote wakaangua kicheko lakini Briston akanyamaza ghafla.
“Vipi?” Kubrah akauliza.
“Nasikitika kwa kifo cha huyu jamaa na Lulu, inabidi tuwe tayari, kesho asubuhi tukimuondoa Malkia na sisi tuondoke kisha plan B ichukue nafasi kwa kuwa kule Mpumbutu jamaa wameshaharibu na Mkuu wa wakuu amekasirika sana, anataka kuongea na huyu Rais wa hapa, sikia tutakuwa na kikao kizito pale Cape Town juu ya hili haraka iwezekanavyo,” Briston akamwambia Kubrah.
“Tuondoke, tushughulike na huyu kimburu,” Kubrah akasema.
“Hayuko peke yake, wako kama wane hivi, wote lazima washughulikiwe,” Briston akiajbu huku akifungua mlango kutoka. Nje ya hoteli hiyo kila mmoja alichukua gari yake na kuondoka. Lakini Kubrah aliitazama sana gari ya Amata na akaiona ikiwa palepale, ina maana huyu mshenzi bado yupo humu ndani? Akajiuliza. Na taratibu akaondosha gari yake pale hotelini huku akimwagiza mmoja wa vijana wake kuiangalia ile gari mpaka itakapoondoka
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom