WanaJF!
Dhana ya kuchangia chama cha siasa kwa kujitolea si vibaya kwa baadhi ya matukio yenye uhitaji wa kuchangiwa kwa hali na mali ikiwemo chaguzi.
Dhana hii imekuwa ikitumiwa kimakosa na viongozi wa CHADEMA kwani wao wameigeuza dhana hii na kuifanya tabia, kwani kila mahali wakikutana na wananchi wao ni kutembeza bakuli tu.
Hali hiyo ya kupitisha maboksi kwa walala hoi na kushawishi kuchangiwa imekuwa ni kama utapeli, kwani ni wazi kuwa CHADEMA ina jitosheleza kimapato ya kuendesha mikutano na ina wadhamini wakubwa tena wafanyabiashara.
Aidha, katika kufanikisha azma yao hiyo ya kutapeli wananchi kwa mwamvuli wa kuchangia mabadiliko, wamebuni mbinu ya kuweka watu wao mbele ili watakapo changia wao kwa wingi iwe chachu ya kuhamasisha na walala hoi nao kuchangia, huu ni usanii wa CHADEMA.
Ikumbukwe kuwa kwa sasa vyama vya siasa vina ruzuku kutoka serikali na kazi mojawapo ya ruzuku kwa vyama vya siasa ni kuwezesha vyama kufanya shughuli za siasa ikiwemo mikutano, sasa kwanini CHADEMA ipitishe kapu kwa walala hoi?
Kwa sasa viongozi wa CHADEMA wapo mikoani kuelimisha wananchi kuhusu suala la katiba mpya, lakini jambo la kusikitisha ni kuona viongozi hao wa CHADEMA wakipitisha maboksi kwa ajili ya kuchangiwa pindi wanapo maliza kutoa elimu hiyo kwa wananchi. Je, hivi ndivyo jinsi elimu kuhusu katiba inavyo tolewa?
USHAURI KWA CHADEMA;
Kwa kutambua kuwa siasa sio uadui, nichukue fursa hii kushauri viongozi wa CHADEMA kuwa wabunifu wa miradi mbalimbali ya chama yenye tija ili kuweza kuingizia chama mapato ya ziada kwa ajili ya chama, badala ya huu utaratibu wa kuwakamua walala hoi unao ongozwa na kamanda Mbowe.
Mbowe akipitisha boksi kwa walala hoi kwa ajili ya kuchangiwa hela baada ya mkutano.