Omba omba wa Leo kanishangaza

Omba omba wa Leo kanishangaza

beco

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
1,339
Reaction score
787
Leo mida ya saa 4 asubuhi nilikuwa nimepaki gari manispaa ya temeke ,akaja mtu wa makamo kavaa kawaida sana akaniomba nauli ya kwenda kawe nikamjibu sina ,baada ya muda roho ikajistukia nikashuka nikamfuata nikampa elfu 2 zilikuwa buku buku akaenda nikapata hamu ya kutaka kujua kuwa ni mkweli au la nikijifanya kama naondoka nikarudi bila ya yy kuniona .
Japo la kwanza alipofika pale stand alikuta kuna vipofu akatoa hela akawapa nahisi ni ile buku 1 na pili kweli alipanda gari la kawe tofauti na omba omba wengi walivyo huyu waleo ni wakipekee
My take akikujia mtu anataka kitu kama unaweza msaidie ,haijilishi km ni mkweli au muongo Kwa kuwa wapo wengine wa kweli na hauwezi kuwajua
Na katu usimnyime anaeomba akale.
 
Sasa kuna chuma ulete,,ukimpa tu imekula kwako,,juzi nimekutana na mmoja mikocheni anatiambia anaomba nauli katoka mlimani city kwa mguu mpka mikochen so nimpe aende kkoo,nikamwambia sikupi naogopa


Hivi kwann wanaonaga rahis kuomba mtu nauli kwann wasiende kwa daldala wamuombe kinda,,kuna tofauti gani, hapo ndo wananitiaga mashaka
 
nimewakumbuka wagosi wakaya."na sasa tumalizie salamu zetu kwa makamba.hawa kina matonya hawako uko tu dar es salama,ata uku tanga wamejazana kiamaaa"
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Si ajabu omba omba professional akawa na account JF.
 
Yaaani huna ulichonisaidia manakee umeamua kuja kunitangaza humu ndani wakusifie ila mbele ya baba yetu we huna uluchopata,next time ukinisaidia ibakie moyoni mwako na sio ulete huku msaada wa wako wa buku beee kila ajue ulinipa
 
Yaaani huna ulichonisaidia manakee umeamua kuja kunitangaza humu ndani wakusifie ila mbele ya baba yetu we huna uluchopata,next time ukinisaidia ibakie moyoni mwako na sio ulete huku msaada wa wako wa buku beee kila ajue ulinipa
Kitu kizuri au kikubwa Mungu anaangalia dhamira ,anajua ya siri na ya dhahiri kama nimefanya nipate ujiko au nimesema nipate ujiko he knws ,kama nimesema tujifunze he knws as well ,na analipa kwa nia.
 
Hahaaa yaani wewe ndo mshamba maneno yooote we umeona gari tu ,sasa ulitaka niseme nilikuwa kwenye guta wakati nilikuwa kwenye gari ?kuwa au kutokuwa na gari ni non issue
We mshamba tu. Kwani lazima utaje gari ? Kwenye ukoo you are number one to own a used car. Ptyuuuuui mshamba kajogoo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom