Omary Mgumba: Hizi ndio sababu za serikali kuhamishia fedha za taasisi zake BOT

Tatizo nikuchukua fedha za serikali kwenda kucheza upatu. Wakati kunafedha haziendikufanya kazi iliyo kusudiwa. Watu wanatengeneza faida alafu wanagawana. Mnaishia kulaumu serikali. Mabenki ya washawishi wateja wao/wananchi wafanyenao michezoiyo.
 
yaani pesa yako alafu uanze kukubaliana na Mtu,hakuna kitu kama hicho benk inatakiwa iwe na mtaji wake,kaza baba hili
Ndio ilivyo tanzania, Huoni mpaka sasa pesa yetu ya mafao bado tunakubaliana na ssra, Wanakomaa nazo utadhani tumewaomba watusaidie uzeeni wakati hata baba yangu alikuwa analima tu na akiugua anauza mahindi ili apate pesa ya tiba.FOOLISH TZ
 
Wewe naona concept ya banking huielewi kabisa. Eti "iwe na mtaji wake"? Hivi wewe unafikiri benki inafanyaje kazi? Inachukua deposits za wateja na kuzikopesha kwa wateja wengine...bank inamtoza aliyekopa riba na inamlipa depositor riba pia. Duniani kote ndivyo benki zinavyofanya kazi. Hiyo inasaidia hela ya depositor..iende kwa mhitaji mwingine na yeye aweze kufanya shughuli ya kuzalisha...na ndio uchumi unavyokua. Sasa zote zimerundikwa BoT...zimekaa tu wala hazisaidii kukuza uchumi. Ni mtu asiyeelewa economics tu atakayefurahia jambo la namna hii.

Naona una ka point hapa ila baada ya mabenki ya tanzania kuzoea kujilimbikizia faida kwa mabidilioni ndio sababu wanapata taabu kujiendesha.wangezoea kufanya fair business wala hawangekuwa na shida?

Mf. Interest za mikopo hapa tanzania ni kati ya 20% to 25% ni biashara chache sana zinaweza kulipa hiyo riba...hapo win win situation ipo wapi? Kama sio kumfilisi muwekezaji ...depositor?

Kila mwaka utasikia tumepata faida ya bilioni 46??? Walikuwa wakifanyia nini hiyo faida? Walitakiwa kupanua uigo wa biashara

Binafsi napata uchungu sana na hiyo interest ya 20 to 25% ya mabenki kwani ni udhibitidho kuwa hayajali wanachi hata kidogo

Nilitanani riba za mabenki ziwe 10 to 15% kama kweli ni win win situation

Katika hiyo 25% wanayopata kwenye mikopo umewahi kujiuliza unapata ngapi wewe muwekezaji (depositor)???

Ukitoa makato ya kila mwezi na makato mengine lukuki waliyo weka unapata kama nyingi sana ni 1%
Hapa mabenki huvuna hela na kuacha watanzania wakiendelea kuwa masikini

Nachelea kusema kuwa mabenki kwa muda mrefu yamefanya Tanzania kama shamva la bibi...wanavuna tuuu na hakuna wakuwauliza
 
Ishu siyo serikali kuondoa pesa zake kwenye mabenki ya biashara ishu hapa ni Uharaka wa kuziondoa pesa hizo bila kuyapa mabenki muda wa kubadirisha business modal zao.

pili serikali ingeweza kukaa na mabenki na kuongea nayo ili iwepo win win situation, kwa mfano serikali ingeyaambia mabenki kuwa na yenyewe ipate asilimia fulani ya faida pindi benki zikikopesha zile pesa kwenda kwa biashara mbalimbali. Na pia yenyewe ikienda kukopa basi isitozwe riba, bali ipunguziwe faida yake pesa za serikali pindi zikikopeshwa kwa firms nyingine.

Yaani badala ya kutoa mapesa hayo kwenye mabenki ya biashara na kwenda kuyaatamia benki kuu, basi yangekuwa katika mzunguuko na kustimulate uchumi!
Ahahaaaaa,, nahitaji pesa yangu iliyopo mezan naiona nianze kukubembeleza wakati muda mrefu ulikuwa ukinicheka,,,, mabank tafuten masoko mpyaaa,, upigaji na kuinyanyasa serikali kwishaaa
 
Hakukuwa na sababu yenye ujazo kuziondoa fedha za mashirika ya umma kwenye mabenki ya biashara kama kigezo pekee mnachokitaja ni hicho.

Walitakiwa kutoa waraka tu wenye maelekezo pamoja na mengine kuwa "itakuwa ni marufuku kuweka fedha za uma kwenye account ya muda maalumu"

Kanuni iambatane na maelekezo ya kupost BOT balance ya akiba ya mashirika yote ya uma kila siku ya kazi.

MCHEZO ULIKUWA UMEKWISHA.

Anachofanya JPM ni chuki iliyozalishwa na kupiga pushups jukwaani (kitendo kilichokejeliwa sana)
Hivi kwani ni mabenki mangapi ya biashara yaliyokuwa na hela ya serikali zaidi ya crdb...?!
 
Mh mbunge na mh rais tupo pamoja msilegeze kamba
Kwa kuwa sikufahamu, na umenishambulia ki psychology natangaza hadharani, mwana ccm yeyote akiniomba msaada nampa makavu nikiamini ndio wewe.
 
Hakukuwa na sababu yenye ujazo kuziondoa fedha za mashirika ya umma kwenye mabenki ya biashara kama kigezo pekee mnachokitaja ni hicho.

Walitakiwa kutoa waraka tu wenye maelekezo pamoja na mengine kuwa "itakuwa ni marufuku kuweka fedha za uma kwenye account ya muda maalumu"

Kanuni iambatane na maelekezo ya kupost BOT balance ya akiba ya mashirika yote ya uma kila siku ya kazi.

MCHEZO ULIKUWA UMEKWISHA.

Anachofanya JPM ni chuki iliyozalishwa na kupiga pushups jukwaani (kitendo kilichokejeliwa sana)
best solution every.

Asante kwa kuja.
 
Kwa kuwa sikufahamu, na umenishambulia ki psychology natangaza hadharani, mwana ccm yeyote akiniomba msaada nampa makavu nikiamini ndio wewe.
Sas unataka nikusifie ki psychology natangaza hadharani, mwana upinzani yeyot akiniomb msaada nampa msaad wa mawazo nikiamin ndo wew
 
Chadema kama kawaida yao, naona wanahangaika kutetea mafisadi


Mbowe umefilisi Nhc, rudisha pesa
Waliofilisi nchi ni ccm. Si mbowe wala Lowassa,

Mbowe na Lowassa hawakuwapo kwenye skendo za ufisadi

1. Epa
2. Escrow
3. Dowans
4. Iptl
5. Bot twin towers.
6. Mabilioni ya Jk.
7. Desi
8. Makontena hewa.
9. Ujenzi wa hoteli ya kitalii bonde la Ngorongoro.
10. Richmond
11. Bomba la mafuta bandarini.
12. Mishahara hewa.
13. Wafanyakazi hewa.
14. Wanafunzi hewa.
15. Nssf, ununuzi wa ardhi Kigamboni.
16. Pspf, mikopo kwa serikali.

Chama chenu ndicho kilichotufikisha hapa.
 
Back
Top Bottom