Omary Kimbau, umeifanyia nini Kijitonyama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Omary Kimbau, umeifanyia nini Kijitonyama?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bujibuji, Jul 22, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Barabara mbovu, maji ya shida maisha magumu.
  Foleni inaanzia Moroko hadi Mwenge, eneo ambalo kata yake ipo.
  Barabara mbadala zipo, haziwekwi lami wala kukwanguliwa.
  Zuzumagic huyo tumemchoka na hatumtaki.
  Akagombee udiwani hukohuko Masaki kwenye maslahi nako.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kimbau!!
  Oh! I know the guy, huwa hakosi kwenye shoo ya FM academia pale katika ukumbi wa kijiji cha Makumbusho.
  Na ni kawaida yake kuwatunza(kuwapa pesa) akina Nyoshi El Saadat sauti ya Simba.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Ndio taabu ya kuwachagua mapedeshee.
  Mwenge Kijijini maji si ya uhakika, kipindi cha mvua ni balaa,
  mifereji hamna.
  Madampo yanaibuka kila siku, sasa dampo limehamia kwenye Zahanati ya Mwenge.
  Ukienda kupata tiba unarudi na mafua huku kifua kikuuma kutokana na harufu kali ya uchafu.
   
 4. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Kwani nyie wakazi wa Kijitonyama mlimchagua huyo kimbau kwa vigezo gani hasa?
  Majuto mjukuu mnalo, limewaganda.
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Msimpe kura tena huyu bitozi.
  Tafuteni watu makini wenye kuelewa nini maana ya dhamana ya uongozi.
   
Loading...