Omarosa na Trump

Omarosa na Trump

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,493
Reaction score
145,853
Omarosa.jpg


Omarosa Manigault-Newman...

Huyu mama huyu...ni bonge moja la drama queen. Sitoshangaa huyu ndo akawa sababu ya Donald Trump kuanguka na kuachia urais.

Mwaka 2004 ndo nilimwona kwa mara ya kwanza huyu mama. Nilimwoma kwenye kipindi cha Apprentice kilichokuwa kinaongozwa na Donald Trump.

Kwenye hicho kipindi huyu mama alijionyesha kuwa ni mpenda drama sana. Mara aligombana karibu na washiriki wote kwenye hicho kipindi kwa wakati huo.

Tokea hapo ndo yeye na Trump wakawa karibu. Baadaye mwaka 2016 akafanya kazi kwenye kampeni ya urais ya Donald Trump.

Baada ya Trump kushinda, akaja kuteuliwa na [Trump] kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya moja ya idara za White House.

Hakudumu sana kwenye hiyo nafasi. Alifukuzwa mwishoni mwa mwaka jana.

Sasa kaandika kitabu kuhusu muda wake hapo White House na kaja na tuhuma kibao.

Moja ya tuhuma ni anadai kuwa Trump alishawahi kurekodiwa akilitumia neno la 'N' [the N word]. Trump mwenyewe kakanusha.

Akiwa hapo White House, Omarosa inaelekea aliwarekodi kwenye mazungumzo watu wengi. Kuanzia Trump mwenyewe, General Kelly, na wengineo.

Sasa kaanza kuachia kidogo kidogo mazungumzo ambayo alikuwa anayarekodi.

Je, hiyo kanda ya Trump anayodai Omarosa kuwa ipo nayo itavuja? Tusubiri tuone.

Ila kusema ukweli huyu Omarosa ni nyoka. Hapo White House inaonekana alikuwa yupo kwa ajili ya mashahi yake tu na siyo kulihudumia taifa lake.

Katika moja ya teuzi mbaya kabisa ambazo rais Trump kazifanya basi ya huyu mama inaweza kabisa kushika nafasi ya kwanza.

Ngoja tusubiri mwisho wake tuone...
 
'N'maanake Nyoko mkuu ama vp basi kumbe so tusi ni kibantu tu hicho
 
We kumbe humfahamu hata kidogo trump,aanguswhe na huyo.amepitia mangapi?wamejitokeza wanawake wengi kwamba aliwadhalilisha kingono imepita.wanasema Russia imemsaidia nayo itapita.wameandika Kitabu first and furry kiko wapi?,mwanasheria wake aliachia audio juzi juzi.iko wapi?
 
Trump hataondoka kwa kujiuzuru Bali mpaka muda wake utakapokwisha..porojo zilikuwa hawezi kumaliza hata miezi mitatu !lakini yupo mpaka sasa..
 
pia trump kamtoomba sana huyo dada mbele na nyuma ndo maana sisita ana hasira
 
Back
Top Bottom