figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Salaam Wakuu,Rais Samia katika Kongamano la Wafanyabiashara wa Oman na Tanzania, amesema kuna umuhimu Mkubwa wa kuangalia Usafiri wa Majini akimanisha Meli yenye Uwezo wa kusafirisha Wanyama wakiwa hai kutoka Tanzania kwenda Oman.
Watu hapa wasifikilie Wanyama Pori tu, Bali ni Habari njema kwa Wafugaji wa Tanzania kwani sasa Wataanza Kusafirisha Ng'ombe, Sungura, Kitimoto, Mbuzi, Swala, Twiga nk hasa kwa wawindaji wenye Vitaru.
Pia kazungumzia kuhusu meli za Kuvua samaki Bahari Kuu.
Amewataka Oman waje kuwekeza Tanzania ardhi ipo ya kutosha.
Watanzania Kaeni Mkao wa kula.
............................................................................
Rais Samia akiwa kwenye kongamano Kiuchumi nchini Oman, amesema kuwepo kwa vyombo vya usafirishaji vya majini kusafirisha wanyama walio hai na bidhaa mbalimbali kwenda Oman kutaboresha biashara kati ya pande hizo mbili
Pia amegusia japokuwa tuna makubwa ya kuvua, kwa sasa hamna uvuvi wenye tija kwa taifa, amesema “kuna nchi zinakuja Tanzania kuvua na hatuwezi kuwafukuza kwa sababu hatuna vifaa, hivyo wanavua na kuondoka, hili ni eneo lingine ambalo tunaweza kushirikiana kwa pamoja”
Amesema kuwa kongamano la mwaka huu limekusudia kuangazia namna Tanzania itashirikiana na Oman katika sekta za utalii, kilimo, Uzalishaji (viwanda) mifugo na uvuvi na usafirishaji wa majini.