Wakuu,
Nilibahatika kukutana uso kwa uso na Mh. Christopher Ole Sendeka katika pita pita zangu.
Baada ya mazungumzo ya hapa na pale nikamchomekea maswali kuhusu siasa ya Tanzania kama ifuatavyo:
1. Swali kwa Mh. Ole Sendeka: unaonaje siasa ya sasa na je, ccm hali mliyonayo mnaridhika nayo kweli?
- Jibu la Sendeka: hali ya siasa ya Tanzania siyo mbaya, lakini lazima nikiri kuwa hali ya ccm ya sasa haielezeki, kuna mambo mengi yanahitaji kiti cha mwenyekiti.
2. Swali kwa Mh. Sendeka kama hali ndiyo hivyo na hakuna hatua inayochukuliwa na kiti cha mwenyekiti, hamuoni kwamba tayari ccm tunaji expose kuelekea 2015?
-Jibu la Sendeka: dogo nakuambia haya yote tunayaona, tunayajua, lakini kwasababu MWENYEKITI WETU HASHAURIKI HAAMBILIKI, wacha chochote kitakachotokea kiwe!
3. Swali kwa Mh. Sendeka: kwakusema hivyo unamaanisha kuwa nawe umekata tamaa kugombea simanjiro au?
-Jibu la Sendeka: unazungumzia 2015, nani anajua tutafika huko dogo? We mwenyewe hiyo picha inaonekana umekoswa koswa na bomu soweto halafu unazungumzia 2015 dogo vipi?
4. Swali: Ole Milya unamzungumziaje kuelekea 2015?
- Sendeka: Namshauri akasome kwanza siasa bado.
5. Swali: Unamaanisha nini kusema Ole Milya akasome? Milya ana degree ya sheria kutoka UDSM, au ubunge unatakiwa kuwa na elimu gani?
Jibu la Sendeka: dogo wacha hayo ni matusi asante kwa msaada wako wa jumper wire. Kwaheri.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums