Hata mimi nilishaongea na diwani mmoja wa CCM huko mbinga,huyu bwana nilikutana naye wakati tumekwenda kukagua mradi wa majibu uliofadhiliwa na UNDP,katika maongezi yetu nilimuomba tuongee kama watanzania na tuache ushabiki wa vyama,nikamuuliza aniambie hali ya SIASA ipoje nchini kwa sasa,yy alisema hali sio mbaya sana ila CCM ndio ina hali mbaya na hali mbaya ya CCM ndio zitafanya SIASA za Tanzania ziwe mbaya.
Nikamuuliza tena nyie kama wana CCM ukiacha kupeana moyo ndani ya vikao vya Chama munauangaliaje uchaguzi 2015?
akaniambia tutakwenda kwenye uchaguzi na hofu,mashaka tele,kiukweli CCM sasa inategemea rehema za Mungu kuvuka 2015,na nilipomuuliza sababu ya yote hayo ni nini,alinijibu mwenyekiti ndio tatizo,hana msimamo katika yale wanayokubaliana ndani ya Chama........
Badae niliongea na dereva wa gari ya halmashauri akaniambia huyo jamaa ni mtu wa Lowasa vibaya mno na ni mmoja wa waratibu wa mipango mingi ya lowasa......so mkuu Mungi ulichoongea na Sendeka ndio hali halisi ya CCM leo.