Wanatoka kote, waweza kuta jamaa ni mkristu na siajabu kama ni mkatoliki anashiriki jumuiya, ila bado yuko kwenye kuamini nguvu za giza. Au Sheikh naye yumo kwenye hayo..
Wasioamini Mungu nao wamo humo, sana tu, ushirikina ni imani kama dini...ni juu yako kuamini au usiamini, ila jiulize, hao washirikina wakiingia lock-up mbona huwa hawajinasaui kwa ndumba?!
Hakuna imani ninayoidharau duniani kama ushirikina au uchawi, ni moja ya mbinu ya kutisha watu, kukosa ajira au utapeli, ujinga na kujipotezea muda...
Topic hapa ni Sayansi Vs Dini, sisi Waafrika siyo siri dini hizi 2 tumeletewa, Sayansi nayo tumeletewa, Sayansi ina majibu zaidi kuliko dini, je baadaye hao Waarabu na Wazungu wakija na mwelekeo mwingine tutaacha kuamini hayo madini yao na Sayansi na kuanza kuamini waliotuletea upya au?!