Tanzania tuna michoro Iringa na kwa warangi, tuna Olduvai Gorge, yenye kila aina ya vivutio na historia ya kudhihirisha binadamu walikuwa jamii ya nyani au sokwe, ndipo wakaanza kutembea, kupoteza manyoya, kubadilika "features", ubongo kukuwa, kupata maendeleo na kadhalika.
Tatizo wazungu hasa wanasayansi ndio wanasema hivi, wanadai mpaka vithibiti vipo kwamba tulikuwa wanyama na kubadilika kuwa binadamu.
Tanzania nasi twajitahidi kutunza hivi vivutio vya kitalii na kisayansi kama Wamisri...
Upande mwingine tena Mwarabu na Mzungu wanadai Mwenyezi Mungu aliumba dunia siku 7! Wote tumesoma maandiko haya kwenye Agano la Kale na kwamba akaumba binadamu wawili Adam na Eve..
Sisi Watanzania hasa, kipi cha kuamini kati ya haya tulioletewa, kwamba tulikuwa nyani au tuliumbwa?!
Ila yote naona twafaidika nayo, ila kama hili Taifa lina waumini wa Kiislamu na Kikristo kweli kuna haja na kuwa na hivi vivutio?! Hamuoni kama twajichanganya imani zetu au imani tulizoletewa na wenyewe?!
Je wakija tena na lingine hawa Wazungu au Waarabu je tutatupa haya madini yao na vivutio, kuanza kuamini mapya sababu wamesema wao?!
Na kama tunaamini hayo yote basi tukubaliane na zile thread humu kwamba Mzungu na Mwarabu wana akili kuliko sisi, wasemacho ndicho tunachoamini, abudu, ndio maisha yetu!
AU?!