Hapa nimejifunza mengi kuhusu uwezo wa silaha za mataifa mengi - asanteni sana wachangaiji.
Tatizo langu ni kuwa:
Hivi haya malumbano (postures) ya haya mataifa makubwa ya kivita (USA, Russia, EU, China, Israel, Pakistan, India, N. Korea, etc.) yanatusaidia nini sisi walalahoi wa mataifa mengine duniani na sisi wa
Bongo tu - (au kama sio vikaragosi au wategemea wakuu wa haya mataifa makubwa?)
Nina tatizo kubwa sana kwa Marekani kuikwaza Urusi kiuchumi eti tu kwa sababu Urusi inawapinga Marekani kuhimilishwa na kuhujumiwa na NATO.
(Kumbuka kuwa - Reagan na Gobachev walikubaliana kuwa NATO haitajisogeza hata mita moja mashariki kuihujumu Urusi walipovunja ukuta wa Berlin).
Hiki kitu cha Urusi kuihimili
Crimea ni sababu tu.
Crimea walijichagulia wenyewe kuhamia Urusi baada ya mapinduzi ya raisi
Yanukovych yaliyotokea February 2014. Kinacholeta huu mtafaruku sasa ni kuwa
NATO wanajikusanyia nchi nyingi ndani ya NATO ambazo katika makubaliano ya awali ya
Reagan na Gobachev walikubaliana kuwa hayatatokea.
Kwa sasa
Marekani (NATO) wanasema kuwa eti enzi hizo "Gobachev na Reagan hawakuyafanya haya makubaliano kimaadishi" - really?.
Mkuu
Nyani Ngabu (na wengine pia - nitawanukuu hapa chini), kwa kuwa wewe (nyie) natumai una(mna) historia nzuri ya
"the cold war", u(m)naweza kunisahihisha vizuri.
Ushauri:
Tusishabikie haya malumbano ya hizi SUPER au superior powers hata kidogo.
Kwa nini?
SISI SOTE NI MAJERUHI TU WA HAWA MAFAHARI WANAOGOMBANA!!
Tukatafute
MIHOGO na
MAHARAGE yetu tu tule!! Au vipi? Tupo Njia panda.
cc.
Dotworld Safari_ni-Safari
Maziku Masunga Jr. kui Somi mohamedidris789
TODAYS INConoclastes
malcolm Lumumba
Njooni huku bwana
Bukyanagandi elingata
TUJITEGEMEE Red Giant