Oh Your Excellence! (Picha)

Dhana ya msaada ina presume mahitaji; misaada inaomba pale ambapo kuna hitaji na hitaji ambalo sisi wenyewe kwa kutumia uwezo wetu wa ndani na raslimali zetu tumeshindwa kulipatia ufumbuzi hitaji hilo. Kwa mfano, je hatuna uwezo wa kutoa dola 50,000 kununua vitu vyote hivyo tulivyopewa na Wachina.. ukisema "hatuna" basi unaingiza ukweli kuwa kuna "hitaji" kwa hiyo wachina wanapokuja na misaada tunawashukuru kwa sababu wameitikia hitaji ambalo sisi hatukuwa nalo.

Bila kufahamu hili utajikuta unakinga mikono kila unachopewa kwa sababu tu ukikataa utaonekana una ringa.
 
Kwani kile kitengo kinachoshughulika na mambo ya maafa na misaada kipo IKULU??
 
ha ha ha ha!
kuna vitu vingi sana huvielewi rafiki.lakini sitapenda kukuelewesha anyway.hapo hakiangaliwi YEBO YEBO!kwa taarifa yako hapo inaangaliwa serikali ya china
So what? Wewe ndio mbumbumbu wa mambo. Nadhani umewekwa kwenye sehemu nyeti bila utaratibu na bila kuelewa utawala wa nchi unakwendaje. Kwa machache uliyojifunza ndani ya muda mfupi unaona ndio umeishajua kila kitu!

Ni yale yale ya utumwa mamboleo. Serikali ya Uchina inaangaliwa itufanyie nini kikubwa ambacho kinasababisha Rais wetu ajidhalilishe kupokea yeboyebo?

Bwana Geoff, asilimia 80 ya Watanzania wanakula wanacholima na kuvuna kwa jasho lao na si la Mchina. Wanavaa mitumba wanayonunua kwa fedha zinazotokana na mauzo ya mazao na ubangaizaji wao hawasaidiwi na Mchina. Hiyo Serikali ya Uchina inaleta yeboyebo ambazo tunazo sokoni na pikipiki ambazo tayari vijana wengi wa Kitanzania wameweza kuzinunua kwa kwa jasho lao na wanazitumia kupakia watu kwa bei nafuu ama kuwavusha kwenye sehemu zisizoweza kufika mabasi.

Acheni kumdhalilisha Rais, midhali alipigiwa kura na wananchi sio Rais wenu peke yenu ambaye mnaweza kumdanganya afanye mambo ya kujidhalilisha na kudhalilisha Umma mzima wa Tanzania.
 

jkviatu.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu YEBOYEBO vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam jana asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.
 
Waswahili tulivyo tena unaweza sikia viatu vilivyotolewa msaada na Wachina havijawafikia walengwa, nusu vyaibiwa! i mean yebo hizo!
 
Ha ha ha!Umenichekesha sana.ndio unagundua leo kwamba we are so cheap? halafu kamsaada kenyewe ka milioni 51...
 
Kweli wametupima na kuona kuwa ni wadhaifu sana katika kufikiria maana mimi sijajua maana ya hii misaada ya mipira yao hao ambayo hata mimi naweza kutoa
 




My Take:



Misaada mingine tunayopokea au kumuacha Rais apokee kwa niaba yetu ni ya kiudhalilishaji wa jumla! Yaani hawa Wachina wameshindwa kupeleka misaada yao Red Cross au kwa taasisi fulani moja kwamoja hadi wapeleke Ikulu?​

jkviatu.jpg



Nimeipenda hii..........naona Muungwana ana appreciate msaada wa YEBO YEBO.

Lakini Mwanakijiji huna haja ya kushangaa, ndio Raisi ambaye zaidi ya Watanzania asilimia 80 walisema anafaa. Ndiye huyu aliyeunguza pesa za walipakodi kwenda Marekani kuomba VYANDARUA!
Mungu ampe maisha marefu................!
 
JK na wote wanaomzunguka nadhani wanahitaji rehab..
 
Sina cha kuongea ila nitaendelea kucheka tu! teteteteteteeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom