Oh Your Excellence! (Picha)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
baada ya kupokea misaada yenye thamani ya shilingi milioni 51 toka Uchina. (Picha na Haki Hakingowi)

Rais Jakaya Kikwete Apokea Misaada Kutoka China

Picha+no+5.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika mahojiano na mwakilishi wa shirika la habari la Xinhua nchini Tanzania Bi. Guo Chunju mara baada ya nchi ya China kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 51 kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini jana jijini Dar es salaam.​

jkpikipiki.jpg


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amepanda katika pikpiki aliyokabidhiwa na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xingshen kama seshemu ya msaada wa China kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Hafla hiyo ilifanyika ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.Misaada mingine iliyokabidhiwa katika hafkla hiyo ni pamoja na baiskeli, chupa za maji na mashine za kushonea nguo.​

jkmpira.jpg

Balozi wa China Nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete mipira soka na vifaa vingine ikiwemo baiskeli,pikipiki, chupa za maji na mshine za kushonea nguo kama mchango wake kwa sekta mbalimbali za maendeleo nchini.Wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko Kilosa mkoani Morogoro​

jkviatu.jpg

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia viatu vilivyotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam jana asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.​
http://1.bp.blogspot.com/_stxylFr6jLM/S7Hrlq-_dEI/AAAAAAAAmBQ/930AHDAQq0k/s1600/2.jpg

jkbaiskeli.jpg

Rais Jakaya Kikwete akiagalia msaada wa baiskeli zilizotolewa na nchi ya China ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 51 vilivyotolewa na nchi hiyo jana Ikulu jijini Dar es salaam.Kulia kwake ni Balozi wa China Liu Xinsheng aliyekabidhi msaada huo.

Picha na Freddy Maro/Ikulu


My Take:

Misaada mingine tunayopokea au kumuacha Rais apokee kwa niaba yetu ni ya kiudhalilishaji wa jumla! Yaani hawa Wachina wameshindwa kupeleka misaada yao Red Cross au kwa taasisi fulani moja kwamoja hadi wapeleke Ikulu?

We are so cheap! This is when I call to mind with some apprehension SWALA and kampuni ya BORA! Mweh Ubepari kweli ni unyama!
 
"Baiskeli za Cheng shang kwa madaha ndio zenyewe zina nguvu imara kama simba. zinabeba mzigo zaidi ya punda."

Nimelikumbuka tangazo la baiskeli. Hivi kiwanda chetu cha baisikeli kipo? kinafanya kazi?
 
Brother MM, na kakako mwenyewe sometimes amezidi mno. Nafikiri wewe ni rafiki yake wa karibu, jaribu basi kumshauri ajaribu kudeligate baadhi ya mambo. Waziri anayeshughulikia maafa si yupo, kwanini asipokee yeye?
 
Yaani msaada wa milioni 51 unapokelewa na Rais! Mkulu anatuaibisha kabisa na kutufanya WaTZ tuonekane so cheap. Kiasi hicho cha pesa kwangu mimi kingepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala na si Rais.
 
Yaani msaada wa milioni 51 unapokelewa nufanya WaTa Rais! Mkulu anatuaibisha kabisa na kutufanya WaTZ tuonekane so cheap. Kiasi hicho cha pesa kwangu mimi kingepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala na si Rais.

mkuu hapo kwenye bluu ni kingazija hicho?
 
Ipo siku wachina watampelekea condom za kichina na
tunaomba azionyeshe hadharani hivi hivi huu ni ukwereeeeee

aibu yao aibu yetuuuuuuuuu
aibu yakeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee shame presida!!!!!
 
jkpikipiki.jpg

mmhh.......mwanawane!!!!

Hivi hii picha wamepanda watu wangapi? au ni macho yangu yamekuwa ya kichina? maana naona kama kuna miguu ya kulia miwili mmoja kwenye paddle na mwingine chini au?? Presidaa alipakia mtu mgongoni???
 
Hivi hii picha wamepanda watu wangapi? au ni macho yangu yamekuwa ya kichina? maana naona kama kuna miguu ya kulia miwili mmoja kwenye paddle na mwingine chini au?? Presidaa alipakia mtu mgongoni???

hapo muheshimiwa amekaa kwa upande mmoja, hajaipanda hiyo TOYO ipasavyo
 
Hivi hii picha wamepanda watu wangapi? au ni macho yangu yamekuwa ya kichina? maana naona kama kuna miguu ya kulia miwili mmoja kwenye paddle na mwingine chini au?? Presidaa alipakia mtu mgongoni???

kuna mtu kwa nyuma alikuwa anastabilize piki isianguke. Jk aoenekane kama anaendesha hivi.
 
Sasa kama kila upenyo wa kufikia maendeleo mmewapa wageni watengeze faida na kuondoka, mnategemea mtakosa rais matonya?
 
mimi sioni tatizo na hiyo misaada!nashindwa kuwaelewa kwanini mmekuwa wakali
 
mimi sioni tatizo na hiyo misaada!nashindwa kuwaelewa kwanini mmekuwa wakali

ningeshangaa kama ungeona kuna tatizo. Ndio uzuri wa fikra tofauti kwenye demokrasia. Misaada haina tatizo lolote, tatizo liko kwa Rais!
 
ningeshangaa kama ungeona kuna tatizo. Ndio uzuri wa fikra tofauti kwenye demokrasia. Misaada haina tatizo lolote, tatizo liko kwa Rais!
tatizo la rais ni KUIPOKEA YEYE MWENYEWE?
au KWAMBA WACHINA HAWAKUCHANGIA RED-CROSS?
 
Back
Top Bottom