squirtinator
JF-Expert Member
- Sep 20, 2015
- 2,765
- 4,174
Petro E. Mselewa huu uzi unamuhusu.Kwa mtazamo wangu,licha ya haki yao ya kutokuwa na upande,hili ni kundi la watu "mzigo" maana ni watu wanaokuwa influenced na matukio yanayofanya na wanasiasa pasipokujali dhamira za wanasiasa hao na wanakuwa ni watu wa kuyumbishwa tu na bahati mbaya kura wanapiga kuchagua viongozi.
Watu wa aina hii,mwanasiasa leo akipata tuhuma za kuua, ufidadi au kudhuru, na kesho akajenga barabara,akawapa hela, n.k, wao watakuja hadharani na kumsifia wanasahau kuwa ni lazima mwanasiasa huyu afanye mazuri machache ili apate kuungwa mkono ili kesho tena aweze kudhuru, kuiba, n.k(anang'ata na kupuliza).
Watu wasio na upande ambao leo watamsifia na kesho watamlalamikia, wanashindwa kuelewa kuwa mwanasiasa wa aina hii lengo lake ni kuwa-fool watu ili aweze kupata kundi la watu wa kuumunga mkono, hata kama ni wache, licha ya madhambi ya makusudi anayoyafanya.
Kwa upande mwingine, watu wenye upande mara nyingi huangalia zaidi dhamira ya kiongozi na sio matendo au maamuzi anayoyafanya ambayo wakati mwingine ndani yake yanaweza kuwa yamejaa hadaa fulani ili kupumbaza watu.
Watu wanye upande wao huangali zaidi dhamira ya mtu na wakishagundua ni mtu wa aina gani, basi hufanya maamuzi ya ama kumuunga mkono au kumkataa (kuwa na upande mmoja) na watu wa aina hii ndio wanaweza kufanya maamuzi sahihi katika sanduku la kura tofauti na wale utakaowasikia wakisema mimi niko neutral ambao huyumbishwa na matukio au maamuzi ya wanasiasa pasipo kuwapma dhamira zao na matokeo yake hufanya maamuzi yasiyo sahihi katika kuchagua viongozi.
Kwahiyo, wale wote ambao leo utwasikia wanamlalamikia mwanasiasa fulani na kesho wanamfagilia,mjue tu watu wa aina hiyo teyari ni mateka wa fikra na hawana tofauti na mwanaume alielishwa "limbwata" na kuwa "zezeta" na hawa wanaponza hata wale walioamua kufanya maamuzi ya kumkataa mwanasiasa au kiongozi wa aina hiyo (mwenye tabia ya kung'ata na kupuliza).
Ni kweli binadamu wote tuna mapungufu lakini kufanya au kutenda mambo mabaya kwa makusudi,hii huwa ni dhamira ya mtu ambayo siku zote tunapaswa kuitumia katika kumpina mtu, kiongozi au mwanasiasa yoyote yule.
Kiongozi bora apimwe wa dhamira iliyo nyuma ya maamuzi au matendo yake na kamwe si kwa kutazama matendo au maamuzi anayoyafanya kwani mtapotea na kudanganyika.